YESU NI JIBU

Jumanne, 5 Julai 2016

KONGAMANO LA SIKU 90 LIMEANZA KULETA MAPINDUZI KATIKA MAISHA YA WATU WENGI AMBAO WAMEKUWA WANATASEKA KATIKA MAISHA YAO.

 Mchungaji Katunzi akimwombea mwanamke ambaye alionewa na nguvu za giza.

 Kijana aliyetapika mia mbili aliyoiokota kwa miaka ya nyuma na kununulia mihogo na mara baada ya kula mihongo hiyo alianza kuwa mwizi na mtukutu
 Mchungaji Katunzi akimwombea mwanamke ambaye aliletwa kanisani hapo ambaye alikuwa hawezi kutembea na Mungu alimsaidia na kuanza kutembea.
 Mchungaji Katunzi akionesha shilingi mia mbili ya Tanzania ambayo alitapika kijana mmoja wakati wa maombi na maombezi ndani ya kanisa hilo.
 Mchungaji katunzi wa kanisa la EAGT City Center akimwombea binti aliyetapika hereni na mkufu akiwa katika maombi na maombezi ndani ya kanisa hilo katika kongamano la siku 90
 mke wa Askofu wawi akipokea zawadi kutoka kwa wanawake wa EAGT City Cente akikabidhiwa na mama Rachael Katunzi
Mke wa mchungaji Katunzi Rachael Katunzi akizungumza katika ibada iyopita mara baada ya wanawake wa kanisa hilo kumpa mke wa mchungaji Wawi zawadi mara baada ya kumaliza  kufundisha kwa wiki nzima katika kongamano la siku 90.
Kwa nini uzao wa mwanamke unaendelea kunyanyasawa,kuteswa na kuonewa na shetani wakati wana uwezo wa kupinga na kusimama katika nafasi ya ushindi.
Katika uzao wa mwanamke alitabiriwa kuzaliwa  kwa mwokozi Yesu kwa lengo la kumpa ushindi tena mwanadamu maana ,shetani anatafuta uzao wa mwanadamu ili usifanikiwe.

Kauli hiyo ilitolewa na mchungaji  Abiudi Misholi wakati akihubiri katika kanisa la EAGT City Center jijini DSM ambapo alisema kuwa shetani anafahamu uzao wa mwanamke hivyo anapambana kuharibu maana anafahamu alichokibeba mwanamke.

Aliongeza kuwa hakuna kinachosababisha maumivu kama ukiona mwanamke amebeba mimba kwa miezi tisa na matokeo yake anazaa mwizi,mvuta unga,tapeli ,shoga ni mbaya sana kwani shetani afahamu kuwa akimpata mwanamke na mtoto wake tayari amefanikiwa kuangamiza familia nzima.

"Neno la mzazi lina nguvu kwa mtoto,Mzazi inatakiwa kumwingizia mtoto wako vitu vya hekima katika maisha yake maana kuna baadhi ya watu wanakuwa na tabia ambazo hawapendi wala haipendezi kwenye jamii ni kwa sababu adui aliwapakiza matatizo hayo kupitia neno la mzazi,alisema mchungaji Abiudi.
Hata hivyo aliongeza kuwa toka mwanamke anapobeba mimba anaanza kupambana na shetani maana anafahamu kuwa mwanamke anayebeba ni nani hivyo anaanza kupambana naye.
Mwanamke ni mvumilivu katika maisha yake na ndiyo maana mara nyingi anasimama na kuwasaidia watoto wake na kudai kuwa wanaume ni wakatili ila kuna wanawake nao ni wakatili sana kuliko kawaida,aliongeza mchungaji Misholi.

Mchungaji Misholi alisema pia kuwa Neno la mzazi lina nguvu katika ukombozi wa mtoto na maendeleo yake,hivyo  Shetani ana tumia neno la mzazi na kuanza kuwaangamiza watoto kupitia neno hilo ila pamoja na hayo yote  Mungu ni hivyo hivyo anasikiliza neno la mzazi na kuwainua na kuwasaidia na ndiyo maana anasema kuwa mlee mtoto katika njia ipasavyo naye hataiacha hadi atakapokuwa mzee.
"Kuna baadhi ya wazazi wanawaharibu watoto wao wenyewe na wengine wanaharibikiwa wakiwa vyuo vikuu ndiyo maana nasema ni heri maombi haya ya uzao wa mwanamke ya siku tisini yanaweza kukomboa uzao wa mwanamke"aliongeza.
mchungaji Misholi hakusita kusema kuwa mzazi ni mungu ndani ya familia na  anauwezo wa kuwapa watoto wake sumu ama uzima kulea kwa ujeuri ama kuwafundisha katika njia za haki.

Kwani wazazi wengi wanawapeleka watoto wao kanisani kwa hiari yao ni makosa sana mtoto kwenda kanisani kwa hiari wakali anakula na kuishi kwa kwa mzaziwake sanjari na kuangalia chanel za tv ambazo hazina maadili bila mipaka.
Alinukuu kitabu cha 1famle 3:16-28
 inayosema Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake.Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani.Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu.Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu. Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme.Ndipo mfalme akasema, Huyu anasema, Mtoto wangu yu hai, na mtoto wako amekufa. Na huyu anasema, Sivyo hivyo; bali mtoto aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu.Mfalme akasema, Nileteeni upanga. Wakaleta upanga mbele ya mfalme.Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu. Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme kwa maana moyoni mwake alimwonea mtoto wake huruma, akasema, Ee bwana wangu, mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue kamwe. Lakini yule mwingine akasema, Asiwe wangu wala wako; na akatwe. Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe huyu wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake.Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.
unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0754367826,0718267171 na 0784367826 pia unaweza kutembelea blog ya www.pastorkatunzi.blogspot.com na www.eagtcc.org

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni