Hoja ya leo
nimeona niwasilishe baadhi ya “kauli tata” ambazo ni maarufu sana kwa waumini
wa madhehebu ya dini kwa kudhaniwa kwamba ni “maneno ya Mungu.”! Sababu ya
kuamua kuzichambua ni kwa sababu, zimekubalika kama ni “Neno la Mungu wakati
zinakinzana na Neno la Mungu”! Nia ni kuweka waziwazi uongo wa Ibilisi
uliojificha kwenye kauli hizo tata ili aliyekuwa amedanganyika afunguliwe
fahamu na kuwekwa huru kwa kuijua kweli.
Kauli tata ya “Sisi
sote ni watoto
wa Mungu”
Ni kweli kwamba kwa asili binadamu wote tunatokana na watu
wawili ambao ni binadamu wa kwanza walioumbwa na Mungu. Na binadamu hawa
waliishi miaka mingi isiyojulikana mpaka wakati walipoasi amri ya Mungu
wakaanguka katika dhambi. Kuanzia wakati huo mpaka hivi leo, vizazi
vilivyofuata viliathiriwa na dhambi na kujulikana kama watumwa wa Ibilisi kwa
sababu hiyo.
Kwa sababu ya upendo wa Mungu, almtuma Mwana wake pekee
Yesu Kristo ilia je kutukomboa katika utumwa wa Ibilisi. Tangu ujio wa Kristo
duniani, ndipo ukaanzishwa uzao mpya wa kiroho ambayo unatoa fursa kwa kila
binadamu mwenyedhambi kuimpokea Yesu na kisha kupata uwezo wa kufanyika mtoto
wa Mungu. Kwa hiyo, tangu Yesu alipokufa na kufufuka katika wafu, tuna makundi
ya aina mbili ya binadamu hapa duniani. Kundi la “watoto wa Mungu”, na kundi la
“watoto wa Ibilisi”.
“Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa
Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye
asiyempenda ndugu yake.” (1 YOH. 3:10)
Kwa hiyo si kweli kwamba, kila binadamu aliye hai hapa
duniani ni “mtoto wa Mungu.”! Haijalishi aina ya tofauti za madhehebu ya dini
na wasio na dini kabisa. Wote ni “watu wa Mungu” kwa maana tu viumbe wake Mungu
kwa asili. Lakini sio wote ni watoto wa Mungu ati kwa sababu ni binadamu. Kuwa
mtoto wa Mungu ni uchaguzi binafsi ambao unafanywa na mtu mwenyewe.
“Wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika “watoto wa
Mungu”, ndio waliaminio jina lake.” (YH.1:12)
Jambo jema na kutia hamasa ni kwamba walio “watoto wa Mungu”
sio kwamba tunajiaminisha tu kwa akili zetu wenyewe. Yesu mwenyewe ametusaidia
kwa kumtuma Roho Mtakatifu ambaye amekuja kufanya makao ndani yetu. Na
tunapompokea Roho Mtakatifu akiisha kujaa kwa wingi ndani yetu, yeye ndiye
hufanya kazi ya kututhibitishia na kutushuhudia kwamba sisi ni watoto wa Mungu:
“Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu;
bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani,
Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto
wa Mungu;” (RUM. 8:15-16)
Je wewe mwenzagu una hakika kwamba ni “mtoto wa Mungu”?
Unaamini hivyo kwa sababu ya kauli ya mazoea kwamba “binadamu wote ni watoto wa
Mungu”; au ni uchaguzi wako binafsi ulioufanya wa kumpokea Yesu Kristo ili
akupe uwezo wake wa kufanyika mtoto wa Mungu?
Kauli tata ya “Sisi
sote
tunamwabudu
Mungu mmoja”
Kauli tata nyingine inayokizana na Neno la Mungu lakini
imeshika akili za watu wengine ni dhana ya kudai kwamba “Sisi sote tunamwabudu
Mungu mmoja”! Ati pamoja na tofuati zetu za kimadhehebu na mitindo mbli mbli ya
kuabudu; bado tunamwamubu Mungu mmoja tu iwe kwa kujua au kutokujua!
Tatizo kubwa linaanzia hapo hapo kwenye tofuati ya itikadi
na mitindo ya kuabudu. Angelikuwa ni Mungu mmoja yule yule kwanini aabudiwe kwa
njia na mitindo tofauti? Wachiliana
mbali tofauti za kiitikadi na kimitindo ya kuwabudu, mbona tunashawishiana na
kuvutiana kila upande unafanya juhudi za kupata wafuasi wa itikadi nyingine
wajiunge na itikadi yao? Majibu ya maswali yataonesha dhahiri kwamba hata kama
yupo Mungu mmoja anayestahili kuabudiwa na sisi sote; lakini sio itikadi
zinamwabudu Mungu mmoja.
