YESU NI JIBU

Jumapili, 29 Desemba 2013

MAOMBI NA MAOMBEZI YANAENDELEA NDANI YA UKUMBI WA PTA KUFUNGULIWA KATIKA VIFUNGO MBALIMBALI

Hivi ndivyo ilivyo katika ukumbi wa PTA mara baada ya mchungaji Katunzi kuanza kuombea watu wanaopita katika mapito magumu na wengine waliweza kufunguliwa katika vifungo vya giza.
Ni jambo la busara sana kuamua kuchagua fungu jema badala ya kuchagua fungu lilobaya tena la mateso sana.
Akizungumza na blog hii mchungaji Katunzi alisema kuwa matokeo ya maombezi na maombi ya siku 21 imeonesha njia sana kiasi kwamba watu wengi waliofika kupata maombi ya uponyaji wa kazi,familia zao wameelezea jinsi walivyofunguliwa katika maombi hayo.
Aidha mchungaji alisema kuwa kwa sasa ni kuwaombea wanandoa ambao ndoa zao hazina amani wana furaha kuna mafarakano sambamba na kuwaombea mabinti ambao hawajaolewa ili wawapate wenza wa maisha wanatoka kwa MUNGU. 
Hivi ndivyo mapambano ilivyokuwa ikiendelea katika ukumbi wa PTA ambapo watu wengi wamefunguliwa 


Watu waliokuwa wakibebwa tayari kwa maombezi katika ukumbi wa PTA










Mchungaji Katunzi akiwaombea watu waliokuwa wakisumbuliwa na matatizo  mbalimbali 

Hivyo ndiyo hali ilivyo ni kuinua mikono juu kuashiria huwezi ama umesarender

MAOMBI NA MAOMBEZI JUU YA WANAFUNZI,WAFANYAKAZI,WAFANYABIASHARA,WAJARIAMALI KWA LENGO LA UPONYAJI WA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU

Hali halisi katika ukumbi wa PTA wakati wa maombi na maombezi kwa wanafunzi kuanzia shule ya awali hadi vyuo vikuu,maombezi hayo yamefanyika kwa lengo la kuwakomboa wanafunzi ambao wamefungwa kwa nguvu za giza,ushirikina ama uchawi. 
Hata hivyo vijana ama wanafunzi wengi walifunguliwa kutoka nguvu za giza kwani wanafunzi wengi huwa wamechukuliwa akili zao kwa njia ya kichawi alisema mchungaji Florian Katunzi,wakati wa maombezi hayo.
Pamoja na kuwaombea wanafunzi uponyaji wa elimu pia mchungaji aliwaombea uponyaji juu ya uponyaji wa wafanyakazi wafanyabiashara,wakulima na wajasiriamali.
Kiukweli shuhuda mbalimbali zimeweza kushuhudiwa ndani ya ukumbi wa PTA sambamba na waumini wengine kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu pamoja na kupiga simu zao kuelezea kilichowatokea.
Hivi ndiyo ilivyokuwa katika ibada ya maombi na maombezi kwa wanafunzi kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu na pia kuna baadhi ya ndugu jamaa waliowawakilisha watoto wao na jamaa zao wanaosoma katika shule na vyuo mbalimbali.
Hivyo jionee matukio yote katika picha.
hapa mchungaji Katunzi amawasha moto ya maombi.




wanafunzi wakifuatilia kwa makini mafundisho ya mchungaji kabla ya kuanza kuombewa.

wanawaza jinsi watakapowekewa mikona na mtumishi wa MUNGU mch.Katunzi






Hapa tayari moto umeanza kuwashwa wa ROHO MTAKATIFU.




Wamepewa maagizo ya kuweka mikono juu ya kichwa kufungua akili zao.




Nyoosha mikono yako tayari kupokea kile ambacho Bwana anaach

Jumamosi, 28 Desemba 2013

MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA NDOA YA ASKOFU DR MWENISONGOLE WA TAG (UPANGA CHRISTIAN CITY CENTER )

Imekuwa ni wakati wa nderemo na shangwe kwa familia na kanisa la askofu na mchungaji kiongozi wa kanisa la Tanzania assemblies of God Upanga Christian City Center Askofu Dr Renwell Mwenisongole kuadhimisha mika 40 ya ndoa yake.
askofu Mwenisingole aliwahi kuwa askofu mkuu wa TAG  na kwa sasa amestaafu na kuwa mchungaji wa kanisa la mahali pamoja UCCC.
Wakati akihubiri katika ibada hiyo ya kuadhimisha mika hiyo 40 askofu alisema anamshukuru Mungu maana amekuwa kimbilio na msaada wa maisha yake na kiukweli alimponya mara nyingi na amepitia na kupata ajali mara nyingi kiasi ambacho mke wake alivunjika mguu na bado haujapona vizuri mpaka sasa. ila anamshukuru Mungu kwa kumponya na hayo yote mpaka sasa anadhimisha miaka 40.
Naye mkurugenzi wa wanawake wa kanisa hilo WWK na pia ni mbunge wa viti maalum mhe.Rebeka Mgodo alisema kuwa ni jambo la furaha sana kusherekea miaka 40 ya ndoa na askofu Mwenisongole na ni mfano wa kuigwa na washirika wa kanisa hilo na watu wengine wanamfahamu mchungaji huyo kwa hiyo ni jambo jema sana.
Askofu Dr Mwenisongole na mkewe wakikata keki kwa pamoja tayari kulishana na kuwalisha  watu wengine.


Askofu akilishana keki na mkewe na sehemu nyinine na mzee walioanza huduma kwa pamoja.


Mheshimiwa mbunge na mkurugenzi wa WWK Mgodo akizungumzia maadhimisho hayo ya miaka 40  ya ndoa ya askofu Dr Mwenisongole na kuwapa mkono wa pongezi kwa niamba ya wanawake wa kanisa hilo waliotoa zawadi ambayo haipo pichani




Picha za matukio mbalimbali ya askofu Dr mwenisongole na mkewe pamoja na waumini.
Mchungaji Eliud Eseko ambaye ni mchungaji msaidizi katika kanisa hilo la UCCC.


Mch,Dr Esseko akiwa na mke wake kanisani

Mchungaji Esseko kulia akifurahia jambo analoambiwa na mkwe huku mke wa mchungaji Emanuel naye akicheka kwa furaha kwenye maadhimisho ya 40 ya ndoa ya askofu.






 Hivi ndivyo ilivyokuwa kanisa la UCCC.