YESU NI JIBU
Jumatano, 27 Januari 2016
Jumanne, 26 Januari 2016
MTUME NA NABII BETHANIA SIMON MWASISI NA MBEBA MAONO YA OPERATION NIBEBE NAMI NIKUBEBE UPOKEE YOTE.
Mtumishi
wakweli wa Mungu hapaswi kuficha mafunuo yake,anapaswa kuyatangaza maana sio
bangi bali ni habari njema kwa watu wote,labda wanao ficha hawayaamini mafunuo
yao kuwa ni ya Mungu Yehova Bwana wangu,waweke wazi kama mimi hapa.
Ufunuo huu ni kama unaleta kichekesho,na kwa wale walio mwilini huenda wasinielewe kabisa,lakini ni ufunuo wenye maana kubwa sana kibibilia.
Ufunuo huu ni kama unaleta kichekesho,na kwa wale walio mwilini huenda wasinielewe kabisa,lakini ni ufunuo wenye maana kubwa sana kibibilia.
Nime anza operation nibebe
na mimi nikubebe,au tubebane ili tufike,kama watu hawawezi kubebana basi maana yake ni kwamba
mtasimama milele na hamtakuja kutembea ili mfike kule mtakako kwenda.
Tokea huu ufunuo uje kupitia mimi hapa,watu hufunguliwa pindi ninapo kuwa
nahubiri huku nimebebwa dede juu kwa juu,kanisa limeanza kuongezeka kwa kasi
kubwa,watu wanatoa shuhuda za ajabu sana.
Nashauri watumishi waumini na wa Tanzania wote muanze kubebana juu kwa
juu,na tuweke wazi mafunuo yetu maana sio bangi wala meno ya tembo.
Karibuni mezani Maana wa Tanzania
wengi huongozwa na hofu badala ya kweli iliyo mioyoni mwao.
Waumini wakiwa katika ibada
Jumatatu, 25 Januari 2016
RAIS MAGUFULI AMETENGUA UTEUZI WA BWANA DICKSON E. MAIMU, MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue akifafanua moja ya swali lililoulizwa kutoka kwa mmoja
Waandishi wa habari (hayupo pichani) kuhusiana na suala zima la kusimamishwa
kwa Mkurugenzi wa NIDA,katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu
jijini Dar es Salaam mapema leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi
wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.
Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar
es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa
NIDA, Dickson Maimu
1.1 Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ametengua
uteuzi wa Bwana Dickson E. MAIMU, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa kuanzia leo, tarehe 25 Januari, 2016.
1.2 Aidha, baada ya utenguzi huo, Bwana Dickson E. MAIMUamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao:
1.2.1 Bwana Joseph MAKANI, Mkurugenzi wa TEHAMA
1.2.2. Bi Rahel MAPANDE, Afisa Ugavi Mkuu
1.2.3 Bi Sabrina NYONI, Mkurugenzi wa Sheria
1.2.4 Bwana George NTALIMA, Afisa usafirishaji
1.3 Taarifa zilizomfikia
Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia Sh.179.6 bilioni. Kiasi hiki ni
kikubwa na Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi jinsi fedha hizi
zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na
kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.
1.4 Hivyo, Rais ameelekeza
Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa
manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.
1.5 Rais pia ameelekeza
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi maalum wa hesabu
za NIDA, ikiwemo ukaguzi wa “value for money” baada ya kuthibitisha
idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa.
1.6 Rais vile vile
ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ifanye uchunguzi
kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.
2.0 Wizara
ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa
2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya
Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania
nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi
hiyo rafiki.
2.2 Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika
Mashariki na Ushirikiano wa Kianda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja
Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa
kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:
2.2.1 Bi Batilda Salha BURIANI, aliyeko Tokyo, Japan
2. 2.2 Dkt. James Alex MSEKELA, aliyeko Rome, Italia.
2.3 Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London,
Uingereza, Bwana
Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya
Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa
atakapopangiwa kazi nyingine.
2.4 Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko
wazi:
2.4.1 London, kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. KALLAGHE
2.4.2 Brussels, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous KAMALAkuchaguliwa kuwa Mbunge.
2.4.3 Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa
mkataba wa Dkt. James Alex
MSEKELA.
2.4.4 Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa
mkataba wa Bibi
Batilda BURIANI
2.4.5 Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia
aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz Ponray MLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.
2.4.6 Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu kwa
aliyekuwa Balozi, Bwana Francis
MALAMBUGI.
3.0 Tawala za Mikoa
3.1 Rais ametengua uteuzi
wa Eng. Madeni Juma KIPANDE kabla hajathibitishwa kwenye cheo cha Katibu
Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.
4.0 Utumishi wa Umma
3.2 Nachukua nafasi hii
kuwahimiza viongozi wote katika Utumishi wa Umma, na watumishi wote wa umma,
kubadilika kwa dhati kwenye utendaji wao na uadilifu wao.
3.3 Napenda kusisitiza
kuwa Rais na sisi tunaomsaidia hatuoni raha kuchukua hatua dhidi ya viongozi na
watumishi wengine. Tungependa kila mtu mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha
Rais mahali ambapo inabidi amchukulie hatua. Mambo yafuatayo ni muhimu:
4.2.1 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu isipate
kigugumizi kusimamia utendaji na maadili ya kazi.
4.2.2 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu asipate
kigugumizi kuchukua hatua za nidhamu, lakini afanye hivyo kwa kuzingatia kwa
ukamilifu sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma.
4.2.3 Lazima uongozi na watumishi wa umma
wawahudumie wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima. Kwa sababu hiyo:
a) Kila ofisi ya Serikali iwe na dawati la kusikiliza
shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
b) Kwenye kila Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
wajenge uwezo wa kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa wakati.
Kwa muundo wa Serikali yetu hakuna sababu kwa mwananchi kufunga safari mpaka
Ikulu Dar es Salaam kwa kuamini kuwa ni Rais tu anayeweza kumaliza matatizo
yake, maana wawakilishi wa Rais wako kila pembe ya nchi yetu. Ikibidi wananchi
wafike Ikulu ina maana hao wawakilishi wa Rais hawakutimiza wajibu wao.
c) Kuanzia sasa watumishi wote wa umma wavae majina yao
ili iwe rahisi kwa mwananchi kumtambua anayemhudumia na hivyo kumsifu mtumishi
wa umma anayewahudumia kwa weledi, uaminifu na kwa wakati, na kumtolea taarifa
yule anayefanya mambo ya hovyo.
d) Kila ofisi ya Serikali iwe na utaratibu wa kupokea maoni ya
wananchi kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo, na kushughulikia haraka
maeneo yote ambayo wananchi wataonesha kutoridhika na huduma.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
25 Januari, 2016
MHANDISI GEORGE SAMBALI ATEULIWA KUWA KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Profesa Makame
Mbarawa amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi George Sambali kukaimu nafasi ya Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kufuatia kifo cha
aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Suleiman S. Suleiman.
Mhandisi Suleiman alifariki dunia tarehe 18 Januari, 2016 wakati
akipelekwa katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam baada ya kuishiwa nguvu
ghafla akiwa katika mazoezi ya kuogelea katika eneo la Feri, jijini Dar es
Salaam.
Akitangaza uteuzi huo kwa niaba ya Waziri Mbarawa mbele ya
Menejimenti ya TAA Jumatano tarehe 20 Januari, 2016 katika Ofisi za Makao Makuu
ya Mamlaka hiyo kwa niaba ya Mh. Waziri, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuliho, alisema uteuzi wa
Mhandisi Sambali umeanza rasmi tarehe 20 Januari, 2016.
Jumapili, 24 Januari 2016
WITO LIMEENDELEA KUTOLEWA NA BASATA KWA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUJISAJILI KWA LENGO LA KUPATA STAHIKI ZAO.
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limezidi kutoa wito kwa Waimbaji wa muziki wa Injili kujisajili katika baraza hilo ili stahiki zao zitambulike inavyotakiwa.
Mkurugenzi wa
ukuzaji Sanaa na Mtukio wa Basata, Maregesi Kwirujira Ng’oko alisema waimbaji
wengi wa muziki wa Injili wa Tanzania kuzingatia hilo.
Ng’oko
alisema kujisajili Basata kuna faida na fursa nyingi ambazo ni msaada ambao
utasaidia kupata haki zao kupitia kazi zao.
