YESU NI JIBU

Ijumaa, 18 Julai 2014

MKUTANO WA INJILI UNAOENDELEA KIMARA TEMBO

Ukweli usiopingika YESU anaendelea kutenda miujija na maajabu kwa kuwatumia watumishi wake ambao wamekubali na kutii sanjari na kujinyenyekesha kwa MUNGU.
 Katika mkunao wa injili unaofanyika katika viwanja vya kanisa la EAGT kimata Temboni unaoongozwa na mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT City Center mchungaji Florian Katunzi umekuwa wa mafanikio makubwa ambapo watu wengi wenye matatizo mbalimbali wamefunguliwa na kupokea nguvu mpya.
Watu wailofika katika mkutano huo wemeelezea wengi walivyofunguliwa sana na nguvu za Mungu.


 Mchungaji Florian Katunzi akihubiri neno la MUNGU katika viwanja vya EAGT Kimara Temboni.



Zoezi la maombi na maombezi likiendelea akiongoza mchungaji Katunzi.



Baadhi ya waimbaji ambao wamefika katika mkutano wa injili huko kimara Temboni Mess Jacob Chengula na Rebecca Magaba


Hawa ni baadhi ya watu waliohudhuria katika mkutano na kupata maombi na maombezi kutoka kwa mtumishi wa Mungu mch.Florian Katunzi
unaweza kuwasiliana na mchungaji Florian Katunzi kwa namba 0718267171,0754367826 na 0784367826

Alhamisi, 17 Julai 2014

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA DVD YAKE MAGIDA TIMOTHEO EAGT YOMBO KISIWANI.

Ni vyema waimbaji wa injili kushirikiana kwa pamoja na kuwasaidia wale ambao ndiyo wanaanza huduma ya injili ili kuwakwamua waimbaji hao.
 Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa sheria na katiba Angela Kairuki kwenye uzinduzi wa Albamu yake mwimbaji Magida timotheo ambayo imezinduliwa hivi karibuni katika kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania lilopo maeneo ya Yombo Kisiwani jijini Dar es saalam.
Akizungumza katika uzinduzi huo mhe.Kairuki alisema kuwa Magida ni mlemavu wa ngozi ila ameamua kutumia kipawa chake cha uimbaji hivyo ni vyema jamii kushirikiana naye kwa kumsaidia ili aweze kufikia malengo yake.
Aidha hakusita kutoa wito kwa waimbaji waliomsindikiza Magida kwenye uzinduzi wake kumsaidia Magida sanjari na kushauri katika uimbaji na pale ambapo hajafanya vizuri ili aweze kuimba katika viwango vya juu vyenye ubora.
Waimbaji ambao wamehuduria katiak uzinduzi huo na kuwavutia watu wengi na kusababisha kanisa kufurika umati wa watu kutoka sehemu mbalimbali ni Boni Mwaitege,Upendo Nkone,Christina Matai,Atosha Kissava, Victor Aron pamoja na waimbajki wengine wengi waliohudhuria uzinduzi huo.
Kwa upande wake mchungaji kiongozi wa kanisa hilo la EAGT mchungaji Aidan Mabuga amesema kuwa ni jambo la kumshukuru sana MUngu kwa kusaidia uzinduzi huo kukamiliaka pia kutoa shukrani za dhati kwa naibu waziri kwa kuacha shughuli zake na kukubali kuuungana na viongozi wa kanisa hilo na wananchi waiohudhulia kanisani hapo kwa ajili ya kuzindua albamu hiyo ma Magida.
 Magida Timotheo hakuwa nyuma kutoa shukrani zake kwa Naibu waziri na kumwomba afikishe salamu zake kwa mhe. raisi wa jamhuri ya muungano na TanzaniaRais Jakaya Mrisho Kikwete.
Hilo ndilo kanisa ambalo uzinduzi wake Magida ulifanyika.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wake Magida Timotheo kushoto naibu waziri wa katiba na sheria Angela Kairuki katikati ni mchungaji Aidan Mabuga na kulia ni mchungaji Matingiza.

Mwandishi wa blog hii na pia ni mtangazaji wa WAPO radio akisoma risala mbele ya naibu waziri wa katiba na sheria  katika uzinduzi wa DVD ya niombee yake Magida.

Hapa namkabithi mgeni rasmi risala.




Mgeni rasmi akianza kudadi DVD ndani ya kanisa la EAGT huku waumini wengi walihudhuria.
Mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT Aidan Mabuga akitoa neno kwa kifupi.
Mchungaji Mabuga katikati akiwa na Magida na mchesha shoo waDVD ya magida ndani ya kanisa. 
Hivi ndivyo kanisa la EAGT lilivyoonekana.

Mwimbaji Bon Mwaitege akiimba katika uzinduzi wa DVD yake magida Timotheo
Bon Mwaitege akizungumza jambo wakati wa tamasha lake Magida.
Upendo Nkone akitumbuiza katika uzinduzi.


Christina Matai ndani ya madhabahu akihudumu kwa njia ya uimbaji.
kundi la waimbaji wakitumbuiza kwa pamoja wakishirikiana anayeshika microphone ni Christina Matai.


Atosha kisava kushoto na mwimbaji mwenzaje Mbigaranda.
Upendo Nkone kushoto katikati Victor Aron ambaye pia ni mtangazaji wa PRAISE POWER na kulia ni Christina Matai.



Magida Timotheo akiwajibika na waimbaji wa kundi lake katika uzinduzi wake.