Wazazi wanatakiwa kuwa makini na watoto wao hasa wale ambao
wanapenda kuwapeleka watoto shule za kulala (boarding)iwe ya wasichana
wenyewe ama ya wavulana wenyewe,ni
vizuri kuwa makini na kuhakikisha kuwa kila unapompeleka shuleni akirudi hakikisha
kuwa unamsikiliza na kukaa naye ili ufahamu kuwa amekutana na changamoto gani
akiwa huko shuleni.
Wazazi wenzangu nimekaa na kutafakari sana juu ya watoto
wanaopelekwa shule za kulala watoto maana hali ni mbaya katika shule hizo
maarufu kama (boarding).