YESU NI JIBU

Alhamisi, 1 Desemba 2016

UZINDUZI WA TAASISI WA ASKOFU MATHAYO SULEIMAN ULIOFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM KWA LENGO LA KUWASAIDIA WENYE MAHITAJI MBALIMBALI

 Wa nne kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Mathayo Suleiman Foundation mchungaji Eliasaph Mathayo  na kulia kwake ni naibu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi balozi Simba Yahya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa taasisi hiyo.

Jumatano, 23 Novemba 2016

MUNGU WA KWELI NI WA MATAIFA YOTE,BILA KUJALI DINI KABILA RANGI,NDIYO MAANA YEYE ANATENDA MAKUU.

Ni katika ibada na kipindi cha maombe na maombezi ambapo nguvu za Roho Mtakatifu zilishuka kwa namna ya tofauti na wengi kunena kwa lugha.
Hapa ni ndani ya ibada maombe na maombezi yakiendelea.

Ijumaa, 18 Novemba 2016

KUWA NA MTAZAMO SAHIHI KWA MUNGU WAKO NAWE UTAMTUMIKIA KWA UAMINIFU:


 Mchungaji kiongozi na pia ni askofu Geoffrey Masawe akifanya maombi madhabahuni.

MWANAMKE AFARIKI AKIOMBEWA KWA ‘NABII’ JIJINI ARUSHA ANYOLEWA NYWELE NA NYUSI.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo
Mwanamke  mkazi wa Unga-Limited jijini Arusha , Lightness Kivuyo ameripotiwa kufa wakati akifanyiwa maombi nyumbani kwa mchungaji aliyejulikana kama ‘Nabii Rajabu’ eneo la Kwa-Mrombo pia jijini Arusha.

CITY HAVERSTY INTERNATIONAL CHURCH YAWASIMIKA VIONGOZI WANANE TAYARI KWA HUDUMA.

 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la City Haversty International Apostle Dr Livistone Banjagala wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati ajiandaa kuwasimika wachungaji wa kanisa lake.

Jumamosi, 5 Novemba 2016

MAHAKAMA KUU YAZUIA KUFUKUZWA MAKAMU ASKOFU WA EAGT

Mapanga yatumika kulinda Kanisa alipozikwa Ask.Kulola,
Miaka mitatu na siku 50 hivi, tangu Askofu Mkuu na Mwanzilishi wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) DK. Moses Kulola kumaliza kazi hapa duniani, (kufariki) hali si shwari ndani ya kansia aliloacha, baada ya Makamu Askofu Mkuu, John Maene kufukuzwa katika uongozi na uchungaji katika kanisa la Bungando, Mwanza, lilipo kaburi la mwanainjili huyo na kuzua kiza kinene katika mustakabali wa kiroho.
Habari za ndani toka ndani ya kanisa hilo zinaeleza kuwa tangu kutwaliwa kwa kiongozi huyo, ilizuka hali ya sintofahamu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutoelewana baina ya wale wanaoelezwa kuwa ni “wa Kulola” yaani wafuasi wake  sugu na wale wa kizazi kipya kinachotaka kubadili mambo na kujenga himaya mpya.
Ni katika hali hiyo, hivi karibuni aliyekuwa Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, John Maene, alifukuzwa uongozi na uchungaji kwa kile kilichodaiwa kuwa alipatikana na tuhuma za ukiukaji wa kimaadili, lakini akapinga tuhuma mbele ya Halmashauri ya kanisa na kasha kufungua Kesi katika mahakama Kuu kanda ya Mwanza.

Jumatano, 5 Oktoba 2016

NI JINSI GANI UNAWEZA KUINUKA AMA KUONDOKA NA KUANGAZA.

 
 Askofu Dkt Lawrence kameta Akifundisha neno la Mungu ndani ya kanisa la amani Christian Center
 Isaya 60:1-2
Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako. 
kuna mambo matano ambayo unaweza kupitia

Jumatano, 21 Septemba 2016

KATIKA KILA JAMBO ILI UFANIKIWE NA KUTENDA KWA UFASAHA ANZA NA MUNGU KAMA KAMOGA MKURUGENZI MTEULE WA WILAYA YA MBULU ALIMUA KUANZA NA MUNGU

Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimwombea Hudson Kamogaakiwa amepiga magoti .
Waumini wa Kanisani Living Water Center Kawe wakiwa wamenyoosha mikono kwa Hudson Kamoga kuomba kwa ajili yake 


Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga 

Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake. 
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake. 

Alhamisi, 4 Agosti 2016

MCHUNGAJI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUNGA SIKU 30 ALITAKA KUVUNJA REKODI YA YESU KRISTU YA KUFUNGA SIKU 40

Katika jitihada imedhamiria kuvunja rekodi iliyowekwa na Yesu Kristo wa Nazareti, 44 mwenye umri wa miaka maarufu wa Afrika Kusini mchungaji, Alfred Ndlovu, amefariki dunia kwa utapiamlo baada ya kufunga  kavu mfungo ambao ulidumu kwa siku 30.

Ijumaa, 29 Julai 2016

WENGI WAFUNGULIWA NA KUWEKWA HURU WAKATI WA UBATIZO:

 Hirizi ambazo zilitapikwa na mmoja wa watu waiofika kanisani na kuanza kuombewa na mara baada ya kutapika alianza kufunguliwa.

JIMBO LA TEMEKE LIMEONYWA KUWA MAKINI NA MGOGORO UNAOENDELEA AMBAO TAYARI UPO UMEFIKISHWA MAHAKAMANI:

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa kansia la EAGT, Mzee Henri Mfuko, ameonya kuwa kansia hilo linakabiliwa na hatari ya kugawanyika kufuatia mgogoro ulioibuka baina ya uongozi wa kanda na ule wa Jimbo la temeke ambao umesababisha kufunguliwa kwa kesi ya madai mahakamani na kusimamishwa kwa viongozi wa Jimbo. Huku ikielezwa kuwa kivuli cha Hayati Askofu Dk. Moses Kulola ndicho kinacholityesa kanisa hilo.
Aidha imeelezwa kuwa  Wothia alioandika kulola Kabla ya kufariki dunia unaompa Katunzi kijititi cha kuhubiri Injili, kukua kwa kasi kwa kansia la EAGT City Centre na mpango wa kujenga majengo ya kisasa ya Jimbo la Temeke viliibua upinzani mkubwa  uliopelekea kuvuliwa  madaraka  na kugawanywa kwa Jimbo bila kufuata taratibu.
Ni kwa sababu hiyo, Askofu Katunzi na wenzake waliamua kufungua shauri la madai Mahakamani na ikatolewa amri ya kuzuia mkutano lakini  haikuheshimiwa na badala yake  mkutano ukafanyika na viongozi wa muda wakateuliwa.

Alhamisi, 28 Julai 2016

PAPA FRANCIS AANGUKA GHAFLA AKIONGOZA MISA POLAND

 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amepata ajali ya kuanguka ghafla alipokuwa akitembea kuelekea kwenye jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuendesha ibada, Czestochowa nchini Poland.

Jumanne, 26 Julai 2016

MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO ANENA MAZITO KUHUSU LOWASSA

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’ amesema kitendo cha viongozi wa CCM kulitaja zaidi jina la Edward Lowassa katika Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho ni ishara kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani ni tishio.

Jumamosi, 16 Julai 2016

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI NA WATENDAJI WA TAASISI ZA SERIKALI NA AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WA POLISI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

1.   Mhe. Augustino Lyatonga Mrema.
·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.

·        Mhe. Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.

2.   Prof. William R. Mahalu
·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.

3.   Prof. Mohamed Janabi
·        Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

4.   Prof. Angelo Mtitu Mapunda
·        Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

5.   Bi. Sengiro Mulebya
·        Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

6.   Bw. Oliva Joseph Mhaiki
·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

7.   Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa
·        Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

8.   Dkt. Charles Rukiko Majinge
·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.

9.   Dkt. Julius David Mwaiselage
·        Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

DK. KIGWANGALLA- “TUTATATUA MGOGORO WA WANAKIJIJI NA HIFADHI YA MSITU WA IPALA KWA MAZUNGUMZO”

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili kwenye kijiji cha Ipala huku akipokelewa na baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo.Msululu wa wananchi wakiwa wamempokea Dk. Kigwangalla wakati akiwasili kwenye kijiji cha Ipala.

Ijumaa, 1 Julai 2016

MARUFUKU WANANCHI KUKATWA ASILIMIA 18 YA VAT KATIKA HUDUMA MBALIMBALI ZA TAASISI ZA FEDHA NA SIMU


Kamishina Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata akizungumza na waandishi habari juu zuio la taasisi za fedha na kampuni za simu kukata miamala ya kodi ya ongezeko la thamani VAT leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kamishina wa Mapato ya Ndani wa TRA, Elijah Mwandumbya. 

RAIS KAGAME AWASILI NCHINI-APOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alhamisi, 9 Juni 2016

DENI LA ZAIDI YA MILIONI 100 LASABABISHA KANISA LA SINZA CHRISTIAN CENTER KUTUPIWA VYOMBO VYAKE NJE:

Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya mil 100 kanisa la Sinza Christian Center  latupiwa nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na mmiliki jengo hilo Bwana Prosper Rwendera , akizungumzia tukio hilo  mke wa mmiliki  wa jengo Hilo Bi. Patricia Prosper Alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu." 
Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.

Jumatano, 8 Juni 2016

KAULI YA MWANGALIZI MKUU WA WAPO MISSION INTERNATIONAL WAKATI WA KUKUMBUKA SIKU YAKE YA KUZALIWA:

Tarehe 6 mwezi wa sita mwaka huu 2016 ni siku ya kumbukumbu ya  kuzaliwa kwa Askofu wa huduma yaBCIC na mwangalizi wa WAPO mission Askofu Sylivester Gamanywa, ambaye ameandika ujumbe ufuatao kwenye akaunti yake ya facebook.
SIKU NA MWEZI KAMA LEO NILIZALIWA DUNIANI!

miaka 59 iliyopita nilifurahia sana birthday yangu nikiwa na raha ya kuongezeka umri! leo ninajishangaa sina tena furaha ya kuongezeka umri kama zamani!
hii ni baada ya kubaini kuwa kwa kadiri umri wangu tangu kuzaliwa unavyoongezeka kama siku ya leo; kumbe muda wangu wa kuendelea kuishi duniani unapungua!

Jumatatu, 6 Juni 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA IBADA KANISA LA MAOMBEZI LA MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO ‘MZEE WA UPAKO’ UBUNGO KIBANGU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabara inayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside.

Ijumaa, 3 Juni 2016

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI LILIAN NAMAN NGOWI AJIPANGA KUWAFIKISHIA WENGI INJILI KWA NJIA YA UIMBAJI



Mwimbaji wa nyimbo za injili Liliana Naman Ngowi akiwa na kwaya uinjilisti Kijitonyama walipofanya Michigan Marekani.
Lilian ni wa pili kutoka kushoto

WALIOFICHA SUKARI ARDHI IWAKATAE-DKT. CHARLES GADI

Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Askofu wa Kanisa la Good News for All Ministry Dkt. Charles Gadi amewapa siku tatu walioficha sukari kuitoa na ikiwa watakaidi agizo hilo basi ardhi iwakatae.

Askofu Gadi ameyasema hayo  jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uhaba wa sukari nchini na maandalizi ya mkutano wa kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika jiji la Arusha.

Alhamisi, 2 Juni 2016

SEMINA YA NENO LA MUNGU MKOANI DODOMA: ZIJUE NJIA AMBAZO MUNGU ANATUMIA KUKUFANIKISHA.


Semina hiyo inaendelea kwa wiki nzima mkoani dodoma unaweza pia kufuatilia semina hiyo kupitia linki hii,blog ya amaninafuraha ukifungua mkono wako wa kulia utaona sehemu imeandikwa mwalimu Mwakasege unaweza kutazama moja kwa moja wanapoanza kurusha matangazo kutoka Viwanja huko Dodoma

Jumatano, 1 Juni 2016

WENGI WAFIKA NA KUFUNGULIWA NA KUWEKWA HURU MBALI NA MATESO NA MAGONJWA SUGU NA NGUVU ZA PEPO WACHAFU ZAWATOKA NA KUWAAACHIA WATU WALOFIKA KANISANI HAPO.

 Waumini waliofika katika kanisa la Jesus Save Fellowship lilopo maeneo ya Airport jijini Dar es salaam washiriki katika maombi wakongozwa na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Zakaria Oswad Lule hayupo kwenye picha.

SIKU 90 ZA MAPINDUZI NA MABADILIKO NDANI YA KANISA LA EAGT CITY CENTER WENGI WAPONA NA KUOKOLEWA KWA JINA LA YESU.

Mhungaji Kiongozi wa kanisa EAGT City Center mchungaji Florian Katunzi,
Siku tisini ndani ya kanisa la EAGT City Center yaleta mafanikio kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limeonekana baadhi ya waumini na watu mbalimbali ambao wamefika katika kanisa hilo awmeliambia gazeti la msema kweli kuwa wamefunguliwa katika vifungo mbalimbali ambzao zimekuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.

Jumanne, 31 Mei 2016

WAUTU WA DINI NA MADHEHEBU MBALIMBALI WAZIDI KUFUNGULIWA NDANI YA KANISA LA EAGT CITY CENTER ILIYOPO MTONI MTONGANI JIJININ DAR ES SALAAM,

Matukio katika picha yakionesha watu walivyokuwa wakifunguliwa katika jina la Yesu mtenda miujiza.
Mungu amekuwa akimtumia mtumishi wake mchungaji Florian Josephat Katunzi katika kuwafungua wengi waliofungwa na nguvu za giza mizimu na uchawi pamoja na usghhirikina na kuwaweka huru na wengi wameshuhudia kufunguliwa kwao bila kujali dini wala madhehebu yao.

wakati wa maombi na maombezi  mwanamama Faith ambaye alikuwa katika vifungo mbalimbali alifunguliwa na kutapika  coin.

MCHUNGAJI ZAKARIA OSWAD LULE AKIFUNDISHA NENO LA MUNGU

Ijumaa, 27 Mei 2016

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ANAONDOKA NCHINI KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANONI PAPUA NEW GUINEA:

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kwenda Papua New Guinea ambako atamwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (ACP) ambao utafanyika kuanzia Mei 30 hadi Juni 01, mwaka huu.

MTU MMOJA MKOANI MWANZA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU:

Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya
kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.

Na BMG
Tukio hilo limetokea hii na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Jumatatu, 16 Mei 2016

WALIOFUNGWA SASA WAWEKWA HURU NDANI YA KANISA LA EAGT CITY CENTER JIJINI DAR ES SALAAM:

 Huyu ndiye mama KIriri ambaye alisimama mbele ya kanisa la EAGT City Center na kushuhudia jinsi Mungu alivyomfungua katika mafungo ya pepo wachafu
 Hapa mama Kiriri akishuhudia akishika kipasa sauti

UMOJA WA WANAUME TAWI LA BUGURUNI WAUNGANA NA KUTOA ZAWADI KWA KANISA NA PIA KUSOMESHA MWANAFUNZI WA CHUO CHA BIBLIA:

Umoja wa wanaume CMF wakiwa katika picha ya pamoja na mchungaji wao kiongozi pamoja na mke wake na viongozi wa umoja huo,
Chama cha wanaume CMF kimefanya shughuli ya kujitolea na  kufanya usafi katika eneo la nyumba ya mchungaji pamoja na kusaidi kanisa kwa kununua viti vya kanisa ya watu wazima na vya watoto.
Akizungumza katika ufunguzi wa sherehe hizo mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Buguruni mchungaji amesema kuwa idara hiyo ya wazee imekuwa msaada mkubwa sana katika kanisa la mahali pamoja na kuomba kanisa la TAG taifa kusimamia nafasi hiyo kwa umakini maana imekuwa msaada kwa jamii.

CHAMA CHA WANAUME CMF TAG BUGURUNI WAJITOLEA KUFANYA USAFI NA UKARABATI KWA MCHUNGAJI WAO KIONGOZI SANJARI NA KUNUNUA VITI KWA KANISA:


Mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Buguruni akiwa na mke wake katika sherhr ya siku ya wanaume CMF inaadhimishwa kila mwaka katika makanisa ya TAG nchini.

Jumamosi, 23 Aprili 2016

UTAKASO NDIYO NJIA PEKEE YA KUMWOKOA MWANADAMU NA KUMWEKA MBALI NA DHAMBI NA MAGONJWA NA SHIDA MBALIMBALI -KWA MCHUNGAJI KATUNZI


Mchungaji Florian Katunzi akimwombea mwanamke ambaye alifunjika mkono na haikupona kwa muda mrefu alipoombewa alianguka na ikamlazimu kumwombe.

Mchungaji Katunzi akimwombe mwanamke aliyefika ibadani na mwanaye kupata maombi na maombei katika ibada maalum ya utakaso.

Alhamisi, 14 Aprili 2016

TAMKO KALI LA ASKOFU GWAJIMA KWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA.

  Tamko la  Askofu Gwajima kwa mkuu wa mkoa wa Arusha aliyekataza ibada za mikesha kwa madai kuwa wanapiga kelele.


Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Arusha amekanusha kauli hiyo na kusema kuwa hakukataza waumini kuabudu 

Jumatatu, 11 Aprili 2016

KANISA LA EAGT CITY CENTER LAJIPANGA KUWALETA WAUMINI ELFU 9 KWA YESU KATIKA KONGAMANO LA SIKI 90



 Mchungaji askofu Katunzi akifundisha neno la Mungu ndani ya kanisa

UZINDUZI WA ALBAMU YA HALELUYA WASTAHILI BWANA UMEPENDDEZA NDANI YA KANISA LA EAGT SINZA JIJINI DAR ES SALAAM.

Kwaya ya Bethlehemu iliyopo katika kanisa la EAGT Sinza linaongozwa na Askofu Dr Alphonce Mwanjala wamezindua rasmi albamu yao  inayojulikana kwa jina la haleluya wastahili Bwana.
Uzinduzi wa albamu ya kwaya hiyo imefanyika ndani ya kanisa la EAGT Sinza na kusindikizwa na kwaya ya majestic Singers kutoka EAGT Temeke,Temeke Revival  kwaya,Yes,Kwaya Next Level na Neema kwaya pamoja na waimbaji binafsi kama vile Joshua Makondeko na Afande Manoti.
 Mc Joshua makondeko akisherehesha katika uzinduzi wa Albamu ya  Kwaya ya Bethlehemu.