YESU NI JIBU

Jumapili, 9 Machi 2014

KUMILIKI KWA MUJIBU WA BIBLIA



Falsafa ya umikilishaji kwa mujibu wa Biblia
Katika toleo lililopita tulisoma kuhusu baadhi ya mambo muhimu katika sera ya MVIMAUTA. Leo nimeona ni muhimu nikushirikishe mambo yaliyojiri siku ya Uzinduzi kwa kukupa sehemu ya Risala niliyoisoma mbele za Mgeni wa Heshima, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na kisha mbeleni niletee sehemu ya hotuba yake ya Uzinduzi. Leo tuanze na Risala ya Uzinduzi:
Risala ya Uzinduzi wa MVIMAUTA


Falsafa ya umikilishaji kwa mujibu wa Biblia
Katika toleo lililopita tulisoma kuhusu baadhi ya mambo muhimu katika sera ya MVIMAUTA. Leo nimeona ni muhimu nikushirikishe mambo yaliyojiri siku ya Uzinduzi kwa kukupa sehemu ya Risala niliyoisoma mbele za Mgeni wa Heshima, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na kisha mbeleni niletee sehemu ya hotuba yake ya Uzinduzi. Leo tuanze na Risala ya Uzinduzi:
Risala ya Uzinduzi wa MVIMAUTA



Taarifa fupi ya Mpango  Mpakati wa kwanza

“Mheshimiwa Rais, huu ni mwaka wa tatu, tangu ulipotutembelea mwaka 2010 na kutuzindulia Mpango Mkakati wa miaka 10 kwa jina maarufu la MAADILI KWA KIZAZI KIPYA. Mpango huo ulizinduliwa ukiwa na mikakati mikuu 3 ambayo ni
1.     Urejesho wa Maadili katika jamii
2.     Unoaji wa vipaji vya uongozi kwa kizazi kipya
3.     Kumilikisha uchumi endelevu





