Imeelezwa kuwa ni vyema
waumini wa dini zote kusimamia na kufuata sheria bila shuruti kwa lengo la
kudumisha amani na usalama katika taifa la Tanzania sambamba na kuachana na
uovu kwani wanaotenda maovu kwa asilimia kubwa ni watu wa dini.
Kauli hiyo imetolewa na
mwinjilisti wa kimataifa Andulile Bwile jijini Dar es saalam katika mkutano wa
injili ambao umeandaliwa na kanisa la EAGT kwembe ambapo amesema kuwa kuna watu
wanafanya kazi ambazo hazipendezi mbele za Mungu na bado hawapendi kuitwa kwa
majina ya kazi wanazozifanya.
Aidha mwinjilisti Bwile
amesema kuwa unamkuta mtu ni mwasherati ni mzinzi,mlevi,mchawi,fisadi
mwizi,muuaji lakini hapendi kutajwa kwa jina la kazi anazo fanya maana mtu
hutajwa kwa kazi anazofanya kama ni fundi huitwa fundi mwandishi huitwa kwa
jina la kazi yake kwanini wewe ukatae na unafanya hayo yote.
Kwa sasa asilimia kubwa ya
watu wanaofanya makosa na uovu ni watu wenye dini,na dini zimekuwepo kwa muda
mrefu lakini zimeshindwa kumbadilisha mwanadamu maana hawana huruma Yesu pekee
ndiye mwenyeupendo kwa mwanadamu na ndiyo maana amekuja kwa lengo la kumkomboa
mwanadamu ili kuacha uovu wake.
Kutokana na hayo ni vema basi
waumini wote kuwa makini na kumfuata Yesu maana yeye ndiye mwenye uwezo wa
kuokoa na kusamehe dhambi pamoja na kuponya magonjwa yanayowakabili wanadamu
bila kujadi dini na hapo mabadiliko yanaweza kutokea na uponyaji wa taifa kwa
ujumla