Hirizi ambazo zilitapikwa na mmoja wa watu waiofika kanisani na kuanza kuombewa na mara baada ya kutapika alianza kufunguliwa.
YESU NI JIBU
Ijumaa, 29 Julai 2016
JIMBO LA TEMEKE LIMEONYWA KUWA MAKINI NA MGOGORO UNAOENDELEA AMBAO TAYARI UPO UMEFIKISHWA MAHAKAMANI:
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa kansia la EAGT, Mzee Henri
Mfuko, ameonya kuwa kansia hilo linakabiliwa na hatari ya kugawanyika kufuatia
mgogoro ulioibuka baina ya uongozi wa kanda na ule wa Jimbo la temeke ambao
umesababisha kufunguliwa kwa kesi ya madai mahakamani na kusimamishwa kwa
viongozi wa Jimbo. Huku ikielezwa kuwa kivuli cha Hayati Askofu Dk. Moses
Kulola ndicho kinacholityesa kanisa hilo.
Aidha imeelezwa kuwa
Wothia alioandika kulola Kabla ya kufariki dunia unaompa Katunzi
kijititi cha kuhubiri Injili, kukua kwa kasi kwa kansia la EAGT City Centre na
mpango wa kujenga majengo ya kisasa ya Jimbo la Temeke viliibua upinzani
mkubwa uliopelekea kuvuliwa madaraka
na kugawanywa kwa Jimbo bila kufuata taratibu.
Ni kwa sababu hiyo, Askofu Katunzi na wenzake waliamua kufungua
shauri la madai Mahakamani na ikatolewa amri ya kuzuia mkutano lakini haikuheshimiwa na badala yake mkutano ukafanyika na viongozi wa muda
wakateuliwa.
Imechapishwa na
Amaninafuraha
kwa
15:07
Hakuna maoni
:
Tuma Hii kwa Barua pepe
Blogu Hii!
Shiriki kwenye Twitter
Shiriki kwenye Facebook
Shiriki kwenye Pinterest
Lebo:
Askofu Dk. Kulola
,
Askofu Katunzi
,
Katibu wa Kanda ya Mashariki na Kusini ya kanisa la EAGT
,
Mch. Dk. Alphonce Askofu Nicodemus Nyenye
,
Mwanjala
,
Mzee Henri Mfuko
Alhamisi, 28 Julai 2016
PAPA FRANCIS AANGUKA GHAFLA AKIONGOZA MISA POLAND
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amepata ajali ya kuanguka ghafla alipokuwa akitembea kuelekea kwenye jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuendesha ibada, Czestochowa nchini Poland.
Jumanne, 26 Julai 2016
Jumamosi, 16 Julai 2016
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI NA WATENDAJI WA TAASISI ZA SERIKALI NA AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WA POLISI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1. Mhe. Augustino Lyatonga Mrema.
· Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
· Mhe. Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.
2. Prof. William R. Mahalu
· Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
3. Prof. Mohamed Janabi
· Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
4. Prof. Angelo Mtitu Mapunda
· Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
5. Bi. Sengiro Mulebya
· Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
6. Bw. Oliva Joseph Mhaiki
· Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
7. Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa
· Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
8. Dkt. Charles Rukiko Majinge
· Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
9. Dkt. Julius David Mwaiselage
· Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
DK. KIGWANGALLA- “TUTATATUA MGOGORO WA WANAKIJIJI NA HIFADHI YA MSITU WA IPALA KWA MAZUNGUMZO”
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili kwenye kijiji cha Ipala huku akipokelewa na baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo.Msululu wa wananchi wakiwa wamempokea Dk. Kigwangalla wakati akiwasili kwenye kijiji cha Ipala.