YESU NI JIBU

Jumatatu, 30 Aprili 2012

HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LA GOSHEN MINISTRY INTERNATIONAL LILOPO CHANIKA JIJI DA ES SALAAM

Kanisa la Goshen Ministries International lilopo Chanika jiji Dar es saalam limeandaa harambe ya kuchangia ujenzi wa kanisa na huduma za kijamii kama vile shule na hospitali.

Akizungumza katika harambe ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo naibu mstahiki meya wa jiji la Dar es salaam Chaurembo Abdala amesema kuwa ni vyema serikali kushirikiana na viongozi wa dini ili kuweza kuleta maendeleo kwa jamii.

Aidha Ndugu Abdala aliongeza kuwa huduma inayotolewa na viongozi wa dini inafahamika hivyo ni vyema kila mtu kujitolea kuchangia huduma hizo.

Naye mchungaji wa kanisa hilo mchungaji Emanuel Chakoa akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ambaye ni naibu mstaiki meye ambaye amemwakilisha meya wa jiji la Dar es salaam amesema kuwa wanahitaji kiasi cha milioni 200 kwa lengo la kujenga kanisa la kisasa


                                   
                                                        

 Kutoka kushoto ni mchungaji Emanuel Chakoa akiwa na Naibu mstahiki meya wa jiji la Da es salaam




Mchungaji Emanuel Chakoa wa kanisa la Goshen Ministries Intenation akizungumza katika harambee ambayo imefanyika jiji Dar es salaam






Jumatano, 25 Aprili 2012

HUDUMA YA MKURUGENZI WA SOS WAKATI ALIPOTEMBELEA KANISA LA DCT

KUTEMBELEA KWA MWINJILISTI WA KIMATAIFA JOHANES AMRIZA KATIKA KANISA LA DCT

Imeelezwa kuwa ili mkristo aweze kuishi maisha ya ushindi na yenye mafanikio siku zote lazima amtegemee Mungu (Yesu) sambamba na kufanya maombi kuwa ni sehemu ya maisha yakena atakuwa mtu wa ushindi.

Kauli hiyo imetolewa na mkurungezi wa huduma ya SOS mwinjilisti Johanes Amriza katika kanisa la Dar es salaam Calvary Temple liloko Tabata shule .
Kanisa hilo linaongozwa na mchungaji Ron Swai ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa  la Tanzania Assemblies of God.

 Kutokana na hilo ni vema basi waumini wa kristo kukaa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu na kujifunza jinsi ya kumtumikia Mungu katika roho na kweli na kumwabudu yeye pekee yake maana ndiye mwenye uwezo.


Jumatano, 11 Aprili 2012

KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD TABATA

 Kanisa la Tanzania Assemblies of God Tabata ambalo hufahamika kwa jina la Dar es saalam Calvary Tembple linaloongozwa na mchungaji R.Swai ambaye ndiye katibu mkuu wa TAG

waumini wa kanisa la DCP wakiwa ibaadani siku ya jumapili ya pasaka

Waumini wakimsifu Mungu na kumwabudu siku ya jumapili ya pasaka katika kanisa la Dar es saalam Calvary Temple

Jumapili, 1 Aprili 2012

KUFUNGULIWA NA KUWEKWA WAKFU KWA KANISA SAHARA SPIRITUAL CENTER

Maaskofu na wachungaji wametakiwa kutumia mtandao kutangaza na kuhubiri neno la Mungu pamoja na kutoa taarifa ya makanisa yao.

Kauli hiyo imetolewa na askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God askofu Barnabas Mtokambali wakati wa ufunguzi wa kanisa la Mabibo Sahara TAG lililopo mabibo jijini Dar es saalam linaloongozwa na askofu wa jimbo la kaskazini mashariki askofu Geoffrey Massawe.

Akizungumza katika ufunguzi huo askofu Mtokambali alisema kuwa ni vema kila kiongozi wa kanisa kutumia mtandao kutangaza kanisa lake pamoja na neno la Mungu maana wewe wanasaidika pale mchungaji anapohubiri neno la Mungu katika mtandao na kuongeza kuwa ni njia mojawapo ya kiuinjilisti.

Aidha aliongeza kuwa kiongozi wa kanisa anpoweka na namba ya simu katika mtandao inasaidia maana kuwa watu wanakuwa na mahitaji mbalimbali hivyo anapiga simu kwa mchungaji akiwa na uhitaji hivyo mchungaji anapata nafasi ya kumwaombea.

Akisoma risala mkungaji kiongozi wa kanisa hilo askofu Massawe alisema kuwa kanisa hilo mpaka kukamilika limegharimu fedha kiasi cha milioni120 kwa awamu ya kwanza na katika awamu ya pili ya upanuzi wa kanisa hilo litagharimu kiasi cha milioni sabini.

Hata hivyo aliongeza kuwa kutakuwepo na awamu nyingine ya ujenzi wa jengo kubwa kwa lengo la kuwafikia watu wengi zaidi na kuwepo mahali pazuri pa kumwabudia Mungu.

Pamoja na hayo kulikuwepo na changamoto mbalimbali ila hazikukwamisha kufanya kazi ya uinjilisti,kuwepo kwa kanisa dogo bado tuliweza kufanya mikutano mbalimbali katika sehemu mbalimbali kama vile Malolo Mozi ,Mamba Kibondo,Mwipenge Musoma,IgowoleMfindi,Bugando Bukoba,Kibeche Mheza,Ludewa Iringa,Kawona Kilindi na Mhoro Rufiji na tnategemea kufanya mikutano mwaka huu wa2012 katika maeneo ya Mchukwi Rufiji,Kimara na Chalinze alisema askofu Massawe.