Jinsi mikakati hii ilivyotekelezwa:
v  Urejesho wa Maadili
Mkakati wa Urejesho wa maadili ulifanyika chini ya kampeni maalum iliyovuma kwa jina la OPERESHENI TAKASIKA ambapo idadi ya watu zaidi ya 72,000 elfu walielimishwa kurejea kwenye maadili ya kiimani.
Kwa upande wa vijana, tuliweza kuwafikia zaidi ya 6,000 kwa kupitia semina na makongamano mbali mbali hapa jijini DSM
v  Unoaji wa vipaji vya uongozi
Mkakati wa kunoa vipaji vya uongozi, tulifanya utafiti ni kwa jinsi gani tunaweza kubaini vipaji wa uongozi miongoni mwa vijana na kuvikuza kwenye misingi ya maadili. Njia pekee tuliyoibani ni kuanzisha Chuo Kikuu cha uongozi wa kimaadili kwa jina la Moral Leadership University. Mpaka hivi sasa mchakato wake umefikia kuundwa kwa Baraza la Chuo, na Utawala wake ambao DVC wake ni Profesa Immanuel Bavu.
Tulikwisha kuwasilisha maombi yetu kwenye Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) pamoja na kwamba tulikamilisha taratibu zote za kupata usajili ikiw ani pamoja na kukodi majengo ya muda ili tuanze kozi za muda mfupi, hatukufanikiwa na tukashauriwa kutafuta eneo jingine tofauti nna mahali pa awali na mpaka hivi sasa tupo katika mchakato huu kutaka kujenga chuo hiki kuanzia katika viwanja hivi!
Baada ya kuona tunazidi kuchelewa, tumeamua kuanza mchakato wa kuanzisha taasisi ya kukuza vipaji kwa jina la TANZANIA INSTITUTE OF TALENTS (TIC), ambao Profesa Bavu anaendelea nao mpaka hivi sasa.
Mheshimiwa Rais, tuna imani kwamba ikiwa tutaweza kupata usajili wa taasisi hizi mbili, tutakuwa na uwezo wa kutekeleza mkakati wa kunoa vipaji vya uongozi wa kizazi kipya kama maono yetu ya awali yanavyoelezea.
v  Utekelezaji wa Mkakati wa kumilikisha uchumi endelevu
Mkakati huu tuliutekeleza kwa kufanya mambo muhimuu yafuatayo:
1.         Mafunzo ya uchumi uliojengwa kwenye maadili
Tuliendesha semina na makongamano na kuhamasisha elimu ya kubuni miradi ya kujipatia kipato cha uhakika badala ya kutegemea ajira ambazo fursa yake ni finyu
2.         Utafiti wa miradi yenye matokeo ya haraka
Kufanya utafiti juu ya miradi ambayo inastahili kuanzishwa na kuleta matokeo makubwa kwa muda mfupi. Mradi ambao tulibaini unaweza kutupa matokeo makubwa kwa haraka ni kilimo cha umwagiiliaji.
Tumeamua kuunga mkono juhudi za serikali yako za mikakati ya kuleta MATOKEO MAKUBWA SASA:
ü  Chanzo cha matokeo makubwa ni “Maono makubwa”
ü  Maono makubwa huzaa mipango mikubwa ambayo huleta matokeo makubwa
ü  Lakini siri kuu iko kwenye neno “SASA”! Huu ni usemi wa kiimani wa uumbaji wake Mungu. Sisi tunaona hii ni kauli ambayo Mungu aliitumia kuumba vitu vikatokea mara moja pasipo kusubiri mchakato
Lakini pia tulibaini changamoto zilizopo katika mradi huu ambazo ni upatikanaji wa ardhi inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, na miundombinu ya umwagiliaji ambayo gharama zake ni kubwa.
            Lakini kwa kuwa tulikwisha kupania kuanza mradi huo tumejitahidi kununua ardhi kiasi cha ekari 430 za kilimo cha mpunga Ifakara, ekari 300 za kilimo cha ufuta Kibaha na ekari 100 za kilimo cha vitunguu Mang’ola juu Arusha.
            Kimsingi, haya tumeamua kuyafanya yawe mashamba darasa kwa ajili ya mafunzo ya kilimo wakati jihudi zinaendelea za kupata hekta 6,000 huko huko Morogoro vijiji vya Kingwa na Kisaki.
Lakini lengo letu kuhusu upatikanaji wa ardhi tunatamani kupata ekari zisizopungua ekari 500,000 ambazo watamilikishwa vijana kwa ajili ya miradi ya kilimo na matumizi mengine ya ardhi
3     Wazo la kuunda mtandao wa vikundi vya maadili na uchumi Tanzania (MVIMAUTA)
Mheshimiwa Rais, suala la umilikishaji uchumi ni zito na si rahisi kummilikisha kila mtu mmoja mmoja katika jamii. Katika kutafuta mbinu za kumilikisha uchumi tumebuni mkakati wa kuanzisha rasmi mtandao wa vikundi vya maadili na uchumi ambao kimaadili utasimamiwa na WAPO MISSION INTERNATIONAL, lakini kiuchumi usimamiwe na BISHOP GAMANYWA FOUNDATION na utunzaji wa fedha usimamiwe na OMEGA SACCOS. Wakati huo huo WMI imeteua Kampuni maalum ya BSHG Consultants Ltd (kwa kushirikiana na wataalamu wa serikali) isimamie mafunzo na uendeshaji wa miradi ya kilimo kwa ajili ya vikundi vya mtando huu mpya.

Sera ya Mtandao wa Vikundi vya Maadili
na Uchumi Tanzania (MVIMAUTA)

v  Maono, dhima na lengo kuu
Maono ya Mtandao wa Vikundi vya Maadili na Uchumi Tanzania (MVIMAUTA) ni;  “Kufikia mwaka 2028, vijana wa Tanzania wawe wanamiliki uchumi endelevu  ambao msingi wake ni  ardhi  inayomilikiwa na watanzania wenyewe”.
Dhima kuu ni; “Kuhamasisha na kuwawezesha vijana kumiliki uchumi kupitia vyanzo vikuu ambavyo ni; ardhi, madini, mifugo, maji, na kilimo”.
Lengo kuu ni; “Kumkwamua kijana kutoka katika hali ya umasikini hadi awe na makazi yake mwenyewe, ardhi kwa ajili ya kilimo, na shughuli halali za kumuingizia kipato”.
Walengwa wakuu wakiwa ni makundi ya: Vijana wanaohitimu katika vyuo vya kati na vyuo vikuu na wanashindwa kupata ajira; Vijana waishio mijini kwa kufanya biashara ndogo ndogo zisizoweza kukidhi mahitaji yao ; Vijana waishio vijijini wenye kutegemea kilimo cha jembe la mkono peke yake; Vijana wajasiriamali walioanzisha miradi midogo ya biashara; Wanandoa na wazazi/walezi kama wadau muhimu katika urithishaji



v  Umuhimu na upekee wa MVIMAUTA
1.   Muunganiko wa maadili na uchumi.
Kwa karne nyingi kanisa la leo limetenganisha ”Maadili na uchumi” kama vitu visivyo na uhusiano. Hali hii imesababisha udhaifu badala ya ufanisi. Kulingana na tafiti zilizokwisha kufanyika huko nyumba, taarifa zake zilibainisha kwamba,  ”uchumi bila maadili” huzalisha ufisadi katika jamii. Na kwa jamii ya kitanzania hiki ndicho kinachosababisha malalamiko na lawama dhidi ya wanaodaiwa kuitwa ”mafisadi”! Pili “Maadili bila uchumi ni kudumisha ufukara katika jamii»
2.   Fursa ya kukuzaji vipaji vya uongozi
UVIMAUTA unakuja na fursa pekee ya kukuza vipaji vya uongozi miongoni mwa vijana watakaojiunga na mtandao huu. Kumbuka kwamba, kila kikundi cha watu ishirini kitakuwa na kiongozi wake. Na kila  kikundi kizima kinapoundwa kitapata mafunzo ya uchumi na uongozi.
Katika mafunzo ya uongozi kila mwanakikundi anatafsiriwa kuwa ni ”kiongozi mtarajiwa” wa kikundi kipya atakachokiunda yeye mwenyewe. Hivyo hivyo zoezi linaendelea la ”vikundi kuzaa vikundi” ambapo mafunzo ya uongozi huendelea na fursa mpya za uongozi kupatikana kwa kuundwa vikundi vipya.
3.   Fursa ya kukuza mitaji kupitia mtandao
Kikwazo kikubwa ambacho kinadaiwa kuendeleza umaskini wa kipato katika jamii, ni ukosefu wa mitaji. Kila mwenye wazo la kufanya mradi wa uzalishaji anajikuta anakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mtaji. Wakati huo huo njia pekee iliyopo ya kupata mtaji ni mikopo kuotka katika taasisi za fedha. Masharti ya kukopesha ni mkopaji kuwa na dhamana ya nyumba au mali yenye thamani inayozidi kiwango cha mkopo anaoutaka. Wengi hawana dhamana na hivyo kujikuta hawakopesheki.
MVUMAUTA unakuja na jawabu la miaka mingi la ukosefu wa mitaji. Mfumo wa kuunda vikundi unashughulikia changamoto ya ukosefu wa mitaji kwa sababu, watu ishirini wanaweza wenyewe kuchangiana mitaji kwa zamu na kila mmoja wao kupata mtaji mkubwa wa mradi anaotaka kuufanya, na bila masharti ya kutoa dhamana.
Aidha, kikundi kinapojiunga katika mtandao huu, tayari kinakuwa kimeingia katika jamuiya ambayo vitakuwepo vikundi vingine ambavyo vimeanzishwa kwa madhumuni ya uwezeshaji wa vikundi visivyo na mitaji; ili mradi vitaingia ubia ambao utahusisha kugawana faida baada ya mauzo.
Huu ni uwezo wa ndani ya vikundi wa mtandao wenyewe. Isitoshe, kwa kupitia mtandao huu, kuna fursa ya kuziendea taasisi za fedha na kuziomba mikopo kwa ajili ya miradi ya mtandao na dhamana ikawa ni mtandao wenyewe kwa taratibu ambazo zi lazima kuzielezea kwa hivi sasa.
Hapa fursa ni Mtandao wenyewe kuwa dhamana ya mikopo ya vikundi badala ya wana vikundi kusumbuka kuweka dhamana ya mali zao binafsi
4.    Fursa ya kuibua na kuendeleza vipaji
Kutokana na ripoti ya maoni ya vijana wasomi wa vyuo vikuu ambayo ndiyo imechangia kuundwa kwa mtandao huu; imebainika kwamba elimu inayotolewa na sekta yetu ya elimu, haina mikakati ya kuibua na kukuza vipaji, bali imejaa nadharia tegemezi. Kwa mantki hii mpaka sasa kuna upungufu wa fursa za kubaini vipaji mbali mbali na kuviendeleza kwa kuviwezesha kimafunzo na mazoezi kwa viwango vya kimataifa
MVIMAUTA utatoa fursa kupitia vikundi vyake kutoa mafunzo na mazoezi ambayo gharama zake zitatokana na miradi maalum kwa madhumuni hayo. Isitoshe, kuna taasisi ya Bishop Gamanywa Foundation (BGF) imeanzishwa kwa maono ya kufadhili mafunzo na mazoezi ya ukuzaji vipaji. MVIMAUTA untanufakika na taasisi hii katika eneo hili lililotelekezwa!

Itaendelea toleo lijalo