Waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Mh.Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
tamasha la amani na upendo litakalofanyika jijini Dar es salaam, Agosti 28
mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa
habri mwenyekiti wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Hope Family Bw.
Omary Kombe amesema lengo la tamasha hilo ni kuenzi amani na upendo hapa
nchini.
Aidha Bw. Kombe ameongeza
kwamba kutokana nan chi nyingi za kiafrika kukumbwa na vita ya wenyewe kwa
wenyewe wameamua kuratibu tamasha hilo kuihamasisha jamii ya watanzania kutunza
amani na upendo sanjari na kuchangisha fedha kwa ajili ya kujengea kituo cha kulelea
watoto yatima kiasi cha shilingi milioni 300.
Hata hivyo Bw.kombe amesema
jamii inapaswa kuenzi amani hasa ngazi ya familia kwani kukosekana kwa amani
katika ndoa ndio chanzo kikubwa cha kuongezeka watoto wa mitaani.
Amani inapotoweka kwenye
familia hupelekea watoto na wazazi kuishi katika hali ngumu kiasi kwamba kila
kukicha watoto wanaongezeka mitaani na wanaishi kwenye mazingira magumu.
Ni vema kuendelea kuenzi na
kusimamia amani na upendo kwa juhudi zote ili kuweza kujenga taifa ambalo
linaweza kustawi kiuchumi na kisiasa.