Kanisa
likitambua thamani ya kristo Yesu haliwezi kuyumbisha na kitu chochote hata
kama litapita katika changamoto litabaki na msimamo wa kumpenda yesu katika
imani na kuvumilia mateso yote.
Amesema hayo
mchungaji Isaac Mwanjabeki wa kanisa la T.A.G Gongo La Mboto Solomoni Temple jijini
Dar es salaam kwamba kanisa la leo linatakiwa liwe na uvumilivu katika
kumtumikia Mungu pia lijifunze kupitia
kanisa la simina katika kitabu cha ufunuo.
Mchungaji
Mwanjabeki amewasihi watu wanaopitia nyakati ngumu za kimaisha kutokata tamaa
na kuwa na subira kwa Mungu kwakuwa jaribu lina muda wake upo wakati litapita.
Mungu
huwaangalia walio waaminifu na wavumilivu hasa pale unapopitia majaribu ni
vyema kukaa karibu zaidi nae ili uone ukuu wake.