YESU NI JIBU

Jumanne, 24 Septemba 2013

KUJARIBIWA SIO DHAMBI,DHAMBI NI KUANGUKA MAJARIBUNI:

  KUMTUMKIA MUNGU NA KUSHINDA MAJARIBU:

Imeelezwa kuwa suala la kumtumikia Mungu na kumwabudu ni la mwanadamu mwenyewe ambaye amejitakasa na kuacha njia zake mbaya,na hapo pia atawepata baraka zake za kiungu pale atakapo tii na kufuata sheria na taratibu za Mungu.

hayo yalinenwa na mchungaji Peace Mazinde kutoka Mombasa kenya wakati akifundisha katika kanisa la Mabibo Sahara TAG katika ibada ya jumapili ambapo alikuwa akihitimisha semina ya wiki moja iliyoendeshwa kanisani hapo.

Aidha alisema kuwa hapo Yesu alipokuwa duniani hajaomba kili waumini ama wafuasi wake wasiingie majaribuni ila aliomba ili washinde majaribu na kuwapa tuzo wale wanaoshinda majaribu,ambapo aliongeza  kuwa, kujaribiwa  sio dhambi, dhambi ni kuanguka majaribuni,

Akinukuu kitabu cha 2 nyakati 15:1-2 alisema kuwa kuna mambo matati ambayo muumini anatakiwa kuyafuata na kuzingatia katika maisha yake ya ukristo siku zote na hapo ataweza kuwa mwamini mzuri wa kristo.

ya kwanza ni kujitakasa,pili ,kunyenyekea na tatu ni kujiachia kwa Bwana na ukifuata hayo kama mwamini utamp-endeza Mungu alisema,

na kwa ujuma alisema jukumu la kutunza wokovu wako ni lako mwenyewe sio la kiongozi wako wa dini sio askofu mchungaji mwinjilisti wala nani ni lako mwenyewe. 

   Hapa mchungaji Peace Mawinde akifundisha katika ibada.mchungaji Mazinde akihubiri neno kanisani.

 

 

 

;

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Sahara Mabibo TAG askofu Jofrey Masawe akihimiza jambo kwa waumini hawapo pichani katika ibada ya jumapili

Mke wa Askofu Masawe mchungaji OLiver Masawe mfupi akiwa na Atho Dave ambaye anaishi Australia na familia yake alipotembelea kanisani hapo.

 Kikundi cha kusifu na kuabudu wakihudumu madhabahuni.

Waumini wakimsifu na kumshangilia Mungu katika ibada ya kusifu na kuabudu.






Jumapili, 1 Septemba 2013

MWILI WA SHUJAA WA INJILI WAAGWA JIJINI DAR ES SAALAM KATIKA VIWANJA NYA KANISA LA EAGT TEMEKE.

Katika hali ya kusikitisha waamekusanyika waumini mbalimbali pamoja na viongozi wa kisiasa,kiserikali maaskofu wameungana kuuaga mwili wa shujaa wa injili askofu Dr Moses Kulola katika viwanja vya kanisa la EAGT Temeke jijini Dar es saalam.
Wakielezea kwa nyakati tofauti tofauti walivyomfahamu Dr Kulola wengi walisema amekuwa akifanya kazi ya injili kwa uaminifu kwa muda wote bila kuangalia suala la fedha wala maslahi yake.
Kwa mrefu wakati wa uhai wake alikuwa akipinga vikali suala la watumishi wa mshahara na wale wanaojiteua na kujiita kwa majina ya mitume na manabii.
Watumishi mbalimbali wa serikali na siasa,viongozi wastaafu ,wabunge,wakuu wa mikoa walihudhurika katika mazishi hayo,maaskofu wa makanisa mbalimbali na wachungaji,mitume,manabii pamoja na waumini mbalimbali walifika katika viwanja vya EAGT Temeke kuuaga mwili wa marehemu askofu Dr Moses Kulola.
Askofu Dr Moses Kulola alizaliwa tarehe 02 June 1930 na kufariki dunia tarehe 29 August 2013 jijini Dar es saalam.
 SHUJAA WA INJILI AAGWA JIJI DSM TAYARI KUELEKEA MWANZA KWA MAZIKO.
Kushoto ni mke wa marehemu askofu Dr Moses Kulola.


  Askofu wa WAPO Mission International Askofu Silverster Gamanywa akimfariji mke wa marehemu moses Kulola.
 Askari wa usalama barabarani akiongoza masafari wa magari wakibeba mwili wa marehemu askofu Kulola.
   Hili ndilo gari lilobeba mwili wa askofu Kulola.
Jeneza alimowekwa mwili wa askofu Kulola na mbele ya jeneza kushoto anaonekana askofu Gamanywa mwenye shati lenye alama nyeupe na nyeusi wakiwa katika hali ya maombi.

  Mtoto wa kwanza wa askofu Moses KUlola,Ndugu William Moses akilias kwa uchungu mara baada ya mwili wa askofu kuwasili ktk viwanja vya kanisa la EAGT Temeke.


Picha ya Askofu Dr Moses Kulola enzi za uhai wake.

Mchungaji wa kanisa la mlima wa moto mikocheni B Assemblies of God akiwasili katika viwanja vya EAGT Temeke kuuaga mwili wa askofu mkuu wa EAGT Moses Kulola.

 Mchungaji Getrude akisaini kitabu cha maombolezo.


Askofu Silverster Gamanywa katika akiwa na maaskofu wenzake.


 Makamu askofu wa Tanzania Assemblies of God askofu mhiche akizungumza katika ibada ya kuuaga mwili wa askofu Dr Moses Kulola nyuma aliyekaa mwenye shati jekundu aliyeshika mdomo ni mchungaji wa Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.
Mzee wa Upako mcungaji Atony Lusekelo akitia saini kwenye kitabu cha wageniu cha maombolezo.

Askofu mkuu wa kanisa la Full Gospel Tanzania askofu Zakaria Kakobe.

 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.Gharib Bilali akiwa anaingia katika viwanja vya kanisa la EAGT Temeke.
Makamu wa rais akisaini kitabu cha kumbukumbu cha wageni.

Mhe. makamu wa rais Gharib Bilali akitoa salamu za pole katika viwanja vya EAGT.
Mchungaji Florian Katunzi akisoma neno la Mungu katika viwanja vya kanisa EAGT Temeke.
Wajukuu wa marehemu askofu Moses Kulola





Askofu David Mwasota mwenye suti blue akiwa na mchungaji Josephat Gwajima ambapo walishiriki katika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Dr kulola.

Askofu Silverster Gamanywa wakiteta jambo na katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dr Wilbrod Slaa.


Askofu wa Full Gospel askofu Zakaria Kakobe akiwa na mzee ambaye alikuwa akishirikiana na Dr Moses Kulola kwenye injili
Akofu Elias Chesa mwenye shati jekundu kulia akiwa na askofu mwenzake.