YESU NI JIBU

Jumapili, 29 Julai 2012

Hili ndilo kanisa la EAGT Utete ambao umesimashishwa kujengwa

Mchungaji Kiongozi wa EAGT Utete Agnes Maliwanga kulia wakiwa na mzee mshauri wa kanisa hilo katikati na mwinjilisti wa kimataifa Mwinjilisti Andulile Bwule wakiwa wamesimama mbele ya kanisa hilo





Mwijilisti Andulile akioneshwa na viongozi wa kanisa hilo jinsi hali inavyoonekana baada ya kusimamishwa ujenzi wa kanisa hilo





Hivi ndivyo ndani ya kanisa hilo inavyoonekana

WAISLAMU WA RUFIJI WAKWAMISHA UJENZI WA KANISA NA KUTISHIA KUCHOMA


 
Katika hali isiyo ya kawaida waislamu katika eneo la utete Wilayani Rufiji Mkoani Pwani wamezuia ujenzi wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania licha ya kuwepo kwa vibali vya ujenzi wa kanisa hilo vilivyotolewa na serikali ambapo wametishia kuwa litaendelea kujengwa watalilipua kama likiendelea kujengwa kinyume na matakwa yao.
Kutokana na hali hiyo uongozi wa kanisa hilo chini ya mchungaji Agnes Maliwanga umeiomba serikali ya jamhuri ya muungano waTanzaniakuingilia kati unyanyasaji unaofanywa na waislamu dhidi ya kanisa hilo mbele ya macho ya watendaji wa wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa Mch. Maliwanga kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo kinamilikiwa kihalali kwa miaka kumi hivi sasana kwamba ni eneo halali kwa ajili ya ujenzi wa kanisa ,likiwa tayari limepimwa na kuidhinishwa na idara ya ardhi ya wilaya ya Rufiji.
Mchungaji Maliwanga alisema kuwa ujenzi wa kanisa hilolilianza toka mwaka 2008lakini ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Rufiji kupita barua yenye kumbukumbu nambari BA73/165/01/23 ya februari 2/11/2011 iliyosainiwa na kaimu katibu tawala wa Wilaya hiyo bwana Milongo Sanga iliwasilishwa kwake akitoa amri ya ujenzi wa kanisa hilo kusitishwa.
“Baada ya kuzuiwa ujenzi tulifuatwa na waumini tunaowafahamu kuwa ni waumini wa dini ya kislamu  wakitamba kuwa wao ndio wameshinikiza kanisa bhilo lisijengwe kwenye eneo hilona badala yake wanata eneo hilo liongezwe kwenye eneo la shule ya mapinduzi ” alisema mch. Maliwanga.
Aliongea kuwa uongozi wa kanisa hilo lilishangazwa na jambo  hilo kwa vile shule hiyo ya msingi imetengewa eneo kubwa la kutosha ambapo alisema waumini hao walifikia hatua ya kutamba hadharani kuwa ikiwa ujenzi wa kanisa hilo utaendelea watahakikisha kuwa linalipuliwa na kuchomwa moto.
Kwa uchungu mchungaji alisema kuwa hali hiyo inapelekea waumini wa kanisa hilo kuwa na hofu wakati wa kuabudu kwani pamoja na kutoa taarifa katika kituo cha polisi cha Utete lakini majibu waliopewa yaliwasikitisha.
Wakati waumini hao wa dini ya kiislamu wakitishia kuchoma moto kanisa la EAGT Utete matukio ya uchomaji wa makanisa nchini yamekuwa yakiripotiwa kutokea mara kwa mara ambapo tangu mwaka 1984 tayari makanisa 46 yamechomwa moto na waumini wa dini ya kiislamu.
Takwimu zinaonesha kuwa makanisa 26 yamechomwa visiwani Zanzibar wakati 20 yameteketezwa kwa moto katika mikoa kadhaa upande wa Tanzania bara,wakati hiyo ikiendelea hakuna taarifaza misikiti kuchomwa moto.


Jumamosi, 28 Julai 2012


Imeelezwa kuwa ni vyema wanadamu kumnyenyekea Mungu katika maisha yao ya kila siku ili waweze kuishi maisha ya amani na usalama katika maisha yao sambamba na kuifuata njia za kweli.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kanisa la EAGT Saranga jijini Dar es salaamu mchungaji Florian Katunzi amesema kuwa imetosha kwa mwanadamu kutenda dhambi katika maisha yake kwani tangu mwanadamu kuanza kutenda dhambi hajawahi kutosheka katika maisha ya dhambi
Aidha mchungaji katunzi amesema kuwa haijalishi kuwa unafanya kazi ya namna gani kama hujaokoka ni kazi bure maana wapo wengine wanaitwa wafia dini kwani wanakuwa walevi na bado wanakwenda makanisani na wakati mwingine anakwenda kwa waganga na wachawi huku akisema wanamwabudu Mungu huku maisha yake hayampendezi Mungu.
Pamoja na hayo aliongeza kusema kuwa ni vyema kumtafuta yesu katika maisha yako na katika makusanyiko mbalimbali kumekuwepo watu ambao  wanakuwa kama ni wasindikizaji katika maisha ya dini na kuendelea kujificha kwa kivuli ya dini na kuendelea kutenda makosa na dhambi.
Hata hivyo mch.Katunzi amesema kuwa wapo wengine wamekuwa wakifuga majini katika nyumba zao badala ya kufuga mifugo na wanyama wengine wa kufugwa badala yake wanafuga majini kwa lengo la kuwatesa wanadamu wengine .
“Bila Yesu mwanadamu huwezi ukakwepa majini na wachawi sambamba na wachawi  bila kumpokea bwana Yesu kama bwana na mwokozi wa maisha yako bila hivyo utaendelea kuteseka katika maisha yako ya kawaida kama wanadamu wengine hivyo ni vyema umkubali Yesu katika maisha yako” alisema mchungaji Katunzi.

Jumapili, 22 Julai 2012

Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha michezo Joseph Mapunda anatazikwa katika makaburi ya chang'ombe jijini Dar es salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mdogo wake marehemu bwana ZICO MAPUNDA amesema kuwa mwili wa marehemu utaagwa nyumbani kwake mtoni kijichi na kupelekwa kwenye makaburi ya chang'ombe kuzikwa.

Marehemu amemwacha mjane na watoto wawili wa kiume ambapo kwa mujibu wa ndugu huyo amesema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la tumbo ambalo alilazwa katika hospitali ya wilaya ya Temeke.
Marehemu amelazwa katika hospitalini hapo kwa muda wa siku mbili na siku ya tatu akapoteza maisha hospitalini hapo


mtagazaji wa kipindi cha duru za michezo dugu Joseph Mapunda enzi za uhai wake akiwa akiwa katikati na jeazi la michezo iliyoandikwa phone doctotor kulia ni meneja wa WAPO radio Barikieli Gadiel na Victoria Mungure               

Jumatano, 18 Julai 2012

MAFUNDISHO YA UJASIRIAMALI YATOLEWA KWA SIKU TATU KIVULE


Wakazi wa Zanzibar na Jamii kwa ujumla, wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria semina ya ujasiriamali ya siku tatu inayoanza kesho hadi  Julai19 mwaka huu.

Akizungumza na Wapo Radio Fm, Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujasiriamali ya I C B Jijini Dar es Salaam, Mchungaji Israel Ernest wa Huduma ya 'Uamsho Kivule', ameeleza kwamba semina hiyo itafanyika Visiwani  Zanzibar katika Uwanja wa CCM Kiembesamaki.

Kwa mujibu wa Mchungaji Israel, kufanyika kwa semina hiyo kunafuatia maombi ya muda mrefu wa wakazi wa Zanzibar ya kufundishwa masuala ya ujasiriamali ili wajikomboe kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Ameongeza kuwa, bidhaa zitakazofundishwa kinadharia na vitendo wakati wa semina hiyo ni pamoja na  utotoaji wa vifaranga,  mafuta ya mgando, chaki, mishumaa, kilimo cha uyoga na keki za harusi.

WAJANE WATAKIWA KUFUNGUKA KIROHO KUJIAMINI NA KUTOJIDHARAU


Wito umetolewa kwa wanawake wajane nchini, kufunguka kiroho, kujiamini na kutojidharau ili waweze kujijengea uwezo wa kiuchumi kupitia ujasiriamali na kulea vyema watoto wao.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Huduma ya Elishadai inayosimamia wanawake wajane, Mwinjilisti Agusta Ernest Kitea kutoka Kanisa la Gosheni lililopo maeneo ya Ilala Mchikichini wakati akizungumza kwenye Kongamano la siku moja la wanawake wajane lililofanyika katika Ukumbi wa Parokia ya Msimbazi Jijini Dar es Salaam.
Mwinjilisti Agusta ambaye alifiwa na mumewe miaka saba iliyopita huku akimwachia mtoto mchanga amebainisha kuwa, huduma yake inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa fedha.
Kongamano hilo la pili kufanyika nchini, limehudhuriwa na takribani wanawake 180  ambapo kongamano la kwanza lilifanyika Julai 16 mwaka jana katika Ukumbi huo na kongamano lingine linatarajiwa kufanyika Desemba 18 mwaka huu.

KIBURI NI MBAYA KATIKA MAISHA YA MWAMINI ALISEMA ASKOFU SYLVERSTER GAMANYWA


Kuwa na kiburi kutokana naulichonacho imeelezwa kuwa ni mojawapo ya njia zinazobasabaisha mwaminini asiweze kupokea Baraka zake kutoka kwa Mungu kwani kiburi kinamfanya mwamini kujiona kuwa bora kuliko mwingine.
Kauli hiyo  ilitolewa hivi karibuni na askofu mkuu wa WAPO Mission international askofu Silvester Gamanya wakati akifundisha juu ya somo la kiburi kwenye mchesha uliofanyika katika ukumbi wa BCIC Mbezi beach jijini Dar se saalam.
Kiburi ni tatizo kubwa linalowakabili waumini wengi kwenye madhehebu yao na dini zao na suala hilo linasababisha uwepo wa Mungu kuwa na mipaka ndani ya waumini,ni vyema kila mwamini kwa nafasi yake kukataa na kupinga kwa juhudi zote juu ya tatizo hilo la kiburi lisiwepo ndani ya maisha yake.
Mwanadamu anaweza kuwa na kiburi ya mali ,elimu aliyonayo ama fedha na inasababisha mwanadamu huyo kujiona kuwa hakuna kinachoweza kumkwamisha ama kumzuia katika maisha yake kufanya jambo ambalo kwa ukweli ni kujidanganya katika maisha yake.
Alisema kuwa na elimu fedha na utajiri wa kila aina ni vizuri kila mwanini ama mwanadamu asiwe na kiburi maana ni mbaya sana  kiasi kwamba inasababisha hata pamoja na kuwa na vitu hivyo kuonekana kuwa haufai mbele za Mungu na mbele za wanadamu.
Mkesha huo ni mfululizo ya mikesha ya urejesho ambayo hufanyika kila mwisho wa mwenzi katika vituo vya BCIC Mbezi beach na BCIC temeke na huwa maombi na maombezi hufanyika kwa wale wenye shida na matatizo mbalimbali katika maisha yao na watu wengi hufunguliwa.
Kutokana na hayo askofu amekuwa akifundisha kwa umakini na ufasaha zaidi juu mafundishao yanayohusu maisha ya wanadamu pamoja na kuwepo kwa malalamiko ya waumini kulalamikia hali ngumu ya maisha basi njia pekee ya kupata ufumbuzi ni kumwamini bwana Yesu.

Jumanne, 10 Julai 2012

MCHUNGAJI KUTAMBULISHA KITABU CHA UTAFITI ILIYOANDIKWA KWA LUGHA YA KISWAHILI





Mwandishi wa kitabu kipya cha utafiti kwa lugha ya Kiswahili kwa elimu ya juu, Mchungaji Dk. Elia Shabani Mligo, amekitambulisha rasmi kitabu hicho kiitwacho, 'Jifunze utafiti'.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mchungaji Elia amesema kuwa, lengo la kuandika kitabu hicho kwa lugha ya Kiswahili ni kuwarahisishia wanafunzi kufanya vizuri katika somo la utafiti  kwani wengi wao wana uelewa mdogo wa lugha ya kiingereza.

Aidha Mchungaji Elia amebainisha kuwa, uwezo mdogo wa wanafunzi kujieleza kupitia lugha ya kigeni, umekuwa ukisababisha kufanya vibaya katika somo hilo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Kwa mujibu wa   Mchungaji Dk.Elia,  kitabu hicho kimechapishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya uchapishaji Vitabu ya Jijini Dar es Salaam, Bw.Mkumbo Mtula.