YESU NI JIBU

Jumatatu, 29 Desemba 2014

INA GOGU NA MAGOGU HATIMAYE KUJA : JE URUSI INAPANGA VITA DHIDI YA SERIKALI YA WAYAHUDI WA ISRAELI:



 Maandiko yanazidi kutimia unabii ulikuwa umetabiriwa kwa sasa unafikia kukamilika ndugu msomaji ni vyema kuchukua hatua mahususi ya kujitakasa na kutafuta uso wa Mungu kwa juhudi maana muda si mrefu mwana wa Adamu atashuka kutoka mawinguni kazi kwako kama hujampokea BWANA YESU kama bwana na mwokzi wa maisha yako ni vyema ujisalimishe mapema maana wewe mwenyewe,ni shahidi mataifa yanainukiana kivita ,ndugu na jamaa wanauana wao kwa wao,watoto wadogo wanabakwa.
Raisi wa Urusi Vladimir Putin akitafakari jambo.
Tel Aviv - Urusi inaandaa mpango wa dharura kwa haraka wa Hezbollah na uwezekano wa serikali ya rais wa Syria Bashar al-Assad katika vita moja kwa moja ya kijeshi na Israeli, sawasawa na rasmi Kifaransa ambaye amekuwa ikijitangazia hali hiyo. 
Mtu mmoja, ambaye alizungumza kwa masharti ya kutotajwa , alisema dharura maana ya kutumika kama kadi dhidi ya West , hasa Marekani na Umoja wa Ulaya , ambayo imekuwa kushiriki katika juhudi za kujitenga kwa Moscow.
 Hii wiki iliyopita, Marekani na E.U. iliwekea stramare vikwazo vya kiuchumi Urusi , ikiwa ni pamoja na vikwazo juu ya uwekezaji katika Crimea, kwa msisitizo juu ya Black Sea mafuta na gesi ya Urusi na utalii.
 Afisa huyo alisema kuna taarifa Russia katika wiki za karibuni mafanikio kusafirishwa kwa Hezbollah convoy kubwa ya Iskandar makombora ballistiska na makombora uso-kwa- hewa. Makombora hayo yalitolewa , licha ya Israel ya madai airstrikes katika Syria kulenga silaha Russia kusafirishwa mapema mwezi huu, alisema afisa huyo.
 Afisa huyo alisema Russia hana uamuzi wowote kuhusu fujo Hezbollah mashambulizi ya Israeli, lakini maoni vita iwezekanavyo katika Mideast kama kadi wanaweza kucheza katika mapambano yake na nchi za Magharibi , hasa katika Ukraine."Mwisho shuhuda wa jarida la Times " ameichukulia juu ya safari mwandishi wa jarida hilo juuya moyo wa ulimwengu kibiblia , kwa mstari wa mbele wa unaoendelea mapinduzi ya Mashariki ya Kati , ni kugundua jinsi utabiri wa unabii kale inavyotimia
 Mapema mwezi huu, Waziri Walid al- Moualem wa Syria alisafiri kwenda Urusi kukutana na rais wa nchi , Vladimir Putin, na Urusiwaziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov katika katiak sehemu ya mapumziko ya Russia Black Sea huko Sochi. Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka kwa chanzo katika utawala Assad , Putin na Lavrov amemwahakikishia Moualem kwamba Urusi " haitasimamia mashambulizi yoyote ya Magharibi juu ya Assad na badala yake Warusi aliwahidi "msaada" na "ulinzi" kwa utawala wa Assad .Kwa maelezo zaidi fuata link WND  
TOA maoni yakoo

Ijumaa, 26 Desemba 2014

WAKATI WA KUSHERHEKIA KRISMASI KATIKA BAADHI YA MAENEO MBALIMBALI DUNIANIJIONEE YALIYOJIRI:

Hali halisi katika maeneo mbalimbali Duniani watu wakisherhekea maadhimisho ya kuzaliwa kwa mwokozi wa ulimwengu Yesu kristo zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita.
Kiukweli baadhi ya watu wanaichukulia siku hiyo kama ya kawaida na kama ni desturi kusherehekea katika siku hiyo maana wengi wanakuwa mapumzikoni,wengine hudhania kuwa ni siku ya kula na kunywa,hata wengine hudiriki kusema kuwa ni kulewa sana maana ni siku ya mapumziko ndugu mpendwa msomaji wa blog hii siku kama hiyo ni kuamini na kukubali Bwana Yesu kuzaliwa ndani ya moyo wako na kumfuata kwa ukamilifu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako katika biblia kitabu cha Matayo 1:18-21 inatuhabarisha juu ya kuzaliwa kwa Yesu nishauku ya moyo wangu ndugu msomaji umtii na kumfuata Yesu kama bwana na Mwokozi wa maisha yako.Ndugu msomaji inakubidi umfahamu Yesu kibnafsi;
YESU ni  
  •  Mtu wa ajabu kupita watu wote katika nyakati zote? 
  • Nani aliyejitokeza kuwa mtu mashuhuri kwa vipindi vyote?
  • Kiongozi mkuu?
  • Mwalimu mkuu?
  • Mtu aliyefanya matendo mema kwa wanadamu kupita mwingine?.
  • Mtu aliyeishi maisha matakatifu kuliko yeyote aliyewahi kuishi? Na hapa utaona matukio mbalimbali ya krismasi.
 Familia ya Uingereza kubwa - Radfords , familia ya yenye watoto 16.
 Mila : Maelfu ya waogeleaji katika Wales kuchukua kila mwaka ya Krismasi yao kuwa kama maonesho.
Askari wa Marekani akipiga picha na mwenzakewakati wa mapumziko wakati wakipata chakula cha mchana wakati wa Krismasi katika msako  msingi Gamberi nchini Afghanistan.
 Mtu akikagua mti katika Guerrero, Mexico , ambayo imebeba majina na picha 43 za  walimu wanafunzi  ambao alipotea karibu pale mwezi Septemba.
Kiongozi wa Kilatini , Fouad Twal , akibeba mfano wa mtoto Yesu wakati wa Misa katika Kanisa la Nativity huko Bethlehem.
Mwamini akiwasha mishumaa wakati wa Misa katika St Alexander Nevski Cathedral huko Sofia , Bulgaria
Maelfu ya wakristo kushikilia mishumaa wakati wa kusanyiko la ibada huko Surabaya , Indonesia , ambayo pia ni nchi inayojulika sana Duniani kuwa ni nchi ya kiislamu.
 Familia Salaj katika mji wa Cazma , Croatia, wamegeuza mali zao katika sherehe za  Krismasi kwa kufunga taa milioni 1.5.
Alpaca  hutumika kwa ajili ya kuwashawishi wanunuzi huko Beijing, China, ambapo Krismasi mara kwa mara nyingine hupigwa marufuku.

Impromptu ni eneo lilojengwa na mti hutengenezwa kwa kutumia mpira yenye uzito  huko  Hamedieh kitongoji cha Homs , Syria.
 Wakristo Pakistan kuimba nyimbo mbalimbali  kusherehekea Krismasi katika kanisa huko Karachi.
 Mvulana Iraq Mkristo, ambaye walikimbia ghasia katika mji wa kaskazini wa Iraq wa Mosul ,akiwa amevaa kofia Baba Krismasi katika viwanja vya Machi Elia Wakaldayo katika Kanisa Katoliki, ambapo Wakristo wengi makazi yao hujengwa kwa mahema, katika Arbil , mji mkuu wa Kikurdi mkoa wa uhuru katika kaskazini mwa Iraq hii ilikuwa tarehe 24 Desemba, 2014.
Hayo ndiyo yaliyojiri katika baadhi ya sehemu mbalimbali duniani na kwa hapa Tanzania kuna baadhi ya watumishi wa Mungu ambao nipata nafasi ya kuwauliza juu ya siku ya Krismasi akiwepo Nabii Honest Mallya wa huduma ya Ebenezer Miracle Service

Tunapo sema maana ya krismass ni tunaazimisha kuzaliwa kwa Kristo ukisoma mathayo 2:1- utaona kuzaliwa kwake. Kuhusu kusherekea ni watu wote kwa sababu hakuja kwa watu fulani bali alikuja kwa kila mtu ili apate uzima. 
Napenda kusema kila anaye mwamini Kristo ataokoka na asiye mwamini atahukumiwa ukisoma Marko 16:16 ina ongelea juu ya kumwamini Kristo, na sasa tunaelekea mwaka mpya lazima roho zetu ziwe mpya maana tutapata yaliyo mapya na lazima tutambue kwamba vile Mungu ana watu wengi ndivo naye shetani anatafuta watu wengi mwaka 2015 usifanye mchezo kama ulikosea hapo nyuma usikosee tena amani kwao mtu wa Mungu.



Kwa upande wa mchungaji wa House of Prayer Apostle PKE nilipo muuliza kuwa kusherehekea krismasi ni dhambi amekuwa na majibu haya  Sio dhambi ila krismas sio kusherekea ila kumbuka Yesu Kristo kwa kazi maalum ambayo alikuja kufanya duniani Wakolosai 2.16 mtu asikuhukumu kwa ajili ya sikukuu.
Na huko mkoani Kilimanjaro waumini walishiriki meza ya Bwana kwa Dr askofu Sixbert  mambo yalikuwa hivi.





 



Ni baraka mno kubarikiwa na kushiriki meza ya ya Bwana hapa ni foleni na uvumilivu mwingi Kuwa nitafika tuu!! na mimi pale kwa mkono wa Bishop dr Sixbert.
Naamini nkuwa umepata matukio mbalimbali ushauri maona yanapokelewa.

Alhamisi, 18 Desemba 2014

SASA BUNGE LA KENYA LAGEUKA KUWA UKUMBI WA MASUMBWI NA KUVUANA MASHATI KWA MUDA MARA BAADA YA WABUNGE KUTOFAUTIANA VIKALI BUNGENI KUHUSU MSWADA TATANISHI WA USALAMA AMBAPO WABUNGE WA UPINZANIWANADAI UNAKIUKA UHURU WA WAKENYA:



Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bungeni  na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.

Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo. 

Seneta Johnston Muthama alijikuta katika sintofahamu mara baada ya suruali yake kuchanika katika mvutano bungeni humo. 
Seneta Muthama alijeruhiwa mguuni

Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyataja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.'

Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.

Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.

Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia

Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangu mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
Naibu spika wa bunge Joyce Laboso amwagiwa maji mara baada ya vurugu kuanza.
Kikao cha adhuhuri cha wabunge nchini Kenya, kinaendelea kuzua hisia kali huku wabunge wakiendelea kuvurugana humo. Wabunge hao wanajadili mswada tatanishi wa usalama ambao upande wa upinzani unasema unakwenda kinyume na katiba na kuwanyima wakenya haki yao ya kujieleza.
Mmoja wa wabunge hao wa upinzani amemwagia soda naibu spika Joyce Laboso ambaye alikuwa anasimamia kikao hicho cha kufanyia mswada huo mabadiliko kabla ya kupitishwa.
Spika wa bunge hilo sasa amechukua usukani na kuamuru kutimuliwa kwa wabunge wawili waliokuwa wamezidi vurugu.

Jumamosi, 13 Desemba 2014

Ukiheshemiwa heshimika-2 ungana na askofu mkuu wa WAPO Mission International na makala haya:



Katika toleo lililopita tulianza mada mpya ya “ukiheshimiwa heshimika” ambapo tulichambua maeneo matatu yaliyojumuisha “Utangulizi”; “Vyanzo vya heshima”; na “Tishio la kujivunjia heshima baada ya kuheshimiwa”! Leo tutaingia katika sehemu muhimu ya sababu kubwa ya kibibilia ambayo husababisha wengi wanaofanikiwa na kuheshimiwa hupoteza heshima zao katika jamii:
Mtazamo wa Yesu kuhusu kujikinai
na kuacha kuheshimika

Bwana Yesu aliwahi kuongelea tatizo la hali ya kujikinai baada ya kufanikiwa kiasi cha kudhani mafanikio ni “kibali cha kuishi milele duniani”! Katika kuweka mkazo kuhusu tabia hii, Yesu alitoa mfano wa mtu mmoja tajiri aliyeonesha kujikinai kwa utajiri wake na kutamba kuishi duniani bila ukomo:
 “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.  Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;  akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.  Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.  Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.  Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?  Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu. “ (LK. 12:15-21)

Kwa kupitia maandiko haya, unaweza kusoma baadhi ya kauli za tajiri jinsi alivyojikinai akisema: “….ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi…” Kumbuka kwamba huyu tajiri hakuupata utajiri wake kwa njia za ufisadi. Aliupata kwa njia halali kabisaaaa. Alilima shamba lake “likazaa sana…”

Aidha, mpango wa kujenga ghala za kuhifadhi mali zake haukuwa jambo baya hata kidogo! Tatizo lake lilikuwa ni kujikinai, na kujisahau, kwa kufikiri kwamba alifikia kilele cha mafanikio hayo kwa nguvu zake binafsi na kwamba uhai wake utalindwa na wingi wa mali zake!

Ni upumbavu kuacha nyuma mali nyingi
uondokapo badala ya kuzitanguliza uendako
Kutokana na maneno ya Yesu, inaonesha kwamba tabia ya kukusanya na kijilimbikizia mali nyingi kisha ukaondoka na kuziacha bila kuzifaidi ni “Upumbavu”! Kwa mujibu wa maneno ya Yesu ni kwamba upumbavu huu hauishii katika kujilimbikizia peke yake, bali kushindwa kuzitumia mali kwenye mambo ya ufalme wa Mungu; na matokeo yake mhusika kuondoka duniani ghafla na mali zake kuchukuliwa na wengine wasiozitaabikia tangu mwanzo:

“….Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?  Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu..”

Uchunguzi wangu wa kimaandiko katika mada hii, nimebaini kwamba, kujikinai sio kujisifia utajiri peke yake, wala sio kumsahau Mungu peke yake, bali ni matumizi ya utajiri wenyewe ambayo Yesu amesema kwamba   “….ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu. 

Mambo mawili muhimu hapa. Kwanza, ni tatizo la kujilimbikizia akiba isiyo na matumizi bali imekaa tu kwenye hifadhi yake. Pili, kukataa kutumia akiba ya mali katika vipaumbele vya Mwenyezi Mungu alivyoamuru kwa wale wanaomiliki mali nyingi!

Yesu aliposema “kujitajirisha kwa Mungu” maana yake halisi kwa tafsiri ya toleo la Biblia ya Kiingereza cha Amplified limesema: “So it is with the one who continues to lay up and hoard possessions for himself and is not rich his relation to God…..”  Haya maneno ya “…to lay up and hoard possessions…” yana maana ya kukusanya na kujilimbikizia..” Maana yake na ulimbikizaji ambao matumizi yake hayana mchango wa uhusiano na huduma za kimungu.

Katika uchambuzi huu kuhusu mfano wa Yesu tunajifunza mambo muhimu yafyatayo:

1.        Tishio la mali kuchukuliwa na wengine

Mtazamo wa kujilimbikizia mali nyingi ili hatimaye ndipo mkusanyaji apate kuzifaidi hapo baadaye si kitu kipya. Yupo mchaji Mungu aliyepata kuwa tajiri sana kuliko wengi duniani, ambaye alifanya utafiti kuhusu hatma ya utajiri ambapo alihitimisha kwa kusema hayo nayo ni ubatili:

"Nami nikaichukia kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo chini ya jua; maana sina budi kumwachia yeye atakayenifuata.  Naye ni nani ajuaye kama huyo atakuwa mwenye hekima au mpumbavu? Hata hivyo atatawala juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo, ambamo ndani yake mimi nimeonyesha hekima chini ya jua. Hayo nayo ni ubatili."(MHU. 2:18, 19)

Kuna maneno haya “……kazi yangu yote niliyojisughulisha nayo chini ya jua,…..” “……..sina budi kumwachia yeye atakayenifuata…….” “…… atatawala juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo…….” hayo nayo ni ubatili.”

Aliyeandika haya ni mfalme Sulemani ambaye alijikusanyia mali na utajiri mwingi kuliko matajiri wote wa ulimwengu waliowahi kuwepo kabla na baada yake. Ushahidi mwingine wa utafiti wa Mhubiri unapatikana katika maandiko yafuatayo:

“Maana kuna mtu ambaye kazi yake ni kwa hekima, na kwa maarifa, na kwa ustadi; naye atamwachia mtu asiyeshughulika nayo kuwa sehemu yake. Hayo tena ni ubatili, nayo ni baa kuu.” (MHU. 2:21)

Katika maandiko haya tunakutana na maneno haya.. “….Mtu ambaye kazi yake ni kwa hekima, na maarifa, na kwa ustadi….” “…….naye atamwachia mtu asiyeshughulika nayo kuwa sehemu yake…”

Hili jambo lilimchanganya sana Sulemani. Mtu anakusanya mali nyingi kwa muda mrefu na nguvu nyingi, akisha kufikia kilele cha ulimbikizaji kabla hajazifaidi anaondoka ghafla, na mtu mwingine anazichukua bila kuzitaabikia!!

2.        Kufananishwa na Mpumbavu

Yesu anamtaja tajiri Yule kuwa “Mpumbavu”! Ukifuatilia kwa makini Bibilia inamtafsiri “mpumbavu” ni mtu yeyote asiyetambua uwepo wa Mungu:

“Mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu; wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, hakuna atendaye mema.” (Zab.14:1)

Hivi ndivyo Yule tajiri mkulima alivyoonnesha upumbavu wake ambapo Yesu aliutafsiri kwamba ni “dhana potofu ya uzima wa mtu kuwa katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo..”

3.        Jinsi ya kuweka akiba yenye tija ya milele

Haya basi, baada ya kuuthibitisha hasara ya kujilimbikizia mali na kisha kufa ukaziacha na kuondoka patupu, Yesu alipendekeza njia ya kunufaika na mali za duniani hata baada ya kuondoka duniani ni kuhakikisha matumizi ya mali hizo yanatoa kipaumbele kwa mambo ya ufalme wa Mbinguni:

“Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi hujunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.” (Mat.6:19-21)

Katika maandiko haya, ukiyatafsiri kwa mtazamo wa mfano wa tajiri aliyejilimbikizia mali kibinafsi, utagundua maana kama ifuatavyo: Kwanza, kukusanya mali na kuzitumia kwenye mambo ya ufalme wa Mungu ndiyo njia pekee ya kulimbikiza mali mahali salama kwa maana kwamba mali zinakutangulia uendako badala ya kuziacha nyuma yako uondokapo.

Majumuisho kuhusu kujikinai na kupoteza heshima

Watu wengi hutumia nguvu na muda mwingi katika kutafuta mafanikio kwa njia mbali mbali. Baada ya kufikia mafanikio na wahusika kupata kutambuliwa, na kupata umaarufu na heshima kutokana na mafanikio waliyoyapata, ghafla hubadilika kitabia na kupotesha heshima ile ile waliyokuwa wameipata kutokana na kazi kubwa waliyokwisha kuifanya.

Moja wapo ya tabia mbaya inayopoteza heshima ni kujikinai na kudhani kwamba, mafanikio hayo ni juhudi binafsi na Mungu hana sehemu wala jamii inayowazunguka. Kimsingi hakuna mtu afanikiwaye yeye peke yake kwa juhudu zake binafsi, pasipo ridhaa ya Mungu, na pasipo mikono ya watu wengine kuhusika kwa njia moja au nyingine. Hata kama maono, mipango na mikakati ya utekelezaji imebuniwa na mtu mmoja; bado ufanisi wake lazima hujumuisha wengi hata kama waliohusika walifanya hivyo kwa malipo.

Aidha, ni upumbavu wa hali ya juu, pale ambapo mtu afikiapo mafanikio ya kiuchumi, kufikiri kwamba ataishi milele duniani ili kunufaika kibinafsi na utajiri aliojilimbikizia hapa duniani. Tunao ushahidi wa maelfu ya watu wengi ambao kwa muda fulani walifanikiwa katika kumiliki uchumi na kupata umaarufu lakinii ghafla wahusika wakatoweka ghafla kwa maradhi yaliyooshindikana kutibika japokuwa walikuwa na mali nyingi. Mali zile hazikuwasaidia kudhibiti na kurefusha maisha yao, wakaondoka pasipo kutaka.
Kana kwamba hii haitoshi, watu wengi waliojilimbikizia mali nyingi, wanapoondoka ghafla haichukui muda mrefu hata na mali zile walizohifadhi huangukia mikononi mwa watumiaji wasio na uchungu nazo, na kisha kutoweka na kubaki historia tu.
Matokeo haya, ya kujikinai na kuishia kupoteza heshima ni changamoto kwa jamii ya kizazi cha wanaofanikiwa katika karne hii ya ishirini na moja. Katika toleo lijalo tutapitia kwa kina matumizi mabaya ya mali na utajiri na athari zake kwa wahusika pamoja na jamii kwa jumla.

Itaendelea toleo lijalo,