YESU NI JIBU

Ijumaa, 31 Julai 2015

UNAIKUMBUKA HII BARUA YA BISHOP KAKOBE KWENDA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE.

Wakati hali ya sintofahamu katika duru za siasa na kile kinachoonekana kama hakikutarajiwa kwa chama tawala kuonekana kama kumeguka kutokana na baadhi ya watu wenye ushawishi kukihama akiwemo alikua waziri mkuu Edward Lowasa na kuleta mpasuko mpasuko mkubwa, Ikumbukwe kua jambo hili si bahati mbaya au ghafla kama wengi wetu tunavyodhani au tunavyoona.
Ikumbukwe kua tarehe 10 machi 2014 Askofu mkuu wa kanisa la FGBF Zachary Kakobe alimuandikia barua ya wazi Rais wa Tz mh Jakaya Kikwete iliyokua na kichwa cha habari…

UJUMBE WA WAZI WA MUNGU KWAKO NA KWA UMMA WOTE WA TANZANIA.
Swala/chanzo kilichompelekea Askofu mkuu Zachary kakobe kuandika ujumbe huu mzito ni baada ya serikali ya chama cha mapinduzi kutupa kapuni majina ya wapentecoste waliopendekezwa kua wawalikishi katika bunge la katiba, Hivyo kufanya taasisi hii kubwa ya kipentecoste yenye waumini mamilioni hapa Tanzania kukosa hata mtu mmoja wa kuwawakilisha hali ya kua hata waganga wa kienyeji walipata wawakilishi.Binafsi ninajiridhisha kua hilo ni moja tu kati ya maovu/upuuziaji ambao umekua ukifanywa kwasababu wameamini wanauwezo wa kufanya lolote wanalojisikia kwa maslahi binafsi na chama chao…..Ninaamini askofu Zachary Kakobe angesema aorodheshe mambo yote katika ile barua kingegeuka kua kitabu na si barua tena.
Sisemi haya kwasababu ni CCM wamefanya la hasha…waraka huu si wa mlengo wa kisiasa au wa kukitetea/kukiumiza chama chochote…..Lengo langu ni kuuweka ukweli wazi na ieleweke kwamba haya ni mavuno ya mbegu iliyopandwa
MUHIMU:
Katika barua ile ya Askofu mkuu mzee wetu Zachary Kakobe ulikua ni waraka wa Mungu alioupata baada ya kuingia katika maombi ya muda kadhaa baada ya swala lile kutokea 
katika barua ile ujumbe hasa ambao ulikua ndio muhimu kwa Rais na chama chake pamoja na umma mzima wa Tanzania uliandikwa kwa maandishi ya rangi tofauti ili kuupa uzito na umakini ulioustahili,ujumbe huo ulikua kama ifuatavyo…
NANUKUU:
Chama unachokiongoza kimekua kikifurahia umoja na mshikamano kwa miaka mingi,Hata hivyo katika miaka ya hivi katibuni umoja na mshikamano huo umechukua sura mpya na kua umoja wenye malengo mabaya kinyume changu .
Kama umoja ule wa watu wa kale waliojenga mji na manara wa babeli kinyume changu na hivyo wakanifanya kuwachafulia usemi wao ili wasisikilizane wao kwa wao na nikawatawanya usonivpa nchi yote wakiwa makundi tofauti tofauti. Vivyo hivyo chama chakokimeiongoza serikali unayoiongoza kufanya mambo mengi yaliyo kinyume nami na kudharau wingi wa wema wangu kwenu na uvumilivu wangu msijue kua wema wangu kwenu umekua na lengo la kuwavuta mpate kutubu.Kwa kadri ya ugumu wa mioyo yenu isiyo na toba sasa mmejiletea hukumu (Warumi 2:4-6)
Sasa ninawachafulia usemi watu wote katika chama chako, kwenye nafasi mbali mbali za uongozi ili msisikilizane ninyi kwa ninyi kuanzia sasa katika vikao vyenu mtafarakana na kutokusikilizana.Mafarakano hayo yatadhihirika hatua kwa hatua na kuongezeka viwango tofauti tofauti na yatafikia kilele chake mwaka kesho 2015 ambapo kutakua na mafarakano makumbwa ambayo hayajawahi kutokea tangu chama chenu kipate kuwapo.
