YESU NI JIBU

Alhamisi, 24 Desemba 2015

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMEMALIZIA KUJAZA NAFASI ZA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU WAZIRI ALIZOBAKIZA WAKATI AKITANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI LA KWANZA KATIKA AWAMU YA TANO YA UTAWALA WAKE.



Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1. Profesa Jumanne Maghembe – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
2. Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
3. Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
4. Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
5. Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
6. Prof. Makame Mbarawa – Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu. 
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015

MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA KRISMASI YAPIGWA MARUFUKU HUKO NCHINI SOMALIA KWA HOFU YA KUSHAMBULIWA NA KUNDI LA KIGAIDI LA ALSHABAB

Wakati wakristo kote duniani wanaadhimisha kuzaliwa kwa Bwana Yesu Mwokozi wao huko nchini Somalia hali imekuwa tofauti baada ya serikali ya nchi hiyo  kupiga marufuku sherehe za kuadhimisha sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu.
Mkurugenzi mkuu katika wizara ya maswala ya dini,Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa maadhimisho kama hayo yasiyofungamana na dini ya kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Al Shabab.

Jumatano, 23 Desemba 2015

MKURUGENZI WA RAHCO ASIMAMISHWA KAZI NA BODI YA MAMLAKA YA RELI TANZANIA (TRL)



Rais wa Jamhuri ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.

Jumatatu, 21 Desemba 2015

MTU MMOJA AMBAYE ANAJIITA MCHUNGAJI WA KANISA HOLINESS OF HEAVEN MINISTRIES MJINI ORLU NCHI NIGERIA AMEKUTWA KWA MGANGA WA KINYEJI.



Mchungaji kiongozi wa makanisa ya Holiness of Heaven Ministries ya mjini Orlu Nigeria, amepata aibu ya mwaka baada ya kubambwa akipaka ‘ndumba’ kwa mganga wa kienyeji.
Inasemekana Mchungaji huyo ni maarufu zaidi kwa miujiza katika Jimbo hilo.
Siku ya tukio wananchi walitonywa na muumini mmoja kuelekea nyumbani kwa mganga, anayesemekana ndiye ambaye humpa nguvu ya kufanya miujiza.
Baada ya kumtia mkononi Mchungaji huyo, wananchi walianza kumtembeza ‘uchi’ mitaani.

RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS WA BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA TEC KUFUATIA KIFO CHA ASKOFU MSTAAFU NKALANGA.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga (OSB) kilichotokea Ijumaa tarehe 18 Desemba, 2015 katika hospitali ya Mtakatifu Joseph Peramiho, Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

Mhashamu Askofu Nkalanga aliyekua Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba alistaafu uaskofu mwaka 1974 na kujiunga na watawa wabenediktini wamonaki ambapo aliamua kwenda kuishi katika Abasia ya Hanga iliyopo katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.  

Katika salamu zake Rais Magufuli amesema  Askofu Nkalanga aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96 atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kuhimiza imani na uchapakazi kazi katika kipindi chote cha miaka 54 ya uaskofu wake na utawa wake akiwa katika Abasia ya Hanga.

Amesema Marehemu Askofu Nkalanga ambaye baada ya kustaafu aliamua kuingia katika utawa akianzia katika ngazi ya chini kabisa ya Unovisi hadi alipofunga nadhili za milele za utawa mwaka 2009, ameacha mfano mzuri unaohimiza jamii kuishi kwa upendo, unyenyekevu na kutokata tamaa. 

"Kupitia kwako Baba Askofu Ngalalekumtwa napenda kuwapa pole nyingi Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Abate wa Abasia ya Hanga, watawa na waumini wote wa kanisa Katoliki kwa kupoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kanisa na jamii kwa ujumla" amesema Rais Magufuli.

Rais John Pombe Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu Mhashamu Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
20 Desemba, 2015

Alhamisi, 17 Desemba 2015

IMERIPOTIWA KUWA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MKOANI ARUSHA IMELETA MADHARA KWA BAADHI YA KAYA KNA KUHARIBU MIUNDO MBINU KATIKA KIJIJI CHA LENGIJAVE NA ILKUROT.

Mvua zinazoendelea kunyeesha mkoani Arusha zinaendelea kuleta madhara katika sehemu mbalimbali ambapo miundombinu ya barabara inaendelea kuharibika huku ikiripotiwa zaidi mifugo 50 kufa kutokana na mvua hizo.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi mhe. Gibson Meiseyeki ametembelea kijiji cha Lengijave na Ilkurot katika kata ya olkokola kwa siku mbili kujionea madhara hayo ambayo yametokana na mvua ziazoendelea kunyesha mkoani humo.
 Diwani wa kata ya Olkokola Kalanga Lendulo akiwa na mbunge wa Arumeru Mashariki Gibson Mesiyeki mwenye suti.
 Mbunge Gibson Mesiyeki akiwa na wananchi wa kijiji cha Ilkurot.

NAIBU WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO,DKT.HAMIS KINGWANGWALA,


 Naibu Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Dkt.Hamis Kingwangwala(wa pili kulia) akikagua kambi ya kipindupindu iliyopo hospitali ya kwamnyamani buguruni.
Dkt.Kingwangwala akimsalimia mmoja wa mgonjwa wa kipindupindu aliyelazwa kwenye kambi hiyo


 Dkt.Kingwangwala akikagua takataka zilizorundikwa katikati ya barabara ya ndani ya soko la matunda la buguruni
 Katika kuhakikisha kama wafanyabiashara wana uelewa juu ya ugonjwa wa kipindupindu,Dkt.Kingwangwala akizungumza na muuza kahawa karibu na mfereji mchafu uliopo sokoni hapo.
 Naibu waziri akikagua soko la matunda buguruni.

MAHAKAMA YA JUU NCHINI KOREA KASKAZINI IMEMHUKUMU MHUBIRI KUTOKA CANADA KIFUNGO CHA MAISHA JELA NA KAZI NGUMU.



Mahakama ya juu zaidi Korea Kaskazini imemhukumu mhubiri kutoka Canada kifungo cha maisha jela na kazi ngumu.
Hyeon Soo Lim, 60, aliyekamatwa mjini Pyongyang baada ya kuzuru taifa hilo Januari kwa kazi ya kibinadamu amehukumiwa kwa makosa ya “uhalifu dhidi ya dola.”
Bw Lim, ambaye ni kiongozi wa Light Korean Presbyterian Church, alikuwa ameenda kusaidia kituo cha kutunza wagonjwa, kituo cha kuwatunza watoto na kituo cha kutunza mayatima.
Mhubiri huyo kutoka Korea, anadaiwa kukiri kuhusika katika njama ya kupanga kupindua serikali na kuunda taifa la kidini.
Shughuli zozote za kidini ni marufuku nchini Korea Kaskazini.
Taifa hilo mara kwa mara huwakamata na kuwazuia wageni wanaoenda huko kwa shughuli za kidini au kimishenari.
Bw Lim alihukumiwa baada ya kesi yake kuendeshwa kwa muda mfupi na mahakama ya juu ya Korea Kaskazini.
Inadaiwa mhubiri huyo amekiri kutoa mihadhara na kusema “Korea Kaskazini inafaa kusambaratishwa na mapenzi ya Mungu”, na kusaidia Marekani na Korea Kusini kutoa usaidizi kwa wanaotoroka Korea Kaskazini.
 Chanzo BBC,