YESU NI JIBU

Jumanne, 27 Januari 2015

CHANGAMOTO 10 ZA KUOA MWANAMKE ALIYEKUZIDI MIAKA MINGI.



Na mchungaji Peter Mitimingi,
Jamii nyingi za kiafrika huamini kwamba siku zote mwanamke ni lazima awe na miaka michache kuliko mume wake. 


Changamoto 10 za Mwanaume Kuoa Mwanamke Aliyemzidi Miaka Mingi:
i. Maneno ya kuvunja moyo kutoka kwa jamii.
Inapotokea mwanamke akawa na miaka mingi sana kuliko mumewe jamii huweza kuongea maneno ambayo wakati mwingine huwakosesha raha na amani.

Unapogundua watu kila ukipita wanakusema wewe na kukusema kwenyewe ni kukusema vibaya sio kukusema kwa mema hilo jambo huumiza sana moyo wa mtu na kumfanya kuamini kwamba kila wakati watu watakuwa wakimsema yeye hata wakati ambapo watu watakuwa wakiongelea mambo mengine yeye atajihisi tu kuwa wanamsema yeye.
Kadri miaka inavyozidi kwenda mmoja anaweza kuona vibaya kuongozana na mwenzake kutokana na hayo maneno ya watu wa nje kwamba hawaendani na kwamba ameoa mwanamke mzee au ameolewa na mwanaume mzee au wengine kumshambulia mwanamke kuwa ameolewa na mwanaume mdogo au mtoto hali hii huchangia kupunguza uhuru wa kimahusiano kati ya wanandoa hawa hasa mbele za jamii. Baadhi ya watu katika jamii wanaweza kuongea juu yao mambo ambayo yatawaumiza sana mioyo yao.
ii. Kukosa Uhuru wa kuwa na Mwenzi wako Hadharani.
Kutokana na maneno ya watu mitaani, kanisani, kazini na kwingineko mnaweza kukosa uhuru wa kuongazana pamoja au kumtambulisha kwa marafiki au inapotokea mmealikwa kwenye sherehe au hafla fulani unapata utata wa kuongozana kutokana na kuhofia kunyooshewa vidole na watu kwa kuwasema vibaya.

iii. Kupishana kwa mapendeleo na maslahi “Hobbies & Interests" Baina ya Wanandoa Hao
Moja ya changamoto inayowakabiri wanandoa ambao wamepishana umri wa miaka mingi ni kwamba mmoja atakuwa anaishi kwenye ulimwengu wa kiujana na mwingine atakuwa anaishi kwenye ulimwengu wa Kiutuuzima au ulimwengu wa uzee. Tatizo litakalotokea hapa kila mmoja anajaribu kumvuta mwenzake kwenye ulimwengu wake. Yule ambaye ni kijana atakuwa anajaribu kumvuta yule mtu mzima au mzee kwake kwa maana kwamba yeye kama kijana hataki kufanya mambo ya kizee anataka kwenda na wakati kwa kufanya mambo ya kiujana ujana. Wakati naye yule mzee atakuwa akimvuta kijana kwake kwamaana kwamba yeye kama mtu mzima au mzee hawezi kufanya mambo ya kitoto kwani hata watu wakisikia anafanya hivyo wataweza kumuuliza kwamba wewe mtu mzima bado unafanya mambo ya vijana!? Kwahiyo kutakuwa na vuta nikuvute ambayo itasababisha mmoja kuona kwamba huyu mtu naona haikuwa chaguo sahihi maana ananitesa badala ya kunifanya nifurahie maisha ya ndoa.

iv. Changamoto ya Kutoendana na Kuangalia Nje ya "Fance"
Kadri miaka itakavyozidi kwenda ile "gap" ya umri itakuwa ikijitokeza kwa ukubwa zaidi. Kijana ataanza kuona huyu mzee hatuendani namimi yupo nyuma ya wakati na kuanza kuvutiwa zaidi na mtu mwingine wa rika lake. Mfano kama kijana ameoa mwanamke ambaye wamepishana sana umri, kijana anaweza kutamani mkewe awe anavaa yale mavazi ya ujana ambayo huvaliwa na wasichana mitindo na mishono ya kiujana ili atakapokutana na marafiki zake waone kuwa ana mwanamke ambaye anakwenda na wakati. Kwa upande wake huyo mwanamke kulinganana umri wake hawezi kuthubutu kuvaa mavazi ya kiujana kama hayo na hapo mgogoro huweza kutokea na wote wawili kuona kuwa hawaendani kabisa.

v. Imani ya kwamba Ndoa ni Kwajili ya Kupata Watoto
Katika tamaduni na mazingira yetu ya Kiafrika, umri wa mwanamke anapoolewa ni wamsingi sana hasa linapokuja swala la kuzaa watoto. Kwa tamaduni za kiafrika swala la kuzaa watoto katika ndoa ni jambo la msingi sana kwa jamii nyingi za kiafrika. Kwahiyo mwanaume anapooa anakuwa na mategemeo kwa sehemu kubwa kwamba atapata watoto kupitia mke ambaye anamuoa.

vi. Jamii Huamini kwamba Mwanamke Mwenye Umri Mkubwa Atashindwa Kuzaa.
Jamii nyingi huamini kwamba kuoa mwanamke mwenye umri mkubwa anaweza kushindwa kumzalia watoto mumewe.
Kulingaana na watafiti wanasema kwamba kadri mwanamke anavyoziku kuongezeka umri ndivyo ambavyo viungo vyake vya uzazi hupoteza uwezo wake wa kushika mimba na kuzaa watoto.

vii. Kiwango Muafaka cha Kupishana Umri Kati ya Mwanamke na Mwanaume.
Kwa Mwanaume:
Inashauriwa kwamba kwa mwanaume miaka 5 hadi 10 inafaa kupishana kati ya mwanaume na mwanamke anayetarajia kumuoa. Kwamaana ya kwamba mwanaume anaweza kuoa mwanamke ambaye yeye mwanaume anakuwa amemzidi huyo mwanamke miaka miwili, mitano hadi 10.

Kwa Mwanamke:
viii. Inashauriwa pia kwa mwanamke kuzidi miaka miwili hadi 5 kwa mwanaume anayetarajia kuolewa naye.

Hii inamaanisha kwamba mwanamke akimzidi mchumba wake au mume wake miaka miwili hadi mitano itakuwa ni sawa hakutakuwa na tofauti kubwa sana wala madhara makubwa.
ix. Kuna Athari kwa wanandoa wakipishaza zaidi ya miaka 10.
Wanandoa wanapokuwa wamepishana kwa zaidi ya miaka 10 kunakuwa na utafauti mkubwa katika kuhusiana kwao kama jinsi tulivyoelezea hapo juu.

x. Ushauri kwa Wachumba Waliopishana Umri Mkubwa
Wachumba ambao wana tofauti kubwa ya umri wao, wanashauriwa kutafuta ushauri kwa washauri wazuri (good counselors) kabla ya kuoana.

Hata hivyo bado Mungu ni wa neema na miujiza anaweza akatenda hata kwa mwanamke au mwanaume mwenye umri mkubwa kuliko mwenzake hata kama ameshapitisha muda wa kuzaa au na mambo mengine Bwana bado hashindwi.
Luka 1:37
Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

Wafilipi 4:13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
ANDIKA JAMBO MOJA LILILOKUGUSA KATIKA SOMO HILI!

TANGAZO LA MKUTANO WA INJILI MABIBO SAHARA SPIRITUAL CENTER JIJINI DAR ES SALAAM:

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG Sahara Spiritual Centre la Mabibo jijini Dar es Salaam, Askofu Geofrey Masawe, anakualika katika mkutano mkubwa wa Injili wa siku tano utakaofanyika katikika viwanga vya kanisa hilo.
Siku ni kuanzia tarehe 28 mwezi wa kwanza hadi tarehe 1 mwezi wa pili mwaka huu.
Wahubiri katika mkutano huo ni Mwinjililisti wa TAG Taifa, Mchungaji Tumaini Chanjarika na Mchungaji Mwenyeji Askofu Geofrey Massawe
Kwaya mbalimbali zitahudumu katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na kwaya ya Shekina ya kanisa hilo
Walete wagonjwa na watu wenye mahitaji mbalimbali wataombewa na kufunguliwa kwa jina kuu la Yesu
Wote mnakaribiswa
Kwa mawasiliano piga namba: 0715304493/ 0754273768

Alhamisi, 22 Januari 2015

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA KIKWETE AKIONGOZA MKUTANO WA KUTILIA SAINI MAKUBALIANO KATI YA RAIS SALVA MAYARDIT KIIR NA MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA SUDANI YA KUSINI DKT RIEK MACHAR,



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie  leo Jumatano Januray 21, 2015 kabla  ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal,, Naibu Rais wa Afrika Kusini,  Mhe Cyril Ramaphosa, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Kikwete, Rais Salva Mayardit Kiir, wa Sudani ya Kusini, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Makamu wa Rais wa Zamani wa Sudani ya Kusini Dkt Riek Machar,  
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya leo Jumatano Januray 21, 2015 kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.  
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Yoweri Museveni  leo Jumatano Januray 21, 2015 kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na viongozi wenzie  leo Jumatano
Januray 21, 2015 kuelekea kwenye chumba cha mkutano kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini

katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Makamu wa
Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal,, Naibu Rais wa Afrika Kusini,  Mhe
Cyril Ramaphosa, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Kikwete, Rais
Salva Mayardit Kiir, wa Sudani ya Kusini, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
na Makamu wa Rais wa Zamani wa Sudani ya Kusini Dkt Riek Machar,
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mjane wa Mwenyekiti wa Zamani wa SPLMMama Rebecca Nyandeng Garang de Mabior leo Jumatano Januray 21, 2015 kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Source ni BBC na fullshangwe blog,
Makundi yanayopingana nchini Sudan Kusini yamekusanyika nchini Tanzania kusaka jitihada mpya za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusababisha maelfu ya watu kuuawa.
Serikali ya Tanzania ambayo inasimamia mazungumzo ya Arusha kupitia chama tawala cha CCM nchini humo, imesema Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na aliyekuwa naibu wake na sasa kuwa kiongozi wa waasi nchini humo Riek Machar walikutana Jumatano na kutiliana saini mkataba mpya wa amani.
Pande mbili hizo zilitiliana saini mkataba unaolenga kukiunganisha chama tawala cha the Sudan People's Liberation Movement (SPLM), ili kumaliza uhasama uliojitokeza miongoni mwa viongozi wa chama hicho kilichopigania uhuru wa Sudan Kusini miaka mitatu iliyopita.
Vita vilizuka nchini Sudan Kusini, taifa changa kuliko yote duniani, mwezi Desemba 2013 wakati Kiir alipomshutumu naibu aliyemfukuza Machar kwa jaribio la kumpindua.
Mara ya mwisho Kiir na Machar walikutana mwezi Novemba, 2014 mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako walikubaliana kusitisha haraka vita, mkataba uliovunjwa katika muda wa saa chahche tangu wakubaliane.
Mapigano katika mji mkuu wa Juba yamesababisha mauaji ya kulipiza kisasi nchini humo na kuisukuma nchi kuingia katika kipindi cha njaa.
Shughuli za kutiliana saini mkataba wa amani kati ya Rais Kiir na Bwana Machar zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kikanda kushuhudia mkataba wa umoja kw makundi tofauti ya chama tawala cha SPLM.
Mazungumzo ya Tanzania yanafanyika sambamba na juhudi za kuleta amani zilizokuwa zikisimamiwa na nchi za IGAD mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Awamu nyingine ya mazungumzo ya IGAD yanatarajiwa kufanyika kando ya kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa mwishoni mwa Januari.
Lakini vita vinaendelea.
Wiki hii msemaji wa jeshi Philip Aguer amesema jeshi na waasi wamekuwa na mapigano makali katika jimbo la Central Lakes, na ameshutumu majeshi ya Machar kwa kulipua kisima cha mafuta katika jimbo la Unity.
"Majeshi ya Machar yamekuwa yakisababisha uharibifu, uchomaji wa vijiji, uharibifu wa visima vya mafuta," amesema.
Ni mara ya kwanza waasi mahasimu hao kukutana tangu waliposaini makubaliano ya kuacha mapigano mwezi Agosti huko Ethiopia, ambayo kama mikataba mitatu iliyopita ilivunjika mara moja.
Viongozi hao wa siasa na kijeshi wamekuwa wakirudia rudia kuvunja ahadi wanazotoa chini ya msukumo wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Sudani ya Kusini uliofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Waziri Mkuu wa Marekani John Kerry.
Safari hii viongozi hao wawili wa Sudani ya Kusini walisema chama tawala kilichogawanyika, Sudan People's Liberation Movement (SPLM), inapaswa kuungana upya. Chama cha SPLM kiliiletea nchi uhuru baada ya vita vya muda mrefu na Khartoum.
"Chama kilichogawanyika cha SPLM kitaigawa nchi katika makundi ya kikabila na maeneo," makubaliano hayo yalieleza, kutoa wito kwa "mazungumzo ya halali na ya uaminifu ambayo yanaweka matakwa ya watu na taifa juu ya wote".
Kiir alitoa ahadi ya "utatuzi kwa amani wa mgogoro" katika nchi iliyokuwa maskini wakati ina utajiri wa mafuta, ambayo ina miaka mitatu lakini iliyokumbwa na vita.
"Hakuna sababu kwa watu wetu kupata shida tena baada ya uhuru," alisema. Machar pia alisema alitaka jambo hilo kumalizika.
"Hatutaki fursa hii kutoweka kama fursa nyingine za awali," alisema. "Tutafanya kwa uwezo wetu wote kuona kuwa mchakato huu unamalizika"
Kikundi cha tatu kilichojitenga katika SPLM -- viongozi wa ngazi ya juu walifungwa kwa miezi kadhaa baada ya vita kuibuka mwezi Desemba, lakini pia walisaini suala hilo la kuunganisha chama.

Jumanne, 20 Januari 2015

WAZIRI AWANGUKIA WANAFUNZI KWA KOSA LA KURUSHIWA MABOMU YA MACHOZI:


Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaisery 
Waziri wa usalama nchini Kenya Joseph Nkaissery amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi wakati walipokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa kipande cha ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa kuchezea.
Bwana Nkaissery amempa mnyakuzi wa ardhi hio siku moja kuondoa sehemu ya ukuta iliobaki baada ya wanafunzi kuuangusha na kisha kuondoka katika eneo hilo.
Nkaisery ameongeza kwamba serikali itaweka uzio katika ardhi hio na kuiwacha kuwa uwanja wa kuchezea wa wanafunzi hao.
Wakati huohuo, amewaonya wanaharakati dhidi ya kukiuka sheria kila wakati wanapojiandaa kufanya maandamano badala ya kuchukua sheria mikononi mwao.
Wanafunzi waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi kwa kuandamana kupinga unyakuzi wa uwanja wao 
Mnamo Jumatatu, wanafunzi watano na polisi mmoja walijeruhiwa katika vurugzu zilizotokea baada ya wanafunzi kuandamana kupinga unyakuzi wa ardhi yao kutoka kwa mtu aliyekuwa na mipango ya kufanya ujenzi.
Wakenya wamekosoa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wanafunzi , hali ambayo imesababisha afisa ammoja mkuu kusimamishwa kazi kwa mda.
Shirika la kutetea masilahi ya watoto, la Save The Children, pia limelaani kitendo cha polisi dhidi ya wanafunzi hao ambao walikuwa wanaandamana kwa amani kutetea uwanja wao uliokuwa umenyakuliwa.
 Source BBC