Nguvu za dola,nguvu za miungu ambazo baadhi yenu mnazitegemea,nguvu za fedha,hekima ya kibinadamu; Vyote hivyo havitaweza kuzuia mafarakano hayo.Kwa tendo hili mtajua kua alie juu ndie anaemiliki katika ufalme wa wanadamu na humpa amtakae awae yote; na wale waenendao kwa kutakabari yeye huwadhiili.”
Katika barua ile ambayo naweza kuiita ya kinabii iliambatana na mambo muhimu matatu(3)
1:Ujumbe wa wazi kuelezea tatizo
2:Madhara ya tatizo/uovu ambao umekua ukifanywa
3:Jinsi gani watazuia madhahara yasitokee(TOBA)
Hayo ni mambo muhimu sana ambayo askofu Mkuu Zachary Kakobe aliyaorodhesha katika waraka ule.
Swala la toba ya kweli juu ya chama hicho na viongozi wake ndio ilikua njia pekee ya kuzuia haya tunayoyaona leo yasiyokee…!Lakini kwasabau walipuuuza kama ambavyo wamekua wakifanya basi si ajabu kuona haya leo yanatokea, na pengine yapo mengine makubwa zaidi ya haya yanakuja.
WAZO KUU LA MWANDISHI WA MAKALA HII (WAZO LANGU)
Kumekua na mitazamo na hisia tofauti sana juu ya haya yanayotokea hivi sasa katika nchi hii…..lakini barua hii ya ya Askofu Kakobe ni kama watu hawaioni hivi…..ninachokifahamu angesema kitu ambacho hakijatokea mitandao yote ya kijamii zingejaa habari zake na watu kusema kila mtu kwa namna anavyojisikia kusema.
Lakini kwa swala hili ukiliangalia kiimani ninapata jibu la moja kwa moja kwamba Mungu yuko kazini na taifa la hili…! Sisemi haya eti kwasababu lowasa kajiunga na ukawa au kwa sababu ya hali ya kisiasa inavyokwenda …La hashaaa!
Ila kiuhalisia mambo yaliyokua yameshindikana kwa muda wa zaidi ya miaka 50 leo kuwezekana kirahisi ndani ya sekunde kadhaa….Kwa mtu mwenye jicho la imani ni lazima tujue kwamba Mungu analiandaa taifa hili na majira mapya.
Kwa namna yeyoye ile ambayo itatokea au kwa mtu yeyote atakaye tumiwa ilikua ni lazima neno la Mungu litimie na limekwiaha kutimia hata sasa…
WITO WANGU KWA KANISA LA TANZANIA
Kama kuna wakati kanisa linatakiwa kua makini sana ni huu,Nyakati kama hizi ambazo mambo yanayofanyika katika ulimwengu wa roho yanaanza kujidhihirisha kwenye macho ya nyama ni wakati muhimu sana kwa kanisa kuingia magotini na kuomba kuliko kuanza kusimama na wanasiasa fulani eti kwasababu kuna muelekeo fulani unaonekana.
Kama Mungu ameweza kufanya haya yanayoonekana leo kutokea basi pia ni vizuri kujua anauwezo pia wa kuugeuza hata huo upepo tunaouhisi kua ni sahihi kuelekea mahali pengine kama jinsi alivyoufanya moyo wa farao kua mgumu.
Ninaomba niseme kwamba hali ilipofika sasa si nzuri hata kidogo na hatima ya nchi hii ipo mikononi mwa kanisa.Tuna muda mchache sana wa kukaa magotini na kumsihi Mungu juu ya hili taifa ila cha ajabu hata kanisa nalo wanaendeshwa na upepo.
Unaweza ukafurahia au usifurahie ukweli huu ila kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa hakika wakati wa uchaguzi lolote linaweza kutokea hasa kama kanisa litasahau kusimama katika nafasi yake na kuendelea kufuata upepo huu
Kama amani inatengenezwa basi na vita hutengenezwa pia.
Mambo yalipofika hapa ni dhahiri hii si akili wa kibinadamu inayoamua, Haya ni maamuzi ya ulimwengu usioonekana (VITA YA ROHONI HUPIGANWA ROHONI)
Nalisihi kanisa la Mungu
1:Jiandikisheni kwa wingi
2:Tunzeni vitambulisho vya mpiga kura
3:Turudini magotini tukakimalize tilichokianza
SHALOOM SHALOOM SHALOM
NA IWE SHWARI KUU JUU YA TANZANIA

UNGANA NA MTUMISHI WA MUNGU PETER LUKUTA KATKA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUMALIZA MAOMBI YA SIKU 120 ZA KUIOMBEA TANZANIA

