YESU NI JIBU

Jumatatu, 11 Aprili 2016

KANISA LA EAGT CITY CENTER LAJIPANGA KUWALETA WAUMINI ELFU 9 KWA YESU KATIKA KONGAMANO LA SIKI 90



 Mchungaji askofu Katunzi akifundisha neno la Mungu ndani ya kanisa

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Faraja Ntaboba kutoka nchini Congo akihudumu ndani ya kanisa la EAGT City Center.
 kutoka kushoto ni mke wa askofu Katunzi,mchungaji Rachael Katundi


 Watoto wa kanisa la EAGT City Center wakimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji ndani ya kanisa wakati wa kutoa sadaka



 Msichana ambaye ni mwanafunzi wa shule Ya sekondani alifikishwa kanisani hapo wakati hawezi kutembea na baada ya maombi ameanza kufunguliwa na kuwekwa huru mbali na mateso na vifungo vya adui shetani.









Dada mwenye Nguo nyekundu katikati aliletwa na mama yake kanisani hapo na amefunguliwa na kuwekwa huru kwa jina la Yesu mtenda miujiza.



 Askofu Katunzi akitoa maelekezo wakati wa ibada maara baada ya kumaliza kufunduisha  neno la Mungu ndani ya kanisa hilo.




 Wauminiwakifuatilia maelezo ya mchungaji na Askofu Katunzi wakati wa ibada kujiombea mwenyewe kwa kuweka mikono juu ya kichwa.

 Viongozi na watendaji wa kanisa la EAGT City Center wakishikilia divai na mkate tayari kwa kushiriki.
 Askofu aKatunzi akisoma neno na kufanya maombi tayari kwa kushiriki meza ya Bwana ambapo wengi walifunguliwa na kuwekwa huru.
 waumini wa kanisa la EAGT wakiinua mikono juu kumshukuru Mungu baada ya kushiriki meza ya Bwana
watu waliofungwa na nguvu za giza wakiombewa maara baada ya kushiriki meza ya Bwana.

Kanisa la EAGT City Center limeweka mkakati wa kuwaleta watu elfu 9 kwa yesu katika kongamano la siku 90 ambapo limeanza rasmi Aprili tatu mwaka huu na linategemewa kuhitimishwa Julai tatu mwaka huu ndani ya kanisa hilo lilopo Mtoni Mtongaji jijini Dar es salaam.
Akizungumza katiuka uzinduzi wa wa kongamano hilo la siku 90 askofu na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Askofu Florian katunzi alisema kuwa wamejipanga katika kuhakikisha kuwa katika siku zote hizo watu wanamrudia Bwana Yesu akma Bwana na mwokozi katika maisha yao na kufunguliwa kutokana na matatizo na shida mbalimbali.
Aidha alisema kuwa wale wote wanaaotaabika na kupitia katika mapito magumu ya ugonjwa biashara na hata katika familia zao wafiki na kumtafuta Mungu wa kweli ndani ya siku hizo tisini na kiukweli Mungu anashuka na kuwatembelea na kuwaweka huru mbali na mateso na maonevu ya Adui.
Aliongeza kuwa katika kongamano hilo la siku 90 watashirikiana na wahubiri wengine katika kuhakikisha kuwa waumini na wasiowaumini watakaofika watafunguliwa na kuinuliwa kutoka hatua moja kwenda nyingine ambapo alisema kuwa ataanza yeye  mchungaji na askofu Katunzi ,Mchungaji Atunus Kamili kutoka mbeya,mchungaji  Abudi Misholi kutoka mbeya ,mchungaji Joshua Wawa kutoka Sengerema na kulola Juounir( Michael) kutoka Mwanza.
Katika maombi haya kila mmoja ataenda kumwona Mungu katika maisha yake ya kila siku na katika sehemu yake ya kazi na  kuleta kibali katika maisha ya kila mmmoja katika kila jambo aingiapo na atokapo maana  Mungu anaenda kufanya Mbingu ikufungukie na kubarikiwa na kuwekwa huru katika maisha na majukumu ya kila siku na kwa kila unachokifanya Mungu anatenda mambo makuu.
"Ndani ya siku 90 inawezekana umekutana na mchungu na magumu ila katika siku hizo Mungu anaenda kuleta mageuzi na kuponya maisha yako, kazi yako, watoto wako nao watakuwa huru na kufunguliwa ambapo alinukuu kitabu 1samweli 22:1-2"alisema askofu Katunzi.
"inawezekana unauchungu na madeni na mpito magumu katika siku zako na maisha yako ya kila siku sasa katika siku zote 90 Mungu anaenda kuondoa uchungu na magumu unayopitia na kuwekwa huru maana   unateseka  katika maisha yako Mungu anaenda kukumbuka na kukutana na maisha matamu, ndoa nzuri, kazi safi hata kama ulidharauliwa Mungu anaenda kuleta mageuzi na kukurudishia heshima na mengi na maajabu mengi unaenda kukutana nayo''aliongeza askofu Katunzi.
Akisoma kitabu cha Ayoubu 15:25-26
Alisema kuwa Yesu ni mtetezi wa kila mwanadamu na hata kama umeonewa na kuteseka unaenda kufunguliwa haijalishi kuwa umekandamizwa na kuumizwa  Mungu anaeonekana na kukusaidia maana yeye anafahamu na kutambua  kesho na mwisho wako na kwake yeye inaenda kuwa mwisho  mwema.
Akiongeza kwa kufafanuzi zaidi na kunukuu kitabu cha Yeremia 33:3 alisema kuwa Mungu anasema kuwa umuuute naye anaenda kukuitikia hata kama watu wamekuona haufai wala hauna thamani mbele zao simama na Mungu mwite atakuonekania na kukuweka huru.

Hata hivyo alisema mapito unayopitia Mungu anaenda kuvusha  yale yanayokusibu ikiwa ni magonjwa,shida,taabu na mateso utawekwa huru na wale waliokuangusha wataanguka wao waliokuinamisha watainamishwa wao,na hata maadui zako wataenda kukatiliwa mbali nawe utapita bila kipingamizi.
Zaburi 1:1
Pia alisema kuwa inawezekana kuna watu walipanga unyauke usifaniukiwe ukwame kiuchumi sasa wao wanaenda kunyauka na kupotelea mbali maana Mungu wa kweli anaenda kukutana nawe hata kama ni magonjwa kama kansa, ukimwi na  magonjwa yote sugu yanaenda kunyauka kwa jina la Yesu na kuwekwa huru na kufunguliwa ndani ya siku 90.
"Waliokupiga wanaenda kupigwa ndani ya siku 90 waliokutesa na kukuinamisha kwa magonjwa wanaenda kuachia maana yupo mtetezi atake kukuinua katika haki utakuwa mbali katika kuonewa na kuteswa, wote waliokuwa kinyume nawe wataanguaka,walioweka mitego na kuuwekea uharibifu wanaaenda kuanguaka na kusambaratika mbele yako"alisema askofu Katunzi kwa masisitizo.

Kutokana na hayo alisema kuwa Hali ya umaskini inaenda kunyaushwa maana Mungu anasema yeye ni moto ulao na anaenda kukutembelea uliyefungwa na kuonewa na adui hata katika familia yako ambapo kila siku saa mbili jumamosi hadi saa nane ibada inaaza na kuhitimishwa na siku ya jumapili ibada inaanza saa 12 hadi tatu ibada ya kwanza na na ibada ya pili inaaza saa tatu hadi saa nane.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni