YESU NI JIBU

Jumatano, 6 Agosti 2014

KUWEKWA WAKFU WACHUNGAJI WA CITY HAVERSTY INTERNATIONAL CHURCH TAYARI KWA HUDUMA.

 Ni dhahiri kuwa wakifundishwa waumini juu ya uwepo wa nguvu za MUNGU wanaamini na kukubali sanjari na kufanyia kazi yake na hapo wengi wanafunguliwa kutoka kwenye madhaifu na matatizo ya kila siku katika maisha.
Kauli hiyo imetolewa na askofu wa huduma ya New life Deliverence Church kutoka Uganda nabii Joseph Kabuye jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwaweka wakfu wachungaji wa huduma ya City Havesty  International Church na kuelezea  uwepo wa nguvu za Mungu  katika maisha ya kila mwamini ndani ya kanisa.
Aidha askofu kabuye alisema kuwa  katika shamba la Bwana mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache hivyo ni vyema kila mwamini ajitolee kufanya kazi  ya Mungu kwa  wakati wote na kuongeza kuwa Mungu ni moto  na hivyo waumini wakimtafuta kwa juhudi ataonekana na kuwasaidia katika maisha yao na zaidi huwaweka huru ndani ya maisha yao ya kila siku.
Akinukuu kitabu cha kutoka 3:1-4 alisema MUNGU alitokewa Musa katika kichaka ambacho hakiteketi huku kikiwaka na hapo alisikia sauti ya Bwana MUNGU ikimwita alipogeuka na kujisemea nitaangali nione maono haya makubwa ndipo Mungu alimwita hivyo ni dhairi kuwa yeye ni moto.
Akielezea umuhimu wa siku hiyo ya kuwaweka wakfu wachungaji mchungaji kiongozi na mwwasisi wa huduma ya City Haversty International Church hapa Tanzania Dr Livingstone Banjagala alisema kuwa huduma hiyo imesambaa katika mataifa mbalimbali hivyo watendakazi ni wachache na ndiyo maana wameamua kuwaweka wakfu wachumbaji hao zaidi ya sita katika ibada hiyo ya jumapili.
Hata hivyo aliongeza kuwa mpaka sasa huduma hiyo hufanya jitihada mbalimbali pamoja na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum pamoja na kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu,na pia wanaweka mikakati ya kujenga kituo cha watoto yatima na wazee kwa lengo la kuwasaidia watu hao ambao wengi jamii imewatenga.
“mpaka sasa tuna huduma katika mataifa mbalimbali hivyo tuna kila sababu ya kuhakikisha kuwa tunawafikia watu wengi kwa wakati kwa lengo ni kuwafikishia neno la MUNU ili wafunguliwe katika matatizo yao”alisema Dr Banjagala.


 Mch. Dr livingstone kushoto amevaa joho akiwa na mke wake katikaibada ya kuweka wakfu wachungaji sita wa huduma hiyo.


Hawa ndiyo wachungaji ambao wamewekwa wakfu.
Kulia ni nabii Joseph Kabuye na katikati ni apostle Dr livingstone kushoto i mtafsiri wake.






Nabii Kabuye akiwaombea waumini katika ibada ya kuwekwa wakfu wachungaji.





Waumini wakiwa katika hali ya maombi.