MAISHA YA KILA SIKU.
Upendo wa kwanza katika maisha ya
kila mtu inaacha nafasi nzuri na kumbukumbu katika maisha ya mtu binafsi.Kama
ulishawahi kuachana na rafiki yako wa kwanza ni vigumu ama sio rahisi kuwa naye
tena ama kurudisha mahusiano tena naye, ila bado inawezekana kuwa naye katika
maisha yako.
Kila mwanadamu kuna kitu anatakiwa
kukumbuka na kufuata ni kutokumbuka kitu ambacho kilishawahi kumuumiza hivyo
endelea kuufuatilia kwa makini mambo sita ambazo unatakiwa kufahamu ili
kumrundisha rafiki yako wa awali ambaye unampenda.
1.Epika
kumtafuta kwenye mtandao wa kijamii (Facebook)
Kama hautaweza kuvumilia kutomtafuta rafiki
yako(mpenzi)wako ambaye mmekosana au mmetofautiana kwenye mtando wa kijamii
Facebook ,basi kuna uwezekano mdogo sana ya kumpata tena.Kwani Itakuwa vigumu
kufahamu kuwa anafanya nini? na anaongea na nani anawasiliana na nani kwa muda
huo.
Hivyo ni vyema kujitahidi kumfungia katika profile
yako maana ataendelea kusababisha maumivu katika maisha yako.
2.Tupilia
mbali vitu vyote ambavyo vinaweza kusababisha ukaanza kumkumbuka.
Njia mojawapo nzuri ya kumpata rafiki yako wa kwanza
ni kutupilia mbali mambo yote ambayo ulikutendea ndivyo sivyo na hapo unaweza
kurudisha upendo wa awali.
Amini usiamini ni lazima utafute njia ya kufuta
kumbukumbu yote ambayo alikutendea ndivyo sivyo.Kama mlitumiana ujumbe
mfupi,barua pepe wakati mmetofautiana ni vyema kufuta hizo jumbe zote hiyo
itakusaidia kumsamehe,ila nji hii inaonekana kuwa ngumu ila ndiyo njia pekee
inayoweza kukusaidia kumsamehe na kutokumbuka.
3. Baadilisha
mtazamo wako wa maisha.
Baadala ya kuendelea kufikiria yaliyopita ni vyema
ukawaza yali yalioko mbele yako.uwe na tumaini jipya,fanya kazi kwa bidii
kuliko kawaida ili kufikia malengo yako.jiweke taratibu ya kujishughulisha kwa ukichoka kwwa ukweli ni njia ya kusahau
yali uliyokosewa ma yule ambaye umekosana naye.
4. Soma
habari ambazo zinasababisha faraja kwako.
Soma vitabu vya hadithi ambazo zinaweza kukusaidia
kupata furaha ambayo itasaidia kusahau yale yote ambayo ulitendewa.Unaweza
kusoma hadithi kwenye majarida,vitabu na hata kwenye mtandaona utambue jinsi
wengine walivyotatua matatizo na kutambua kuwa kumpoteza rafiki wako wa kwanza
ni jambo la kawaida
5.Fikiria
juu mazuri ambayo ulikuwanayo katika mahusiano yako.
Acha kuwa na kumbukumbu mbaya juu ya
mahusiano yako ulikuwa nayo badala yake fikiria juu ya mazuri ambayo ulikuwa
nayo na rafiki yako.Ni vyema kukumbuka kuwa muda uliyokuwanayo haikuwa bure.
6. Upate
muda wa kutosha na marafiki zako.
Kwa kuhitimisha ni vyema
kushikishana uzoefu na marafiki zako wa karibu na kusikiliza maoni yao na
itakusaidia kujisikia vizuri katika maisha yako.Msaada wao wa kimawazo
itakusaidia kujisikia vizuri na kuona kuwa maamuzi uliyochukua nia sahihi na
utaanza kumsahau rafiki yako wa mwanzo.
Kama rafiki yako atakuwa naye
amepitia kama hayo ambayo umepitia unaweza linganisha na kuona kuwa kumrudisha
rafiki yako wa mwanzo(mpenzi) ni jambo ambalo linawezekana.
Nawe msomaji umempataje rafiki yako wa mwanzo Tafadhali
tushirikishe.