Baada ya kusema yaliyotangulia, nije kwenye maandiko
yasemavyo kwa habari ya Mungu anayestahili kuabudiwa na wote na jinsi ya
kumwabudu. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinatupa ukweli kama ifuatavyo:
“….jueni ninyi
nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,
ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu
huyu anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lile
lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la
pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana
jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa
kwalo.” (MDO 4:10-12)
Unaona? Kisa cha Mungu kumtuma Mwanawe licha ya kutukomboa
toka utumwa wa Ibilisi, lakini pia kutuwezesha kumwabudu Mungu Baba kwa njia ya
Yesu Kristo ambaye ni mlango wa kuingilia patakatifu pa patakatifu pa Mbinguni.
Kwa mantiki hii, hakuna mtu mwingine awaye yote chini ya
mbingu ambaye inatupasa kuokolewa isipokuwa Yesu Kristo mwenyewe. Msingi wa
maandiko haya ni kukanusha uvumi na itikadi za dini nyingine zote zisizomtambua
Yesu Kristo kuwa ndiye peke ambaye anatupeleka kwa Mungu wa kweli kwa sababu
Mungu huyo ni Baba yake halisi. Kwa hiyo, dhana kwamba sisi sote tunamwabudu
Mungu mmoja si kweli. Kila dini ina Mungu wake ambaye wafuasi wake wanamwabudu.
Hata kama majina yanaweza kufanana lakini, kigezo cha kumwabudu Mungu wa kweli
ni kupitia Yesu Kristo peke yake.
Kauli tata
kwamba “sisi sote
twaenda sehemu moja
baada ya kufa”
Kauli tata ambayo imeshika hisia na akili za wengi kwamba
ni Neno la Mungu, ni dhana hii inayodai kwamba, “sisi sote tukifa tunaenda
kumoja, yaani kukaa na Mungu milele.” Ati “SISI SOTE KAMA BINADAMU TUNAELEKEA
SEHEMU MOJA BAADA YA KUFA.” Dhana hii inadai kwamba bila kujali maisha ya mtu
anayoishi hapa duniani, yawe machafu au masafi kulingana na dhamiri yake kwa
itikadi ya dini yake akifa lazima anaenda sehemu moja ile ile ambayo binadamu
wanapokufa wanakwenda kuishi na Mungu milele.
Tena wengine wanachanganya zege zaidi, kwamba tofauti za
madhehebu ya dini ni sawa na njia nyingi tofauti lakini zinaishia na kuunganika
kwa Mungu mmoja baada ya kufa. Ni kweli kwamba, kila anayekufanya atakutana na
Mungu siku ya kiyama. Lakini inategemea unakutana na Mungu kwa kupitia NJIA
ipi. ZIko njia mbili kuu hapa duniani. Kuna njia iendayo upotevuni, na kuna
njia iendayo uzimani aliko Mungu baba.
Kana kwamba hii haitoshi, siku hizi kuna kauli tata za
nyongeza zinazotoa faraja kwa wafiwa zinazosema; “Mungu amempenda zaidi.”! Ninatambua
sana umuhimu, ya kwamba, wakati wa msiba wafiwa wanahitaji faraja za karibu ili
kutuliza huzuni na maumivu yatokanayo na kuondokewa na mpendwa wao. Pamoja na
juhudi na huruma za kuwafariji wafiwa, haifai kabisa kutoa kauli ambazo sio
Neno la Mungu kwa sababu kwanza zinazidi kushindilia uongo wa kiimani na wengi
wanazidi kupotea kwa uongo huo.
Jamani kama ingelikuwa ni rahisi kwamba kila mtu anayekufa
anakwenda kukaa kwa Mungu na kupumzika moja kwa moja, pasingelikuwepo haja ya
kuwahubiriwa watu Injili ya wokovu wa Yesu Kristo ili watubu na kuzaliwa upya
kiroho! (MK.16:16)
Yesu alisema kwamba, “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba;
maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendnayo upotevuni, nao ni wengi
waingiao kwa mlango huo.” (MT.7:13-14)
Mfani mwingine unaoshuhudia kwamba sio kweli kwamba watu
wote wanapokufa wanaenda sehemu moja, ni mfano vifo vya “Tajiri Lazaro na
maskini” kama ilivyosimuliwa katika Injili ya Luka. (Lk.16:19-26) Humo tunasoma
Tajiri alipokufa alikwenda mahali pa mateso na maskini alipokuwa alikwenda
kifuani pa Ibrahimu mahali pa mapumziko. Hizi ni sehemu mbili tofauti na kila
anayekufa huenda upande wake kulingana na aina ya njia aliyoichagua tangu
alipokuwa angali hai.
Somo ambalo Askofu Gamanywa amefundisha,
wasiliana nasi kwa 0682672828.