Nina mengi ya kusema lakini nasema machache tu Kwa wale wale wafwatiliaji waaminifu wa Post zangu bila shaka watakumbuka vuzuri kwa habari ya yale ambayo Mungu alisema nami kuhusu Tanzania na nikaweka Share humu fb lakini wengi walinipinga sana hata baadhi ya watumishi wakapinga sana wakakejeli wengine wakasema Kuwa natafuta umaarufu ijapokuwa pia kutafuta umaarufu si jambo baya maana Mungu aliahidi kuyakuuza majina ya watu wake na maandiko yananiambia habari Yesu zilienea kwenye miji yote ya kando kando si hilo tu bali Yesu ametutuma tuhubiri Ulimwenguni kote hii inamaana Ulimwengu woote umtambue yeye kupitia sisi hivyo umaarufu ni mapango wa Mungu kabisa acha watumishi wawe maarufu kusudi injili iendelee hamkumbuki hata yale pepo alisema Paulo tunamjua na Yesu tunamfamu hii inamaana watumishi ni maarufu kuzimu inawatambua. Ok tuyaache hayo tuendelee na kusudi la ujumbe wangu
Baada ya watu kupinga yale ambayo Mungu alisema nami hatimaye miezi michache baadaye yakaanza kuonekana kwa kishindo na yalipoonekana wazi kabisa ndipo Mungu akaniambia tena Kuwa niwakumbushe watu kuwa Mungu alisema mkapinga sasa yanatokeae. Kwa kweli wale wapinzani sikuwaona tena kwenye Post ya pili sijui walijificha wapi. Na mara hii ya pili Mungu aliagiza tufanyeje mfungo wa siku 120 ambao tulianza Tarehe 1March hadi na kuhitimisha Tarehe 28 July kwa kweli maombi haya yamekuwa na mwitikio mzuri na mpenyo mzuri na hata huduma zote nalizozifanya mikoa ambayo nimetembelea yote nalifanya nikawa kwenye mfungo huu na hata siku ya Arusi yetu mimi na mke wangu Vailethy Peter ilinikuta kwenye mfungo na nikawa mwaminifu hadi jioni ndipo nikala kwenye sherehe.
SHUKRANI ZA PEKEE
Kwanza kwa Mungu na pili kwao wote ambao wamekuwa waaminifu watumishi wa Mungu ambao tumekuwa pamoja siku zote kwenye Group letu la WhatsApp la MFUNGO WA SIKU 120 nawapongeza watanzania wote kutoka nchi mbali mbali duniani ambao mliitikia mwito huu na kweli mlitutia moyo sana pia wachungaji ambao mliitisha maombi haya kwenye makanisa yenu najua si kwa uwezo wala nguvu bali ni kwa Roho wa Mungu tu baada ya siku zote hizi sasa natangaza ramsi kwamba Mfungo huo umekwisha

Sasa lile Group letu la WhatsApp la Maombi haya litageuka kuwa Group la maombi na ukombozi wa watu wa Mungu
Lakini hii isiwe mwisho wa kufunga bali kufunga na kuomba kuwe ni destuli yenu kama ilivyo kwangu tutaeendelea na harakati zetu za uamsho wa kanisa la Tanzania
Yapo mengi ya kufahamu juu ya hili bali kwa leo naomba kuishia hapa pia karibu kwenye Group zetu mimi na mke wangu MLIMA WA UAMSHO kwenye telegram na FUNGUO ZA UFALME pamoja na KISIMA CHA UTAKASO ukitaka tukuunganishe kwenye Group hizi Tutumieni Masage Kwenye WhatsApp No 0767 503054 na Telegram  0767 503054 tutakuunganisha.
SIMAMA KISHUJAA AMINI UNAWEZA FANYA UTASHINDA


Jumatano, 29 Julai 2015

"NI SAA YA USHINDI NA KUFUNGULIWA UNGANA NA MCHUNGAJI KATUNZI KATIKA KUENEZA INJILI KWA SADAKA YA INJILI”

