YESU NI JIBU

Jumatano, 22 Januari 2014

ENDELEA NA FALSAFA MILIKISHA KWA MUJIBU WA BIBLIA KAMA UNAVYOLETEWA NA ASKOFU GAMANYWA SEHEMU PILI

Falsafa ya umikilishaji kwa mujibu wa Biblia

Katika toleo lililopita tulianza hoja hii kuhusu falsafa ya kumilikisha kwa mujibu wa Biblia. Aidha, tulipitia vipengele vya Mpango wa kwanza wa Mungu kwa binadamu na jinsi ulivyolenga kumfanya binadamu kutawala nchi na vitu vilivyomo. Kisha tukapitia anguko la binadamu wa kwanza na athari zake. Sasa katika toleo hili tunaendelea na sehemu ya pili kuhusu mpango wa pili wa Mungu wa ukombozi wa binadamu na matokeo yake:

Mpango wa pili wa Mungu ukombozi wa binadamu
Baada ay binadamu wa kwanza kupoteza haki, mamlaka na fursa za kumiliki, na kusababisha athari mbaya za mapigo ya magonjwa na umaskini wa kipato; Mungu aliamua kuonesha upendo wake kwa binadamu kwa kumtuma Mwanawe Pekee ulimwenguni kama tunavyosoma: “Kwa maana jinsi hii, Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na zima wa milele.” (Yh.3:16)
Ujio wa Yesu Kristo duniani ulibeba misheni yenye mambo mawili muhimu ambayo binadamu aliyapoteza ambayo ni: i) Kurejesha mahusiano yaliyovunjika kati ya binadamu na Mungu ii) Kurejesha mamlaka aliyonyanganywa binadamu na Ibilisi.
Kwa habari ya kurejesha mahusiano yaliyovunjika kati ya binadamu na Mungu, Yesu Kristo alikuja akiwa kufanyika dhabihu ya dhambi iliyomtenga binadamu na Mungu kama ilivyoanidkwa:“Siku ya pili yake akamwoma Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama Mwakandoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yh.1:29)
Kupitia mateso na kifo cha Yesu Msalabani, Yesu aliupatanisha ulimwengu na Mungu kwa yeye kulipa fidia ya adhabau ya dhambi, tena ya kosa la binadamu wa kwanza. Lakini kwa Yesu kushuka kuzimu na kufufuka katika wafu kulisababisha kurejeshwa mamlaka zote zilizoporwa na Ibilisi pamoja na haki ya kumiliki.
Mtume Yohana aliyekuwa mwanafunzi aliyependwa sana na Yesu, anatusimulia katika Injili aliyoiandikwa akisema kwamba, ujio wa Yesu Kristo ulilenga kurejesha mamlaka ya kifalme kwa wote watakaomwamini Yesu Kristo:“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.” (Yh.1:11)
Tendo la mtu kufanyika mtoto wa Mungu limebeba ahadi na mamlaka ya kumiliki mali za mfalme, ambaye ni Mungu Baba, kwa kupitia Mwanawe Pekee. Huwezi kufanyika mtoto wa mfalme ukaendelea kuishi maisha ya ufukara, labda kama unafanya igizo!
Majibu ya maswali nyeti kuhusu falsafa ya kumiliki
Ninafahamu kwamba yako maswali sugu tena ya miaka mingi ambayo huulizwa na kila mwenye mashaka na falsafa ya kumiliki. Maswali hayo ni kama haya yafuatayo: i) Hivi huu Ukombozi wa Yesu Kristo kwa binadamu ni maisha ya sasa au siku ya kiyama? ii) Kwanini wengi wanaodai kumfuata Yesu Kristo maisha yao ni yale yale ya mateso na umaskini wa kipato? Iii) Je Yesu mwenyewe si alishasema kuwa ulimwenguni tunayo dhiki, na mitume wake nao wakathibitisha kwamba tunaingia mbinguni kwa njia  ya dhiki nyingi? 
Majibu ya maswali haya ni muhimu sana kwa kila asomaye makala haya, na bila shaka atapata fursa ya kuzipima nadharia zilizopo na majibu yangu:
1. Majibu ya ukombozi wa Yesu ni maisha ya sasa au siku ya kiyama?
Ukombozi wa Yesu Kristo kwa binadamu ni maisha ya sasa na kilele chake ni kunyakuliwa kwa kanisa duniani. Ukifuatilia kwa makini katika Injili zote kuhusu maisha ya Yesu Kristo duniani, utakuta alihubiri Injili ya ufalme iliyoambatana na udhihisho wa mamlaka ya kifalme katika kutatua matatizo sugu matatu: kusamehe dhambi, kuponya ulemavu na magonjwa yote; na kushughulikia mahitaji ya chakula yalipojitokeza. 
Aidha, kanisa la kwanza lililoanzishwa na mitume jijini Yerusalemu nalo lilidhihirisha maisha ya kifalme kwa kuhakikisha watu wanatubu dhambi na kuzaliwa mara ya pili, kuponywa magonjwa yote, na kila aliyejiunga na kanisa hilo aliacchana na umaskini wa kipato. Kwa hiyo maisha ya ukombozi wa Yesu Kristo yanaanzia hapaa hapa duniani kama yalivyodhihirishwa na Yesu Kristo, mitume wake na wakristo wa kanisa la kwanza! 
Hata hivyo, bado mchakato wa kumiliki unaendelea na utafikia kilele chake wakati Yesu Kristo atakapolichukua kanisa lake na kwenda kukaa nalo pale mahali aliposema anakwenda kuliandalia makao.
Kwa kusema haya, sipuuzii uhalisia wa mambo jinsi yanavyoonekana kwa macho hapa duniani kwa hivi sasa. Uhaalisia unaonesha jinsi ambavyo maisha ya wengi waitwao wachaji Mungu, wafuasi waamini wa Yesu ni duni na kujaa changamoto nyingi za kiuchumi. Mimi pia nimepitia maisha haya haya tangu mwanzoni mwa uchanga wa imani yangu katika Kristo na mapokeo niliyofundishwa hapo awali.
Naomba nijibu sio kama majivuno bali kwa unyenyekevu mkubwa kwamba, changamoto zote zinazoonekana hivi sasa, hazitokani na wala sio sehemu ya Injili ya Yesu Kristo na Mitume wake. Haya ni matunda ya ukengeufu wa karne nyingi huko nyuma ambao ulizalisha “Ukristo bandia” katika ulimwengu huu! 
Nadhari ya kwamba, maisha ya dhambi na umaskini ndio dhiki za mkristo duniani mpaka Yesu atakaporudi mara ya pili ni matokeo ya ukengeufu ule ambayo Yesu Kristo mwenyewe aliutabiri kuwa utakuja na kuwakumba walio wengi! Kumbukeni mfano wa ngano na magugu ambao Yesu aliwaambia waanfunzi wake na tafsiri aliyoitoa. 
Ukristo bandia umeshika nafasi kubwa ulimwenguni kwa kuwaaminisha watu kuishi katika dhambi kisha kuungama na kuendelea maisha ya dhambi kanisani; badala ya kuzaliwa mara ya pili na kupokea uwezo wa kushinda dhambi (wanaona  ni fahari kuitwa wenyedhambi)
Hata kwa wale wanaopokea neema ya kuujua Ukristo wa kweli, na kuzaliwa mara ya pili, kwa sababu ya mapokeo ya ukristo bandia, bado huendelea kuaminishwa kwamba, maisha ya umaskini wa kipato ni njia mojawapo ya utakatifu, na kumiliki uchumi na tamaa za kiulimwengu. Kwa imani hii, huendelea kuishi maisha duni, ambayo matokeo yake walio wengi huiacha imani na kurudi duniani. Mungu atusaide sana!!!
Lakini tukumbuke kwamba KANISA LA KWANZA kwa muda wa miaka 40 mfululizo, likiwa na zaidi ya washirika 30,000 lilidhihirisha maisha ya ukombozi wa Kristo duniani; dhambi ilikemewa, wagonjwa wote waliponywa, na hapakuwepo na maskini wa kipato!
2. Majibu kuhusu dhiki iliyotajwa na Yesu na mitume wake
Neno hili “dhiki” limekuwa likitafsiriwa kinyume ili kuhalalisha maisha ya mikandamizo ya kipepo, nagonjwa na umaskini wa kipato kwa wachaji Mungu kanisani. Yametumika kama faraja lakini nyuma yake ni mbinu za adui za kufanya wahusika kuchukuliana na maisha haya kwa kudhani ni mapenzi ya Mungu wawe hivyo haoa duniani! 
Kwa kifupi Maneno ya Matoleo ya Biblia za Kiingereza yaliyotumika kutafsiri neno hili “dhiki” ni “hard times” “persecutions” na “tribulations”! Tafsiri ya maneno haya ni “Nyakati ngumu”, “mateso” na “mateso makali” au adha! Hapa hatusomi habari za dhiki kuitwa “magonjwa” wala “maskini uliokithiri”!
Baadhi ya maandiko ambayo yametumiwa sana ni kauli ya Yesu Kristo aliwapowambia kwmaba: “..Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.” (YH.16:33)
Maana ya neno “dhiki” lililotajwa hapa ni upinzani mkali dhidi ya imani katika Kristo wenye kuambatana na vitisho, na mateso ya mapigo ya viboko, na vifungo  vya gerezani. Hii ndiyo dhiki aliyomaanisha Yesu. Isitoshe, Yesu aliwoanya pia wanafunzi wake kwamba sio kwamba watateswa kwa sababu ya imani yao kwake, bali hata kuuawa pia: “watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.” (Yh.13:2)
Baada ya Yesu kupaa, na mitume wake kuchukua nafasi ya kuhubiri Injili ambayo ilikuwa imepigwa marufuku na wakuu wa dini na dola, ndipo yalipotimia maneno ya Yesu Kristo ya kupatwa na “dhiki nyingi” ambazo zimetajwa na Luka alipoandika: “Wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.” (Mdo.14:22) 
Majumuisho ya majibu ya maswali
Kama nilivyokwisha kuanisha hapa juu, falsafa ya kumilikisha ni urithi wa Agano Jipya kwa wote wanaomjia Yesu Kristo. Ukombozi wa Yesu Kristo unajumuisha msamaha wa dhambi, unaosababisha kufutwa kwa adhabu ya maradhi na umaskini wa kipato. Jamii ya waaminio imeahidiwa kuishi maisha ya kifalme duniani na kilele chake ni mbinguni Yesu atakapolichukua kanisa lake. Dhiki inayotajwa duniani sio umaskini wa kipato bali chuki na upinzani dhidi ya imani unaoambatana na vitisho na mateso ya kimwili pamoja na kuuawa inapobidi.
Katika makala nyingine baada ya hii, nitaongelea changamoto za “Injili ya utajirisho” iliyojengwa kwenye “utoaji wa mali na fedha” kuwa ndiyo njia pekee ya kupata utajiri duniani. Aidha tutapitia maswali tata yanayohoji: Kwanini wanaotoa sadaka hawapokei matokeo ya utoaji wao kama wanavyoahidiwa? Je! Kwanini “utoaji wa siku hizi” unaonekana kuwanufaisha “wapokeaji” kuliko “watoaji”? Na utoaji ulio kamili wenye matokeo kama ilivyoandikwa katika Biblia ukoje? Nitaweka bayana tofauti kubwa iliyopo kati ya “Falsafa ya kumiliki” na “Injili ya utajirisho”!

Itaendelea toleo lijalo

Ijumaa, 17 Januari 2014

JE HUU NI UNABII AMA NI KITU GANI, KUWALISHA WAUMINI NYASI NA KUTAPISHA?

Hivi ndivyo hali halisi katika huduma ya Rabboni ya huko Afrika ya kusini ambapo kwa taarifa yako waumini wake wanaambiwa kuwa wakati wa kufunga na kuomba,pesa zile ambazo utatumia kwa kunywa chai ,chakula cha mcha na cha jioni fanya  mahesabu na kuwapelekea watu wanaopita katika mapito magumu na kuwapa sio kupeleka kanisani ila wape wao wasio nacho.
Huduma hiyo inayongozwa na kiongozi wake anayefahamika kwa jina la Lesego Daniel imekuwa ya namna yake jambo ambalo linaweza kuwa la kushangaza sana katika imani.
Ila yeye alikinukuu kitabu cha Yohana 14:12-14 ambayo inazungumzia pale YESU alivyosema kuwa yeye aniaminiye mimi na kazi nizifanyazo mimi yeye naye atazifanya naam na kubwa kuliko hizo atafanya kwa kuwa mimi naenda kwa BABA.
Sasa ndugu msomaji wangu hofu yangu ni hapa kulisha waumini nyasi je huo ndio unabii ama ni nini? ndiyo matendo ya kinabii au ndiyo matendo mkuu.





Hayo ndiyo yanayoendelea ndani ya huduma ya Rabboni center ministries ya huko Afrika ya kusini kazi kwako msomaji.






Mchungaji Lesego akitembea juu ya waumini wake



 Hapa zoezi la maombi na maombezi linaendelea mchungaji Lesego kupita juu ya waumini kwa kuwakanyaga.









Zoezi la kuaanza kutapika ndiyo unaoendelea kwa sasa




unaweza kutembela facebook ya kanisa hilo la Rabboni center ministries uli uweze kufahamu zaidi kinachoendelea katika huduma hiyo kwa sasa mwenye macho haambiwi tazama.

Jumatano, 15 Januari 2014

FALSAFA YA UMILIKISHAJI KWA MUJIBU WA BIBLIA



Kutana na askofu mkuu wa WAPO mission International uweze kufahamu kwa undani juu falsafa ya umilikishaji kwa mujibu wa biblia

Baada ya kutoa taarifa ya kongamano la vijana na tamko lao; leo naomba
nikutambulishe rasmi kuhusu kampeni mpya ambayo WAPO MISSION INTERNATIONAL imeitangaza mwaka huu inayoitwa OPERESHENI MILIKISHA. Hoja ya leo ni kuitambulisha kwako kampeni hii kuanzia sababu zake, malengo yake na matarajio yake nini:



Propaganda za kulinda amani

na kufuta umaskini wa kipato



Amini usiamini, humu duniani kuna mambo ya kustaajabisha ukiyagundua katika uhalisia wake.  Naomba nitumie mfano hai wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea Sudani ya Kusini. Mpaka ninapoandika makala haya; wakati vita vinaendelea kwenye uwanja wa mapambano, na raia wasio na hatia wanauawa na wengine kukimbia na kuyaacha makazi yao; eti vikao vya kutafuta amani nchini humo vinaendelea jijini Adis Ababa Ethiopia, na pande mbili husika zinajadiliana jinsi ya kusitisha vita!!  Swali la msingi ambalo haliko kwenye mjadala wa AdisAbaba ni Nani anadhamini vita hivyo? Nani anayefanya biashara ya silaha zinazotumika kuuana nchini Sudani? Je naye yuko kwenye kikao cha kujadili ajenda ya kusitisha vita Sudani?

Ndivyo ilivyo na Vita dhidi ya Umaskini wa kipato katika jamii za nchi zenye majina rasmi ya nchi za ulimwengu wa tatu. Wakati rasirimali za asili (ambazo zina uwezo wa kufuta 100% umaskini wa kipato wan chi husika) zinaendelea kuchukiliwa bure, au kwa manunuzi yasiyo na tija kwa nchi husika; na kisha rasirimali hizo  hizo zinazalisha bidhaa ambazo hurejeshwa kwenye soko la nchi maskini  kwa bei za juu; na kutenegeza faida kubwa; eti matajiri wa ulimwengu wa kwanza wanasadikiwa kudhamini mipango ya kufuta umaskini wa kipato katika nchi hizo hizo zinazoporwa utajiri wake wa asili!

Hivi kweli kuna nia ya dhati (kutoka kwa matajiri wa ulimwengu wa kwanza), ya kufuta umaskini wa kipato kwa nchi maskini? Hivi kama kweli matajiri hao wangelitaka kuufuta kweli umaskini ingewachukua zaidi ya miaka ya 50 kukamilisha zoezi hilo?

Nadhani tumefika wakati muafaka wa kutokumung’unya maneno. Amani na utulivu, na kufutwa kwa umaskini wa kipato haviwezi kutoweka kwa juhudi za matajiri wa ulimwengu wa kwanza, wakati biashara zao zimejengwa katika misingi ya biashara ya kutengeneza na kuuza silaha, na kupora rasirimali za asili kwa nchi maskini. Mwenye kutaka kuamini kwamba kuna siku umaskini wa kipato utatoweka kutoka kwa matajiri atambue kwamba umaskini wake ndio unaowaneemesha matajiri hao.

Mwenye nia ya dhati ya kuleta amani

na kufuta umaskini ni Mungu peke yake.



