Mwimbaji wa nyimbo za injili Liliana Naman Ngowi akiwa na kwaya uinjilisti Kijitonyama walipofanya Michigan Marekani.
Lilian ni wa pili kutoka kushoto
Akiwe sehemu ya kuchukulia video
Mwimbaji Liliana Naman Ngowi akirekodi akiwa studioni kurekodi nyiz za albamu yake ya
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Liliana Naman Ngowi amesema
kuwa amejipanga kupeleka injili kwa wengi kwa njia ya uimbaji katika sehemu
mbalimbali ndani na nje ya Taifa la Tanzania.
Alisema hayo wakati akizungumza na blog hii ambapo aliweka
bayana mikakati yake ya kuwafikia wengi kwa njia ya uimbaji,ili kuwafikia hasa
wale watu wa vijijini.
Aidha alisema kuwa huduma ya uimbaji alianza toka akiwa
mdogo katika shule ya jumapili maana wazazi wake walikuwa ni wakristo hivyo
walimlea katika njia ya kikristo hadi hapo alipokuwa mtu mzima na sasa ni
mwimbaji binafsi.
"Mimi toka mwanzo nilikuwa napenda kuimba na nimeshirikiana na
wenzangu toka shule ya msingi hadi sekondari nimekuwa nikiwaongoza wenzangu
katika kuimba katika jumuiya ya wanafunzi UKWATA,na nimeshaimba na vikundi mbalimbali
kama vile KKKT ,kijitonyama kwaya ya uinjilisti kwa zaidi ya miaka 14,nimeimba
kwenye mass kwaya yenye waimbaji mia mbili",alisema Lilian.
Aliongeza kuwa amekuwa na uzoefu katika kuimba kwani pia
ameshirikiana na kikundi cha kusifu cha kijitonyama na cha Anzania Front na pia
alishiriki katika semina na huduma mbalimbali na wengi walifunguliwa kwa njia
ya uimbaji.
Mbali na kushiriki katika uimbaji wa Injili alisema kuwa
alishirikiana na Tm Music na walipata fursa ya kuhudhuria mkutano wa kupambana
na kuzuia Rushwa ,na hadi sasa albamu yake yenye nyimbo tisa imekamilika katika
mfumo wa CD na DVD.
Liliana Naman Ngowi mbali na kuwa mwimbaji wa nyimbo za
injili bado ni mjasiriamali na sasa anenda kuzindua albamu yake tarehe 19 June 2016 katika kanisa la KKK Kinyerezi kuanzia
saa nane mchana na kuendelea na hakuna kiingilio,na waimbaji mbalimbali
watamsindikiza Lilian Naman Ngowi katika uzinduzi wa Albamu yake ya Tumaini
limerudi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni