Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa kansia la EAGT, Mzee Henri
Mfuko, ameonya kuwa kansia hilo linakabiliwa na hatari ya kugawanyika kufuatia
mgogoro ulioibuka baina ya uongozi wa kanda na ule wa Jimbo la temeke ambao
umesababisha kufunguliwa kwa kesi ya madai mahakamani na kusimamishwa kwa
viongozi wa Jimbo. Huku ikielezwa kuwa kivuli cha Hayati Askofu Dk. Moses
Kulola ndicho kinacholityesa kanisa hilo.
Aidha imeelezwa kuwa
Wothia alioandika kulola Kabla ya kufariki dunia unaompa Katunzi
kijititi cha kuhubiri Injili, kukua kwa kasi kwa kansia la EAGT City Centre na
mpango wa kujenga majengo ya kisasa ya Jimbo la Temeke viliibua upinzani
mkubwa uliopelekea kuvuliwa madaraka
na kugawanywa kwa Jimbo bila kufuata taratibu.
Ni kwa sababu hiyo, Askofu Katunzi na wenzake waliamua kufungua
shauri la madai Mahakamani na ikatolewa amri ya kuzuia mkutano lakini haikuheshimiwa na badala yake mkutano ukafanyika na viongozi wa muda
wakateuliwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ndani ya kanisa hilo, lililomiongoni
mwa makanisa makubwa ya kipentekoste Tanzania, hali ya kutofautiana baina ya
Uongozi wa kanda chini ya Askofu Nicodemus Nyenye na kamati yake, na uongozi wa
Jimbo la Temeke chini ya Askofu Floriana Josepah Katunzi na Kamati yake umeshindwa kupata ufumbuzi na kupelekea kufunguliwa kwa shauri la madai namba 70 ya mwaka 2016, katika mahakama ya Wilaya ya Temeke.
Habari kutoka mahakamani hapo zinaeleza kuwa Kesi hiyo ilifunguliwa na Askofu Katunzi na
wenzake, dhidi ya Bodi ya wadhamini ya
kanisa la EAGT, Jumatatu iliyopita ambapo pia waliomba amri ya mahakama ya
kuzuia mkutano wa dharura ulioitishwa na
uongozi wa kanda bila kutaja agenda
zake.
Pamoja na amri hiyo ya mahakama kikao hicho kiliendelea kama
kilivyopangwa na kikafanya mambo mawili ambayo ni kuligawa Jimbo la Temeke na
kuzaliwa Jimbo la Ilala na kutangazwa kwa viongozi wa muda wa Jimbo la Temeke
naada ya uongozi wa kanda kusimamisha kamati iliyoongozwa na Askofu Katunzi.
Katibu wa Kanda ya Mashariki na Kusini ya kanisa la EAGT, Mch.
Dk. Alphonce
Mwanjala, akiongea mbele ya wajumbe wa mkutano huo wa dharura
alisema kuwa maono yao (kanda) sio kujenga bali ni kuhubiri Injili, lakini
Jimbo la Temeke maono yao ni kujenga.
Alisema kuwa uongozi imewasimamisha viongozi hao na kuteua vionmgozi wa muda kwa kuwa waliwaita Askofu
Katunzi mara tatu, lakini hawakufika
hivyo hawana njia nyingine isipokuwa kuweka kando.
Baada ya kauli hiyo hali
ilichafuka kumbuni baada ya baadhi ya wachungaji kupaza sauti zao
kupinga hatua hiyo hadharani wakisema kuwa inauonevu na harufu ya hofu kutokana
na kasi ya maendeleo ya Jimbo na mpango wao wa kujenga jengo la ofisi za lenye
ghorofa tatu.
Mmoja wa wachungaji aliyekuwa akilia machozi alisema: “Hiki ni
kivuli cha Askofu Dk. Kulola kinachoendelea kulitesa kansia letu. Tumekuwa na
mpango wa maendeleo ya jimbo ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa jingo la ghorofa tatu
na michoro ilishakabidhiwa kanda na hilo ndilo limewafanya wagawe Jimbo
ili kutudhoofisha. Unajua Kanisa letu la EAGT halina ofisi rasmi, Kanda haina
ofisi n ahata makao makuu ni jina tu, hatua ya sisi kupeleka mchoro wa Jengo la
Ghrofa tatu ndio chanzo cha yote haya…..”alisema Mchungaji huyo ambaye hakutaka
jina lake liandikwe gazetini.
MSIMAMO WA MDHAMINI
Akiongelea mgogoro huo, Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa
kansia la EAGT, Mzee John Henri Mfuko, alisema kuwa kwa hali ilivyo kanisa hilo
linakabiliwa na hatari kubwa ya kugawanyika vipande viwili kwa kuwa kuna baadhi
ya viongozi wanaofanya mambo kinyume na katiba tena kwa kutofuata utaratibu.
Mdhamini huyo alisema kuwa mgogoro uliopo baina ya Jimbo la Temeke
na Kanda ya Mashariki usingefika mahali ulipo sasa kama katiba ya kanisa
ingelifuatwa na viongozi kushughulikia matatizo kabla ya kukua na kuwa migogoro
mikubwa.
Alitoa mfano wa mgogoro uliotokea huko Shinyanga ambapo yeye
alikwenda na kusimamia suluhu ambayo hatimaye ilipatikana na pande mbili
kumaliza tofauti zao.
“Kuna kiongozi wa kanda alikuwa hapa juzi nikamwambia haya mambo
si mgeyamaliza tu kwanini mfikia hatua ya kuondoana? Akanisambia huyo jamaa
amemtukana kiongozi wetu siwezi kumacha lazima aondolewe tu,”alisema mzee huyo
huku akiinamisha kichwa kuonyesha ishara ya kuumizwa na mgogoro huo.
wameusimamisha uongozi wa
Jimbo la Temeke kwa kuwa ulipinga
kugawana.
Wakati uongozi wa kanda ukidai kuwa uongozi wa Jimbo uliitwa
mara tatu ili kusaka suluhu na kisha
kutohudhuria, madai ya Uongozi wa Jimbo kulingana na barua waliyomuandikia Askofu Mkuu wa Kanisa hilo
wakikata rufaa kupinga tatibu zilizotumika kugawa Jimbo hilo ni kuwa, utaratibu wa kawaida wa
kugawa Jimbo haukufuatwa kwa kuitishwa kwa halimashauri ya jimbo kujadili kabla ya mpango kufikishwa kanda.
Uongozi wa Jimbo pia katika malalamiko yake kwa Askofu Mkuu
walitaka awasikilize yeye kwa kuwa hawakuwa na Imani na uongozi wa kanda, hata
hivyo uongozi wa taifa uliandika barua na kurejesha shauri hilo ngazi ya kanda
ambayo jimbo haikuwa na Imani nayo katika kushughulikia mgogoro huo.
Habari za ndani zinadai kuwa kumekuwa na njama mbaya za
kumzushia Katunzi kashfa ili kumvua cheti cha uchungaji na kuleta hofu miongoni mwa wachungaji wa Jimbo
la Temeke ambao hawakubaliani na hatua ya kumvua uongozi.
Wengi wa wachungajin wa Jimbo hilo walisema wazi kuwa hawako
tayari kukubaliana na maamuzi hayo kwa kuwa hawakupewa nafasi ya kusikia pande
zote n ahata kulipigia kura jambo hilo.
KIVULI CHA KULOLA
Habari za ndani zionaeleza kuwa
baada ya Askofu Kulola kumaliza
kazi, ulisomwa wosia alioandika kuhusu familia yake ambao ulimtaja Katunzi kuwa msimamizi wa mirathi ambapo pia alitajwa
kukabiziwa kijiti cha kuhubiri injili katika ziara ambazo kiongozi huyo alikuwa
akizifanya.
Ni kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni hofu ya kile
kilichoandikwa katika wothia huo, mambo kadhaa yametokea ikiwa ni pamoja na
baadhi ya wanadugu wa Dk. Kulola kupinga Katunzi asisimamie mirathi ya kulola na hata alipochaguliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Temeke kivuli cha
yale yaliyoandikwa katika wothia kiliendelea kumwandama.
Kanisa la EAGT, lilianzishwa
baada ya kutoke mgogoro baina ya
Dk. Kulola, na Immanuel Lazaro waliokuwa vionmgozi wa juu wa kansia la TAG, Lazaro
akiwa Askofu Mkuu na Kulola akiwa makamu wake.
Inaelezwa kuwa mgogoro mkubwa ulianzia katika kuhamisha
wachungaji na uliposhindwa kusuluhishwa ndani ya kansia na kufikia hatu ya kupigana ulifikishwa mahakamani
na mahakama iliamua kila mmoja afanyekazi kivyake na wagawane mali.
Ni kutokana na hitoria hiyo hofu ya kumeguka tena kwa kanisa la
EAGT imejitokeza miongoni mwa waumini n
ahata mdhamini pia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni