YESU NI JIBU

Jumatatu, 18 Machi 2013

SOMO LA UAMSHO LIMEANZA KUFUNDISHWA NA MCHUNGAJI MOSSES MAGEMBE

 

 MCHUNGAJI MAGEMBE AKIFUNDISHA SOMO LA UAMSHO KATIKA KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD UKONGA MAJUMBA SITA.

 Somo la uamsho limeanza kufundishwa kwa lengo la kuwafundisha na kuleta uamsho ndani ya Taifa.

Akielezea maana ya uamsho mchungaji Mosses Magembe ambaye ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Majumba sita amesema uamsho ni kuwa hai tena baada ya kufa ambalo limetokana na (neno la kiingereza revival)
maana ya pili ni kurudi kwenye  uzimaa baada ya kufa. Hapa mchungaji Magembe anazungumzia juu ya suala la kanisa kufa kiroho .Aidha alisema kuwa suala la uamsho limepotea ndani ya kanisa la uamsho ilionekana katika miaka 1975 na kuongeza kuwa uamsho umepotea katika Taifa la Tanzania kwa hiyo ni lazima kanisa lirudi katika viwango vya juu sana.Neno uamsho limekuwa likitumiwa kwa muda mrefu nna watumishi mbalimbali bila kujua hali halisi ya neno hilo.Uamsho unawainua watu/waumini upya kuamka kaniaka maisha ya kupoteza fahamu kiroho.












waumini wakifuatilia somo la uamsho kwa makini wakiwa kanisani




 http://www.wapofm.org/wp-content/uploads/2013/03/DSC098761.jpg

TAMASHA LA WAKONGWE LAFANA DAR

 Kongamano la wakongwe ambalo limefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar limekuwa la ajabu sana.
Katika tamasha hilo wameshiriki waimbaji mbalimbali wakongwe ambao waliimba nyimbo ambazo waliziimba na zilivuma wakati wa zamani sana




Mgeni rasmi katika tamasha la wakongwe ndugu Patric Chokara,akizungumza katika tamasha hilo amesema ni vyema waimbaji wakongwe waenziwe maana kazi walizofanya ni njema.


Ndugu Emanuel akiwa na mke wake ambaye ndiye mratibu wa tamasha akizungumza katika tamasha la hilo wakongwe amesema kuwa amekutana na vikwazo mbalimbali wakati akitangaza tamasha hilo



 Mke wa waziri wa uchukuzi Linna Mwakiembe akikabidhi cheti kwa mwimbaji mkongwe wa injili

 Waimbaji wa kundi la New life bendi wawajibika jukwaani.



 Abednogo akipapasa kinanda ktk tamasha la wakngwe


Mchungaji Amon Kilahiro akifurahia jambo na mwimbaji wa New Life Band ndugu Abednego katika ukumbi wa Diamond Jubilee

Waimbaji wakongwe wakifuatilia kwa makini tamasha la wakongwe.


Upendo Nkone akifurahia tamasha la wakongwe.

Mchungaji Safari akiimba jukwaani katika tamasha



Linna Mwakyembe akimkabidhi pastor Safari cheti
 Mwimbaji Mwalukasa akionesha cheti aliyopokea katika tamasha la wakongwe.



Kiongozi wa Messengers bend ndugu Noeli akionesha cheti kushoto mke wa waziri wa uchukuzi Linna Mwakyembe.
 Mchungaji Amon na Upendo Kilahiro akiwa na picha ya pamoja na mtoto wao katika tamasha la wakongwe.
Waimbaji wakongwe wakiwa katika picha ya pamoja katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mchungaji Olgenesi akiwepo kwenye jukwaa baada kupokea cheti.
Mkongwe wa nyimbo za injili mzee makasy wakihojiwa na mwandaaji wa kipindi cha televisheni cha Clouds.