YESU NI JIBU

Jumanne, 26 Desemba 2017

KUZALIWA KWA YESU NI LEO AMA ILISHATABIRIWA KWA MIAKA YA NYUMA .

Waumini wa dini ya kikristo wameungana na waumini wengine duniani kusherehekea siku hiyo ambayo ni chanzo cha kalenda ya dunia.
Hii siku mara nyingi husherehekewa na waumini wa dini hiyo pamoja na wale ambao si wafuasi wa dini hiyo na imekuwa na mvuto mkubwa sana,
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu na wapo Radio baadhi ya wachungaji na maaskofu wamesema kuwa siku hiyo ni muhimu kusherhekewa kwa kumpokea Bwana  Yesu na kutii maagizo yake ambayo anaagiza kupitia neno lake,Aidha wengine wamesema kuwa baadhi ya watu hutumia siku hiyo vibaya.
Nimezungumza na mchugaji Joseph mwangomola la EAGT makongo juu ambapo amliema kuwa watu wengi hutumia siku hii vibaya kwa kufanya mambo ya anasa ambayo mwisho wa siku ni kumtenda Mungu dhambi.
kuzaliwa kwa Bwana yesu ni ishara ya mabadiliko na mageuzi ndani ya mioyo ya watu hasa wale wenye mrengo wa kutafuta MUNGU wa kweli na kuachana na mambo yale yasiompendeza.
Mchungaji Leornad Manyama wa TAG MABibo Sahara aalisema kuwa ni siku Muhimu sana katika maisha ya kila mwanadamu maana ndiyo chanzo cha kalenda inayotumiwa duniani,
Alisistiza kuwa wanadamu wanapokumbuka siku hiyo ni vyema kujitakasa na kutafuta kwa bidii kumpendeza Mungu katika maisha yao ya kila siku.
 Askofu Florian Katunzi Akisalimiana baadhi waumini
Na kwa upande wa askofu Florian Ktunzi wa EAGT City Center alisema kuwa hii ni siku ya Muhimu sana na ilitabiriwa na Isaya kutoka agano la kale mpaka agano jipya ilitabiriwa juu ya siku hiyo.

Jumatano, 6 Desemba 2017

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA JOEL BENDERA


Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia na wote walioguswa na kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr Joel Nkaya Bendera kilichotokea jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.