·      Kanuni ya Mungu ni kupanda na kuvuna
            (Isaya 6:8)
 Katika mfululizo wa makala haya, tumekuwa tukijifunza umuhimu wa kujitolea muda wetu, mali zetu na akili zetu kumtumikia Mungu kama alivyotuagiza katika Neno lake. Leo Mtumishi wa Mungu, Mchungaji Florian Josephat Katunzi, anaeleza  kwa kina umuhimu wa kila aliyeokolewa kuamka na kwenda kumuokoa mwingine anayeangamia dhambini, kuzimu ikipanua mdomo kumdaka. Tafadhali ungana na Yonathan Landa katika makala haya...
Jukwaa ambalo mtumishi wa Mungu mch.Florian Josephat Katunzi analihitaji kwa ajili ya kazi ya MUNGU ya kueneza injili kwa watu wote.
Yapo maswali makuu anayouliza Bwana kwetu sisi tunaolicha jina lake. Maswali yenyewe ni haya; 1. Nimtume nani? Hapa Muumba wetu, akiisha kutuokoa kwa damu yake ya thamani atutaka tusikae chini na kufikiri tumefika. Laa anataka mtu wa kumtuma kuwaendea wale wengine ambvao bado wanamtumikia shetani.
Ni hapa swali libngine linapokuja kwetu, Je ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu. Bwana anamtafuata mtu atakayemtuma kumletea wanakondoo wengine waliopotea. Anawahitaji zizini mwake.
Inatupasa hapa kukumbuka kuwa mtu huyu hatakwenda kwa niaba yuetu tu, bali atakwenda kwa ajili yetu. Mpango  wa injili wa miaka 20 unahitaji Mtu atakayekwenda  kuhubiri habari njema za ufalme wa Mungu, mtu huyu lazima aenda kwa niaba yetu. Hivyo basi, unaposhiriki kwa sadaka yako maana yake ni kuwa umemtuma mhubiri aende shambani mwa bwana kwa niaba yako na watoto wako.

Mimi nilipoupokea mpango huu nilikubalia kwenda kwa ajili yanu  kuhubiri pamoja nanyi katika mpango huu  wa miaka 20 ya safari ndefu za kuwakoa wale ambao bado hawajaokolewa ndabni na nje ya nchi yetu.

Mtumishi wa Mungu , Musaa alipokuwa kwenye misheni ya kuiokoa wana wa Israeli kutoka utumwani Misiri aliulizwa na Farao (mtawala wa Misri) “Utaenda na akina nani huko Jangwani kumtumikia huyo Mungu wako?”

Majibu ya maswali haya yanapatikana katika Biblia kitabu cha Kutoka 10:9, jibu lenyewe ni hili:
“Musa akamjibu; tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda nma kondoo zetu na ng’ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia Bwana siku kuu.”
Katika mpango huu wa wokovu inatupasa kumtumikia Mungu sisi na watoto wetu, tutakwenda na mali zetu (sadaka zetu). Malizetu lazima zitumike katika kazi ya Injili, tupate vyombo, gari na Jenereta. 
Ni muhimu sana watoto wetu wawe sehemu ya huduma, vijana wako wawe sehemu ya huduma ili kwa sadaka zako tuwe alama ya ukumbusho katika Ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Leteni sadaka hizi, imje mbele zake katika utukufu  ili sifa zimuendee yeye, kama maandiko matakatifu katika zaburi  yasemavyo: “Mpeni Bwana utukufu wa jina lake, leteni sadaka mkazingie nyua zake.”
(Zaburi 96:8)
Sdaka yako ni kiunganishi na Mungu aliye hai kwa kuwa kupitia utoaji Yeye huuona unyofu wako kwake. Neno la Mungu linasema: “Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.” (Mithali 3:10). Sadaka yako ya Injili itakuondolea msiba  usiwe katika nyumba yako na raha siku ya mapito yako uwe na kitu cha kumkumbusha Mungu aliye hai jkama alivyofanya  Ezekia.
“Siku hizo Ezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa, na Isaya mwana wa aAmuzi, akaenda kwa Mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, tengeneza mambo ya nymba yako; maana utakufa, wala hutapona . basi Ezekia akajigeuiza akaelekeza uso wake ukutani akaomba Bwana, akasema, eeBwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyomema machiini kwako. Ezekia akalia san asana. Ikawa neno la Bwana likamjia Isaya, kusema, enenda ukamwambie Ezekia, Bwana , Myungu wa daudi, baba yako, asema hivi, mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka 15.” (Isaya 38:16).
Nakaribisha marafiki wa Injili tushirikiane ili kutimiza mpango huu ambao si wa kidhehebu wala haufungwi na kundi lolote; tunaalika watu 200 watakaojitoa kwa sadaka ya shilingi 1,000,000, kwa ajili ya maandalizi haya ya ununuzi wa vifaa vya Injili, watu 200 watakaojidhabihu kwa sadaka ya shilingi 500,000. Lakini pia tunawaalika wengine kuungana nasi kwa njia ya utoaji wa sadaka zao ili kukamilisha mpango huu mkubwa unaolenga kufika kila kijiji cha Tanzania kukabiliana na giza hili la kiroho.

Aina ya magari ambayo ndiyo yanahitajikwa kwa ajili ya kueneza injili kwa kusafirishia vyombo na jukwaa.
Mimi pamoja na wewe uliyepokea neema hii ya Injili hatuwezi kutulia wakati shetani akihubiri hadharani na kuchukua watoto wetu kila dakika wakijiunga na ibada za kishetani kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka haraka.
Nawaomba wana-injili watuunge mkono katika mpango huu mkubwa na maono haya, yenye lengo la kuwafikia wenzetu kokote waliko, ili tuweze kununua vyombo hivyo, jukwaa na gari kwa ajili ya safari za injili nchi nzima.
Unaweza kushirikiana nasi katika mpango huu wa ki-Mungu kwa kuchangia kupitia akaunti zetu zifuatazo:
Jina la Akaunti: Florian Josephat Katunzi
Benki: CRDB no. 01j1028426200
M-Pesa - 0754367826
Tigo Pesa: 0718-267171
Airtel money: 0784-367826
UKITAKA KUWASILIANA NASI WANABLOG HII WHATSAPP NI 0752834514.

Jumanne, 28 Julai 2015

UJUMBE MAALUM KWA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI DINI,DHEHEMU WALA KABILA NA RANGI WATUMISHI WANENA KATIKA STUDIO ZA WAPO REDIO.

ASKOFU SYLVESTER GAMANYWA,
Nafasi ya kanisa la Tanzania katika changamoto zinazolikabili taifa ambazo ni ya changamoto za kiuchumi,kijaami na kisiasa.

askofu mkuu wa WAPO Mission Internatinal Slyvester Gamanywa akizungumza katika studio za TIT Dar es salaam.
Kanisa la Tanzania nafasi yake ni ipi na mchango wake ni ulipi hizo ndiyo agenda na kuanzia tarehe 31 Ijumaa  na 1 jumamosi ukumbi wa mwalimu julias kambarere
Aidha askofu Gamanywa alisema kuwa maaskofu,wachungaji,mitume,manabii wanaalikwa kuhudhuria na wacha Mungu ambao wana taaluma mbalimbali ambao zitasaidia kanisa kusimama katika nafasi yake.
Aliongeza kuwa Roho mtakatifu anazungumza na watumishi wa Mungu katika nafasi mbalimbali na katika jumbe mbalimbali ambazo yeye anataka taifa lisikie.
Na Katika mkutano huo watumishi watapitia jumbe mbalimbali ambazo zilitolewa na watumishi mbalimbali na kinachotakiwa ni kutubu tu na kugeuka na kufanya kile ambacho Mungu yeye anataka maana
yeye sio wa malumbano wala sio maandamano.
Hata hivyo alisema kuwa Kadi kwa wale ambao watahudhuria katika kongamano hilo zimekabidhiwa kwa viongozi wa kanisa na madhehebu mbalimbali na pia mtu .
Kiashirio cha kutoweka kwa amani katika taifa la Tanzania vimeanza kuonekana na kiukweli hakuna amani kuna utulivu ndani ya nchi.
Hata hivyo askofu Gamanywa hakuchelea kuelezea nini kinachosababisha haya yote ambapo alisema kuna watu wanaonufaika na mazingira ya vita na fujo zinazotokea na wao wanaochangia na wapo ndani na nje ya nchi.

 Alisema pia vita vya kiraia na jeshi usiombe, nchii kuingia mikononi mwa jeshi sio jambo la kuliombea,na haya nasema sio kwa lengo la kuwatisha wananchi hapana nafahamu maana wakati wa vita vya Uganda na Tanzania limepigana nafahamu sana tu madhara ya vita. 
ASKOFU DEO LUBAMA AKIWA KATIKA STUDIO ZA TIT MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM.
Katika miaka ya hivi karibuni Mungu amekuwa akizungumza mambo mengi kuhusu kanisa na Taifa la Tanzania.
kuanzia Mwaka 2002 Mungu alizungumza na watumishi kuwa maaskofu,wachungaji na watumishi wake wengine,wakae pamoja ili kuomba  na kutafakari Neno lake katika umoja
Mwaka 2008 Julai Mungu alisema yupo karibu kuingia Tanzania.
Mwaka 2014 katika mkutano wa madhehebu mbalimbali uliofanyika DAR es salaam,Mungu alisema kuwa  endapo kanisa halitaingia katika  toba na maombi,amani iliyopo itatoweka na hali ya nchi itakuwa mbaya kuliko ile ya Somalia.
Mwaka 2015 kupitia watumishi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi,Mungu anasema tena kanisa linahitajika kuinuka na kuchukua nafasi yake ya katika nchi.
kwa mawasiliano

