YESU NI JIBU

Jumatatu, 29 Juni 2015

CHUMBA ZA KUTOLEA USHAURI KINAPASWA KIWEJE? (The counseling environment). KUTANA NA MSHAURI NA MWALIMU PETER MITIMINGI KATIKA SOMO HILI.



 COUNSELING TRAINING
1. Ni muhimu kutilia maanani mpangilio wa viti, fanicha, ni aina gani ya viti vilivyopo kwenye chumba cha ushauri. (masofa) huwa sio mazuri wakati wa ushauri.
2. Zingatia ukubwa wa chumba cha kutolea ushauri.
3. Chumba kidogo sana kinaweza kumfanya mshauriwa ajisikie vibaya hasa kwa wale ambao wamefanyiwa ukatili wa kubakwa au ukatili.
4. Pia kisiwe chumba kikubwa sana kitakacho watengenisha mshauri na mshauriwa kwa umbali.
5. Mshauri kukalia kiti cha kuzunguka hakiruhusiwi kwenye chumba cha ushauri.
6. Mshauri na mshauriwa wakae katika viti vinavyofanana yaani vya aina moja sio mshauri anakaa kwenye kiti kama bosi na mshauriwa anakaa kwenye kiti kidogo, hiyo hairuhusiwi.
7. Meza (desk) hairuhusiwi wakati wa ushauri kusiwe na meza kati ya mshauri na mshauriwa. Mshauri anapaswa kuweza kumuona mshauriwa kuanzia kichwani mpaka miguuni wakati wa ushauri sasa ukiweka meza hutaweza kumuona mshauriwa in full.
8. Chumba cha ushuuri hakipashwi kuwa na Tv au Radio iliyowashwa wakati huduma ya ushauri inaendelea.
9. wa tendo la ndoa. Hata hivyo mshauri anaweza asiwe na chumba kizuri cha kutolea ushauri kwa hiyo mteja anapaswa kukubaliana na hali inayo kuwepo.
10. Chumba cha kutolea ushauri kisiwe kimebandikwa mapicha picha ya aina yoyote kwani baadhi ya mapicha yanaweza kumfanya mshauriwa akajaa hofu zaidi au yakamkumbusha vitendo vibaya alivyowahi kufanyiwa.
Mfano:
Picha za watu wanpigwa au kunyanyaswa
Picha za vitisho
Picha za manyoka
Picha za watu wanagombana
Picha za mambo ya mapenzi
Picha za walevi au wavutaji
Picha za makahaba nk.

TGNP IMESEMA HAIPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WALE VIONGOZI AMBAO HATAWAHAKIKISHIA WANAWAKE NA WALEMAVU HAKI ZAO.



Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP  umeeleza kuwa hauko tayari kuwaunga mkono wale watu wanaohitji kuwa viongozi wa Taifa endapo hawatawahakikishia wananchi kuwa watatetea haki zote za  wanawake na walemavu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TGNP LILIAN LIUNDI Wakati akiongea na waandishi wa habari katika warsha ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari mbalimbali zinazilohusiana na masuala ya uchaguzi pamoja na bajeti kwa mrengo wa kijinsia.
Liundi amesema kuwa wanachotaka ni kuona kuwa
viongozi watakaoingia madarakani wanakuwa na tamko mahususi linalolenga kumtetea mwanamke na kumuondoa katika matatizo mbalimbali yanayomkabili yakiwemo yale ya kuwa na haki ya kumiliki rasilimali pamoja na haki nyingine anazopaswa kupata.

Naye mkurugenzi wa bodi TGNP VICENCIA SHULE ameeleza kuwa ili nchi iweze kuimarika kimaendeleo serikili haina budi kuweka usawa wa kijinsia katika bajeti.
Ameeleza katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wagombea wengi wanatumia kiwango kikubwa cha rasilimali wakati wanapokuwa wanatangaza nia hivyo kukatisha tamaa watu

Ijumaa, 19 Juni 2015

KUTANA NA MTUMISHI WA MUNGU PETER LUKUTA KATIKA SOMO LA IKIMBIENI ZINAA (1WAKORINTHO 6:18):


ZINAA NI NINI? 
 Zinaa inahusisha tendo la ndoa kwa watu ambao si wanandoa kuna tofauti kati ya uasherati na uzinzi, uzinzi unawahusu wanandoa ambo siyo waaminifu kwenyendoazao, na uasherati unawahusu watu ambao siyo wanandoa ila wanaingiliana kimwili, sasa hizi zote kwa ujumla wake zinaitwa ni ZINAA, miongoni mwa zile dhambi nane kwenye UFUNUO 21:8. dhambi ya tano imewekwa kuwa ni zinaa, sasa hii ni dhambi pana sana kwasabu upo uzinzi wa kiroho ambapo ni pale mkristo yoyote anapotenda dhambi anaitwa kuwa ni mzinzi kwasabu ametoka nje ya ndoa yake na Mungu wake. sasa leo sizungumzii uzinzi wa kiroho bali nauzungumzia uzinzi wa kimwili au zinaa ya kimwili,

ZINAA CHUKIZO KUBWA SANA MBELE ZA MUNGU.
Zinaa ni dhambi inayomkasirisha sana Mungu kutokana na uzito wake, pia ni dhambi iliyowashinda watu wengi siyo vijana wala wakubwa wala wazee ukweli ni kwamba zinaa imewanasa watu wengi sana, napia hata watumishi nyakati za leo wamekuwa wakianguka anguka sana kwenye kona hii ya zinaa si wa kike wala wakiume waimbaji na wahubiri kutokana na kutokuwa na kiasi kwao kwasababu wameupa Mwili nafasi kubwa utawale maisha yao kuzidi roho , na kutokana na sababu hiyo ya wengi kunaswa kwenye zinaa. Sasa wengi wameamua kuihalalisha dhambi hii katka maishayao ili ionekane kuwa ni kitu cha kawaida lakini si kweli kwamba zinaa ni kitu cha kawaida zinaa si kitu cha kawaida hata kidogo, watu wengi wanaishi maisha ya uchafu kabisa huku wadhania kuwa ni ndoa lakini kihalali si ndoa bali ni ubatili tu na kujidanganya kwasababu ndoa inao msingi wake na sharti ufatwe.



KWANINI MUNGU HUICHUKIA SANA ZINAA
1>Mungu huchukizwa sana na kuingiliana kimwili kusiko halali kwasabu tendo la ndoa ni Agano kati ya mwanamke na mwanamume, mwanamke amepewa kitu kinachoitwa Bikira hii Bikira siku inapoovunjwa kwa mwanamke kuingiliwa kimwili hutoa damu na ile damu ni udhihirisho wa Agano analofanya mwanamke na mwanamume sasa baada ya tendo hilo kunakuwa na kifungo katika ulimwengu wa roho ambacho ni kama mnyororo unaowaunganisha wahusika hawa wawili ambao hawapaswi kuachana tena, sasa kitendo cha kufanya tendo kwa watu wasiyo wanandoa ni kuuvuruga mpango wa Mungu wa aliyouweka na kuisambaza roho chafu ya Shetani kwa kufanya umalaya wa kuungana na mwili wa kahaba,
na ndiyo sababu kwenye agano la kale Mungu aliagiza kwamba mtu akimbikiri binti ni sharti skamtolee mahari na awe mkewe kabisa KUTOKA 22:16-17. kwasabu kulala na mwanamke ni kuungananaye na kuwa mwili mmoja naye. sasa

1KORINTHO 6:15 Je hamjui ya kwamba miili yenu ni viungo vya Kristo? Je nichukue viungo vya mwili wa Kristo na kuviunga na mwili wa kabaha? la hasha! Hamjui kwamba aliyeungwa na kahaba anakuwa mwili mmoja naye? kwa kuwa imenenwa "hawa wawili watakuwa mwili mmoja."
Hapo unaona kuwa watu wanapokutana kimwili wanakuwa ni mwili mmoja yaani wanaunganishwa kwa agano la tendo la ndoa na sasa mtu mwenye tabia ya umalaya anakuwa anafanya maagano na watu wengi na kuunganishwa nao katika ulimwengu wa roho jambo ambalo ni baya sana kwasbu lina madhara makubwa ikiwemo kutumiwa kama agent wa majini mahaba na mwishowe ni kutupwa kwenye ziwa la moto.

2>Zinaa ni dhambi pekee inayovihusisha viungo vyote vya mwili wa mtu hivyo ni tusi kubwa sana kwa Mungu, kwasabu inauaibisha uumbaji wa Mungu na kuutia unajisi mwili wote kwasabu ni dhmbi pekee inayofanyika ndani ya mwili tofauti na zile zingine.
1KORINTHO 6:18 Ikimbieni zinaa. 
Dhambi zingine zoote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe. Je hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho mtakatifu, akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? ninyi si mali yenu wenyewe.
Tumeona hapa kwamba nidhambi inayofanyika ndani ya mwili ambalo ndilo hekalu la Mungu, na hii ndiyo sababu mtu akiishakufanya zinaa ile hukumu hamwondoki hata afanyeje na uwepo wa Mungu humwacha papo hapo na huduma inakufa kwasabu kibali kinatoweka ule utukufu uliyomzuunguka unaondoka kwasabu Roho mtatatifu ameondoka, Dhambi hii huondoa hata ujasiri wa kuomba kuhubiri nk na pai haimpi mtu ujasiri au msukumo wa kutubu kwasabu imefanyika ndani ya mwili na kumfanya Roho aondoke ambaye huwa ndiyo mwenye kukumbusha kutubu sasa kwasabu ameondoka basi mtu hsikii hamu mguso wa kutubu na ndipo atajikuta ankiendelea na dhambi hiyo huku moyoni akijihalalishia kwa utashi wake mwenyewe na mwishowe najikuta miongoni mwa waenda Ziwani kwenye ule moto wa milele.

3>Zinaa inaleta kizazi au uzao wa haramu, katika biblia mtoto wa nje ya ndoa huitwa ni mtoto wa haramu=KUMBUKUMBU LA TORATI 23:2. Na lazima tutambue kuwa anaitwa haramu kwa sababu ametokana na tendo la haramu na Siku zote haramu huzaa haramu sasa haimaanishi kuwa huyu ni Mtoto asiyefaa no maana yeye hana kosa lolote bali kosa ni la wazazi ni sawa na sisi sote tulizaliwa na laana ya kurithi kutokana na dhambi ya Adamu ijapokuwa sisi hatujahusika kwasababu hatukuwepo. likini ashukuriwe Yesu ambaye ukimpokea basi unafanyika mwana wa halali hivyo kuna ulazima wa kila mtu kuokoka ili atoke kwenye uharamu wowote aliyonao maana kwenye kile kitabu cha Mwanzo kuna mstari unasema kila mbegu izae kwa jinsi yake, sasa mbegu haramu huzaa haramu na Mungu yeye hapendi uharamu hivyo zinaa huleta uzao wa haramu na hata ukichunguza utagundua unakuta babu, baba, na mtoto wote hajawahi ku oa ila wanazaazaa hovyo tu lakini hapa chimbuko la yote ni yule mzao wa kwanza aliyepenyeza mbegu mbaya kwa kizazi chake ambaye ni babu, na hii ndiyo sababu zinaa inafedhehesha inaleta hasara kubwa inaangamiza kabisa hatima ya maisha ndiyo maana imeandikwa Aziniye na Mwanamke hana akili (MITHALI 6:23.)
Hizo ni sababu chache miongoni mwa nyingi zinazomfanya Mungu achukizwe sana na zinaa. na Mungu ameachilia mapigo mbali mbali kwenye zinaa kama magonjwa ya Gonoria, Kaswende, Malengelenge na pia Ukimwi ambao umefyeka ma mia ya mamilioni ya watu duniani ili kudhihirisha jinsi Mungu anavyochukizwa na dhambi hii ya zinaa. Mfalme Daudi alipofanya dhambi hii urafiki wake na Mungu ulikomea pale hata ilipomlazimu kutubu sana lakini bado Mungu hakumrehemu ndipo Daudi akasema Heri mtu aliye samehewa ndhambi zake ZABURI 32:1. Daudi alisema hivyo kwasabu ya aliuona uchungu na mateso ya maisha ya mtu anayeishi na hatia kwa Mungu na si hilo tu balli Daudi katika toba yake kwenye ile ZABURI 51 sura yote kuna mtari mmoja anasema Narudishie furaha ya wokovu wako Daudi alitamka maneno haya baadaya kuona hana furaha hana amani kwasabu zinaa aliyoifanya ilimwondolea furaha ya wokovu waken Hakuna furaha yoyote ndani ya maisha ya zinaa ni machungu matupu, mzinifu kamwe hawezi kuufurahia Wokovu rohoni mwake kumejaa ubatili ile amani ya Shetani ya kujifariji kutokana na udanyanyifu wa moyo ambao mwisho wake ni kifo cha ghafla =YEREMIA 17:9.
USHUHUDA WA MCHUNGAJI ALIYEZINI.
Nilienda kuhudumu knisa flani lakini baada tu ya kuhubiri pale nilikemea sana habari ya zinaa, baada ya kumaliza mahubiri ndipo mama kanisa mlezi akaniomba tuonane akanambia kwa habari ya mchungaji kwamba anafanya uzinzi na binti mmoja na inajulikana kabisa kwa baadhi ya watu lakini mchungaji akiulizwa anakana, sasa watu wakaanza kumdharau yule mchungaji hata watu ambao hawakuijua ishu ile pia wakaanza kumdharau, akawa akisema kitu hwakifanyi na akiitisha kikao wanapingana naye hawamtii, sasa yeye akawa analazimisha anafokafoka hovyo watu wakaanza kuhama wakahama wakahama akastuka akawaacha akawa hawafokeifokei hovyo lakini ikamsumbua sana kwanini sikuhizi watu wananidharau nikisema kitu hawafanyi. ndipo siku hiyo akakutana na somo langu moja nikaeleza jinsi Mungu anavyoweka utiisho juu ya mtumishi wake na kuwatiisha watu chini yake pia nikafundisha jinsi zinaa inavyouondo utiisho wa Mungu kwa mtumishi na watu kuanza kumuona kama mtu wa kawaida tu. sasa baada ya somo hili ndipo huyu mchungaji akafunguka kufahamu kwamba kumbe kilichokuwa kinamfanya asikilizwe siyo uhodari wala ukali wake bali ni utiisho wa Mungu ambao sasa haupo umemwacha kwasabu ya zinaa, ndipo akamtuma mama wa kanisa aje kuniuliza jinsi ya kufanya maana mama kanisa anaijua ishu yote hivyo hakuweza kumficha ndipo nikamshauri atubu mbele ya kanisa na pia aende kwa askofu mkuu wake akatubu, lakini hakuipenda jia hiyo hivyo hakufanya hivyo na sasa kanisa limekongoloka watu wametawanyika.

ONYO
Dhambi ni dhambi tu hakuna ndogo wala kubwa zoote zitawapeleka watu motoni na ndiyo maana hathii ya zinaa imeorotheshwa pamoja na hizi zingine kama vile uoga, uuaji, kutuamini, nk ilitu kuonyesha kwamba zoote ni sawa na wazitendao wataishia Motoni ila tofauti ya hii ni kwa hapa Duniani tu kwamsabu inamfungulia Sheta mlango na kummiliki mtu kwa haraka zaidi na pia inamfukuza Roho wa Mungu ndani ya mwili wa mtu kwa haraka sana na kumfedhehesha mbele za ulimwengu kwa fedheha isiyoisha siku zote za maisha yake.

WITO WANGU KWAKO.
Achana kabisa na maisha ya dhambi kwasababu yanakuzibia mpenyo wa kufika mahali anakotaka Mungu ufike pia na kukudumaza kiroho, kuacha dhambi ya zinaa ni jambo rahisi sana endapo tu utakubali kuwa mtumwa wa Yesu, na endapo umekuwa unaishi maisha haya machafu tambua kabisa hujaokoka bado haijalishi umeingia kanisani mara ngapi umetoa sadaka na kuomba marangapi hembu amua kuokoka leo sasahivi hapa.

SALA YA KUMKARIBISHA YESU KATIKA MAISHA ATAWALE
Sema Mungu Baba, Hakika mimi ninadhambi nakubali kwamba ni mkosaji, ba hata haya yanayonipata ni kutokana na dhambi zangu, nzitubia dhambi zangu zote namaanisha kuziacha kabusa, Namkataa ibilisi na kazi zake zote kuanzia sasa najikabidhi mikononi mwako Yesu unitawale, Ahsante kwa kunipokea katika Jina la Yesu Amina.
baada ya sala hii sasa umeokoka hivyo tafuta kanisa la kiroho au mtumishi yeyote wa Mungu umwambie ili azidi kukusaidia pia kama utahitaji msaada wamngu nitumie masage uzidi sana kubarikiwa Amina.