YESU NI JIBU

Ijumaa, 18 Novemba 2016

CITY HAVERSTY INTERNATIONAL CHURCH YAWASIMIKA VIONGOZI WANANE TAYARI KWA HUDUMA.

 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la City Haversty International Apostle Dr Livistone Banjagala wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati ajiandaa kuwasimika wachungaji wa kanisa lake.

 Mke wa mchungaji Dr Livingstone Banjagala mchungaji Jackline wakati akitoa maelekezo ndani ya kanisa la City Haversty International iliyopo Tabata Magengeni jijini Dar es salaam.
 Apostle Dr Livistone akihubiri kanisani na mtafsiri wake mchungaji Samwel Lukindo 

 Baadhi ya wachungaji waliosimikwa tayari kuanza kazi ya Mungu chini ya kanisa la City Haverst International Church 




 Apostle Dr Livistone Wakiwapaka mafuta watumishi aliowaweka wakfu tayari kwa huduma.
 Mchungaji Kanuni Kayombo wa Kanisa la city haversty International tawi lilopo kitunda  akiwa na mke wake mara baada ya kusimikwa tayari kwa huduma.

Watumishi wakiwa katika picha ya pamoja maara baada ya huduma kusimikwa kwisha.

Watumishi wa Mungu wametakiwa kuwa makini na kutumia karama walizopewa na Mungu kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu.
Kauli hiyo imetolewa na mchungaji kiongozi wa kanisa la City Haversty International Apostle Dr LIvistone Banjagala wakati akiwasimika watumishi nane tayari kuanza kumtumikia Mungu chini ya kanisa hilo.
Aidha Dr Banjagala alisema kuwa ni vyema kila mwamini kumzalia Mungu matunda katika nafasi yake aliyepo ambapo alisema vigezo vya kumzalia Mungu matunda ni kuwa na maono ya kufanya kazi.
"Kufanya kazi ya Mungu inaitaji bidii na kujitolea na kuacha kusikiliza maneno ya watu zaidi ya kudumu katika maombi na kusoma neno la Mungu,hapo utaweza kufanikiwa kumletea Mungu matunda",alisema mchungaji Banjagala.
Aliongeza kuwa kuna njia nyingine ambayo ni kuwa na upendo na watu woote haijalishi kuwa kunawatu wanakukwaza na kukukasirisha ukiwa kama mtumishi ni vyema kuwapenda na kuwa karibu nao bila kuhesabu makosa waliokukosea katika maisha yao.
Uwapende watu wote wala usikubali kuwa na makundi wakati unafanya huduma,maana utakaporuhusu makundi kuwa hawa ni watu maalum na hawa sio utaharibu na kautamzalia Mungu matunda.
Alisema pia inawezekana wengine wakajionesha kwako kama marafiki kumbe ni maadui ila wewe unatakiwa kuwapenda na kuwanao pamoja maana hata wengine wanaweza kukupa sumi ama kukunenea maneo magumu ambayo hata kuyabeba ama kusikiliza yanaumiza ila wewe mtumishi unatakiwa kuwapenda na kuwaombea.
Hatua nyingine ya kumzalia Mungu matunda ni kujiungamanisha na neema ya utumishi uliyoitiwa na kuwa nayo,hapa inamaanisha kuwa kujiungamanisha na mafuta ya mtumishi amabaye unakuwa chini yake.
Inawezekana ukawa na neema ya kusikilizwa na kupendwa sana na pia unaweza ukawa na kibali mbele za watu kutokana na neema ya kiongozi wa huduma unatumika nayo sasa ukijiondoa katika huduma hiyo kibali na neema nayo inatoweka maana ulikuwa ukitembea juu ya neema na kibali cha kiongozi wako wa huduma.
unaweza kuwasiliana na kanisa la C.H.I.C kwa namba 0784551492 na 0783325082

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni