YESU NI JIBU

Jumanne, 26 Desemba 2017

KUZALIWA KWA YESU NI LEO AMA ILISHATABIRIWA KWA MIAKA YA NYUMA .

Waumini wa dini ya kikristo wameungana na waumini wengine duniani kusherehekea siku hiyo ambayo ni chanzo cha kalenda ya dunia.
Hii siku mara nyingi husherehekewa na waumini wa dini hiyo pamoja na wale ambao si wafuasi wa dini hiyo na imekuwa na mvuto mkubwa sana,
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu na wapo Radio baadhi ya wachungaji na maaskofu wamesema kuwa siku hiyo ni muhimu kusherhekewa kwa kumpokea Bwana  Yesu na kutii maagizo yake ambayo anaagiza kupitia neno lake,Aidha wengine wamesema kuwa baadhi ya watu hutumia siku hiyo vibaya.
Nimezungumza na mchugaji Joseph mwangomola la EAGT makongo juu ambapo amliema kuwa watu wengi hutumia siku hii vibaya kwa kufanya mambo ya anasa ambayo mwisho wa siku ni kumtenda Mungu dhambi.
kuzaliwa kwa Bwana yesu ni ishara ya mabadiliko na mageuzi ndani ya mioyo ya watu hasa wale wenye mrengo wa kutafuta MUNGU wa kweli na kuachana na mambo yale yasiompendeza.
Mchungaji Leornad Manyama wa TAG MABibo Sahara aalisema kuwa ni siku Muhimu sana katika maisha ya kila mwanadamu maana ndiyo chanzo cha kalenda inayotumiwa duniani,
Alisistiza kuwa wanadamu wanapokumbuka siku hiyo ni vyema kujitakasa na kutafuta kwa bidii kumpendeza Mungu katika maisha yao ya kila siku.
 Askofu Florian Katunzi Akisalimiana baadhi waumini
Na kwa upande wa askofu Florian Ktunzi wa EAGT City Center alisema kuwa hii ni siku ya Muhimu sana na ilitabiriwa na Isaya kutoka agano la kale mpaka agano jipya ilitabiriwa juu ya siku hiyo.

Jumatano, 6 Desemba 2017

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA JOEL BENDERA


Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia na wote walioguswa na kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr Joel Nkaya Bendera kilichotokea jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Jumatano, 29 Novemba 2017

SOMO:PONYA VIDONDA VYA MCHUNGAJI WAKO.

Luka 16:19-31" akasema,palikuwa na mtu mmoja,tajiri,aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi,na kula siku zote kwa anasa.na maskini mmoja jina lake lazaro,huwekwa mlangoni pake,ana vidonda vingi,naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka ktk meza ya yule tajiri;hata mbwa wakaja wakamlamba vidonda vyake.
Ikawa yule maskini alikufa,akachukuliwa mpaka kifuani kwa ibrahimu.yule tajiri naye akafa akazikwa.basi,kule kuzimu akayai ua macho yake,alipokuwa ktk mateso,akamwona ibrahim kwa mbali,na lazaro kifuani mwake.akalia,akasema,ee baba ibrahimu,nihurumie,umtume lazaro achovye ncha ya kidole chake majini,auburudishe ulimi wangu;kwa sababu ninateswa ktk moto huu.

Alhamisi, 16 Novemba 2017

ASKOFU MWAMAKULA ATOA WITO KWA WATANZANIA NA AFRIKA JUU YA ZIMBABWE.

 ZIMBABWE! ZIMBABWE! ZIMBABWE! 

Kumekuwa na sintofahamu nchini Zimbabwe tangu juzi.
 Kikosi Kikuu cha Inkomo kiliripotiwa kuondoka katika ngome yake na kuingia mjini na kuziba njia kuu.

Jumatano, 2 Agosti 2017

USHAURI KWA WAZAZI JUU YA WATOTO WAO WANAOSOMA SHULE ZA KULALA.

Wazazi wanatakiwa kuwa makini na watoto wao hasa wale ambao wanapenda kuwapeleka watoto shule za kulala (boarding)iwe ya wasichana wenyewe  ama ya wavulana wenyewe,ni vizuri kuwa makini na kuhakikisha kuwa kila unapompeleka shuleni akirudi hakikisha kuwa unamsikiliza na kukaa naye ili ufahamu kuwa amekutana na changamoto gani akiwa huko shuleni.
Wazazi wenzangu nimekaa na kutafakari sana juu ya watoto wanaopelekwa shule za kulala watoto maana hali ni mbaya katika shule hizo maarufu kama (boarding).

WAWAUMINI WASHAURIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO ILI KUJIKWAMUA NA UMASKINI:

ASKOFU wa kanda ya kati kanisa la Pentecostal Holliness Association Mission (PHAM) Julias Bundala amewataka waumini wa  madhehebu ya dini kuhakikisha kuwa wanatumia fursa zinazojitokeza kwa wakati huu ambapo serikali imeamua kuhamishia makao yake makuu mkoani Dodoma.

Kiongozi huyo wa kanisa hilo ametoa ushauri huo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi mbalimbali wakiwemo wachungaji,wainjilisti,wazee wa kanisa na mashemasi kwenye semina ya siku nne iliyoandaliwa na kanda ya kati iliyofanyika kijiji cha Chiwe wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Jumapili, 16 Julai 2017

Jumatano, 31 Mei 2017

WALIOFUNGWA NA KUKATA TAMAA SASA WAFURAHIA UPONYAJI NA UKUU WA MUNGU KATIKA MAISHA YAO BAADA YA KUPOKEA MIUJIZA YAO.

 baadhi ya waumini waliohudhuria kongamano wakimshika Mtumishi wa Mungu mchungaji Florian Katunzi kabla ya maombi na maombezi wakati wakihitimisha kufundisha neno la Mungu hali ambayo ilikuwa tofauti sana,

Ijumaa, 27 Januari 2017

KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA.



Mchungaji  AP Hosea Shabban kanisa la ufufuo na uzima Moshi Kilimanjaro akifundisha neno.
Waumini wakifuatilia kwa makini neno la Mungu ambalo mchungaji Hosea Shabban alifundisha hayupo pichani.





 Mith 8:13, Mith 9:10, Mith 14:26,
Tunahitaji maaarifa katika utendaji wote wa kazi zetu na zaidi sana Kazi ya Bwana. Na maandiko yanatuambia;
Mithali 1:7imeandikwa kuwa "Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu “
Ni kweli kwamba tunaweza kupata maarifa kwa kuwaangilia watu wengine namna wanavyotenda, kwa kuwaangalia waliotutangulia lakini biblia imetuelezea KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA.

Tukiisha kujua kumcha Bwana ndio chanzo cha maarifa sasa tunamchaje Bwana?
Jibu ni Tunamcha Bwana Kwa kuchukia uovu.
Tunapomcha Bwana, tunapewa maarifa ya Kimungu yanayotuwezesha kukabiliana na changamoto au matatizo mbalimbali. Maarifa haya yatatuongoza kunena kwa usahihi, yatatuelekeza namna ya kutoka kwenye vifungo na matatizo tuliyoshikiliwa kwayo. Ili tuweze kuitenda kazi ya Mungu kwa usahihi tunayahitaji maarifa haya.

Maandiko mengine yametueleza wamba, Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu za kuishi, Kumcha Bwana ni tumaini imara, Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.
Ni maombi yangu kwamba Mungu afanyike chemichemi ya uzima, siku zako za kuishi ziongezeke, akuepushe na tanzi za mauti, Bwana afanyike tumaini imara kwako wakati ukiongeza maarifa mengi kwa kumcha Bwana na chochote kilichotengenezwa kwa kukosa maarifa haya kivunjike, tanzi za magonjwa na kuonewa ziharibike na ufanikiwe kwa haya Maarifa ya Kimungu Amen.
unaweza kuwasiliana na blog hii kwa 0682672828