YESU NI JIBU

Jumatatu, 16 Mei 2016

UMOJA WA WANAUME TAWI LA BUGURUNI WAUNGANA NA KUTOA ZAWADI KWA KANISA NA PIA KUSOMESHA MWANAFUNZI WA CHUO CHA BIBLIA:

Umoja wa wanaume CMF wakiwa katika picha ya pamoja na mchungaji wao kiongozi pamoja na mke wake na viongozi wa umoja huo,
Chama cha wanaume CMF kimefanya shughuli ya kujitolea na  kufanya usafi katika eneo la nyumba ya mchungaji pamoja na kusaidi kanisa kwa kununua viti vya kanisa ya watu wazima na vya watoto.
Akizungumza katika ufunguzi wa sherehe hizo mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Buguruni mchungaji amesema kuwa idara hiyo ya wazee imekuwa msaada mkubwa sana katika kanisa la mahali pamoja na kuomba kanisa la TAG taifa kusimamia nafasi hiyo kwa umakini maana imekuwa msaada kwa jamii.


Akifundisha katika ibada ya CMF bwana Masuninga alisema kuwa ushirika ni jambo la muhimu katika ushirika wowote maana itasaidia wengi kutambua nafasi zao.
Aidha aliongeza kuwa kila mtu au mwamini akijikita katika ushirika ni rahisi kufanikiwa na kuinuliwa hasa pale atakapojitambua kuwa ni kwa nini amejiunga na ushirika kwani ndiyo inayompelekea mwanaume kujitambua katika nafasi yake.
"mwanaume unatakiwa ujioneshe kuwa wewe ni mwanaume kwa kushiriki katika majukumu mbalimbali ya kanisa,familia na hata jaifa kwa ujumla",alisema bwana Mwasuninga.
Aliongeza kuwa ushirika inapelekea mtu kujijengea ujasiri na uhodari pale atakaposhirikiana na wenzake na kujitambua kuwa ni kwanini yupo katika ushirika huu.
Pia alisema kuwa ni vyema mwamini kukaa mbele za mungu kila unapopata muda badala ya kushabikia mambo ya ulimwengu huu kama vile wengine wanakuwa na muda mwingi wa kushabikia mpira na kusahau hata kutenga dakika kadhaa za kumwomba Mungu awasaidie katika maisha yao ya kila siku.
Naye mwenyekiti wa CMF Mathew Mhagama alisema kuwa tangu 2006 chama hicho kimeonesha mafanikio makubwa maana lengo la idara hiyo ni kumtumikia Mungu katika nyanja mbalimbali kama vile kumtegemeza wachungaji,kuwatembelea waatoto yatima na pia kuwasaidia kuwasomesha wale watakao kuwa na uhitaji.
Aliongeza kuwa katika wiki ya CMF waliweza kutumika na kufanya usafi katika eneo la nyumba ya mxhungaji kiongozi na kuhakikisha kuwa mazingira yamekuwa mazuri na safi.
Aliwasii vijana kujiunga na chama cha CMF ili wapate ujuzi na elimu ambayo itakuwa inatolewa na CMF hasa inayohusiana na ndoa malezi maana vijana wengi wamekuwa wahanga katika suala la mahusiano.
CMF buguruni walinunua viti vya kanisa vya watu wazima na vya watoto kama.zawadi kwa kanisa na ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya mwaka huu kitaifa 2016ni basi uwe hodari jioneshe kuwa mwanaume 1wafalme 2:2

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni