YESU NI JIBU

Ijumaa, 29 Julai 2016

WENGI WAFUNGULIWA NA KUWEKWA HURU WAKATI WA UBATIZO:

 Hirizi ambazo zilitapikwa na mmoja wa watu waiofika kanisani na kuanza kuombewa na mara baada ya kutapika alianza kufunguliwa.



 Kijana aliyetapika shilingi mia mbili iliyotengenezwa mwaka 1998 na toka atumie hela aliyoiokota alianza kuwa mwizi
 Noti ya shilingi miambili ambayoi alitapika mama alijulikana kwa jina la mama Kirikiri.
 Umati wa watu walofika tayari kubatizwa na mchungaji Florian Katunzi ambapo watu zaidi ya 150 walibatizwa.
 Zoezi la ubatizo likendelea ndani ya bahari ya hindi
Zoezi la ubatizo likiendelea huku watu waiokubali kubatizwa kuanza kukimbia na kusema kuwa hapo tayari kumbe walikuwa wamefungwa na nguvu za giza mara baada ya kubatizwa wamekuwa huru
Kwa nini unakubali kuteseka wakati Mungu amefungua mlango wa neema na kuinuliwa na kufunguliwa vifungo ambazo zimekuwa zikiwatesa wanadamu kwa muda mrefu bila mafanikio.
Hili limebainika ndani ya kanisa la Evangelistic Assemblies of God maarufu kwa jina la EAGT City Center iliyopo mtoni mtongani ambapo wengi wanaendele kufunguliwa na kuwekwa huru kabla ya kongamano la siku tisini kuisha.
Waumini wengi waliofunguliwa kupitia huduma hiyo inayoongozwa na mchungaji Florian Katunzi walisema kuwa hakika walikuwa wanateseka sana katika maisha yao na huku wengine mara baada ya kufunguliwa wameanza kufukuzwa na kutengwa na ndugu na familia zao.
wakieleza kwa nyakati tofauti baadhi ya watu waliofunguliwa wakizungumza na gazeti hili la msema kweli walisema kuwa walipokuwa katika mateso na kuteseka hakuna aliyewatenga ila kwa sasa kwa sababui wamefunguliwa wameanza kutengwa na hata wengine kufukuzwa nyumbani.
Kijana mmoja ambaye amejitambulisha kwa jina la Idrisa alisema kuwa alikuwa mwizi na alipigwa na wananchi wenye hasira kali na kunusurika kuuwawa zaidi ya mara tatu na ndipo wazazi wake waliamua kuwa apelekwe kanisani na sasa baada ya kufunguliwa na kuwekwa huru ndiyo sasa wazazi wake wanamtenga na kumfukuza.
"Mbona nilipokuwa naiba na kuleta hasara nyumbani walikuwa hawanikatazi kufanya hayo maana walikuwa hawawezi nimepelekwa kwa wataalamu mbalimbali bila mafanikio sasa nimefunguliwa ndiyo naambiwa nisiende kanisani,hilo mimi sikubali kurudi nyuma",alisema Idrisa.
Aliongeza kuwa mpaka sasa nimewekwa huru ila baba yangu aliniambia nisikanyage tena kanisani sasa itakuwaje wakati nilikuwa nauwawa na wao wenyewe kama wazazi walishindwa kunisaidia maana hata fedha haikuweza kuniponya ila huyu Yesu mtenda miujiza alinifungua na sasa nipo huru na ninajisikia furaha na amani na ile hamu ya kuiba imeondoka kabisa.
Akitoa ushuhuda kijana mwingine ambaye jina lake ambaye alikuwa anafanya kazi na badhi ya vijana baharini alisema kuwa siku moja aliokota shilingi mia mbili iliyotengenezwa mwaka 1998 na akaenda kununua vitu na kuala na kuanzia pale alianza kuwa mwizi na mpaka walezi wake wakamchoka ila kupitia jina la Yesu sasa nimefunguliwa nimewekwa huru.
Mara baada ya kuzungumza na mashuhuda hao mchungaji kiongozi wa kanisa hilo mchungaji Katunzi alisema kuwa mpaka sasa watu wengi wamefunguliwa kabla ya kongamano hili la siku 90 kwisha ameona Mungu akiwatembelea watu kwa namna ya tofauti sana kuliko kawaida.
Akinukuu kitabu cha Ezekiel 11:1-13 inasema  Tena roho ikaniinua, ikanileta hata lango la upande wa mashariki wa nyumba ya Bwana, lililoelekea upande wa mashariki; na tazama, mahali pa kuingilia pa lango walikuwako watu ishirini na watano; na katikati yao nikamwona Yaazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, nao ni wakuu wa watu. Akaniambia, Mwanadamu, hawa ndio watu wale watungao uovu, na kutoa mashauri mabaya ndani ya mji huu; wasemao, Wakati wa kujenga nyumba si karibu; mji huu ni sufuria na sisi ni nyama. Basi toa unabii juu yao, Ee mwanadamu, toa unabii. Roho ya Bwana ikaniangukia, naye akaniambia, Nena, Bwana asema hivi; Mmesema maneno hayo, Enyi nyumba ya Israeli; maana mimi nayajua yaingiayo katika mioyo yenu. Mmewaongeza watu wenu waliouawa ndani ya mji wenu, nanyi mmezijaza njia kuu zake waliouawa. Mtaanguka kwa upanga; nitawahukumu katika mpaka wa Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Mji huu hautakuwa sufuria lenu, wala ninyi hamtakuwa nyama ndani yake; nitawahukumu katika mpaka wa Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni Bwana; kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka. Ikawa, nilipotoa unabii, Pelatia, mwana wa Benaya, akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, Ee Bwana MUNGU, je! Utawakomesha kabisa mabaki ya Israeli? 
Mungu alimwonesha Ezekieli watu waliokuwa wanawanuizia 

Aliongeza kuwa katika Maombi ndani mwa maombi kipengele cha kuvisha nguvu za kiganga na kichawi watu wengi walifunguliwa na kuwekwa huru mbali na mateso ya mwovu shetani .
"Wapo watu ambao walilongwa, walifungwa, wanateseka ila sasa vifungo vyao vinaachia  maana  Mungu anaenda kuwafinyanga wale wote ambao waliharibiwa katika maisha yao kwa njia ya kichawi na kishirikina.


Aliongeza kuwa endapo kuna mtu alikufunga kwa njia ya uchawi na kiganga anaenda kukuachia na Mungu anaenda kukufinyanga upya katika maisha yako ya kila siku.
"Kuna watu wamefungwa na kuwekwa kuwa duni katika maisha yao sasa tunamwendea Mungu mwenye uwezo kumwomba awafungue na kuwaweka huru mbali na mateso ya kila siku",alisema Katunzi
Pia Mchungaji Katunzi alifafanua  hatua tano za kiimani za kuwezeshwa mwanadamu kufunguliwa na kuwa huru mbali na vifungo vya adui ambapo alisema kuwa hatua ya kwanza ni jitamkie baraka wewe na familia yako.
Alinukuu kitabu cha Waefeso 6:10
inasema Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 
"Huwezi kupambana na nguvu za kichawi na mizimu kama haupo vizuri kiimani,Kama mtu anavyoweza kujikinga asinyeeshewe na mvua sasa unaweza pia kujikinga ili usiguswe na dhambi"alisema mchungaji katunzi huku waumini wakishangilia.
Hakuishia hapo aliongeza kuwa Kuna watu wanataja mabaya juu yako kila unachofanya wanakunenea mbaya kwenye madhabahu zao ila wewe mwamini taja jina la Bwana wa Majeshi juu ya maisha yako, ndoa yako na familia yako kwa ujumla maana Bwana amewapa mamlaka juu ya kukanyaga na kukemea matatizo yote kwa jina la Yesu na vinaenda kuvunjika kwa jina la Yesu na kutoweka.
Luka 10:19
inasema Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni