YESU NI JIBU

Ijumaa, 28 Agosti 2015

VIONGOZI WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KANDA YA KASKAZINI WAWAONYA VIONGOZI WA DINI KUTORUHUSU VIONGOZI WA SIASA KUTOTUMIA MADHABAHU KUNADI SIASA BADALA WASISITIZE AMANI KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA OCTOBA MWAKA HUU.

Viongozi wa dini hapa nchini wametakiwa kutoruhusu wanasiasa kuyatumia madhabahu yao na nyumba za ibada kuzungumzia mambo ya kisiasa katika wakati huu wa uchaguzi ili kuilinda amani hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la wakristo hapa nchini na  Askofu wa kanisa la Aglikana la mt.Kilimanjaro Stanley Hotay kwenye kongamano la mbegu ya amani Tanzania  lililofanyika jijini hapa na kuwashirikisha viongozi wa madhehebu ya kikristo kanda ya kaskazini.

Alisema kuwa mimbari zetu zisitumiwe kinyume cha sheria kwa kuwaelekeza waumini wao kuhusu mgombea ama chama cha siasa cha kukichagua wao wapewe uhuru wa kufanya maamuzi yao ni yupi wa kumpa kura zao kwa kuwa wanasiasa hao wote ni waumini wao.
Aliwataka viongozi hao wa dini kukataa rushwa za pesa,na bakshishi zingine kwa ahadi ya kulindwa na kupewa nyadhifa za kuteuliwa iwapo wanasiasa hao watapata nafasi hilo ni suala la kuliepuka kabisa.

Alhamisi, 27 Agosti 2015

ASKOFU MKUU WA WAPO MISSION INTERNATIONAL ASKOFU SYLVESTER GAMANYWA ATANGAZA MSIMAMO WAKE KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK.


Askofu Mwizarubi akiwa na askofu Gamanywa kwenye mkutano wa injili Arusha.
askofu Kazio waWAPO Mission Mbeya akiwa na askofu Gamanywa kwenye mkutano wa injili Mbeya
Kufuatia vuguvugu kubwa la kisiasa ambalo limeyakumba hata madhehebu ya dini, nimeamua kutangaza msimamo wangu kwa mambo ambayo nimeamua kuyapa kipaumbele ambayo ni haya yafuatayo:
1. Nitaendelea kuhubiri Injili ya ufalme wa Yesu Kristo ili kuendeleza kampeni ya usajili wa majina mapya kwenye kitabu cha uzima

2. Nitaombea na kuhamasisha amani na utulivu katika jamii hususan pale nitakapoona viashiria vya kuvunjika amani vinaingilia uhuru wangu wa kutoa huduma za kiinjili kwa walengwa
3. Kuanzia Mwezi wa Septemba nakwenda shambani kulima maharage, nyanya na matikiti na Mwezi wa Novemba nitakuwa navuna mazao yangu nikauze na kupata fedha za kuendesha huduma na maisha!
Natekeleza mithali isemayo: " ndugu wakigombana shika jembe ukalime; wakipatana chukua kapu ukavune"
Baada ya tarehe 25/10/2015 na 30/11/2015 tutawasiliana kwa ajili ya kufanya tathmini kuhusu matokeo ya nani kashinda na nani kashindwa!
Kwa hiyo kuanzia sasa mtu yeyote asinitaabishe na mambo ya siasa kabisaa!

Jumanne, 25 Agosti 2015

AMA KWELI MUNGU ALIONEKANA KWA NAMNA YA KIPEKEE KATIKA MKUTANO WA SIKU TATU MKOANI ARUSHA AMBAPO WENGI WALIFUNGULIWA NA KUMPOKEA BWANA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAO.

Ni kwanini mpaka sasa wanadamu wanaendelea kuteseka na na kubaki utumwani.
unaweza ukajiuliza katika maisha yako juu ya suala la kuwa utumwani kiuchumi,ufukara, kiafya na hata katika dhambi
hapa askofu mkuu wa wapo mission international askofu Sylvester Gamanywa alifafanua kwa kina juu ya suala la kukombolewa ambapo amesema vyama vya siasa na dini hajaweza kuleta msaada wowote kwa wanadamu.
Askofu Gamanywa amefafanua kwa umakini juu ya aina mbili za roho ambazo zipo ulimwenguni nazo ni roho zilizo kufa na roho zilizo hai ndani ya kristo.
Aidha ameongeza kuwa kuwa watu wote wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji na wachawi wamekufa ingali bado wanatembea.

Askofu mkuu wa WAPO Mission International askofu Gamanywa akimtambulisha mke wake Alhappyness ndani ya kanisa la EAGT Sinai Unga limited Arusha.

Mara baada ya kutoka ibadani askofu gamanywa akimshukuru mke wa askofu Leonard Mwizarubi.

Askofu Mwibarubi kushoto akiongozana na askofu Gamanywa mara baada ya kutoka ofisini kwake maeneo ya kanisani.
Katika viwanja vya sheikh Abedi Amni Karume askofu Gamanywa na askofu mwizarubi.

Askofu Gamanywa akiwaongoza watu waliotoa maisha yao kwa Yesu katika sala .

Watu waliosalimisha maisha yao kwa Yesu.





Ndani ya kanisa kusifu na kumwabudu Mungu kila mmoja anafurahia huku wazee wa kanisa na washirika nao wakifuatilia kwa maini ibada. 


Mara baada ya kusifu na kuabudu zoezi la shukrani ndani ya kanisa la EAGT ambapo askofu Mwizarubi na familia yake walimshukuru Mungu kwa binti yao kufunga ndoa na kuolewa kwa heshima.


Zoezi la kuwapongeza waliotoa maisha yao kwa bwana Yesu Kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao.




kilichofuata kabala ya askofu Gamanywa kupata nafasi ya kfundisha neno la MUNGU ndani ya kanisa ni zoezi la kutangaza uchumba mambo yalikuwa hivyo kama unavyoona katika picha ni hatari kama ndiyo harusi tayari kumbe ni uchumba tu

Moja kwa moja uwanjani hapo ni mwimbaji wa nyimbo za injili Belgano Bukuku akiimba wimbo wake wenye ujumbe ni Mzuri Bwana Yesu.
Alhappyness Gamanywa kulia akiwa na Edina Malissa wakati wa kusifu Mungu katika mkutano wa injili ndani ya viwanja vya sheikh Abedi Amani Karume.






Timu ya kusifu na kuabudu inayoongozwa na Abednego ikiongoza zoaezi na kumsifu MUNGU.
Hata hivyo askofu Gamanywa kawasihi watanzania kuwa makini na kuanza kumiliki na kuachana na njia za udanganyifu ambazo adui shetani anatumia kuwarubuni na kuwapoteza matokeo yake wanakuwa wakiwa masikini kutokana na maradhi,yanayosababishwa na kutokumtii Mungu wa kweli.

Ijumaa, 21 Agosti 2015

ASKOFU GAMANYWA ANGURUMA KATIKA VIWANJA VYA SHEIKH ABEDI AMANI KARUME JIJINI ARUSHA KATIKA MKUTANO WA INJILI.


Kamanda Liberatus Sababas.
Watanzania wameaswa kuwa makini sana katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu maana mara nyingi uchaguzi ndiyo chanzo cha mfarakano na ukosefu wa amani katika baadhi ya mataifa ambayo uchaguzi ulifanyika na kusababisha machafuko.
Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusaha Reberatus Sababas wakati wa ufunguzi wa mkutano wa injili wa siku tatu ambao unafanyika katika viwanja vya Sheikh Abedi Amani Karume jijini Arusha.
Aidha Kamanda Sababas Amesema kuwa chaguzi ndiyo chanzo cha wananchi kuwa wakimbizi na kupoteza haki zao za msingi kutokana na uchaguzi kutokuwa wa haki na uhuru.
 Ameongeza kuwa watanzania wakiwa wanamcha Mungu hatakuwepo mtu ambaye atamtendea mwenzake jambo baya hasa pale ambapo watakuwa wamejazwa na roho mtakatifu katika maisha yao.
Hata hivyo amewasihi watanzania kulinda amani ambayo ni tuni ta Taifa la Tanzania na kusema kila mmoja popote atakapo kwenda awe balozi wa Amani.

 Kamanda Sababas akihutubia katika viwanja vya Sheikh Abed Amani Karume.
 Askofu Mwizarube wa kanisa la EAGT unga limited akisisitiza jambo katika mkutano wa injili.
 Kamanda Sababas Akiwa na Askofu Gamanywa.
 Kamanda Sababas akiwa na Askofu Mwizarube.
 Askofu Gamanywa akisisitiza jambo mara baada ya kamanda Sababas kumaliza kuhutubia mkutano.



Zoezi la maombi linaanza mara baada ya kamanda kuwasihi maaskofu na wachungaji pamoja na waumini wao kuombea amani wakati wa uchaguzi. 
 Askofu Gamanywa akishikana mikono  na kamanda Sababas. 
 Kamanda Sababas Akiwa na askofu Gamanywa katikati na kulia askofu Mwizarube.

Kulia ni mke wa askofu Gamanywa Alhappness Gamanywa akiwa na askofu Mwizarbi na mke wake.