Na Stelius
Sane,
Wadau wa
maendeleo wameaswa kuwasaidia watu wasiojiweza katika maisha yao kuhakikisha
kuwa wanafanikiwa na kuishi watu wengine wanavyoishi bila kujali dini kabila
rangi wa utaifa wake.
Hili
limetokea kwenye uzinduzi wa taasisi ya askofu Mathayo Suleman ambayo
imezinduliwa na rasmi na naibu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi
balozi Simba Yahya jijini Dar es salaam.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Balozi Yahya alisema kuwa serikali inatoa huduma kwa jamii
yote inawazunguka ila kutokana na nchi inayoendelea na uchumi wake ni mdogo
amewasihi wadau mbalimbali na taasisi za
kibinafsi kujitokeza na kusaidia serikali kutoa huduma ambazo serikali pekee
yake haiwezi.
Aidha Balozi
Yahya alisema kuwa serikali inaangalia taasisi mbalimbali na asaszi za kijamii
ambazo wanaweza kujiunga na kukusanya nguvu pamoja na kuwasaidia wanachi kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakumba kama vile huduma za kiafya.
Akifafanua
juu ya huduma za afya alisema kuwa serikali inashirikiana na asasi binafsi na
tasisi za kidini kuwapa huduma wananchi wanaowazunguka na serikiali nayo
inawaongezea nguvu ili kutatua changamoto za kiafya kwa wanachi wake.
Kwa upande
wa mwenyekiti mtendaji wa Mathayo Suleiman Foundati Bwana Eliasaph Mathayo
alisema kuwa taasisi hiyo inaungana na wanchama mbalimbali wa tasisi hiyo na
kuchanga fedha na mahitaji mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia wale wenye
uhitaji.
Alisema kuwa
taasisi hiyo inamalengo ya kuwasaidia watu wasiojiwezakwa kutoa fursa za
mafunzo ya elimu ya ufundi stadi na ujasiriamalikwa makundi yenye shida ili
yaweze kujitegemea katika maisha yao ya kila siku.
Bwana
Mathayo aliongeza kuwa taasisi hiyo inampango wa kuanzisha vituo vituo vya afya
vitakavyotoa huduma bora za afya sehemu zenye mapungufu pamoja na elimu ya uzazi
na malezi ya mtoto pamoja na kuanzisha miradi ya kiuchumi kwa wanawake na
vijana ili wawe na uhakika wa kupata mahitaji yao ya msingi ya maisha.
"Tuna
lengo la kuanzisha vituo vya habari na usambazaji habari na kutoa misaa wa hali
na mali kwa wafungwa na wakimbizi", alisema Bwana Mathayo wakati
akizungumza na gazeti hili wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo.
Hata hivyo
amesema wataendelea kuishi kwa kufikia malengo ya watu wasiojiweza ili
kuhakikisha kuwa nao wanasaidika na kuishi katika maisha nzuri kama watu
wengine wanavyoishi,na pia kuhakikisha kuwa wanawake na vijana wanawezeshwa ili
kuinua hali zao kimaisha kwa kuwapa fursa za kujiendeleza kielimu na kupata
huduma bora za afya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni