Madiga Timotheo ni mmoja wa waimbaji wa nyimbo za injili wa hapa nchini Tanzania,amekuwa akishirikiana na jeshi la polisi katika kuhamasisha juu ya ulinzi shirikishi ambayo imekuwa ikisaidia sana kuwafichua wahalifu mbalimbali.
Amekuwa pia akihudumu kwenye makongamano mbalimbali ya injili katika sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzania akitumika kueneza injili ya Yesu na pia amekuwa akishiriki shughuli mbalimbali za kiserikali.na pia unaweza kuwasiliana naye kwa shughuli mbalimbali kama mikutano ya injili semina tumia namba 0752187043 na 0714267875.
YESU NI JIBU
Ijumaa, 14 Desemba 2012
Jumapili, 9 Desemba 2012
Hatuwezi kuzuia mfumuko wa “imani Potofu” hata kama zina madhara kiimani
Tafsiri mpya ya msamiati wa
“Imani potofu”
Siku
hizi jamii imeanza kuchanganyikiwa na kile kinachoitwa “kuongezeka kwa imani
potofu” zenye kudanganya na kuathiri imani za wengi kiitikadi.
Kutokana
na uchunguzi wangu binafsi, nimekuja kubaini kwamba, mahali tulipofikia kumbe
tafsiri yake ina utata mkubwa na maana nyingi tena tofauti hata kama matamshi ni yale yale. Ninachotaka kuelezea hapa ni
kwamba, kila inayoitwa “imani potofu” na wengine, kumbe nayo inaziona imani
nyingine nje yake ndizo zimepotoka! Kwa maelezo mengine, tumefikia mahali
ambapo “Usahihi” wa imani yako ni “upotofu” wa imani kwa mwingine aliye tofauti
na wewe kiitikadi.
Ni
kutokana na utata huu, Mamlaka za nchi mbali mbali duniani zilifikia hatua za
ama kupiga marufuku “imani zote” na kubakia dini moja au chache zinazokubalika.
Kisha baadaye ikaonekana huu ni udikteta usiotenda haki kwa binadamu na hivyo likaanzishwa “Tamko la Haki za
binadamu ulimwenguni” ambalo pamoja na mambo mengine limejumuisha “haki ya
kuabudu” na kujiunga au kubadili dini. Kwa mujibu wa tamko hili fursa imetolewa
kuwepo kwa imani nyingi, zilizopo hivi sasa, na kuanzishwa mpya, ili mradi mtu
havunji sheria za nchi
Kwa
kupitia haki ya uhuru wa kueneza imani, kila mtu anapata fursa ya kuchagua au
kuacha, kujitenga au kujiunga na imani ile ambayo anaiona ndiyo sahihi kwa
uelewa na utashi wake binafsi. Kwetu sisi Tanzania, uhuru wa kuabudu ni haki
ya kikatiba.
Baada
ya kutoa maelezo ya msingi kuhusu utata wa tafsiri ya “Imani potofu”; naomba
sasa nije kwenye kuwasilisha tafsiri mpya ya msamiati wa “Imani potofu”.
Tafsiri hii kwa hivi sasa ndiyo inayotumika na sehemu kubwa ya jamii. Tafsiri
yenyewe ni kama ifuatavyo:
“imani yoyote inayokera imani nyingine; na
inapata umaarufu mkubwa kiasi cha kuwa tishio la kuvutia wafuasi wa imani
nyingine kujiunga nayo”
Imani
hiyo inaweza kuwa ni sahihi au potofu kulingana na mtazamo wa kila mtu kwa
itikadi yake, lakini kigezo kinachozingatiwa katika kuibatiza jina la “Imani
potofu”; ni pale ambapo “wafuasi wengi wa imani za dini nyingine wanaondoka au
kuyahama madhehebu yao na kujiunga na imani hiyo” ! Katika harakati za kujaribu
kudhibiti matishio ya imani hiyo, na kuwakinga waumini wao wasijiunge nayo ni
kuitangaza rasmi kuwa ni “imani potofu”
Naomba
nijihami mapema msomaji kwa kusema kwamba, kwa kusema haya sina nia ya
kuhalalisha “Imani potofu” kupitia mada hii. Naomba nisieleweke kwamba sio kila
“imani inayoshawishi maelefu ya watu kujiunga nayo ni sahihi au ni potofu”.
Hoja
ninayotaka kuiweka bayana ni kuhoji uhalali wa matumizi ya kigezo cha
“ushawishi na umaarufu mkubwa” kutafsiriwa kuwa imani husika ni potofu kwa
sababu hiyo tu! Ingelikuwa kigezo hiki kina mantiki, basi tungeweza kutilia
mashaka imani zote zenye wafuasi wengi kuwa zimefanikiwa kwa sababu nazo ni
“imani potofu”!
Mtazamo
wangu, na uzoefu wangu binafsi, imani zote, ziwe potofu au sahihi, ziwe mpya au
za zamani, zote zikiweka bidii kikamilifu katika kujieneza kwa jamii zinaweza
kuwa na wafuasi wengine pasipo kujali sana
usahihi au upotofu wake kiitikadi. Lakini naweza kukubali kwa sehemu kwamba
usahihi au upotofu wa imani unaweza kuchangia kwa kiasi fulani kufuatwa na
wafuasi wengine kwa kutegemea ni mbinu gani ya kimawasiliano inayotumika.
Dhana ya imani potofu kuwa na
wafuasi wengi kuliko imani sahihi
Baada
ya kuelezea tafsiri ya msamiati wa imani potofu kwamba ni ushawishi na umaarufu
wa kupata wafuasi wengi kwa haraka; na baada ya kubainisha waziwazi kwamba nia
ni kujaribu kuwakinga waamini wasihame na kujiunga na imani inayovuma kwa
wakati husika; sasa nije kwenye chimbuko la tafsiri hii iliyoshika hatamu
katika jamii.
Kwa
karne nyingi imekuwepo dhana kwamba, imani potofu ina uwezo wa kuwa na wafuasi
wengi kwa sababu zimetokana na Shetani mwenyewe. Tena yapo na maandiko
yatumikayo katika kusimamia dhana hii ua kwamba hata Yesu mwenyewe alitabiri
juu ya manabii wa uongo ambayo watadanganya wengi. (Math…….) Maandiko mengine
ni ya mitume akina Petro na Paulo yaliyolitahadharisha kanisa kwamba watakuwepo
mitume na manabii wa uongo ambao watatengeneza wafuasi wengi kwa ushawishi na
udanganyifu wao.
Kwanza kabisa, naomba kuthibitisha kwamba ni
kweli imani potofu zinapata wafuasi wengi kwa sababu zimejaa udanganyifu wa
Shetani. Tena naweza kuongezea uzito katika hoja hii kwa kusema kwamba,
kinachofanya imani potofu kupata wafuasi wengi ni kwa sababu hazina masharti
yenye maadili ya kiungu, na zimejaa uwashiwi unaohamasisha tamaa binafsi au
wanaotafuta msaada binafsi.
Lakini,
ninapenda kuzungumuzia udhaifu wa dhana hii. Sio kweli hata kidogo kwamba,
imani sahihi haipati wafuasi wengi kwa sababu yenyewe ndiyo imetokana na Mungu
wa kweli. Ingelikuwa hii ndiyo maana sahihi, basi Yesu Kristo mwenyewe, enzi za
mwili wake duniani, asingefuatwa na makumi elfu ya wafuasi wengi! Maneno yake
na mafundisho yake yalikuwa magumu na mifano mingi ilikuwa na mafumbo lakini
bado umati mkubwa wa watu ulimfuata na kumsikiliza na kushuhudia kwamba huyu ni
Mwalimu kweli kweli!
Kana
kwamba hii haitoshi, baada ya kufufuka na kupaa kwake, mitume wake nao
walitengeneza maelfu ya wafuasi na wanafunzi wengi kama
ilivyokuwa nyakati za Yesu mwenyewe. Kanisa la kwanza lilianza kwa kishindo cha
wafuasi 3000 kwa siku moja na katika muda wa miaka 40 mfululizo lilikuwa na
wafuasi wasiopungua 30,000 wanaokusanyika kwa wiki jijini Yerusalemu!
Ni
nini ninachotaka kusema hapa? Napenda kuweka bayana ukweli huu, kwamba hata
“Imani sahihi katika Kristo”, kama kweli kweli ikihubiriwa kwa usahihi kama Yesu na mitume wake wa kwanza; kazi zile zile
zilizofanyika enzi za karne ya kwanza pia zitatendeka hata sasa. Kwa matokeo
hayo makumi elfu ya watu wataikimbilia imani hii kwa wingi kama
ilivyokuwa karne ya kwanza.
Pamoja na ukweli kwamba “Imani potofu” zina
ushawishi wa kupata wafuasi wengi; lakini sio kwamba hao wafuasi wenyewe hutoka
kwenye imani sahihi na kisha kuijunga na imani potofu! Wengi wao hawakuwahi
hata kuijua “imani sahihi” tangu kuzaliwa kwao na ndio maana ni rahisi kwao
kujiunga na imani nyingine potofu!
Kwanini imani potofu
zimeruhusiwa
kuwepo sambamba na imani sahihi?
Kitu
ambacho kinatatiza watu wengi na hasa wale ambao ni wapenzi wa imani sahihi, ni
kuona jinsi ambavyo imani potofu zinaendelea kufumuka na kuendelea kupoteza
wafuasi wengine wasioijua au kuwa na imani sahihi. Wengine wanafunga na kuomba
wakijaribu kudhibiti ongezeko la imani potofu. Hata hivyo, ukweli halisi bado
imani potofu zinaongezeka kila siku.
Ningependa
kujibu swali hili gumu kwanza kwa kutahadharisha athari zitokanazo na shinikizo
la kutumia nguvu za dola kudhibiti imani potofu. Kujaribu kudhibiti mfumuko wa
imani potofu kupitia nguvu za Dola, kwanza ni kinyume cha katiba na tamko la
haki za binadamu. Pili, kila itikadi katika dini inatafsriwa kuwa potofu na
itikadi nyingine zinazotofautiana kiitikadi. Tatu nitalieleza kwa mujibu wa
mafundisho ya Bwana Yesu Kristo. Kabla sijaanza kufafanua hebu tuyasome maneno
ya Yesu kwa mfano alioutoa:
“Akawatolea
mfano mwingine, akisema, ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu
njema katika konde lake; lakini watu walipolala akaja adui yake akapanda magugu
katikati ya ngano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa,
yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana,
hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia
adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, basi wataka twende
tuyakusanye? Akasema la; msije mkakusanya magugu na kuzing’oa ngano pamoja
nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno
nitawaambia wavunao, yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome;
bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.” (Math.13:24-30)
KANISA LACHOMWA MARA TATU MARA TATU LIKIKARABATIWA HUCHOMWA TENA WAHUSIKA WADAIWA NI WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU
Wakati serikali ikijitahidi kukabiliana na vitendo vya uchomaji
moto makanisa nchini vinavyofanywa na baadhi ya wanaharakati wa Kiislamu,
imebainika kuwa Kanisa la Salvation
Ministry for all Nations (SMAN) lililoko Mbezi Juu Jijini Dar es Salaam, limechomwa moto zaidi ya mara
tatu.
Uongozi wa Kanisa hilo umelimbia Gazeti hili kuwa licha ya
matukio hayo ya hujuma wanazofanyiwa na waumini wa Kiislamu kutoka katika
msikiti wa Al Mubarak ulioko jirani na Kanisa hilo, usiku wa Jumapili iliyopita
ya Desemba 2, 2012 , waumini hao walilibomoa Kanisa hilo na kufanya jaribio
jingine tena la kulichoma moto.
Kwa mujibu wa Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo
la SMAN Freddy Mwamtembe na Msaidizi
wake Mch. Eliya Sudi, matukio matano ya hujuma mbaya dhidi yao yameripotiwa katika vituo vya polisi Mbezi
Juu na Kawe na kufunguliwa majalada yanayoeleza
jinsi hujuma hizo zilivyofanyika kwa muda na nyakati tofauti.
Hujuma ya kwanza ya uharibifu mali na uchomaji moto wa
Kanisa hilo iliripotiwa katika akituo cha polisi Kawe Februari 25, 2012 na kufunguliwa jalada nambari KW/RB/1743/2012
la kuchoma moto choo cha kanisa hilo,
ambapo jalada la pili la siku hiyo hiyo lilifunguliwa katika kituo cha Polisi
Mbezi Juu likiwa na nambari MBJ/RB/586/2012 likitaarifu juu ya tukio la
kuchomwa moto Kanisa hilo na kuharibu mali majira ya saa saba usiku.
Jalada jingine lilifunguliwa Machi 10, 2012 katika kituo cha
Polisi Mbezi juu na kupewa nambari
MBJ/RB/714/2012, likitoa taarifa juu ya hujuma ya kuchomwa moto kwa Kanisa hilo
la SMAN.
Hujuma nyingine lililofanyiwa kanisa hilo imo katika jalada
la kituo cha Polisi Kawe lenye nambari KW/RB/7974/2012 kama taarifa ya tukio lililofanywa Agosti 12, 2012 na waumini
28 wa msikiti wa Al Mubarak kwa kuvamia ibada,
kujeruhi waumini na kuharibu mali za Kanisa hilo, ambapo Mchungaji Msaidizi
Eliya Sudi alijeruhiwa akiwa madhabahuni.
Aidha uongozi wa Kanisa hilo ulilikabidha gazeti hili waraka
unaoelezea jinsi waumini wa msikiti huo wanavyoshirikiana na mama mmoja
kulifanyia fujo kwa kufukia msingi wa jengo lake na kisha mama huyo kuchimba
msingi na kuanza ujenzi wa nyuma yake katika kiwanja cha Kanisa hilo.
Uongozi huo wa Kanisa la SMAN ulisema ulilifikisha suala hilo katika ofisi
ya Serikali ya Mtaa wa Ndumbwi kupitia
mjumbe wa nyumba kumi shina namba 40 Mbezi
Juu Bwana Bonifasi Matiku kwa ajili ya
utatuzi, lakini hawakupatiwa msaada wowote, hadi ikabidi wamwandike barua Afisa
Mtendaji wa kata ya Mbezi Juu, kumtaarifu juu ya kiwanja cha kanisa lao kuvamia
na mama huyo ambaye kwa sasa jina lake limehifadhiwa.
Mjumbe huyo alidhibitisha juu ya kuwepo kwa hujuma dhidi ya
Kanisa hilo na
hatua alizochukua,ambapo liitaka serikali kutumia sheria ili kukabiliana nazo
na kuzikomesha.
“Nakumbuka siku nilipofika ofisini kwa Mtendaji wa Kata ya Mbezi Juu, niliishia kutukanwa na wajumbe niliowakuta
pale (majina tumeyahifadhi kwa sasa), wakinieleza mbele ya Mtendaji huyo kwamba
ni lazima mama huyo atajenga katika eneo
la kiwanja chetu cha Kanisa. Nilimtahadharisha Mtendaji juu ya matusi
niliyotukanwa lakini akanitaka niondoke akidai atashughulikia suala hilo. Mwandishi hadi leo hakuna kilichofanyika”, alisema
Mchungaji Mwamtembe.
Alisema tayari amelifikisha suala la hujuma za Waislamu dhidi ya Kanisa lake katika
ofisi za Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni alikoahidiwa kushughulikiwa
haraka kwa mujibu wa sheria.
“Kwa kweli sisi Wakristo ni wavumilivu sana kwa vile tunapenda amani na utakatifu.
Tunaiomba sana
serikali iwashughulike watu hawa wachache wasiopenda amani na wanaochochea
vurugu za kidini. Ugomvi wa kidini ni mbaya sana. Tunaomba serikali iwe makini katika
hili”, alisema Mch. Mwamtembe.
Alisema waumini hao korofi wa Kiislamu wanaolihujumu Kanisa lake
kwa kulichoma moto, kuharibu mali na kujeruhi
washirika ni watu wanaofahamika wazi na hufanya hujuma hizo wazi wazi,
wakitamka wazi kuwa hawataki Kanisa
katika maeneo yao; jambo ambalo ni kinyume kabisa na Katiba ya nchi inayoruhusu uhuru wa kuabudu kwa kila mtu
Mmoja wa Mashehe wa Msikiti
wa Al Mubarak Mbezi Juu aliyetajwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha
waumini wake kulihujumu kanisa la SMAN, hakuweza kupatikana kutokana na
kutofika msikitini hapo kwa uwazi, akiogopa kukamatwa na Polisi wanaomsaka.
Aidha juhudi za kumpata mama aliyetajwa kushirikiana na
waumini wa msikiti wa Al Mubarak kulihujumu kanisa hilo hazikuzaa matunda, kutokana na makazi yake kutojulikana.