0754507230 na 0784847070
MZEE GOFREY LEMA AKIELEZEA KWA MAKINI JUU YA KIONGOZI BORA NDANI YA STUDIO ZA TIT huku askofu Gamanywa akimsikiliza kwa makini na Mhe Kaduma kulia.
Kiongozi mzuri hasubiri mambo yaharibike ila anafanya kila jitihada kutafuta ufumbuzi mapema.
luka 19:41-43
Maneno ya manabii yanatimia maaana Mungu amekuwa akisema juu ya Taifa la Tanzania kwa muda mrefu sana,amekuwa kama anatubembeleza watanzania maana yeye anajua kilichopo mbele wakati sisi tunajua ya leo tu.
Mungu anataka kuingia Tanzania kufanya kile anachotaka kufanya na hawezi kufanya jambo bila kuwashirikisha watumishi wake.
Amosi 3:7

Wataalamu mbalimbali wanakaribishwa na wale wanasiasa wanaowania nafasi mbalimbali katika taifa hili ili wapate cha kuwaambia wapiga kura wao
Aidha Mzee Lema alisema kuwa mkutano huo hakuna kiingilio  na litanza saa tano kami asubuhi hadi jioni.
Hata hivyo alisema kuwa vyakula vitakuwepo ambavyo vitauzwa kwa bei ndogo sana kutakuwepo na kadi ya kutambulisha.
Hakukawia kuwataja wanenaji katika mkutano huo kuwa ni
Askofu Bernard Nwaka kutoka Tanzania na Emanuel Kure kutoka Marekani.

Hta hivyo alisema ujumbe juu ya Tanzania kwa itampata kiongozi anayetokana na Mungu 14 Agosti  2008 ulirudiwa na  Moris Cerullo 2008 Taifa hili litapata  Rais ambaye ni mteule kutoka kwa Mungu.
 IBRAHIMU KADUMA NDANI YA STUDIO ZA TIT.
Kauli ya mh. Ibrahim Kaduma ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kingdom Leadership Network Tanzania alisema kuwa julai 2008 unabii ulitolewa juu ya Tanzania sasa  ni vyema wateule waombe kwa bidii maana hatujui huyo mteule ni nani na unabii unapomkuja haubadiliki na anayetokana na Mungu atatenda kwa haki.
Askofu Deo Lubama
Ndugu msomaji wetu huu ni ujumbe juu ya Tanzania na sasa unaenda kutimia wewe unachukua hatua gani na unaweza kujiuliza kuwa walengwa katika mkutano huo ni viongozi wa makanisa hasa maskofu,wachungaji na watumishi wengine,wanasiasa,wafanyabiaashara na viongozi mbalimbali wa umma na sekta binafsi. 

Jumatatu, 27 Julai 2015

IBADA YA UTAKASO WA DAMU YA MTU KATIKA HUDUMA YA NEEMA YA KITUME KIMARA.



HUYU NDIYE Mtume Bethania akiwa katika hali ya majozi kuomba kwa uchungu juu ya kutakasa damu ya Mtu.

 MAJI AMBAYO WALIOFIKA KATIKA HUDUMA HIYO HUPEWA TAYARI KUTAKASA DAMU ZAO
Hivi ndivyo alivyosema Apostle Bethania Simon wa huduma ya Imani ya Kitume wakati akizungumza na blog hii ambapo alisema kuwa BWANA AMENIAMBIA NIANZE IBADA ZA, OPERATIONS TAKASA DAMU ZA WANADAMU ZINAZOLIA.(Mwanzo 4:9_10 firee)
Uchawi na mateso yote yata waachia watu hadharani, Bwana ameniambia nigeuze haya MAJI kuwa Damu ya YESU na dawa halisi ya MUNGU kisha niwatakase TANZANIA Damu zao.
Damu zinazolia,Kansa,Vidonda vya tumbo,Malaria sugu,Presha,Typhoid,Utasa,Moyo mpana,Unamafuta,Umetoboka,H.I.V, Unene feki,Kiharusi,Kutokwa damu,Kwenda hedhi mfululizo,Kutoa Nuksi na Mikosi,Mabaka mwilini.
IPO ROHO NDANI YA MWANADAMU,NITAING"OA KATIKA JINA LA YESU,NJOO UONE UPAKO HALISI, (Ayubu 32:8_9)
mtume betahania hakuishia hapo aliendelea kusema kuwa  baada ya kulia sana kwa mungu,ili yeye awaangalie watanzania,sasa amejibu kilio chetu.
mungu ameniambia, nianze ibada maalumu,za kikombe cha utakaso wa damu za watu,unakuja na kikombe chako,na utapewa maji ya utakaso wa damu yako,hakika damu yako itatakasika ghafla tu,utajishangaa umetakasika,ukienda hospital ukapima watakwambia umepona  ugonjwa uliokuwa ubakusumbua.
hii ni saa ya utakaso imeanza rasmi,ili uhai wako ubakie damuni mwako (walawi 17:10_11) njoo uone upako halisi wa NEEMA YA KITUME.
Ndugu msomaji mahali alipo huduma ya mtume Bethania Ni mbezi ya kimara,na unaweza kuwasiliana naye kwa namba ya  simu +255715 79 66 67 Utaongea na yeye moja kwa moja.
Kumbuka ni juma pili hii ambayo imepita ndiyo zoezi la utakaso wa damu za wanadamu ilipoanza kuanzia  Muda wa saa nne asubuhi mpaka saa tisa alasiri.


 

 Mtume Bethania akiwa madhabahuni.







 WAumini wakiomba kwa kulia kanisani hapo kwenye huduma ya neema ya KITUME.
 
Hayo ndiyo maji ambayo waumini walitumia siku ya jumapili.
Nao watoto walishirikishwa kwenye zoezi.
Ndugu msomaji wangu nimekuletea haya ambayo yameanzishwa na mtume Bethania ili nawe ufahamu kuwa tumetoka wapi na tunaelekea wapi hayo ni mafunuo ambayo yeye alisema kuwa amepewa na Mungu mara baada ya kulia sana mbele zake kuwa kwa nini watanzania wanateseka na magonjwa na shida mbalimbali ndiyo Mungu akajibu kilio chake pamoja na waumini wake.
KAMA UNA JAMBO USISITE KUWASILIANA NASI KWA WHATSAPP +255752834514 AU TUPIGIE KWA 0779632616  AMA KWA EMAIL YA SANEJULIAS@GMAIL.COM

Jumapili, 26 Julai 2015

HATIMAYE BWANA GEORGE RUNGU LA YESU AJITWALIA JIKO LAKE BI NURU KAMA ILIVYORIPOTIWA NA BLOG HII HAPO MWANZO UCHUMBA WAKE KATIKA KANISA LA DCR TAG TABATA SHULE.

Shangwe za AMANINAFURAHA KWA NDUGU GEORGE NA BI NURU.
 Hili ndilo kanisa ambalo Harusi ya Rungu la Yesu imefungiwa TAG Dar es salam Calvary Temple.




 BLOG hii inawatakia maisha mema na faraja na mafanikio George na Bi Nuru  maana apataye mke apata kitu chema. Hongera sana kaka kwa hatua kubwa maishani,Nawatakia Maisha marefu yenye furaha.

HALI ILIVYOKUWA KWA SIKU YA USIKU WA JUMAMOSI RAIS OBAMA AKICHEZA MZIKI WA KENYA AKIJUMUIKA NA WAKENYE WENGINE .

President Obama on Saturday night busted some moves to the music of Kenya’s Sauti Soil duting a State Banquest organized in his honor by President Uhuru Kenyatta. Obama received instructions on how to dance the LIPALA and the President can bust a move.




Rais Kenyetta pamoja na mgeni wake rais Obama wakijumuika na watu wengine katika kucheza.
Endelea kuangalia video hiyo hapo.

Jumamosi, 25 Julai 2015

HATIMAYE RAIS OBAMA NA MWENZAKE UHURU KENYATTA WAMEFUNGUA KONGAMANO LA SITA LA KIMATAIFA KUHUSU UJASIRIAMALI KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA MJINI NAIROBI.


