YESU NI JIBU

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

ASSA WAFANYA MAHAFALI KATIKA SHULE YA BROTHERS ACADEMY NA KUHUDHURIWA NA WATU MBALIMBALI


 kutoka kushoto ni mkuu wa idara ya elimu masafa katika taasisi ya elimu ya watu wazima wakiwa na mkurugenzi wa Brothers Academy katikati na kulia ni makamu mkuu wa shule ya hiyo Kelvin Oguta wakiwa katika mahafali.

 Mkuu wa idara ya Elimu mmasafa Taasisi ya watu wazima ndugu Baraka Kionywaki akizungumza katika mahafali ya ASSA katika shule ya Brothers Academy iliyopo Banana jijini Dar es salaam.



 Mkurugenzi wa BROFOA akizungumza katika mahafali ya ASSA katika shule hiyo iliyoko Banana jijini Dar es salaam


 Mkurugenzi wa Brothers Academy akimlisha keki mmoja wa wanafunzi wa ASSA katika shule ya Brothers Academy
Vijana wa Brothers  Academy wa Adventist secondary student association ASSA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti.


Na Stelius Sane,
Wanaomiliki vituo vya kutolea elimu isiyo katika mfumo rasmi wameaswa kusajili vituo hivyo kwa lengo la kutoa elimu bora na kutambuliwa na serikali maana kuendesha shughuli ya kutoa elimu bila kusajiliwa na serikali ni kinyume cha sheria.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa idara ya elimu masafa taasisi ya elimu ya watu wazima ndugu Baraka Kionywaki wakati akizungumza katika mahafali ya Adventist secondary student association iliyofanyika katika shule ya Brothers academy iliyoko Banana jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika mahafali hayo amesema kuwa kazi kubwa ya shule na vituo vinavtyotoa elimu ya sekondati ya miaka miwili katika mfumo usio rasmi ni toa elimu kwa akushirikiana na serikali katika jitihada ya  kutoa elimu huria kwa watanzania .
Aidha aliongeza kuwa serikali ilitoa maagizo mwaka 2013 ya kusajiliwa kwa vituo vyote vinavyotoa elimu ya mfumo usio rasmi ili kupatiwa namba ya usajili na taasisi ya elimu ya watu wazima ndiyo iliyo pewa mamlaka ya kufuatilia ubora wa elimu inayotolewa na vituo hivyo na kutokana na hilo kituo cha brothers Academy ilimepewa usajili wa kutoa elimu kwa jamii katika mfumo usio rasmi yaani Qualified Test(QT).
Alisisitiza kuwa ni vyema vituo vyote vinavyotoa elimu katika mfumo huo visajiliwe na kutambuliwa na serikali  ili kuweza kutoa elimu ili serikali ikague na kuruhusu kutumika maana elimu inayotakiwa kutolewa kwa watanzania kuwa ni elimu bora.
Kwa upande wa shule ama kituo cha brothers Academy ndugu Kionywaki alisema kuwa ni moja ya shule ambayo imesajiliwa chini ya elimu ya watu wazima na imekuwa ikifanya vizuri katika vituo vilivyotambulika na serikali kutokana na kuwa na walimu waliopata elimu ya juu kutoka  katika vyuo vikuu vya ualimu vinatambuliwa na serikali.
"Brothers Academy ni moja ya shule ambayo imefanya vizuri katika mitihani ya maarifa na katika mkoa wa Dar es salaamu imekuwa ni shule ya kwanza na katika shule bora tano Tanzania zinazotoa elimu katika mfumo usio rasmi ni mojawapo hivyo inafanya vizuri sana",aliema ndugu Kionywaki.
Hata hivyo alitoa wito kwa wadau wote wanaotoa elimu katika mfumo usio rasmi nchi nzima kufuata utaratibu ambayo umetolewa na serikali wa usajili ili kutoa elimu bila tatizo lolote maana serikali inaunga mkono mfumo wa utoaji wa elimu katika mfumo huo.
Na amesema kuwa ikiwa wadau hao watashindwa kufuata taratibu ambazo zimewekwa na serikali basi sheria itafuata mkondo wake maana elimu inatakiwa elimu bora kwa watanzania na sio bora elimu kwa sababu ya tamaa ya fedha.
Naye mzee wa kanis la waadvetisti Mzee Kasaja amesema kuwa maadaili ndiyo njia pekee inayosaidia mwanafunzi kufanya vizuri pale aatakapoamua kufuata na kuachana na njia ambazo hazimpendezi Mungu.
Aliongeza kuwa wadau wa elimu wanaotoa elimu kwa jamii katika mfumo usio rasmi kwa ujumla inasaidia kupunguza uhalifu mitaani maana vijana wengi watakuwa wanajishugulisha na masuala ya kupata elimu tofauti na kukaa bure mtaani.
Kwa upande wa mkurugenzi wa shule ya Brothers Academy ndugu Robart Rwezaura alisema kuwa wanaendesha huduma ya kutoa elimu katima mfumo usio rasmi,elimu huria kwa lengo la kuhakikisha kuwa watanzania wanapata elimu bora itakayowasaidia kufanya vizuri katika maisha yao.
Alisisitiza kuwa chanzo cha mafanikio kwa kila mwanafunzi anayesoma hapo Brothers ni kumcha na kumtanguliza Mungu katika maisha yao na ndiyo maana wamewaruhusu wanafunzi kumtafuta Mungu katika maisha yao ya kila siku.
Ndugu Rwezaura ameongeza kuwa wao hapo kituoni wanawalimu waliohitimi katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali na hao wanawasaidia wanafunzi kwa kuwafundisha na pia hiyo inachangia sana wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao.
Hata hivyo hakuwa nyuma kuelezea suala la maadili katika shule yao kuwa kwa asilimia kubwa mwanafunzi akiwa namaadili mema ni rahisi kusaidika na kuelekezeka na njia hiyo kuwasaidia kufikia malengo yao ya kupata elimu bora.
Shule ya Brothers Academy inapatikana maeneo ya Banana jijini Dar es salam kw amawasiliano ya namba 0717280669, 076780669  na 078780669

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni