YESU NI JIBU

Alhamisi, 9 Juni 2016

DENI LA ZAIDI YA MILIONI 100 LASABABISHA KANISA LA SINZA CHRISTIAN CENTER KUTUPIWA VYOMBO VYAKE NJE:

Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya mil 100 kanisa la Sinza Christian Center  latupiwa nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na mmiliki jengo hilo Bwana Prosper Rwendera , akizungumzia tukio hilo  mke wa mmiliki  wa jengo Hilo Bi. Patricia Prosper Alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu." 
Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.

Jumatano, 8 Juni 2016

KAULI YA MWANGALIZI MKUU WA WAPO MISSION INTERNATIONAL WAKATI WA KUKUMBUKA SIKU YAKE YA KUZALIWA:

Tarehe 6 mwezi wa sita mwaka huu 2016 ni siku ya kumbukumbu ya  kuzaliwa kwa Askofu wa huduma yaBCIC na mwangalizi wa WAPO mission Askofu Sylivester Gamanywa, ambaye ameandika ujumbe ufuatao kwenye akaunti yake ya facebook.
SIKU NA MWEZI KAMA LEO NILIZALIWA DUNIANI!

miaka 59 iliyopita nilifurahia sana birthday yangu nikiwa na raha ya kuongezeka umri! leo ninajishangaa sina tena furaha ya kuongezeka umri kama zamani!
hii ni baada ya kubaini kuwa kwa kadiri umri wangu tangu kuzaliwa unavyoongezeka kama siku ya leo; kumbe muda wangu wa kuendelea kuishi duniani unapungua!

Jumatatu, 6 Juni 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA IBADA KANISA LA MAOMBEZI LA MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO ‘MZEE WA UPAKO’ UBUNGO KIBANGU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabara inayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside.

Ijumaa, 3 Juni 2016

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI LILIAN NAMAN NGOWI AJIPANGA KUWAFIKISHIA WENGI INJILI KWA NJIA YA UIMBAJI



Mwimbaji wa nyimbo za injili Liliana Naman Ngowi akiwa na kwaya uinjilisti Kijitonyama walipofanya Michigan Marekani.
Lilian ni wa pili kutoka kushoto

WALIOFICHA SUKARI ARDHI IWAKATAE-DKT. CHARLES GADI

Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Askofu wa Kanisa la Good News for All Ministry Dkt. Charles Gadi amewapa siku tatu walioficha sukari kuitoa na ikiwa watakaidi agizo hilo basi ardhi iwakatae.

Askofu Gadi ameyasema hayo  jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uhaba wa sukari nchini na maandalizi ya mkutano wa kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika jiji la Arusha.

Alhamisi, 2 Juni 2016

SEMINA YA NENO LA MUNGU MKOANI DODOMA: ZIJUE NJIA AMBAZO MUNGU ANATUMIA KUKUFANIKISHA.


Semina hiyo inaendelea kwa wiki nzima mkoani dodoma unaweza pia kufuatilia semina hiyo kupitia linki hii,blog ya amaninafuraha ukifungua mkono wako wa kulia utaona sehemu imeandikwa mwalimu Mwakasege unaweza kutazama moja kwa moja wanapoanza kurusha matangazo kutoka Viwanja huko Dodoma

Jumatano, 1 Juni 2016

WENGI WAFIKA NA KUFUNGULIWA NA KUWEKWA HURU MBALI NA MATESO NA MAGONJWA SUGU NA NGUVU ZA PEPO WACHAFU ZAWATOKA NA KUWAAACHIA WATU WALOFIKA KANISANI HAPO.

 Waumini waliofika katika kanisa la Jesus Save Fellowship lilopo maeneo ya Airport jijini Dar es salaam washiriki katika maombi wakongozwa na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Zakaria Oswad Lule hayupo kwenye picha.

SIKU 90 ZA MAPINDUZI NA MABADILIKO NDANI YA KANISA LA EAGT CITY CENTER WENGI WAPONA NA KUOKOLEWA KWA JINA LA YESU.

Mhungaji Kiongozi wa kanisa EAGT City Center mchungaji Florian Katunzi,
Siku tisini ndani ya kanisa la EAGT City Center yaleta mafanikio kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limeonekana baadhi ya waumini na watu mbalimbali ambao wamefika katika kanisa hilo awmeliambia gazeti la msema kweli kuwa wamefunguliwa katika vifungo mbalimbali ambzao zimekuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.