YESU NI JIBU

Jumatatu, 14 Januari 2013

WANAWAKE WATUMISHI WAMTEMBELEA MAMA SIMBA NYUMBANI KWAKE

Ukimtumikia Mungu kwa uaminifu lazima utavuna baraka za kazi uliyofanya ya kumtumikia Mungu kwa uaminifu na hayo yote yamethihirika mara baada ya chama cha wanawake watumishi kuamua kumtembelea aliyekuwa mkurugenzi wa wanawake watumishi jimbo la Temeke Claudian Simba nyumbani kwake.

Wakizungumza nyumbani hapo wanawake hao watumishi wakiongozwa na kaimu mkurugenzi wa sasa na katibu akishirikiana na mweka hazina wamesema kuwa mama simba amekuwa ni mfano mkubwa wa kuigwa na wanawake wote wa jimbo la Temeke na katika majimbo mengine.

Aidha akizungumza na mwaandishi wa habari hizi makamu mkurugezi Mrs Salome Chissolo amesema kuwa mama Simba ni hazina kubwa ambaye ni lazima jimbo la temeke liweze kumtumia kwa faida ya jjimbo kwani tayari yeye ana mambo mengi ambayo kwa sasa anayafahamu.
Pamoja na hayo alisema kuwa jimbo hilo linamhitaji kwa lengo la kuwa mshauri wa chma hicho cha wanawake watumishi wa kristo ili waweze kufikia malengo yao ambayo tayari walishajiwekea wakati mama Simba ni mkurugenzi wa jimbo hilo la Temeke.

 Naye katibu Mrs Grace  Kazoka ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mtoni Kijichi alisema kuwa anamfahamu mama Simba kwa muda mrefu na wakati wa uongozi wake alijifunza mambo mengi kutoka kwake hivyo amedai kuwa maono na miksksti sliyokuwa ameweka mama Simba wanatekeleza moja baada ya nyingine




 kutoko kushotowa kwanza ni kamweka hazuba na chama cha WWI Mrs Carolyne Kilango wa poli ni kaimu mkurugenzi Mrs Salome Chissolo mwenye taji ni mama Simba  pamoja na katibu wa WWi Mrs Grace Kazoka wakiwa pamoja na mama Simba walipomtembelea nyumbani kwake maeneo ya Madafu huko Gongo la Mboto jijini Dar es saalam





 Viongozi wa WWI wakimkabidhi  mama Simba risiti ya zawadi waliyomnunulia walipokuwa nyumbani kwake






 Hivyi ndivyo walivyoonekana wakinamama wakicheza kwa furaha  nymbani kwa mama Simba