YESU NI JIBU

Jumatano, 31 Oktoba 2018

KUMTAMBUA THAMANI YA YESU MWISHO WA MATATIZO


Kanisa likitambua thamani ya kristo Yesu haliwezi kuyumbisha na kitu chochote hata kama litapita katika changamoto litabaki na msimamo wa kumpenda yesu katika imani na kuvumilia mateso yote.
Amesema hayo mchungaji Isaac Mwanjabeki wa kanisa la T.A.G Gongo La Mboto Solomoni Temple jijini Dar es salaam kwamba kanisa la leo linatakiwa liwe na uvumilivu katika kumtumikia Mungu pia lijifunze  kupitia kanisa la simina katika kitabu cha ufunuo.
Mchungaji Mwanjabeki amewasihi watu wanaopitia nyakati ngumu za kimaisha kutokata tamaa na kuwa na subira kwa Mungu kwakuwa jaribu lina muda wake upo wakati litapita.
Mungu huwaangalia walio waaminifu na wavumilivu hasa pale unapopitia majaribu ni vyema kukaa karibu zaidi nae ili uone ukuu wake.