YESU NI JIBU

Ijumaa, 14 Desemba 2012

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI MAGIDA AKIZUNGUMZA JAMBO NA MHE.RAIS JAKAYA KIKWETE

Madiga Timotheo ni mmoja wa waimbaji wa nyimbo za injili wa hapa nchini Tanzania,amekuwa akishirikiana na jeshi la polisi katika kuhamasisha juu ya ulinzi shirikishi ambayo imekuwa ikisaidia sana kuwafichua wahalifu mbalimbali.
Amekuwa pia akihudumu kwenye makongamano mbalimbali ya injili katika sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzania akitumika kueneza injili ya Yesu na pia amekuwa akishiriki shughuli mbalimbali za kiserikali.na pia unaweza kuwasiliana naye kwa shughuli mbalimbali kama mikutano ya injili semina tumia namba  0752187043 na 0714267875.

Jumapili, 9 Desemba 2012

Hatuwezi kuzuia mfumuko wa “imani Potofu” hata kama zina madhara kiimani




Tafsiri mpya ya msamiati wa “Imani potofu”

Siku hizi jamii imeanza kuchanganyikiwa na kile kinachoitwa “kuongezeka kwa imani potofu” zenye kudanganya na kuathiri imani za wengi kiitikadi.
Kutokana na uchunguzi wangu binafsi, nimekuja kubaini kwamba, mahali tulipofikia kumbe tafsiri yake ina utata mkubwa na maana nyingi tena tofauti hata kama matamshi ni yale yale. Ninachotaka kuelezea hapa ni kwamba, kila inayoitwa “imani potofu” na wengine, kumbe nayo inaziona imani nyingine nje yake ndizo zimepotoka! Kwa maelezo mengine, tumefikia mahali ambapo “Usahihi” wa imani yako ni “upotofu” wa imani kwa mwingine aliye tofauti na wewe kiitikadi. 
Ni kutokana na utata huu, Mamlaka za nchi mbali mbali duniani zilifikia hatua za ama kupiga marufuku “imani zote” na kubakia dini moja au chache zinazokubalika. Kisha baadaye ikaonekana huu ni udikteta usiotenda haki kwa binadamu  na hivyo likaanzishwa “Tamko la Haki za binadamu ulimwenguni” ambalo pamoja na mambo mengine limejumuisha “haki ya kuabudu” na kujiunga au kubadili dini. Kwa mujibu wa tamko hili fursa imetolewa kuwepo kwa imani nyingi, zilizopo hivi sasa, na kuanzishwa mpya, ili mradi mtu havunji sheria za nchi
Kwa kupitia haki ya uhuru wa kueneza imani, kila mtu anapata fursa ya kuchagua au kuacha, kujitenga au kujiunga na imani ile ambayo anaiona ndiyo sahihi kwa uelewa na utashi wake binafsi. Kwetu sisi Tanzania, uhuru wa kuabudu ni haki ya kikatiba.
Baada ya kutoa maelezo ya msingi kuhusu utata wa tafsiri ya “Imani potofu”; naomba sasa nije kwenye kuwasilisha tafsiri mpya ya msamiati wa “Imani potofu”. Tafsiri hii kwa hivi sasa ndiyo inayotumika na sehemu kubwa ya jamii. Tafsiri yenyewe ni kama ifuatavyo:
 “imani yoyote inayokera imani nyingine; na inapata umaarufu mkubwa kiasi cha kuwa tishio la kuvutia wafuasi wa imani nyingine kujiunga nayo”
Imani hiyo inaweza kuwa ni sahihi au potofu kulingana na mtazamo wa kila mtu kwa itikadi yake, lakini kigezo kinachozingatiwa katika kuibatiza jina la “Imani potofu”; ni pale ambapo “wafuasi wengi wa imani za dini nyingine wanaondoka au kuyahama madhehebu yao na kujiunga na imani hiyo” ! Katika harakati za kujaribu kudhibiti matishio ya imani hiyo, na kuwakinga waumini wao wasijiunge nayo ni kuitangaza rasmi kuwa ni “imani potofu”
Naomba nijihami mapema msomaji kwa kusema kwamba, kwa kusema haya sina nia ya kuhalalisha “Imani potofu” kupitia mada hii. Naomba nisieleweke kwamba sio kila “imani inayoshawishi maelefu ya watu kujiunga nayo ni sahihi au ni potofu”.
Hoja ninayotaka kuiweka bayana ni kuhoji uhalali wa matumizi ya kigezo cha “ushawishi na umaarufu mkubwa” kutafsiriwa kuwa imani husika ni potofu kwa sababu hiyo tu! Ingelikuwa kigezo hiki kina mantiki, basi tungeweza kutilia mashaka imani zote zenye wafuasi wengi kuwa zimefanikiwa kwa sababu nazo ni “imani potofu”!
Mtazamo wangu, na uzoefu wangu binafsi, imani zote, ziwe potofu au sahihi, ziwe mpya au za zamani, zote zikiweka bidii kikamilifu katika kujieneza kwa jamii zinaweza kuwa na wafuasi wengine pasipo kujali sana usahihi au upotofu wake kiitikadi. Lakini naweza kukubali kwa sehemu kwamba usahihi au upotofu wa imani unaweza kuchangia kwa kiasi fulani kufuatwa na wafuasi wengine kwa kutegemea ni mbinu gani ya kimawasiliano inayotumika.



Dhana ya imani potofu kuwa na
wafuasi wengi kuliko imani sahihi

Baada ya kuelezea tafsiri ya msamiati wa imani potofu kwamba ni ushawishi na umaarufu wa kupata wafuasi wengi kwa haraka; na baada ya kubainisha waziwazi kwamba nia ni kujaribu kuwakinga waamini wasihame na kujiunga na imani inayovuma kwa wakati husika; sasa nije kwenye chimbuko la tafsiri hii iliyoshika hatamu katika jamii.
Kwa karne nyingi imekuwepo dhana kwamba, imani potofu ina uwezo wa kuwa na wafuasi wengi kwa sababu zimetokana na Shetani mwenyewe. Tena yapo na maandiko yatumikayo katika kusimamia dhana hii ua kwamba hata Yesu mwenyewe alitabiri juu ya manabii wa uongo ambayo watadanganya wengi. (Math…….) Maandiko mengine ni ya mitume akina Petro na Paulo yaliyolitahadharisha kanisa kwamba watakuwepo mitume na manabii wa uongo ambao watatengeneza wafuasi wengi kwa ushawishi na udanganyifu wao.
Kwanza kabisa, naomba kuthibitisha kwamba ni kweli imani potofu zinapata wafuasi wengi kwa sababu zimejaa udanganyifu wa Shetani. Tena naweza kuongezea uzito katika hoja hii kwa kusema kwamba, kinachofanya imani potofu kupata wafuasi wengi ni kwa sababu hazina masharti yenye maadili ya kiungu, na zimejaa uwashiwi unaohamasisha tamaa binafsi au wanaotafuta msaada binafsi.
Lakini, ninapenda kuzungumuzia udhaifu wa dhana hii. Sio kweli hata kidogo kwamba, imani sahihi haipati wafuasi wengi kwa sababu yenyewe ndiyo imetokana na Mungu wa kweli. Ingelikuwa hii ndiyo maana sahihi, basi Yesu Kristo mwenyewe, enzi za mwili wake duniani, asingefuatwa na makumi elfu ya wafuasi wengi! Maneno yake na mafundisho yake yalikuwa magumu na mifano mingi ilikuwa na mafumbo lakini bado umati mkubwa wa watu ulimfuata na kumsikiliza na kushuhudia kwamba huyu ni Mwalimu kweli kweli!
Kana kwamba hii haitoshi, baada ya kufufuka na kupaa kwake, mitume wake nao walitengeneza maelfu ya wafuasi na wanafunzi wengi kama ilivyokuwa nyakati za Yesu mwenyewe. Kanisa la kwanza lilianza kwa kishindo cha wafuasi 3000 kwa siku moja na katika muda wa miaka 40 mfululizo lilikuwa na wafuasi wasiopungua 30,000 wanaokusanyika kwa wiki jijini Yerusalemu!
Ni nini ninachotaka kusema hapa? Napenda kuweka bayana ukweli huu, kwamba hata “Imani sahihi katika Kristo”, kama kweli kweli ikihubiriwa kwa usahihi kama Yesu na mitume wake wa kwanza; kazi zile zile zilizofanyika enzi za karne ya kwanza pia zitatendeka hata sasa. Kwa matokeo hayo makumi elfu ya watu wataikimbilia imani hii kwa wingi kama ilivyokuwa karne ya kwanza.
 Pamoja na ukweli kwamba “Imani potofu” zina ushawishi wa kupata wafuasi wengi; lakini sio kwamba hao wafuasi wenyewe hutoka kwenye imani sahihi na kisha kuijunga na imani potofu! Wengi wao hawakuwahi hata kuijua “imani sahihi” tangu kuzaliwa kwao na ndio maana ni rahisi kwao kujiunga na imani nyingine potofu!
Kwanini imani potofu zimeruhusiwa
kuwepo sambamba na imani sahihi?

Kitu ambacho kinatatiza watu wengi na hasa wale ambao ni wapenzi wa imani sahihi, ni kuona jinsi ambavyo imani potofu zinaendelea kufumuka na kuendelea kupoteza wafuasi wengine wasioijua au kuwa na imani sahihi. Wengine wanafunga na kuomba wakijaribu kudhibiti ongezeko la imani potofu. Hata hivyo, ukweli halisi bado imani potofu zinaongezeka kila siku.

Ningependa kujibu swali hili gumu kwanza kwa kutahadharisha athari zitokanazo na shinikizo la kutumia nguvu za dola kudhibiti imani potofu. Kujaribu kudhibiti mfumuko wa imani potofu kupitia nguvu za Dola, kwanza ni kinyume cha katiba na tamko la haki za binadamu. Pili, kila itikadi katika dini inatafsriwa kuwa potofu na itikadi nyingine zinazotofautiana kiitikadi. Tatu nitalieleza kwa mujibu wa mafundisho ya Bwana Yesu Kristo. Kabla sijaanza kufafanua hebu tuyasome maneno ya Yesu kwa mfano alioutoa:


“Akawatolea mfano mwingine, akisema, ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, basi wataka twende tuyakusanye? Akasema la; msije mkakusanya magugu na kuzing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.” (Math.13:24-30)



KANISA LACHOMWA MARA TATU MARA TATU LIKIKARABATIWA HUCHOMWA TENA WAHUSIKA WADAIWA NI WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU




Wakati serikali ikijitahidi kukabiliana na vitendo vya uchomaji moto makanisa nchini vinavyofanywa na baadhi ya wanaharakati wa Kiislamu, imebainika kuwa Kanisa la Salvation Ministry for all Nations (SMAN) lililoko Mbezi Juu Jijini Dar es Salaam, limechomwa moto zaidi ya mara tatu.
Uongozi wa Kanisa hilo umelimbia Gazeti hili kuwa licha ya matukio hayo ya hujuma wanazofanyiwa na waumini wa Kiislamu kutoka katika msikiti wa Al Mubarak ulioko jirani na Kanisa hilo, usiku wa Jumapili iliyopita ya Desemba 2, 2012 , waumini hao walilibomoa Kanisa hilo na kufanya jaribio jingine tena la kulichoma moto.
Kwa mujibu wa Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo la SMAN Freddy Mwamtembe na Msaidizi wake Mch. Eliya Sudi, matukio matano ya hujuma mbaya dhidi yao yameripotiwa katika vituo vya polisi Mbezi Juu na Kawe na kufunguliwa majalada   yanayoeleza jinsi hujuma hizo zilivyofanyika kwa muda na nyakati tofauti.
Hujuma ya kwanza ya uharibifu mali na uchomaji moto wa Kanisa hilo iliripotiwa katika akituo cha polisi Kawe Februari 25, 2012  na kufunguliwa jalada nambari KW/RB/1743/2012 la kuchoma moto  choo cha kanisa hilo, ambapo jalada la pili la siku hiyo hiyo lilifunguliwa katika kituo cha Polisi Mbezi Juu likiwa na nambari MBJ/RB/586/2012 likitaarifu juu ya tukio la kuchomwa moto Kanisa hilo na kuharibu mali majira ya saa saba usiku.
Jalada jingine lilifunguliwa Machi 10, 2012 katika kituo cha Polisi  Mbezi juu na kupewa nambari MBJ/RB/714/2012, likitoa taarifa juu ya hujuma ya kuchomwa moto kwa Kanisa hilo la SMAN.
Hujuma nyingine lililofanyiwa kanisa hilo imo katika jalada la kituo cha Polisi Kawe lenye nambari KW/RB/7974/2012 kama taarifa ya  tukio lililofanywa Agosti 12, 2012 na waumini 28  wa msikiti wa Al Mubarak kwa kuvamia ibada, kujeruhi waumini na kuharibu mali za Kanisa hilo, ambapo Mchungaji Msaidizi Eliya Sudi alijeruhiwa akiwa madhabahuni.
Aidha uongozi wa Kanisa hilo ulilikabidha gazeti hili waraka unaoelezea jinsi waumini wa msikiti huo wanavyoshirikiana na mama mmoja kulifanyia fujo kwa kufukia msingi wa jengo lake na kisha mama huyo kuchimba msingi na kuanza ujenzi wa nyuma yake katika kiwanja cha Kanisa hilo.
Uongozi huo wa Kanisa la SMAN  ulisema ulilifikisha suala hilo katika ofisi ya Serikali ya Mtaa wa  Ndumbwi kupitia mjumbe wa nyumba kumi shina namba 40  Mbezi Juu Bwana Bonifasi Matiku  kwa ajili ya utatuzi, lakini hawakupatiwa msaada wowote, hadi ikabidi wamwandike barua Afisa Mtendaji wa kata ya Mbezi Juu, kumtaarifu juu ya kiwanja cha kanisa lao kuvamia na mama huyo ambaye kwa sasa jina lake limehifadhiwa.
Mjumbe huyo alidhibitisha juu ya kuwepo kwa hujuma dhidi ya Kanisa hilo na hatua alizochukua,ambapo liitaka serikali kutumia sheria ili kukabiliana nazo na kuzikomesha.
“Nakumbuka siku nilipofika  ofisini kwa Mtendaji wa Kata ya Mbezi Juu,  niliishia kutukanwa na wajumbe niliowakuta pale (majina tumeyahifadhi kwa sasa), wakinieleza mbele ya Mtendaji huyo kwamba ni lazima mama huyo  atajenga katika eneo la kiwanja chetu cha Kanisa. Nilimtahadharisha Mtendaji juu ya matusi niliyotukanwa lakini akanitaka niondoke akidai atashughulikia suala hilo. Mwandishi  hadi leo hakuna kilichofanyika”, alisema Mchungaji Mwamtembe.
Alisema tayari amelifikisha suala la  hujuma za Waislamu dhidi ya Kanisa lake katika ofisi za Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni alikoahidiwa kushughulikiwa haraka kwa mujibu wa sheria.
“Kwa kweli sisi Wakristo ni wavumilivu sana kwa vile tunapenda amani na utakatifu. Tunaiomba sana serikali iwashughulike watu hawa wachache wasiopenda amani na wanaochochea vurugu za kidini. Ugomvi wa kidini ni mbaya sana. Tunaomba serikali iwe makini katika hili”, alisema Mch. Mwamtembe.
Alisema waumini hao korofi wa Kiislamu wanaolihujumu Kanisa lake kwa kulichoma moto, kuharibu mali na kujeruhi  washirika ni watu wanaofahamika wazi na hufanya hujuma hizo wazi wazi, wakitamka wazi  kuwa hawataki Kanisa katika maeneo yao; jambo ambalo ni kinyume kabisa na Katiba ya nchi  inayoruhusu uhuru wa kuabudu kwa kila mtu
Mmoja wa Mashehe wa Msikiti  wa Al Mubarak Mbezi Juu aliyetajwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha waumini wake kulihujumu kanisa  la SMAN, hakuweza kupatikana kutokana na kutofika msikitini hapo kwa uwazi, akiogopa kukamatwa na Polisi wanaomsaka.  
Aidha juhudi za kumpata mama aliyetajwa kushirikiana na waumini wa msikiti wa Al Mubarak kulihujumu kanisa hilo hazikuzaa matunda,  kutokana na makazi yake kutojulikana.


Jumatano, 31 Oktoba 2012

ELIMU YA UJASIRIAMALI NA USHAURI KUTOLEWA VIJANA NMA WAJANE NA TAASISI YA RUTH'S FAITH RFO



Elimu ya ujasiriamali na ushauri ni vyema ikatolewe kwa vijana na wajane ili kuweza kuwakwamua la tatizo la umaskini ambalo linawakabilisanjari na kuwafundisha neno la Mungu.
Kauli hiyo ilitolewa na jijini Dar es saalam naaskofu wa huduma ya Pentekoste Gospel Mission Askofu Barnabas Kimbe wakati wa uzindizi wa taasisi ya Ruth's Faifh Organization ambapo alisema kuwa ni vyema elimu ya ujasiria mali itolewe kwa vijana na wajane hasa itolewe kwa vitendo.
Aidha alisema kuwa katika nyumba ya Mungu kuna vipawa mbalombali na inastahili kutumiwa kwa lengo la kuujenga mwili wa kristona kuu shauri pia ili kuweza kuondokan na wimbi la umaskini ambalo linawakabili watu wengi kwa sasa.
Huduma hii ya RFO ni vyema zaidi ikaenea nchi nzima ili kuwakwamua vijana na wajane na wimbi la umaskini kwa kutoa elimu ya ujasiriamali itakayowasaidia.
Naye mwenyekiti wa taasisi ya Ruth's Faith mwalimu Claudia simba alisema kuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kuwasaidia ,kufundisha na kushauri vijana ambao wengi wao wamekosa washauri na kubaki kujiongoza wenyewe katika ujana wao hususani vijana wa kiume na watoto wa wachungaji.
Aidha Bi Simba alisema kuwa taasisi hiyo itakuwa ikitoa ushauri  katika maeneo ya mahusiano katika uchumba na ndoa kwa wazazi hususani wachungaji ambao ndoa zao zinalegalega na kutoa elimu kwa jamii hasa upande wa kukopa na kurejesha mikopo hiyo.
Kutokana hayo taasisi hiyo ilibaini kuwa ndani ya jamii kuna watu wengi wanaoweza kukopa na kushindwa kurudisha mikopo hiyo hivyo elimu itatolewa ya ujasiriamali ,utunzaji wa fedha na juu ya biashara kwa ujumlasambamba na kuwasaidia wajasiria mali hao kuwatafutia masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi ili waweze kujiendeleza katika shughuli zao bila kuwa na mashaka wapi watapeleka bidhaa zao wakisha tengeneza.
Hata hivyo itahusika kutoa ushauri kwa wake wa viongozi wa dini kwa kuwafundisha ujasiriamali na kujitegemea kuwatia moyo kufanya changizoili kuwawezesha kupata mitaji bila kubagua dini, dhehebu ,rangi jinsia ,utaifa na kabila.
Pamoja na hayo taasisi hiyo itahusika na jamii ya watu wenye ulemavu ,wajane ,yatima,watatoto wanoishi katika mazingira magumu kwa kuwapa nyenzo zitakazowasidia katika maisha yao.Taasisi hiyo ilianzisha juni mwaka 2011 ikiwa na maona hayo ya kusaidia jamii ila kutokana na kutokuwa na wafadhili ilikwama mpaka kufikia wakati huu.

MAOMBI YA KUHAMASISHA AMANI KATIKA TAIFA LA TANZANIA




MAOMBI YA KUHAMASISHA AMANI KATIKA TAIFA LA TANZANIA

Suala la amani na usalama ndani ya nchi ama taifa ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa unadumu sanjari na kumwomba Mungu juu ya jambo hilo.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es saalam na askofu Daktari Mgulu kilimba wa huduma ya christian mission Fellowship wakati wa ibada maalum yamaombi ya kuhamasisha amani nchini.
Aidha askofu DK Kilimba alisema neno la Mungu limetuagiza katika 1timotheo 2:1-2; kuwa kabla ya mambo yote nataka dua, sala, maombezi na shukurani vifanyike kwa watu wote; kwaajili ya Wafalme na wenye mamlaka, tuishi kwa utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu ,tukiwa Kanisa la Mungu, tumechukua hatua hii ya kuanza kuliombea Taifa kwa kuugua mno ili Amani  tuliyopewa na Mungu na kuenziwa na waasisi wa Taifa hili iweze kudumishwa.
"ndugu zangu watanzania sote tufahamu kuwa, msimamo tuliyojiwekea katika katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa tanzania, ni kupiga marufuku kila namna ya ubaguzi ukiwemo wa kijinsia, rangi na kidini. Katiba ya 1977 ibara 13(5) ambapo kwa upande wa madhehebu ya dini tanzania tuna dini kubwa tatu na nyingine ndogondogo dini kubwa ni ukristo, uislamu na dini za kijadi.toka mwanzo wakristo na waislamu tumekuwa tukishirikiana pamoja katika misiba, sherehe mbalimbali, kuoleana, kuishi katika nyumba moja  na kufanya shughuli za kijamii kwa pamoja bila kubaguana kabla na baada ya  miaka hamsini ya uhuru nchi yetu" alisema askofu dk kilimba .
Aliongeza kuwa wakristo na watanzania kwa ujumla ni vyema kufahamu kuwa, hakuna nchi  yeyote katika  bara la afrika yenye idadi kubwa ya wakristo na waislamu wanaoishi kwa amani na upendo  kama tanzania,ila kwa sasa watu wasioitakia amani nchi yetu wanataka kupenyeza chuki za kidini  ili isiwe nchi ya amani bali ya vurugu.
Kutokana na hayo hivi karibuni tumeshuhudia kuwepo kwa vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa kidini kwa baadhi ya vikundi toka makundi ya dini kubwa kudai haki zao ambazo kimsingi wanaona wanastahili kuwa nazo sawa na dini nyingine, hali hii imefanya vikundi hivi vitumie vyombo vya habari hususani redio, magazeti na machapisho mbalimbali kueleza hisia zao kwa jamii, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa mgawanyiko katika jamii iliyokuwa imeshikamana na mgawanyiko huu unazidi kukua siku hadi siku na kusababisha hali ya chuki kwa mamlaka ya nchi na hatimaye dini moja na nyingine.
"Baada ya kufanya utafiti wa kina kwanini kuwepo na chuki baina ya makundi ya dini na serikali tumeona kuwa, makundi haya ya dini yanaiona serikali inawanyima haki zao na inapendelea  dini moja na hivyo kutumia mfumo wake katika utawala, ambapo  madai ya kundi hilo yanawapelekea kuwafanyia vurugu waumini wa kundi wanalosadiki kuwa linapendelewa na serikali, jambo ambalo linawafanya wanaofanyiwa vurugu wasitumie  uhuru wao wakufanya ibada ambayo kimsingi walipewa mungu na kuandikwa katika katiba ya nchi yetu", aliongeza.
Pamoja na hayo tukiwa kanisa la mungu, hali hii inatupelekea kuona kuwa bado serikali yetu haijawajibika ipasavyo katika kuelekeza sera na shughuli zake kwa lengo la kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa, kimsingi haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma vinapaswa kutoathiriwa kabisa na  matumizi mabaya ya uhuru wa haki za watu binafsi.
Hivyo askofu Dk Kilimba aliongeza kusema kanisa baada ya kumlilia mungu kwa machozi na maombi mengi, tumeamua kuchukua mwelekeo wa uwajibikaji  usio wa maneno tu, kwani suala la  kutoa matamko ya kulaani limefanywa na dini na serikali kwa mkazo mkubwa. Na kwa upande wa serikali,  watawala wa nchi yetu wamekuwa wakilaani na kukemea, ubaguzi wa dini,  rushwa na ufisadi katika taifa hili bila mafanikio na hata leo tunawaona vijana wanatwangana hadharani kutokana na kushamili kwa rushwa ,hii yote ni kwa sababu  hayo ni vita ya kiroho na inapaswa kukemewa na viongozi wa dini na watawala wanapaswa kuchukua hatua. Kwa jinsi hii, kanisa limelitazama jambo hili kiroho zaidi kwa kutambua kuwa chuki na rushwa ni roho kamili inayotoka kwa shetani, hivyo watu wa kiroho tunalo jukumu la kuzipinga hila zote za shetani kwa dua, sala na maombi ili kuleta amani ya kudumu katika taifa letu, ambalo linasifika kuwa ndiyo kitovu cha amani afrika na duniani.
Akielezea kwa hisia alisema "Ndugu zangu wakristo na viongozi wa dini,  ikumbukwe na izingatiwe kuwa  nyumba za ibada ni sehemu ya kumwabudu mungu,  hivyo zitumike kuhubiri dini tuliyo amuriwa na mungu na sio siasa, na  pasiwe mahali  pa kuandaa na kuchochea vurugu na chuki miongoni mwetu kwani viongozi wa dini wanaaminiwa  sana na waumini wao na  lolote watakalo waambia waumini, huaminiwa kuwa limetoka kwa mungu".
Aidha aliongeza kuwa ikumbuke kuwa, tunafanya kila kitu vizuri zikiwemo ibada zetu kwasababu ya amani tuliyonayo, amani isipokuwepo hakuna kitu kinaweza kufanyika katika nchi iwe kwa waumini na wasio wauimini, iwe kwa maskini au matajiri. Amani ikishaondoka, matajiri au wenye pesa watakimbia na kuwa wakimbizi wa nchi zingine, huku masikini wakikosa mahali pa kwenda na kuishia kuuawa na kupoteza maisha. Kwa hiyo ni vema kuitunza amani yetu na kuilinda,kamwe tusiichezee amani tuliyonayo katika nchi yetu, hii ni tunu tuliyopewa na mungu na kuachiwa na waasisi wa nchi yetu ili tuienzi, hivyo kila mmoja wetu ni mdau wa amani. Mkulima anahitaji amani ili aweze kupata mazao shambani mwake; daktari anahitataji amani ili afanye kazi zake vema hospitalini, kadhalika mfanya biashara na mwanasiasa wote wanahitahi amani.
Pamoja na hayo yote askofu Dk Kilimba alisema kuwa kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya dar es saalamkwa ameonesha juhudi  zake za kuifanya Dar-es-saalam iendelee kuwa bandari ya amani, ameonesha ushupavu na umadhubuti mkubwa katika kauli zake, kwani mchango wake umeleta heshima iliyotukuka katika vyombo vya dola nchini  na kwa watanzania wote.
Katika maombi hayo ya kuhamasisha amani nchini yalitanguliwa na maombi ya watu 12 waliowakilisha zaidi makabila 120 ya tanzania kwa kutumia lugha  za makabila hayo kama alama ya umoja na mshikamano.