 Hatimaye naibu wa rais wa Kenya William Ruto amefanikiwa kusalimiana na rais wa Marekani Barrack Obama baada ya kukosekana hapo jana katika ujumbe uliomkaribisha rais huyo alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. William Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC mjini the Hague.
Ikulu ya Nairobi kenya
 Ikulu
Mkutano wa kibiashara kati ya mataifa ya kenya na Marekani umeanza katika ikulu ya rais nchini Kenya.Rais Barrack Obama na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta wanawaongoza wajumbe kutoka mataifa hayo mawili katika mkutano huo.Swala la ugaidi ni miongoni mwa maswala tata yanayotarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho.
Rais ‪Obama pia anatarajiwa kutia sahihi ya mikataba ya kibiashara na mwenyeji wake rais Kenyatta katika ikulu ya Nairobi
Ruto
Rais Barrack Obama kukutana na makamu wa rais wa kenya William Ruto ambaye anakabiliwa na mashataka ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa ya ICC katika mazungumzo ya kibiashara kati ya Kenya na Marekani yatakayoandaliwa katika ikulu ya rais.
13.50pm:Rais Obama akiweka mauaObama
Rais Barrack Obama akiweka shada la maua katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa Marekani katikati ya jiji la Nairobi

Memorial Park


Rais Obama na Uhuru Kenyatta wawasili katika eneo la shambulizi la kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa Marekani katikati ya jiji la Nairobi.Baadhi ya barabara katika jiji la Nairobi zimebakia kuwa mahame

 
 
Manusura 1998,
Raia Walionusurika shambulizi la 1998 kenya wabeba mabango wakidai kwamba hawakufidiwa.Wanamtaka rais Obama kutowatupa na badala yake kuangalia maslahi yao.

Wachezaji densi Nairobi
Wachezaji densi ya kimasai wakisubiri kumtumbuiza rais Barrack Obama aliyetarajiwa kuwatembelea katikati ya jiji la Nairobi

 
M-kopa M-kopa
Rais Obama kwa sasa ametembelea maonyesho ya uvumbuzi jijini Nairobi ambapo alikutana na June Muli afisa anayesimamia maslahi ya wateja M-Kopa ambao hutoa huduma ya kawi ya jua ya 'pay as you go' katika makaazi.
 
Obama-uhuru Memorial Park
Obama na Uhuru sasa waelekea katika eneo la shambulizi la kigaidi la mwaka 1998 jijini Nairobi
Obama na Uhuru
Obama amaliza hotuba yake
BBC hewani moja kwa moja
Runinga ya BBC inapeperusha moja kwa moja kongamano hilo hewa
Obama
Kenya inaongoza katika teknolojia za kibiashara.Kwa mfano utumizi wa Mpesa-ni vyema kwamba teknolojia hiyo ilianza hapa Kenya
Obama 'Tutazindua mfuko wa kudhamini biashara zinazoanzishwa na wanawake
Kina mama ndio injini ya maendeleo barani Afrika.
Vituo vitatu vitafunguliwa Mali,Kenya na Zambia barani Afrika ili kuwasaidia wanawake wajasiriamali
Rais Obama
Rais Obama awasalimia wakenya kwa neno 'niaje' na
Hawayuni na kusema kuwa familia yake inatoka nchini kenya.
Lengo la mkutano huu aliouzindua miaka mitano iliopita mjini Washington ni kuwapiga jeki wafanyibiashara duniani.
Amesema kuwa kuna umuhimu wa kukabiliana na ufisadi ili biashara kushamiri.
Kenya ilikumbwa na chanagamoto chungu nzima ikiwemo majanga lakini imesimama imara na kusonga mbele.
Bara la Afrika haliwezi kutegemea mataifa ya magharibi .
Taifa la kenya ni chimbuko la makabila tofauti.
Mkutano wa wajasiriamali umeanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia mkutano
Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta Ges tweet
Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta ukiwa tayari umewasili katika eneo la mkutano wa wajisiriamali unaotarajiwa kufunguliwa na raia wa marekani Barrack Obama
Waandishi habari Waandishi
Waandishi wa habari wakijiandaa kuliangazia kongamano la kibiashara la wajasiriamali katika eneo la Gigiri jini Nairobi.
Vifaa vya waandishi hao vimepekuliwa na maafisa wa usalama wa Marekani.
Ndege za kijeshi
Ndege za kijeshi za Marekani zimeanza kuzunguka katika anga ya jiji la Nairobi kuimarisha usalama.

Barabara za Jijini Nairobi:
Barabara nyingi za mji wa Nairobi zimeonekana kuwa bila watu na magari kufuatia kuwasili kwa rais Obama.Mapema leo maafisa wa polisi walionekana katika barabara zinazoelekea katika eneo la Gigiri ambapo rais Obama atafungua rasmi kongamano la kibiashara.
Obama na familia yake Sara Obama,Barrack Obama na Daktari Auma
Mama Sarah Obama,Rais Obama na dadaake Daktari Auma Obama wakijumuika katika chakula cha jioni katika hoteli moja jijini Nairobi.
 Chanzo ni BBC.