Ni Mungu peke yake ndiye awezaye kutuliza ghasia na kurejesha amani na utulivu katika jamii; na kisha ndiye mwenye nia na uwezo kufuta umaskini wa kipato kwa maskini.

Kwanini nasema hivi?  Majibu ya swali hili ndiyo hoja maalum katika makala haya. Naomba nistafsiriwe kuwa naleta majibu mepesi kwa maswali magumu. Naomba nitumie fursa hii kuthibitisha ukweli, uzito na ushahidi ni kwanini nasema Mungu peke yake ndiye mwenye ufumbuzi wa changamoto nilizozitaja hapa juu.

Maono asilia ya Mungu kuhusu binadamu

Kwa wale tunaoamini kwamba binadamu ameumbwa na Mungu kama livyoandikwa katika Biblia, tunao ushahidi wa kimaandiko kwamba maono ya Mungu kuhusu binadamu hayakuwa na nia ya kumfanya binadamu kuwa fukara na maisha ya fujo na ghasia duniani.

Tukisoma maandiko kuhusu maono ya Mungu juu ya binadamu tusoma kwamba: “Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu; na kwa sura yetu; wakatawale…..” (Mw.1:26)

Andiko hili linadhihirisha bayana kusudi la Mungu kuhusu binadamu hata kabla hajamuumba. 1. Kuumbwa kiumbe anayeshabihiana na Mungu kwa fikra, hisia na utashi; 2. Kuumbwa kiumbe atakayemwakilisha Mungu katika utawala wa dunia na viumbe vyote vilivyomo.

Kutokana na Maono haya Mungu aliyatimiza kwa kuwaumba binadamu wa kwanza, Mwanamume na mwanamke, kama ilivyoandikwa: “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale…..” (Mw.1:27-28)

Kutokana na ushahidi wa kimaandiko tuliyosoma hapa juu, tunathibitisha kwamba binadamu wa kwanza waliumbwa katika hali ya utukufu wa Mungu, na wakamilikishwa kuitawala nchi na viumbe vyote vilivyomo. Kwa maelezo mengine ni kwamba, haki na mamlaka ya kumiliki ni ya kimaumbile. Hisia ya kumiliki ni sehemu ya maumbile ya  kila binadamu.

Pasipo kujali binadamu yuko katika mazingira ya aina gani hisia ya kumiliki imo ndani yake. Maswali mengi yanayojitokeza ni kama huu ndio ukweli tena wa kimaumbile kwa kila binadamu, kwanini basi hivi sasa kuna matabaka ya maskini na matajiri, watumwa na mabwana, waajiri na wajiriwa? Majibu ya maswali haya yanatupeleka kwenye sehemu ya pili ya falisafa ya umilikishaji.

Kuvunjika kwa mahusiano na kupoteza mamlaka

Baada ya binadamu wa kwanza kuumbwa, na kumilikishwa kama Mungu alivyowakusudia, binadamu hao hao walifanya maamuzi mabaya ambayo yaliwagharimu matokeo mabaya. Mungu alipowamilikisha aliwapa sheria ya kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, na akawaonya kwamba siku watakapokiuka sheria hiyo, watavunja mahusiano na yeye, na pia watapoteza sio mamlaka ya utwala peke yake, bali wasitisha na maisha ya umilele duniani.

Adamu na Eva walipokiuka sheria ya Mungu; ghafla wakajikuta wamefarakana na Mungu kama livyoandikwa: “…kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;..” (Rum.3:23)

Kwa bahati mbaya, uvunjwaji wa sheria ya Mungu ulifanywa na binadamu wa kwanza wale wale ambao ndio walitakiwa kubaki mfano wa vizazi vya binadamu vinavyofuatia. Biblia imeandikwa kwamba:“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa             dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote             wamefanya dhambi.” (Rum.5:12)

Kutokana na maandiko tunaona kwamba kwa kosa la binadamu kuliathiri vizazi vyote vya binadamu waliofuata baada yao. Na athari hazikuishia katika kupoteza utukufu wa Mungu, bali ulisababisha kunywang’anywa ile mamlaka ya utawala. Lakini Mungu atukuzwe kwa sababu hakuridhika na athari zilizomsibu binadamu bali aliandaa mpango maalum wa kumkomboa na kumrejesha katika asili yake ya kwanza. Mpango huu tutaupitia katika makala yajayo.


