Mapanga
yatumika kulinda Kanisa alipozikwa Ask.Kulola,
Miaka mitatu na siku 50 hivi, tangu Askofu Mkuu na
Mwanzilishi wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) DK.
Moses Kulola kumaliza kazi hapa duniani, (kufariki) hali si shwari ndani ya
kansia aliloacha, baada ya Makamu Askofu Mkuu, John Maene kufukuzwa katika
uongozi na uchungaji katika kanisa la Bungando, Mwanza, lilipo kaburi la
mwanainjili huyo na kuzua kiza kinene katika mustakabali wa kiroho.
Habari za ndani toka ndani ya kanisa hilo zinaeleza kuwa
tangu kutwaliwa kwa kiongozi huyo, ilizuka hali ya sintofahamu kwa kile
kilichodaiwa kuwa ni kutoelewana baina ya wale wanaoelezwa kuwa ni “wa Kulola”
yaani wafuasi wake sugu na wale wa
kizazi kipya kinachotaka kubadili mambo na kujenga himaya mpya.
Ni katika hali hiyo, hivi karibuni aliyekuwa Makamu Askofu
Mkuu wa Kanisa hilo, John Maene, alifukuzwa uongozi na uchungaji kwa kile
kilichodaiwa kuwa alipatikana na tuhuma za ukiukaji wa kimaadili, lakini
akapinga tuhuma mbele ya Halmashauri ya kanisa na kasha kufungua Kesi katika
mahakama Kuu kanda ya Mwanza.