Ng’oko
alisema kwa kuwa wao ndio wasimamizi wa kazi za sanaa ni jukumu lao
kuwakumbusha mara kwa mara wasanii kujisajili.
Aidha Ng’oko
alisema wanatoa salamu hizo kwa wasanii pindi inapotokea mikinzano katika ufanikishaji
wa kazi zao.
Naye Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Abihudi Mang’era
alisema wanafikiria kuongeza msukumo kwa waimbaji wa muziki wa Injili kuhusu
kujisajili Basata katika baadhi ya matukio.
Mang’era
alisema wanafikiria kutoa elimu ya kujisajili Basata katika matamasha yao ama
kusaka namna ya kufanikisha utambuzi wa waimbaji katika baraza hilo.
Jumamosi, 23 Januari 2016
,HUKO NCHI DEMOKRASIA YA CONGO MTU MMOJA AJIITA MUNGU KAMA YULE WA HUKO NCHINI KENYA AMBAYE ALIJIITA MUNGU NA BADO AMEFARIKI.
Unaweza ukawa na maswali mengi katika maisha yako ila kumbuka maandiko yanavyosema juu ya siku za mwisho,kuwa watatokea manabii wa uongo,na watawadanganya wengi.
Ndugu msomaji wa blog hii hili sasa ni tukio la pili la mwanadamu kujiita mungu mara baada ya yule raia wa Kenya ambaye naye alijiita mungu na hatimaye akafariki baada ya kuugua ila waumini wake walikataa na kusema hajafariki wakati ni tukio la kweli kuwa amefariki.
Sasa hapa ni nchini Demokrasia ya Congo huyu naye anajiita mungu,ila ikumbukwe kuwa na hata Tanzania alishawahi kutokea mtu mwingine naye alijiita Adamu wa pili ila naye alifariki na waumini wake yaani wafuasi nao walidai kuwa amepaa kwenda mbinguni jambo ambalo lilionekana kuwa sio la kweli.
Source ITV,
MSOMAJI WA BLOG HII TUPE MAONI YAKO,
MSOMAJI WA BLOG HII TUPE MAONI YAKO,
Jumatatu, 11 Januari 2016
KANISA LA ANGLIKANA TANZANIA DAYOSISI YA VICTORIA NYANZA (DVN) LILILOPO JIJINI MWANZA, LIMEMTIMUA RASMI ASKOFU KANISA HILO, BONIFACE KWANGU, KUTOKANA NA UBADHILIFU WA wa MAMILIONI YA FEDHA.
Mwenyekiti wa nyumba ya wahudumu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza ,mchungaji Andrew Kashilimu akisoma tamko la wachungaji.
Askofu huyo ni wa pili kutimuliwa na
uongozi wa kanisa hilo baada ya mwaka 2007 aliyekuwa Askofu wa dayosisi hiyo,
John Changae na yeye kufukuzwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kitendo
ambacho kinaonesha taswira mbaya kwenye kanisa hilo.
Jumanne, 5 Januari 2016
Jumapili, 3 Januari 2016
KILA MTANZANIA ATAKIWA KULIOMBE TAIFA AMANI ILI AMANI NA USALAMA UENDELEE KUDUMU NA WANANCHI WAINULIWE KIUCHUMI.
Watanzania wametakiwa kuliombea taifa amani ili liendelee kudumu
katika hali ya utulivu upendo na mshikamano na kuepukana na machafuko
yanayoweza kutokana na viongozi kushindwa kuongoza kwa haki na hivyo kujenga
chuki miongoni mwa wananchi wake.
Ijumaa, 1 Januari 2016
HOJA YA ASKOFU GAMANYWA JUU YA VITU AMBAVYO HAVINA MAANA YA KUMALIZA MWAKA
Kumaliza mwaka sio tu kubadilisha namba
ya mwaka toka 2015 kwenda 2016. Kubadilisha namba hakuleti mabadiliko yoyote
zaidi ya kubadili namba tu.
Na wala kumaliza mwaka hakuna maana ya kubadilika
kwa mazingira toka kwenye uchakavu kwenda kwenye upya. Wala kubadili mwaka sio
kuondoa changamoto za maisha ulizokuwa nazo na kuingia kwenye maisha raha bila
masumbufu yoyote ya maisha.