Itaendelea wiki ijayo

Jumapili, 12 Januari 2014

KUTANA NA MC MACHACHARI TENA MAKINI ZAIDI YA MAKINI NANI ENDELEA KUSOMA?


 Hapa tunamzungumzia mwanadada makini tena zaidi ya makini na si mwingine ni dada Ritha Chuwalo Mtangazaji wa WAPO Radio FM ambaye amebobea zaidi katika vipindi vya habari kam vile patapata ,yaliyotokea,yasemavo magazeti ambaye kwa jina lingine anafahamika kwa jina la Mwisraeli namba mbili katika kipindi cha Ijue Israeli.
Mbali na kuwa mtangazaji pia ni mshereheshaji (MC) makini na mbunifu katika sherehe mbalimbali kama vile Harusi,Sendoff,Kitchen party,Kipaimara, Matamasha pamoja na Dhifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa.
Kwa sasa mwanadada huyu amefungua kampuni yake inayojihusisha na masuala hayo inayojulikana kwa jina la MC RITHA CHUWALO INTERTAINMENT tazama hapo chini ujionee mwenyewe.


kwa mawasiliano chukua namba zake kwenye busness kadi yake hapo juu na kwa picha za hapo chini utamuona akiwa katika matukio mbalimbali.





 Hapa chini akiwa studio za WAPO Radio FM akipiga kazi.


Jumamosi, 4 Januari 2014

MOTO WA INJILI WAWASHWA NA MCHUNGAJI MTARAJIWA MASANJA MKANDAMIZAJI.

Mchungaji mtarajiwa awasha moto wa Injili katika viwanja vya serikali ya Mtaa Tabata Savana ambapo watu wengi walijitokeza kumpokea bwana YESU kama BWANA NA MWOKOZI wa maisha yao.
Kiukweli watu wengi wanapitia katika mapito magumu sana,akizungumza wakati wa kuhubiri mchungaji mtarajiwa Emanuel Mgaya maaru kwa jina la Masanja mkandamizaji ambaye pi ni mwigizaji wa komedi alisema kuwa MUNGU yupo tayari kuwasaidia qanadamu pale ambapo wameamua kujitoa kwake na kufuata maagizo yake kama alivyoagiza wanadamu kumtii yeye.
"Akinukuu kitabucha Yohana 5:5-11 alisema kulikuwa na mtu aliyekuwa mgonjwa kwa muda wa mika 38 kila wakati akitaka kuingia kwenye birika inapotibuliwa na malaika anashindwa kutokana na kutojiweza na ndugu zake wamwemwacha bila msaada wowote na YESU alimuuliza unataka nikufanyie nini? yeye kwa sababu ni mgonjwa anaanza kuta maelezo wakate angetakiwa kujibu nataka kupona,ndivyo ilivyo misha ya wengi sasa wanapitia katika mapito na magumu wanaanza kulalamika na kunung'unika"alisema mchungaji Mgaya.



Mtangazaji wa WAPO redio na pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili Sila Mbise kushoto akiwa Masanja Mkandamizaji katikati na kulia nia mtume Peter Nyaga wakihojiwa katika studio inayotembea ya WAPO redio (OB VAN) katika viwanja vya Savana Tabata.
Mtume Peter Nyaga kulia akiwa na mchungaji mtarajiwa Emanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji).


 Mwimbaji Silas Mbise akiwajibika jukwaani.




Emanuel Mgaya mchungaji mtarajiwa akihubiri katika viwanja vya savana. 








Umati wa watu maelfu wakiwa wamekusanyika katika viwanja vya serikali ya mtaa wa Savana wakifuatilia kwa makini mahubiri na wengine wakiombewa katika viwanja hivyo.

Mwimbaji Ibrahimu Sanga awakiwajibika na vijana wake jukwaani.
NeemaJekoni hakuwa nyuma ya jukwaa wakati wa kuhudumu naye alipamba mkutano wa wimbo wake maarufu TUNAYE MWENYE UWEZO

Chezea Neema Gaspal wakati akiangusha kibao cha NI SHUJAA ambacho kwa sasa kinatamba katika redio mbalimbali za dini.

Neema GAspal kulia akiwa na Tumaini Njole wakiwa jukwaani kwenye mkutano wa injili savana.