YESU NI JIBU

Jumamosi, 25 Aprili 2015

ENDELEA KUFUATILIA SOMO LA VITI VYA ENZI KUTOKA MWALIMU : CHRISTOPHER MWAKASEGE KATIKA SEMINA AMBAYO ILIENDESHWA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI DAR ES SALAAM.



Mambo Muhimu yakuyajua tunapozumgumzia juu ya kiti cha enzi.
Ufunuo 13:2,7
(1)Shetani huwa anatumia kiti cha enzi kuwatawala watu na makundi yao
Mat 23:1,2
Shetani huwa anatumia mtu aidha katika kabila,taifa,lugha au kanisa nk na kumpa nguvu zake ili apigane na waatakatifu wote na kutengeneza mfumo ambao utafanya utendaji kazi wake uwe wa urahisi
(2)Kanisa linatakiwa kutumia kiti cha enzi cha kristo ili kushinda vita na shetani
Efeso 2:6
Efeso1:17-24
Efeso 6:10-12
Kanisa la efeso lisingeweza kufanikiwa kama lisingekaa katika kiti cha enzi na kristo Yesu
Ufunuo 5:9,10
(a)Kiti cha enzi na madhabahu vinaenda pamoja
Mungu alilisimisha kanisa la efeso na akalipa nguvu na kiti cha enzi na mamlaka na kutengeneza mfumo ambao utafanya kazi ya Mungu iende kwa urahis


(3)Pamoja na kiti cha enzi kuwepo ili kuwasaidia watu wake bado kuna uwezekano wa wale walio wake kushindwa kukaa katika kiti hicho

Ufunuo 3:21
Kanisa la waadokia lilishindwa kuketi kwenye kiti cha enzi na sio kwamba lilikataa kuketi,na kwakushindwa kwao kuketi kanisa lilikua likiishi chini ya viwango na shetani alikua anatumia kiti chake kuwashambulia

(4)Unaketije kwenye kiti cha enzi ulichopewa au unaketije kwenye nafasi ambayo Mungu ameweka katka ulimwengu wa Roho?
Jibu :Unaketi kwa ishara ya imani ambayo inaonyesha umekubali mambo mawili yafuatayo,
1.Nafasi
2.Agano lililotengeneza iyo nafasi
Zab 89:3,4,20
Yeremia 33;20,21
Kol 1:16
Kumbuka ; viti vinatambulika kwa majina(mfano ;kiti cha Musa,kiti cha Daudi....),au vinatambulika kimajukumu (mfano ,kiti cha Hukumu,Kiti cha Rehema)
Musa alipotengenezewa kiti alikataa kwanza,Yeremia nae alipotengenezewa kiti alikataa kwanza,pia Ester alipotengenezewa kiti alikataa kwanza

Je unakubalije kiti cha enzi?
Ili ukubali kiti upate kuketi ni lazima uingie katka maombi ya kukubali kuonyesha kwamba umekubali
Ester 4:12-17
Ester aliwaambiwa akina mordekai waombe kabla haja sign ile nafasi yakupewa kiti
Esta 5:1
Esta alipovaa mavazi alionyesha tayari yuko katka ofic na alionyesha tayari kaket katka kiti cha enzi

(5)Utajuaje kama umeketi?
Ufunuo 3:21
Ishara ambazo zitakusaidia kujua kwamba umeketi
(a):Angalia kibali ulichonacho kutoka katka viongoz wa ngazi yako(ktk ulimwengu wa Roho ukipewa kiti kina eneo lake na ngazi yake ya kumiliki)
Ukipewa kiti na ukiket ni lazima upewe heshima na kibali kwa watu wanaokuzunguka au unaowaongoza,kinyume na hapo ni kwamba umeket katka kiti ambacho haujakikubali katka ulimwengu wa Roho
Esta 5:1-2
Mfano:Angalia vijana katka makundi yao ni nani mwenye mamlaka na ushawish,huyo huwavuta vijana wenzake wengi kuj upande wake
(b)Jinsi ambavyo Mungu anakupa kujua namna yakupigana na icho kiti kinachopingana na ww
Esta 2:,(mordekai alikua akikaaa au akiketi katika lango..)
Mordekai alipata ufahamu na kujua hayo mambo na vita alivyokua akipambana navyo vinawinda kiti cha ester kwasab alikua amekaa kweny kiti
(c)Angalia utiiisho wa Mungu unaokuzunguka unao ambatana na sauti ya mamlaka unaoambatana na kuzaliwa kwa maadui ambao hukututarajia

Uko upako wa mtu anayekaa katka kiti na kutumika mbele za Bwana
Kama umeshindwa kuketi kitu gani kimekushinda na kukufanya usiketi?
Ufunuo 3:21
Kama Yesu alishinda na yy anataka ushinde
Je alishinda katika nini na wapi?
Efeso 2:6
Mamlaka ya Yesu aliyokua nayo baada ya kufufuka ni ya tofauti na ni ya juu sana kuliko kipindi kile alichokua akiishi kabla hajafa
Yesu alipewa kuketi baada ya kushinda
Alishinda katika lipi?
Kuna mahali alisema ktk biblia
Roho i radhi lakini mwili u dhaifu......(Vita ya kimwili)
--Roho yangu inahuzuni kiasi cha kufa.......(vita ya kiroho
Waebrania 12:2
Itaendelea ndugu msomaji usikose toleo linalofuata,mawasiliano ambayo unaweza kutumia ndugu msonaji kuwasiliana nasi blog hii ni 0682672828,

IFAHAMU BIBLIA YAKO KUPITIA AMANINAFURAHA.BLOGSPOT.COM.



1.Karama ya kupambanua Roho inatolewa kwa lengo Gani?
1.  kutambua chanzo cha miujiza ,ishara na maajabu matendo 8:4-13
2.  Kutambua mawakala wa ibilisi matendo 13:6-12
3.  Kutambua aina ya roho chafu zinazotenda kazi matendo 16:16-18
4.  Kutambua vyanzo vya magonjwa na udhaifu katika miili na nafsi za watu mathayo 12:22-23
5.  Kutambua mafundisho potofu au ya uongo waebrania 1:1-2; 1thethalonike 4:13-17
2.Daudi na Jonathani walikuwa marafiki ni kitu (siri)gani kilichosababisha urafiki wao udumu toa sababu  sababu nne ama siri nne.
1.  mwambatano ulianzia katika roho zao.
2.  upendo wa kweli kati yao(1sam 18:1)
3.  utayari wa kila mmojaa wao kuwa mwaminifu katika patano la urafiki wao(1sam18:3)
4.  upendo wenye msukumo wa kutoa na kujitoa kwa hiari kila mtu kwa mwenzie(1sam18:4)

3.Ni watoto wangapi wa mfalme Sauli waliuwawa na wafilisti katika mlima Gilboa
Jibu;Ni Yonathani,Abinadabu na Malkishua
1Nyakati 10:1-2
4.mfalme Sauli aliuwawa na nani?
Alijiua mwenyewe
1Nyakati 10:4-6
5.Ni mtu yupi alikuwa anatumia uchawi na watu wengi walimogopa sana na yeye kusema kuwa ni mtu mkubwa?
Simoni
matendo 8:9-13
6.Roho mtakatifu anatusaidia katika sehemu mbalimbali ama nyingi ila katika suala la maombi hutusaidia kufanya nini na katika biblia ibapatikana wapi?
Hutusaidia katika udhaifu wetu
Warumi 8:26-27
7. Ni nani alifundisha neno la Mungu kwa nguvu sana na kuwaonya watu kutenda mabaya wapinge Roho Mtakatifu badala yake walimpiga kwa mawe hadi kufa.
Stefano
matendo 7:51-60


Alhamisi, 23 Aprili 2015

KUTANA MTUMISHI WA MUNGU MWALIMU VALENCE VICENT,WA HUDUMA YA NURU YANG'AA GIZANI KATIKA SOMO LA ROHO YA UNYONGE (INFERIORITY SPIRIT):


Hapo tulipoishia mpenzi msomaji wa amaninafuraha blog sasa endelea kufamu roho ya ungonge ili isiwe kikwazo katika maisha yako sasa endelea,
Yeremia 1:1-7
Roho ya unyonge inaambatana na roho ya woga na msomaji kumbuka kuwa roho hizo zinzkuwa kama majitu hivyo imewakamisha watu wengi katika misha yao.
Musa alivyotokewa na Mungu akitaka kumtumia ameanza kukatishwa tamaana roho hiyo ya unyonge,
Mara nyingi tumeenda kwa Mungu tukiwa na matatizo ila ni wachache sana wemeenda mbele za Mungu kwa kumuuliza juu ya kundi analoliongoza na kuwasimamia
Ila mara nyingi wamekuwa wakiwapelekea Mungu mipango yako na hujawahi kuhitaji mipango ya Mungu katika maisha yako,Hata ukitazama na katika historia ya hana ,yeye Mungu anaangalia tumbo la hana na kumwona Samweli kwa Ibrahimu Mungu alikuwa anamwoana Isaka kwenye tumbo la sara wakati yeye Ibrahimu amempata ishmaeli kwa mafanyakazi wa ndani ila Roho wa mungu yeye anamwaona mafanikio katika maisha yako.
Mungu anapompa mtu kuwa mtumishi wake anaondoa kwanza roho ya unyonge na ndipo anakupa upako juu ya kazi ambayo amekuuitia .
Kuna kitu kinaandelea ndani ya moyo wa Munguu juu yako wewe unayeteseka na kukatishwa taamaa na kusumbuliwa na roho ya unyonge hivyo ni vyema kusimama katika nafasi yako na kukemea roho hiyo ya unyonge ikuachie maana imekuwa ikiwakandamiza watu wengi katika maisha yao na kaytika nafasi zao mbalimbali.
Kuna watu wengi wemekalia nafasi zao kwa kutishiwa tu kidogo anakata tamaa na kuanza kutumikia dini badala ya kusimama na kukwema roho ya unyonge,usikubali mtu yeyote ekuingizie roho ya unyonge simama katika zamu yako wewe kama wewe na kukaataa roho hioyo ya kukatisha tamaa hata kama umiambiwa kuwa huwezi kata ili ufikie mafanikio yako
Hesabu 13:27-37 Kalebu na Yoshua walikuwa na roho ya ushujaa ila wale wwengine kumi wameingiwa na roho ya unyonge na wakaona kuwa hawawezi kuwakabili wana wa wanaanaki na wanefili ,aonavyo mtu nasini mwake ndivyo alivyo.
Kuna wakati watu wanakuona kama hufai ila simama wewe kama wewe maana Mungu unaye mwamini anaweza kukusaidia na ukafanikiwa sana
Usipoishinda roho ya unyonge utashindwwa kufiukia mafanikio yako na kushindwa kumtumikia Mungu.
Barikiwe sana msomaji kwa kuendelea kutembelea blog yetu,na pia unaweza kutoa maoni yako,

 wasiliana nasi kwa namba 0682672828,

Jumapili, 19 Aprili 2015

KUTANA MTUMISHI WA MUNGU MWALIMU VALENCE VICENT,WA HUDUMA YA NURU YANG'AA GIZANI KATIKA SOMO LA ROHO YA UNYONGE (INFERIORITY SPIRIT):

Roho ya unyonge imekuwa ikiwatesa watu mbalimbali katika maisha yao,imekuwa ikiwasumbua watumishi ,wafanyakazi wa ndani na hata viongozi wa siasa ,inakuonesha pia Adui yako aliyeko mbele yako jinsi alivyo kuwa na mwenye nguvu kuliko wewe.
2 samweli 33
Unaona Sauli anamwambia Daudi kuwa huwezi hata kidogo  kupambana na Goliathi mfilisti na wewe unaweza ukakaa na marafiki zako ambao wana elimu kubwa kuliko wewe  na roho ya unyonge inakukatisha tamaa kuwa huwezi kukaa wala kuzungumza na watu hao maana huna elimu kama yao.
Roho ya unyonge inamwonesha mtu historia ya maisha yake na ya familia yake,kuwa huwezi maana familia yako ni maskini sana huwezi na kukaa ama kuishi na watu wengine wenye uwezo ni vigumu.
Roho hiyo inafanya historia ya maisha yako ikutangulie na kuona kwamba hauwezi kama ulishafanya kosa ama dhambi ndani ya kusanyiko na hata kama hakuna mtu aliyekuona ama kushuhudia roho hiyo inakukwamisha na kukufanya ushindwe hata kumtumikia Mungu.
Waamuzi 6:11-15
Roho ya unyonge ilimshika hata Gideoni na kuona kuwa hawezi maana familia yake ni maskini sana kuliko familia nyingine.
Ni roho ya kukatisha sana tamaa na kukufanya kushindwa,kufanya kile ambacho kitakusaidia hivyo nivyema  kusimama na kukemea na kuacha kabisa maana imekuwa ikiwakwamisha wengi.
Biblia inasema kuwa kweli yenu iwe kweli,ndiyo na iwe ndiyo na  hapana iwe hapana usiangalie roho ya unyonge maana itakukatisha tamaa na kukukwamisha,maana kuna baadhi ya watu hata wamekufa bila kufanya kazi ya Mungu na badala yake wamekufa wakiwa na mambo ya kimungu bila kutumia hata kidogo.
Hata wengine wameshindwa kufanya biashara kutokana na kuwa na  roho hiyo,ila kila jambo ambalo unataka kufanya ni vyema kumshirikisha Mungu na hapo unaendelea na kazi yako maana ukimshirikisha Mungu yeye anaongeza mara dufu.
Na hata Mungu amezungumza na Yeremia na akakataa na kudai kuwa yeye ni mtoto hawezi kumtumikia Mungu.
Hakuna mwanadamu ambaye amekamilika ,mwandamu ni mwanadamu tu ila anakamilishwa na Mungu kupitia jina na damu ya Yesu hivyo ni vyema kusimama na kukataa Roho ya unyonge ambaye imekuwa ikiwatesa watu wengi hata washirika .
Je wewe unamaoni gani ama nawe unakandamizwa na roho ya unyonge ambayo inaambatana na woga.
Itaendelea......

Jumamosi, 18 Aprili 2015

MTUMISHI WA MUNGU AONGOZA IBADA YA KINABII KATIKA HUDUMA YA EBENEZER MIRACLE CENTER.



 Ibada ya kinabii kuvunja vioo vya kiganga,
Mtumishi wa Mungu nabii Honest aongoza kanisani ibada ya  kuvunja dira zote za waganga wa kienyeji na kuwasihi waumini kuja na vioo kwa kumanisha wanavunja kwa maelekezo ya kinabii.
Watu wengi waliofika katika ibada hiyo wamefunguliwa na kupokea ushindi kwa jina la Yesu.
 Maombi na maombezi yakiendelea ambayo yameongozwa na mtumishi wa MUngu nabii Malya
 Zoezi la kuvunja vioo vikiendelea kanisani ikiongozwa na Nabii Malya.


 Hivi ndivyo ibada ilivyoendelea,
wewe una maoni gani kwa ibada kama hii.