YESU NI JIBU

Jumamosi, 28 Machi 2015

HALI YA ASKOFU WA HUDUMA YA UFUFUO NA UZIMA ASKOFU jOSEPHAT GWAJIMA INAENDELEA VIZURI KWA SASA.

 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na uzima ,Josephat Gwajima akihudumiwa na muuguzi wa hospitali ya TMJ, Dar es Salaam baada ya kulazwa katika chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalum.


Picha na Salim Shao,
Mtumishi wa Mungu na pia ni askofu wa huduma la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima amelazwa mara baada ya kuzimia wakati akihojiwa kwenye kituo kikuu cha kati kanda maalum jijini Dar es salaam inaendelea vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari daktari Fortunatus Mazingo wa hospitali ya TMJ amesema kuwa hali ya mgonjwa inaendelea vizuri kwa sasa pamoja na kuwa amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalum. Aidhaa Dr Mazingo amesema kuwa hali ya mgonjwa inaendelea vizuri ila vipimo vyote bado havijakamilika ila anaendelea vizuri.
 Askofu Gwajima akiwaelekea kituo cha polisi akiwa na watumishi wenzake.
wewe unamaoni gani juu ya tatizo hilo la ghafla kwa askofu Gamanywa,

LEO NI SIKU NYINGINE AMBAYO TUNAKUTANA KWENYE ENEO LA IFAHAMU BIBLIA YAKO.



1.Ni mtu yupi ambaye Bwana Mungu alitaka kumtumia katika nchi ya Benjamini kuwaonya watu makosa yao na hakuwa tayari kutokana na umri wake na katika biblia inapatikana katika kitabu gani?
Jibu:Ni Yeremia,
Kitabu cha Yeremia 1:1-7
2.Mshauri wa ajabu,Mungu mwenye nguvu,Baba wa milele,mfalme wa Amani;hayo yote ni majina ya nani na kwa ufafanuzi tunapate wapi?
JIBU ni Bwana YESU
Isaya 9:6
3.Katika wanafunzi wa Bwana Yesu (Tenashara) ni yupi ambaye ameamua kumkana kwa sababu ya fedha bwana Yesu.
JIBU;Yuda ambaye pia aliitwa Iskariote
luka 22:3-6,yohana13:2,27,Marko 14:10-11.
4.Ni mfalme yupi ambaye amemwomba Mungu juu ya hekanu kwa kusema ikiwa mbingu zimefungwa hata hakuna mvua ,kwa sababu wanadamu wamekukosea wewe Mungu ,wakiomba kwa kukabili hekaluni Mungu asikie dua zao na na kuwa samehe dhambi yao.
JIBU:mfalme Suleimani
1wafalme 8:35-40;
2 wafalme 7:12-15
5.Kwanini malkia Esta aliwaamuru wayahudi waliokuwepo Shushani kufunga na kuomba kwa siku tatu bila kula mchana na usiku.
JIBU:Kwa lengo la kuingia kwa mfalme kinyume cha sheria maana hamani bin hamedatha  alipanga kuwaangamiza wayahudi wote.
esta 4:15-17,
6.Ni Sababu gani kuu ya wayahudi kuuuwawa na hamadi nani alisababisha kutokea kwa kosa hilo la wayahudi kuuwawa.
JIBU:ni kwa sababau mara baada ya kupandishwa cheo kuwa mkuu wa maakida wote alitaka kuinamiwa na kusujudiwe na kila mtu,alipoona Mordekai hamsujudii aligadhibika sana,
Esta 3:5(-10).


Ijumaa, 27 Machi 2015

MAENDELEO YA TEKNOLOGIA IMEONGEZEKA SANA DUNIANI MTU AWEKEWA MOYO WA MTU MWINGINE NA KUENDELEA KUISHI:



Cambridgeshire

Madaktari wa upasuaji huko Cambridgeshire wamefanya upandikizaji wa kwanza wa moyo barani Ulaya kwa kutumia moyo mwengine uliosimama kufanya kazi.
Myoyo hiyo hupatikana kutoka kwa watu waliokufa lakini ambao myoyo yao bado inafanya kazi.
Katika upasuaji huo,moyo huo ulitoka kwa mtu ambaye mapafu yake na moyo wake ulikuwa haufanyi kazi.
Hospitali ya Papworth inasema kuwa mbinu hiyo huenda ikaongeza idadi ya myoyo inayopatikana kwa asilimia 25.
Mgonjwa aliyewekwa moyo mpya kwa jina Huseyin Ulucan, mwenye umri wa miaka 60, kutoka London,alikabiliwa na shinikizo la moyo mwaka 2008.
Alisema:kabla ya upasuaji,sikuweza kutembea na nilichoka sana,kwa hakika siku na maisha mazuri.
Upandikizaji wa moyo
Lakini anasema kuwa amefurahishwa na kuimarika kwa afya yake tangu upandikizaji huo.
Kwa sasa najisikia mwenye nguvu kila siku,na nimetembea hadi haospitalini asubuhi hii bila tatizo.
Kumekuwa na visa 171 vya upandikizaji wa myoyo katika kipindi cha miaka 12 iliopita nchini Uingereza.
Lakini mahitaji yanashinda myoyo iliopo ,hivyobasi wagonjwa wengine hungoja kwa miaka mitatu kupata kiungo kinachowafaa.
Wengi ya wagonjwa hao hufariki kabla ya kiungo kupatikana.
Wewe unamaoni gani?kuhusu hili,
chanzo BBC,

Jumatano, 25 Machi 2015

WAIMBAJI WA INJILI MNAENDA MBINGU YA NANI SEHEMU YA PILI



NA MCHUNGAJI MWANGOMOLA,
Kijana mmoja alipotaka kuoa akaniambia “nataka kuoa mwimbaji wa Nyimbo za Injili na huyo mwimbaji ni maarufu” nikwamuuliza swali “unaoa umaarufu au unaoa mke”, akaniambia “vyote viwili yaani umaarufu na mke”. Wapo rafiki zangu wengine wengi walioniambia muonye kijana wako, nilipomwambia juu ya tahadhali hiyo na kwamba sio mimi tu ninayejaribu kushauri bali pia hata rafiki zangu wanaokufahamu na kumfahamu huyo mwimbaji. Alikataa katakata akisema hayo ni maneno ya mtu aliyekosa na mwenye wivu juu ya watu wanaopata vitu vizuri kama yeye alivyompata mwimbaji huyo wa nyimbo za Injili.

Ndugu msomaji wangu leo hii napoandika makala haya, Ndoa haipo tena maana baada ya kuoana ilikuwa timbwili timbwili ndani ya nyumba haikuwepo amani kabisa. Mke aliondoka atakavyo akiulizwa anasema “mimi nimealikwa kwenda kuimba huniambii kitu, siwezi kuacha kumtumikia Mungu kwa sheria zako”, manjonjo, sifa, umaarufu aliokuwa akiuona madhabahuni vyote vilipotea kabisa maana mke sio sifa za uimbaji mke ni utii alionao kwa mumuwe hata angekuwa maarufu kiasi gani, hata angekuwa Raisi wa Nchi bado akiolewa anakuwa mke wa mtu, Uraisi unabaki Ikulu, nyumbani ni mke wa mtu, mama wa nyumbani. Basi sasa hayo waimbaji wa nyimbo za Injili kwao hayako wakiolewa hawataki kutii na wanaona wewe umeoa umaarufu na uimbaji wake, utamweleza nini yeye nafahamika kuliko wewe na ndio maana hata wakiolewa hawatumii majina ya waume zao, wanatumika ya kwao maana ndio wayayojulikana, labda awe aliolewa kabla hajawa maarufu hapo atatumia jina la mumewe maana umaarufu umemkuta na jina hilo, vinginevyo kila mtu ataitwa kivyake.

Katika dunia hii tuliyonayo hakuna watu wagumu kuwachunga kama waimbaji wa nyimbo za Injili, hawashiriki Ibada wao ni mialiko tu. Januari mpaka Desemba hawasikilizi Neno la Mungu hawana muda huo, ni kuimba tu. Mwimbaji wa nyimbo za Injili anaweza akakaa mwaka mzima hajashiriki Ibada kwa ukamilifu zaidi ya kuimba kwenye mialiko na kuondoka, yaani akimaliza tu kuimba anaishia anaenda kuimba Kanisa lingine, nalo akimaliza anasepa kwenda Kanisa lingine, yaani wako kawa njiwa anayerukia mti huu kisha mwingine, jamani waimbaji mnaboa sana. Na Mitume wanawapa vichwa sana wakiwemo na baadhi ya wachungaji wanaowaalika kila mara mwende mkaimbe kwenye makanisa yao na mikutano yao, huku wakiwapa Utukufu uliopitiliza kwamba mwimbaji fulani atakuwepo usikose, wanainuliwa kuliko Bwana Yesu, matangazo yanatangazwa kwamba mwimbaji fulani atakuwepo na sio Bwana Yesu tena, hivyo mmewaongezea kifo. Hawana Neno la Mungu ndani yao maana hawasomi Biblia hawana muda wa kukaa kwenye viti wahubiriwe, wao ni kuimba tu wakimaliza hao huwaoni tena. Ndio maana nyimbo zao hazina Upako tena zaidi ya kelele na hazina ujumbe  maana ujumbe unapatikana kwenye Neno la Mungu sasa wao hawana Neno, watapata wapi ujumbe.

Utanimbia mbona nyimbo zao zinapendwa na watu, waangalie hao watu wanaozipenda hizo nyimbo zao uone ni watu wa namna gani, nyimbo zao siku hizi zinapigwa mpaka bar, nyimbo za zamani thubutu! Huwezi kupiga kwenye bar kwa sababu nyimbo zile zilikuwa na maonyo na ujumbe ambao umebeba Injili ya kweli na toba, wimbo unamwonya mlevi kwamba asipotubu anaenda jehanamu au ulevi ni dhambi nani atakayepiga kwenye bar wimbo huo.

Lakini ukiimbwa nibebe, kila mtu mvivu anataka kubebwa au ukiimba mizaha (comedy) kila mtu atataka apige wimbo huo. Kwa sababu watu wengi sana siku hizi wanapenda mizaha, ndio maana siku hizi watu wanaingia na simu kanisani na huku wakila chingamu na mchungaji nae ana maji ya kunywa madhabahuni, mizaha mitupu, hao lazima watapenda nyimbo kama hizo, zinazokutajia Baraka kila siku.

Lakini kwa watu wa Rohoni nyimbo hizo haziwasaidii lolote zaidi ya kuwa makelele masikioni mwao. Tunataka nyimbo zenye ujumbe, zenye kumfanya mtu atubu, zenye Upako si vinginevyo. Zamani wimbo ukipigwa machozi yatakutoka utafarijiwa, utakuletwa kwenye kumtafakari Mungu. Kama umeokoka na kama bado unaokoka, watu wengi waliookoka kupitia nyimbo zile za zamani, watu hao wapo na wanandelea na wengine wamemaliza mwendo (wamelala) nawafahamu.

Waimbaji wa siku zile walikuwa watu wa rohoni walituliwa miguuni pa wachungaji wao pamoja na kuwa na adabu nzuri na kusikiliza maonyo za si kusikiliza tu maonya bali kuyashika (kuyatendea kazi). Ndio maana walidumu na nyimbo zao zina upako mpaka leo, japo nyombo vya habari hawazipigi mara kwa mara nyimbo hizo. Mambo yalianza kuharibika baada ya kuanza kuimba kila mtu kivyake kwa lengo la kupata pesa na sio kumtumikia Mungu, hapo mambo yakawa mabaya sana, hata maadili yanapotea, waimbaji wa nyimbo za Injli hawana maadili (Ethics) ndio maana hata nyumba (Ndoa) zenu zinashida tupu kila mtu anajuta, hakuna Amani katika ndoa zenu, ndio maana mnaamua kwenda huko kwenye vyombo vya habari kufichua mkidhani huko mtapata majibu, majibu yako kwa Bwana Yesu aliyewapa vipawa hivyo, waimbaji mmemwaibisha Kristo kiasi cha kutosha sasa rudini kundini mkamtumikie Mungu kwa Moyo na Utakatifu ambao hapana mtu atayemwona asipokuwa nao EB. 12:14 si vinginevyo ili pia mpate amani katika ndoa zenu zinazowaka moto. Kila mtu akiomba kimoyo moyo mwenzi wake afe ili awe huru. Na hakuna anayekufa wote mko hai muonje joto la jiwe maana hamsikii maonyo kama yule kijana wangu ambaye aliniambia anataka kuoa umaarufu wa mkewe, alinilalamikia juu ya ndoa yake sijibu neno namtizama tu. Biblia inasema Mithali 29:1 “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafula wala hapati dawa”.

Kwa hiyo mnapoonywa mara nyingi jaribuni kusikia na kuacha yale mabaya ambayo kwayo mnaonywa, Biblia inaonya juu ya kushupaza shingo (kutosikiliza maonyo) kuwa mtu wa namna hiyo atavunjika ghafula na wala hapana dawa. Sasa wewe mwimbaji wa nyimbo za Injili kwa nini uvunjike shingo wakati dawa ipo. Kazi yako ni kusikia na kujirekebisha na kuacha kabisa.

Mimi hapa ni mwonyaji wala msinichukie mna hiari, kama nilivyokwisha tangulia kusema kwenye makala ya mwanzo kabisa, kwamba unaweza kuyachukua maonyo haya au ukayaacha lakini katika umilele mtakuja kukumbuka siku moja kwamba tulionywa katika njia zetu hatukusikia, mimi leo nawaonya  waimbaji wote, wote kila anayejiona ni mwimbaji apokee ujumbe huu uwe maarufu au unayeanza kuimba maana na wewe unaelekea huko, pata dawa mapema ili usije ukavunjika shingo.

ITAENDELEA WIKI IJAYO!!!!!!!!

JIFUNZE BIBLIA YAKO KILA ITWAPO LEO.



1.Ni watoto wangapi wa mfalme Sauli waliuwawa na wafilisti katika mlima Gilboa
Jibu;Ni Yonathani,Abinadabu na Malkishua
1Nyakati 10:1-2
2.mfalme Sauli aliuwawa na nani?
Alijiua mwenyewe
1Nyakati 10:4-6
3.Ni mtu yupi alikuwa anatumia uchawi na watu wengi walimogopa sana na yeye kusema kuwa ni mtu mkubwa?
Simoni
matendo 8:9-13
4.Roho mtakatifu anatusaidia katika sehemu mbalimbali ama nyingi ila katika suala la maombi hutusaidia kufanya nini na katika biblia ibapatikana wapi?
Hutusaidia katika udhaifu wetu
Warumi 8:26-27
5. Ni nani alifundisha neno la Mungu kwa nguvu sana na kuwaonya watu kutenda mabaya wapinge Roho Mtakatifu badala yake walimpiga kwa mawe hadi kufa.
Stefano
matendo 7:51-60