NAMNA YA KUMSIFU NA KUMWABUDU MUNGU--MWALIMU MGISA


Tumejifunza mambo mengi sana yaliyokuhamasisha na yaliyokupiga deni uwe
kiumbe wa kumsifu na kumtukuza Mungu. Tunapomsifu mtu, huwa
tunaelezea yale ambayo yanamtofautisha na wengine. Hivyo basi, ufikapo
katika muda wa kumsifu na kumwabudu Mungu, ujue namna ya kuifanya sifa
yako na ibada yako kwa usahihi.  
                   
Na ili kumpa Mungu sifa na ibada, ni lazima na ni muhimu sana ujue
mambo ambayo yanamstahilisha Mungu wetu kusifiwa na kutukuzwa. Kwa
kutumia sifa na tabia za Mungu, utaweza kumsifu na kumwabudu vizuri.
Hakuna kiumbe kingine chochote kinazo zile sifa kuu tano za Mungu,
isipokuwa yeye Mungu Jehova peke yake.  
                    
Kwahiyo, na hizo ndizo zinayomstahilisha yeye kusifiwa na viumbe
wake. Katika sura ya nane, tumeshajifunza mambo yanayomstahilisha Mungu
kupewa sifa. Kwakuwa sasa unayajua, basi tumia mambo hayo uendapo
mbele za Mungu katika katika ibada yako ili kumsifu na kumwabudu.
Unapomueleza Mungu sifa zake na tabia zake (vile alivyo) hapo unakuwa
unamsifu na kumwabudu.

Tofauti ya kusifu na kuabudu
Naomba urudie kuisoma sura ya kwanza ya kitabu hiki, ambapo nimefundisha
vizuri maana ya kumshukuru Mungu, kumsifu Mungu na kumwabudu Mungu.
Hii itakusaidia kutofautisha mambo haya kwa nia ya kuyaelewa au kuyaelezea
kwa mtu mwingine. Nilisema hivi,  
Ibaba ni kitendo cha mtu kumtukuza, kumhimidi, kumwinua, kumwadhimisha,
kumshukuru na kumheshimu Mungu kwa vile alivyo na kwa yale aliyoyatenda.
(Appreciation and admiration for who God is and for what He has done).
Lakini haya mambo matatu, yanayofanana sana na si rahisi sana
kuyatenganisha kimaelezo au kivitendo.
                
Lakini tuendapo mbele za Mungu kwa ibada, iwe ni chumbani kwako
au sebuleni kwako au kwenye gari lako au kanisani kwako, kusifu na kuabudu
na kushukuru, ni mambo yanayofanyika kwa kuingliana sana. Sio sheria
kwamba, hautakiwi kuchanganya sifa na kuabudu na kushukuru, hapana.
Hebu soma tena sura ya kwanza vizuri. Kati ya mengi, nilisema hivi;
                
Haya mambo matatu, kusifu, kushukuru na kuabudu, ni mambo
yanayofanana sana. Inaweza ikawa vigumu kidogo kuyatenganisha kimaelezo
au kivitendo. Ni ngumu kidogo, kufanya kimoja pasipo wenzake, kwasababu ni
mambo yanayokwenda kwa pamoja sana. Lakini kwa tafsiri zake, yako hivi;
1. Kumshukuru Mungu;‐  Ni ile hali ya kumueleza Mungu jinsi
tunavyothamini (Appreciate and Admire) wema wake, fadhili zake na
baraka zake katika maisha yetu.
2. Kumsifu Mungu;  ‐ Ni kumueleza Mungu juu ya matendo yake makuu
na ya ajabu aliyoyafanya. Au ni kuwaeleza wengine kuhusu matendo
makuu ya Mungu aliyoyafanya katika maisha yetu au kwa watu
wengine.
3. Kumwabudu Mungu; ‐ Ni kumueleza Mungu tukuzo zetu, heshima yetu
na upendo wetu kwake kwasababu ya uzuri wa tabia zake kwetu.
(Credentials and Characters).   
Kwahiyo, tuendapo mbele za Mungu kwa ibada, iwe ni chumbani kwako au
sebuleni kwako au kwenye gari lako au kanisani kwako, ili kumsifu na
kumwabudu na kumshukuru Mungu, uwe huru kujimimina mbele za Mungu
kwa kufanya vyote vitatu, kwa namna moyo wako utakavyokuwa unaongozwa
na Roho Mtakatifu. Vyote vitatu vinatengeneza ibada takatifu kwa Mungu.
                Katika sura inayokuja, nimefundisha vizuri namna ya kuingia katika
ibada na hata kupenya na kufika katika chumba cha ndani kabisa cha uwepo
na utukufu wa Mungu; ili unapokwenda mbele za Mungu wetu, uweze
kukutana na nguvu zake katika utukufu wake.  
                
 Lakini hapa chini nimeziweka kwa ufupi ili kukukumbusha. Na pia
nimekuongezea na mambo mengine yanayotakiwa katika kumsifu na
kumtukuza Mungu. Kwahiyo, utengapo muda wa kukaa mbele za Mungu wetu
kwa ibada, msifu na kumtukuza Mungu kwa mambo yafuatayo,
1. Mtukuze Mungu kwa Sifa zake za Uungu (ambazo hakuna mwingine
aliye nazo) Kwamba;
a) Jehova ni Mungu wa Milele
b) Jehova ni Mungu Mtakatifu
c) Jehova ni Mungu Aliye kila mahali
d) Jehova ni Mungu Anayejua mambo yote
e) Jehova ni Mungu Aliye na nguvu zote na    
      anaweza kufanya mambo yote kabisa.
Nimezielezea vizuri hizi sifa za Uungu, katika sura ya kwanza. Hizi ni baadhi tu
ya sifa za Mungu, sio zote. Kwa hivyo basi, pamoja na namna nyingine ambazo
utajifunza kumsifu na kumwabudu Mungu, hebu uwe unamsifu Mungu kwa
mambo haya au kwa sifa zake hizi pia.  
Msifu Mungu kwa;  
2. Kwasababu ya Tabia zake
3. Kwasababu ya Matendo yake ya Ajabu
4. Kwasababu ya Fadhili nyingi na kuu mno
5. Kwasababu ya Ahadi zake kubwa za thamani2.   Mtukuze Mungu  kwa Tabia zake
Neno la Mungu, linatuonyesha jinsi ambavyo Mungu wetu ana tabia na
kawaida nyingi nzuri ambazo kwa hizo, tunavutiwa na tunapigwa deni kumsifu
na kumwabudu. Kwa mfano ; Biblia inasema kwamba, Mungu wetu amejaa
Upendo, usio na mwisho. Ni Mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, sifa
yake ni kuwa na rehema daima. Soma mistari ifuatayo, ili uone zaidi. Lakini
kwasababu ya sifa hizi (Tabia zake), tunapigwa deni kumsifu na kumwabudu.
*Zaburi 103:8, Kutoka 34 :6,  
*Efeso 3 :18‐19, Daniel 9 :4, Ufunuo 19 :11
3. Mtukuze Mungu  kwa Matendo yake ya ajabu.
Mungu wetu ni Mungu aliyefanya mambo ambayo hakuna tena, awezaye
kufanya. Kwa mfano; ndiye aliyeziumba na kuzitundika sayari zote za
ulimwengu huu, bila minyororo wala nguzo. Mungu wetu ndiye
anayesababisha mioyo yetu inadunda, bile kuwekewa betrii wala chaji
(charge). Au ni lini ulichomeka moyo wako katika soketi ya umeme kama
unavyochomeka simu yako ili kupata umeme?
       
 Nina uhakika, hakuna mtu anayefanya hivyo. Sasa unadhani moyo
wako unadundaje? Hizo ni kazi za ajabu za Mungu wetu.na hakuna mtu
awezaye kuzifanya. Kwasababu ya matendo yake ya ajabu, Mungu wetu
anastahili kusifiwa na kutukuzwa. Soma mistari ifuatayo kwa umakini.
Utaweza kuona kwa uchache, jinsi maandiko yanavyoeleza juu ya matendo
makuu ya Mungu.  
Haya ni maelezo ya watu wa Mungu ambao kwa kumjua Mungu, waliweza
kueleza ukuu wake vizuri, ili na sisi tunaosoma maandiko yao, tunajifunza juu
ya ukuu wa Mungu, uweza wa Mungu na tabia za Mungu wetu. Soma vizuri
Kitabu cha Daniel 6:25‐27,  Nehemia 9:6,  Zaburi 147:1‐18,  na Zaburi sura ya
136:4‐26
4. Mtukuze Mungu  kwa Fadhili zake.
Mungu wetu ni Mungu atupaye baraka na fadhili nyingi kila siku. Fikiri wema
ambao Mungu amekufanyia maishani mwako, na hata katika siku ya leo tu.
Kuna vingi ametupa ambavyo wengi walitamani, lakini hawakupewa. Uhai,
afya, ulinzi, rehema, chakula, fedha, shule, simu, gari, nyumba, ajira, mke,
mume, watoto, na hata wazazi.
                  Sio kila mtu bado ana wazazi. Na wengine wamezaliwa hawajawahi
kuwajua wazazi wao. Kwakweli fadhili na baraka za Mungu ni nyingi sana;
ukiamua kuziorodhesha, utakesha. Sasa, kwa fadhili zote hizi alizotujalia, basi
Mungu wetu anstahili kusifiwa.
*Zaburi 103:1‐5,  Zaburi 107:21,  2Nyakati 20:21
5. Mtukuze Mungu  kwa Ahadi zake.
Ni Mungu aliyetuahidi watu wake, mambo mengi sana mazuri. Ametupa ahadi
kubwa mno na za thamani sana. Ni ahadi za kutupa baraka, heshima na utajiri.
Kwa ahadi hizi pia, anastahili kusifiwa * 2Petro 1:3‐4,  Efeso 1:3‐4,  Kumbu 4:4‐
      8  Kwa ufupi, hivi ndivyo unavyotakiwa kumsifu na kumwabudu Mungu.
Kadri unavyoanza kufanya hivi kwa vitendo, utaendelea kujifunza kufanya
huduma hii ipasavyo, nawe utajikuta unakutana na nguvu za Mungu kwa
namna ya tofauti maishani mwako.
                              MSIFU MUNGU KWA MAJINA YAKE.
Majina ya Mungu, hueleza sifa za Mungu, Tabia za Mungu au Matendo ya
Mungu. Mfano; Wayahudi wanamwita Mungu El‐Shaddai. Ni neno lenye
majina mawili ndani yake. ‘El’ maana yake Mungu, na ‘Shaddai’ lenye maana
itokanayo na neno ‘Shad’ yaani Titi (Ziwa) la mama anyonyeshaye.  
        Kutokana na ukweli kwamba, titi/ziwa la mama anyonyeshaye,
linampa mtoto mchanga kila kitu anchohitaji. Maziwa ya mama yake, humpa
mtoto kila kitu mtoto anachohitaji. Ndani ya maziwa kuna vitamini, protini,
wanga, mafuta, madini, maji, na kila kitu mtoto anachohitaji. Maziwa ya
mama, yanamtosheleza mtoto kwa kila kitu. Hivyo, Waisraeli wanapomwita
Mungu El‐Shaddai, wanamaanisha kuwa, kama ziwa linavyo mtosheleza
mtoto, vivyo hivyo, Mungu ni ‘Mtoshelezi’ kwetu. Halleluyah!
       Hivyo, kila jina la Mungu, linabeba aidha Sifa yake au Tabia yake au
Matendo yake. Ndio maana Mfalme Daudi anasema  
“Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu … Mpeni Bwana utukufu kwa
jina lake. Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.” (Zab 29:1‐
2) Msifuni Bwana kwa kuwa Bwana ni mwema, Liimbieni Jina
lake, kwakuwa lapendeza.(Zaburi 135:3).
Na Bwana Yesu alitufundisha kuanza sala namna hii;
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako tukutuzwe, hakafu Ufalme
wako uje hapa duniani.  
Kwahiyo, unaweza pia kumsifu Bwana kwa majina yake. Majina ya Mungu,
hueleza aidha sifa za Mungu au tabia za Mungu au Matendo makuu ya
Mungu. Yafuatayo hapa chini, ni baadhi ya majina ya Mungu kwa lugha ya
Kiebrania, yatakayokusaidia kumsifu, kumwabudu na kumshukuru Mungu.
                                   
                                           MAJINA YA MUNGU
   
       Jina la Mungu                 Maana yake       Mstari wa Biblia         
1. Adonai ‐ Mungu Mwenye enzi yote ‐ Mwa 15:2‐8, Kut 6:2‐32. El‐Ohim ‐  Mungu Muumbaji       ‐  Mwa 33:20, Kol 1:16‐17
3. El‐Elyon ‐  Mungu Aliye juu zaidi       ‐   Mwa14:18, Dan 4:34
4. El‐Gibbor  ‐ Mungu Mwenye Nguvu    ‐       Isa 9:6,  Zab 147:5
5. El‐Hai ‐  Mungu Aliye Hai/Anaishi   ‐  Josh 3:10,  1Sam17:26
6. El‐Olam ‐  Mungu wa Milele                 ‐  Ufu 4:8,  Kut 3:14
7. El‐Roi ‐  Mungu Aonaye kila kitu       ‐ Mith 15:3, Zab 32:8
8. El‐Shaddai ‐  Mungu Mtoshelezi      ‐  Mdo 17:28, Kumb 8:4
9. Jehovah ‐  Ajitegemeaye kuwepo ‐Kut 6:2‐8,  Mdo 17:24‐25
10. Jehovah Shalom    ‐Mungu Amani yetu           ‐ Amu 6:22‐24
11. Jehovah Rapha   ‐  Mungu Atuponyaye                ‐  Kut 15:26
12. Jehovah Jireh   ‐  Mungu Mtoaji wetu           ‐ Mwa 22: 8, 14
13. Jehovah Nissi  ‐  Mungu Ushindi wetu          ‐ Kut 14:13‐14  
14. Jehovah Saboath  ‐  Bwana wa Majeshi             ‐  Malaki 3:7  
15. Jehovah Shammah ‐  Bwana ni Aliyepo                  ‐  Kut 3:14  
16. Jehovah Rohi   ‐  Bwana  ni Mchungaji wangu   ‐  Zab 23:1
17. Jehovah Tsidkenu  ‐  Bwana ni Haki yetu              ‐  Yer 23:6
18. Jehovah Mekaddishem  ‐  Bwana Atutakasaye  ‐  Kut 31:13  
Namna  za  kumshukuru, kumsifu,  na  kumwabudu Mungu  wetu.
Kwahiyo, katika maisha yetu sisi, kama waumini, tunatakiwa kumpa Mungu
wetu ibada, (kumshukuru, kumsifu na kumwabudu) kwasababu ya mambo
yote hayo niliyoyataja. Tunatakiwa kumtukuza Mungu kwasababu ya sifa zake,
na kwasababu ya tabia zake, na matendo yake na fadhili zake na ahadi zake
kwetu.  
    
  Sasa basi, hapa chini, nimekuwekea njia kuu tatu ambazo unaweza
kumsifu na kumtukuza Mungu kwazo. Utengapo muda wa kwenda mbele za
Mungu, unaweza kutuia njiia kuu zifuatazo; Kumtukuza Mungu kwa,
1. Kumwimbia nyimbo za kumsifu na kuwabudu
2. Kumweleza au kusimulia kwa maneno
3. Kumtolea Mungu sadaka na dhabihu 
 
                                          Wako katika kazi ya Mungu
                                            Mwl. Mgisa Mtebe
                                           +255 713  497  654
                                      mgisamtebe@ yahoo.com
                                          www.mgisamtebe.org

Jumatano, 24 Oktoba 2012

KANISA LA KKKT KUFUNGA NA KUOMBA TAREHE 28 OCTOBA 2012 KUOMBEA AMANI TAIFA

Kufuatia matukio ya Uvunjifu wa Amani unaofanywa na kikundi cha watu wachache kwa mwamvuli wa "dini". Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa waraka elekezi wa wachungaji Wake Wote Tanzania kuelekeza kuifanya siku ya tarehe 28 Oktoba, 2012 kuwa ya Kufunga na Kuomba kwa ajili ya amani nchini.

KKKT linakuwa kanisa la kwanza Tanzania kupitisha siku ya kikanisa la kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya nchi ilivyo Sasa.

Blog hii ambayo imefanikiwa kuutia machoni waraka huo uliotumwa na Maaskofu Dayosisi zote KKKT Wakuu wa Vituo vya Kazi za Umoja, KKKT na nakala yake kutumwa manaibu katibu wakuu, wasaidizi wa Maaskofu, Dayosisi zote KKKT, makatibu wakuu dayosisi zote kuwaelekeza kwamba tarehe 28 Oktoba ni siku ya kufunga na kuomba. 
Waraka huo umeelekeza "Kufuatia matukio ya kuchoma Makanisa yaliyotokea hivi karibuni,barua  inawataarifu kuwa siku ya Jumapili tarehe28 Oktoba 2012 imepangwa kuwa siku maalum ya kuombea amani katika nchi yetu. Pamoja na mambo mengine yaliyokwisha kupangwa kufanyika siku hiyo (28 Oktoba 2012)' tafadhali sharika, mitaa na vituo vya kazi za umoja vyote vya Kanisa letu vifanye maombi  hayo"

Kwa mujibu wa barua hiyo ya mtendaji mkuu wa KKKT, inawataka waumini wa Kanisa hilo kuendelea kuhimizwa kufunga na kuomba kwa kadri Roho wa Bwana atakavyowaongoza kuombea amani ya Tanzania. 
Blog ikinukuu sehemu ya mwisho ya barua hiyo inaeleza kuwa "Baada ya maombi ya siku hiyo, washarika wahimizwe kuendelea kufunga na kuomba kadiri Roho wa Mungu atakavyowaongoza"

Ipo haja na kanisa la Tanzania kuungana pamoja na Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania katika kuombea amani ya nchi.
SamSasali.Blogspot.com

Ijumaa, 19 Oktoba 2012

KIKAO CHA MAASKOFU NA WACHUNGAJIWA UMOJA WA MAKANISA YA KIPENDEKOSTE MKOA WA DSM WALIPOKUSANYIKA KWENYE KIKAO

Maaskofu na wachungaji wameitaka serikali ichukue hatua madhubuti kutokomeza wimbi la uchomaji wa makanisa sambamba na uharibifu wa mali kwani hali hiyo inaweza kusababisha amani kupotea katika taifa hili la Tanzania
Kauli hiyo imetolewa na umoja wa makanisa ya kipentekoste kupitia kwa katibu wake jijini Daar es salaam ambao wamekutanika kutafuta ufumbuzi wa tatizo la uchomaji wa makanisa

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika kikao hicho askofu DAvid Mwasota ambaye ndiye katibi alisema kuwa kikao hicho kilikuwa na lengo la kutathimini uharibibu wa majengo na mali zingine za kanisa na jinsi ya kumaliza tatizo hili ambalo linaonekana kama ni endelevu


  Askofu Bruno Mwakibolwa ambaye ndiye mwenyekiti wa makanisa ya kipentekoste mkoa wa Dar es saala akimsikiliza kwa makini mchungaji ambaye kanisa lake liliharibiwa.

 Baadhi ya wachungaji pamoja na mbunge wa kigamboni mhe. Faustine Ndungulile wakitembelea makanisa ambayo yameharibiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni waislamu

 Mheshimiwa Ndugulile akizungumza na maaskofu na wachungaji kuendelea kuwa na uvumilivu kwa tatizo lililojitokeza
 Mwenyekiti waumoja wa makanisa ua kipentekoste mkoa wa Dar es salaam askofu Bruno Mwakibolwa akimwelezea mbunge jambo mhe. Ndugulile



hivyo divyo hali ilivyokuwa

Askofu John Zakaria jimbo la Kinondoni na askofu Bruno Mwakibolwa wa jimbo la Temeke wakimsikiliza  mbunge wa Kigamboni kwa makinisa Mhe.Faustine ndugulile.

 Katibu wa PCT askofu David Mwasota akielezea hali ilivyojitokeza juu ya suala la uchomaji wa makanisa


waandishi wakichukua habari baada ya kikao cha maaskofu na wachungaji waliofika kutathmini hasara na jinsi ya kutafutia ufumbuzi tatizo hilo



Hizi ni baadhi ya CD ambazo ni vielelezo ambazo viongozi hao walisema kuwa wamepeleka kwa viongozi wa serikali jinsi walivyokuwa wajipanga kuangamiza ama kuaharibu makanisa.

Alhamisi, 4 Oktoba 2012

Hatimaye ufumbuzi wa mafundi mitambo wa vitengo vya sauti umepatikana mara baada ya wakufunzi kutoka Afrika ya kusini kuwasili nchini na kuanza kuwafundisha ili kuweza kutafutia ufumbuzi tatizo hilo.

Wataalamu kutoka makanisa mbalimbali wamefika kujifunza jinsi ya kutatua tatizo hilo katika sehemu zao za kazi na wakufunzi hao wameletwa na HUDUMA VOICE OF HOPE MINISTRY.
Mafunzo hayo yalifanyika kwa muda wa siku mbili 28 na 29 septemba katika ukumbi  wa kanisa TAG Mwenge iliyopo Mwenge jijini Dar es saalam

 Mchungaji Gay kutoka Afrika ya kusini akiwa na mtafsiri wake ambaye alikuwa akifundisha somo katika semina ya siku mbili ya mafundi mitambo wa sauti na viongozi wa vikundi vya kusifu na kuabudu.

Mchungaji Gay akiwa na mke wake pamoja na mtaalamu wa sauti bwana Wesley ambaye yeye alikuwa akifundisha juu ya soun engineering kwa wataalamu mbalimbali waliofika katiak ukumbi wa kanisa la Mwenge kujifunza.

Mmoja wa wanafunzi waliofika kwenye Kongamano la mafundi mitambo akifuaatilia kwa makini akielekezwa na maalamu na pia ni mmoja wa waimbaji wa bendi ya Dar es saalam Goespel


Engineer Wesley akiwa na mtafsiri wake Mbuto wakati akitoa mafunzo juu ya vifaa vya sauti( sound system)

Waimbaji wa kikundi cha Messengers Band wakitumbuiza katika kongamano la mafundi mitambo.




Kiongozi wa Messengers Band ndugu Noel akiongoza katika kusifu na kuabudu katika kongamano.


Mmoja wa wapiga vyombo wa benbdi ya Messengers ndugu Waziri akionesha umahiri wake.




Ndug Gadrody Mng'anga mwenye shati blue pamoja na wanafunzi wenzake waliofika katika kongamano la mafundi mitambo.


Ni mafundi mitambo kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia kwa makini mafunzo ambaye yalitolewa na wataalamu kutoka Afrika ya Kusini.

Jumatano, 26 Septemba 2012

MCHUNGAJI MTIKILA ASHINDA KESI, ASEMA YESU AMEMJIBU MAOMBI YAKE.


Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.
Inadaiwa kuwa Oktoba 21 mwaka jana katika  maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi, dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.
Akizungumza na mtandao wa Global Publishers baada ya kushinda kesi hiyo, Mtikila amesema “Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu”.
Mara baada ya kushinda kesi hiyo lilizuka timbwili lingine baada ya mtu mmoja kujitokeza akiwa na RB (Report Book) akimtuhumu Mchungaji Mtikila kuwa alimtishia kumuua na ni mwizi wa viwanja. Baada ya kutaka kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye cheo cha Koplo, labda polisi mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of Police). Kwa kauli hiyo polisi alishindwa kumtia nguvuni.

MKUTANO MKUBWA ULIOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA KWEMBE JIJINI DAR ES SALAAM


MWINJILISTI BWA KIMATAIFA ANDULILE BWILE ALIKUWA AKIHUBIRI NENO LA MUNGU KATIKA MKUTANO WA SIKU SABA KWEMBE

Ni vyema kutii sheria bila shuruti imekuwa ni mojawapo ya njia yav kuwafundisha wananchi kutojichukulia sheria mkononi.
Mwinjilisti Andulile amesema ni vyema wananchi weakatii sheria na kuacha uovu na kumrudia Mungu na hiyo itasaidia sana katika maendeleo ya taifa 


Hapa mwinjilisti Andulile akifurahia jambo na wachungaji wenzake madhabahuni



Mwinjilisti Andulile akisoma neno la Mungu wakati akihubiri






Hapo ni maeneo ya kwembe ambapo Magida alikuwa mmoja wa waimbaji katika mkutano wa injili



Wacheza shoo wa kikundi cha Enock Jonath wakichekesha umati wa watu waliofika katika viwanja Kwembe kusikiliza neno la Mungu mara baada umeme kukatika wakati mkutano tayari umeanza




umati wa watu wakisikiliza neno la Mungu kwa makini likihubiriwa na mwinjilisti Andulile wakiwa na shauku ya kutaka kufahamu kwa undani neno la Mungu























MMOJA WA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AMBAYE AMEKUWA AKIMBA KATIKA MIKOA MBALIMBALI TANZANIA

Madida Timotheo ni miongoni mwa waimbaji wa nyimbo za injili ambaye amekuwa akishirikiana na wainjilisti mbalimbali kueneza neno la Mungu kwa njia ya uimbaji.

Hata hivyo mwimbaji Magida amewahi kuimba wimbo wa polisi jamii unahusu utii wa sheria bila shuruti kwa kushirikiana na baadhi ya waimbaji wa jeshi la polisi


Hapa ni jukwaani mwimbaji Magida akiwatumbuiza watu waliofika kusikiliza neno  la Mungu hawapo pichani









 Hapo anaonesha umahiri wake kwa kuimba huku akipiga magoti






hapa shughuli ilikuwa kubwa mtumishi wa Mungu akiimba kwa staili zote ili watu waweze kumfahamu kristo na kumkubali kama bwana na mwokozi wa maisha yao

 Kazi kweli kiasi kwamba watoto waliofika katika wamefurahisha na huduma ya mwiimbaji huyu kiasi kwamba wamekuwa wakimwangalia kwa makini sana katika viwanja vya Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani



Mwenyewe utashuhudia watu walivyojitokeza na kukaa kando ya nyumba zao kuangalia na kufurahia huduma ya uimbaji ambayo Magida alikuwa akitoa










 Hivyo ndivyo mtumishi wa kristo alivyokuwa akiwajibika katika jukwaa kuhakikisha kuwa watu wanfikiwa na injili kwa njia ya uimbaji



 Mdida akishirikiana na mimbaji Pascal Kasian ambaye alishawahi kuwa mshindi wa bongo star search wakiimba pamoja na Sapula katika jukwaa moja katika mkutano wa injili.

























































Waimbaji wakisimama mbele ya kanisa kujitambulisha mmoja baada ya mwingi hapa yupo Enock Jonath na vijana wake wawili anaoshirikiana nao  akiwa  amevaa suti na shart njano ,mwenye microphone ni Pascal Kasian mwenye suruali nyeupe ni Sapula na mwenymiwani meusi na suti na Magida Timotheo,
hapo ilikuwa siku ya jumapili.