YESU NI JIBU

Ijumaa, 18 Novemba 2016

KUWA NA MTAZAMO SAHIHI KWA MUNGU WAKO NAWE UTAMTUMIKIA KWA UAMINIFU:


 Mchungaji kiongozi na pia ni askofu Geoffrey Masawe akifanya maombi madhabahuni.
 
 kutoka kushoto ni mchungaji Olivia Masawe katikati mwenye kipasa sauti ni mchungaji Blanka na mchungaji Leonard Manyama wakiombea cd ya mwimbaji ambaye ni mshirika wa kanisa hilo.


Askofu Masawe akimwombea mwimbaji binafsi chipukizi.




Ni ukweli usiopingika kuwa mwanadamu anapokuwa na mtazamo uwe hasi ama chanya hawezi kuondolewa kwenye mtazamo huo hadi hapo atakapotambua.
Mtazamo ni nini?Ni hali ya ndani ya mtu inayosema juu ya msimamo aliyonayo juu ya mtu fulani ama hali fulani.Hivyo mtazamo aliyonayo mtu unaweza kuwa sahihi ama sio sahihi.
Hii imeelezwa na mchungaji Leonard Manyama wakati akifundisha neno la Mungu ndani ya kanisa la TAG Mabibo Sahara spiritual Center lilopo Dar es salaam chini ya askofu Geoffrey Masawe ambapo amesema kuwa mtazamo wa mtu juu ya Mungu unatakiwa uwe sahihi.
Aidha aliongeza kuwa mtazamo humpelekea mtu kutenda,kuamuana kushauri kwa usahihi katika maisha yake.
Akitolea mfano kwa Mwanafunzi mchungaji Manyama alisema kuwa yeyote akiwa na mtazamo tofauti hata mwalimu vanapoingia anatamani kutoka na hakuna mafanikio juu ya somo hilo analofundisha mwalimu.
Ufahamu na uelewa mtazamo unaweza kuharibu na kubomoa uhusiano kati ya mtu na mtu.
Taarifa tunazopokea kama sio sahihi.
Mtazamo usio sahihi huvuruga uhusiano wako na Mungu,na kwa mwanadamu mwenzako.
Shetani anatafuta njia ya kuvuruga mtazamo kati ya mume na mke na kusababisha ndoa kuvurugika.
Ni hatari sana kukaa na watu ama kuwaongoza watu ambao hujui mtazamo wao ni nini 
hasa.na itakuwa vigumu kuwaongoza.
Ukiwa na mtazamo sahihi unatembea katika njia sahihi
Jambo la 1,Mungu anatupenda sana kama kitabu cha Yohana 3:16 inavyosema
 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 
Mungu anauwezo wa kutuhamisha katika mapito tunayopitia

Waebrania 4:14-16
Yermia 9:23-24
Jambo la pili Mungu wetu ni wa rehema, katika maisha ya kila mwanadamu ni vyema atambue kuwa Munu ni wa Rehema.
Mungu anawawazia yaliyomema,Mungu wa rehema ni mhukumu wa yote.

Jambo la tatu Mungu anaheshimu maamuzi yake
Wafilipi4:11-13  
Mathayo 16:13-18.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni