YESU NI JIBU

Jumamosi, 28 Februari 2015

ENDELEA KUJIFUNZA KILA SIKU BIBLIA YAKO POPOTE ULIPO IFAHAMU BIBLIA YAKO:


1.Kuabudu maana yake ni nini?
Answer:Ni tendo linalogusa akili,hisia,nafsi na utu wa mtu na mwili pia kwa kusujudu,kuanguka kifudifudi,au uso kwa uso.
Mwanzo 17:3
Kuabudu katika Roho na Kweli kunaweza kukafanywa wakati wowote na mahali popote mradi lengo ni kufanyia Mungu Ibada.
2.Kwa nini malkia esta alimwaambia  Mordekai awakusanye wayahudi na wakufunga na kuomba bila kula wala kunywa kwa muda wa siku tatu usiku na mchana kwa ajili yake,naye atafanya hivyo pamoja na wajakazi  wake
Answer:
Kwa lengo la kuingia kwa mfalme ,kinyume cha sheria(maana Hamani amepanga wayahudi wote katika ufalme wa Ahusero waangamizwe na kupanga kuwa hamani atundikwe Esta 3,4)esta 4:16-17.
3.Karama ya kupambanua Roho inatolewa kwa lengo Gani?
 Jawabu:
1.   kutambua chanzo cha miujiza ,ishara na maajabu matendo 8:4-13
2.   Kutambua mawakala wa ibilisi matendo 13:6-12
3.   Kutambua aina ya roho chafu zinazotenda kazi matendo 16:16-18
4.   Kutambua vyanzo vya magonjwa na udhaifu katika miili na nafsi za watu mathayo 12:22-23
5.   Kutambua mafundisho potofu au ya uongo waebrania 1:1-2; 1thethalonike 4:13-17
4.Toa maana sita za rafiki wa kweli kwa mfumo wa kiblia ni nani?
Jawabu:
1. Rafiki ni mtu anayekupenda (yohana15:12)
2.ni mtu aliyetayari kujitoa maisha kwa ajili ya marafiki zake(yohana 15 :13) Yesu pia alionesha hilo kwa kutufia msalabani (rumi 5:8)
3.ni mtu ambaye yupo tayari kukutendea lile jema utakalomwomba akutendee (yohana 15:14)
4. ni mtu anayehusika na kushirikiana nawe(yohana15:15)
maombezi ,mafundisho na makemeo ya urafikiYesu anainua ,kuponya na kuadibisha.
5.ni yule anayejitolea kwa hiari kudumisha urafiki uliopo(yohana 16:16)
kujitoa kwa  moyo wa hiari kulinda kudumisha uhusiano wa kirafiki(yoh 7:17)
6.ni yule ambaye anaendelea  kuchagua kuwa  rafiki wakati wengine wote wanajitenga na kukimbia kwa sababu mbalimba(yoh15:17)

Alhamisi, 26 Februari 2015

VIONGOZI MBALIMBALI WAWEKWA WAKFU TAYARI KWA KUMTUMIKIA MUNGU KATIKA JIMBO LA MASHARIKI KASKAZINI



Kiongozi ni mtu mwadilifu ,mwenye imani,asiyelaumiwa kwa jambo lolote baya sanjari na kuwa na imani ya kuwatumikia jamii inayomzungukwa kwa lengo la kuwaleta maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na askofu wa jimbo la Mashariki kaskazini askofu Geofrey Massawe katika hafla ya kuwasimika na kuwaweka wakfu viongozi wa sehemu mbalimbali katika jimbo hilo ambapo amesema kuwa sifa ya kiongozi ni kuwatumikia waumini na jamii inayomzunguka.

 Askofu Geofrey Masawe akiwaweka wakfu viongozi mbalimbali katika jimbo la mashariki kaskazini.





 Kutoka kushoto ni katibu wa jimbo la mashariki kaskazini Charles Shilla na katikati niaskofu jimbo hilo Askofu Geofrey Masawe na kulia ni makamu askofu.
 Zoezi la kuwaweka wakfu viongozi
 Katibu akimpa Askofu majina ya viongozi wanaowekwa wakfu walioteuliwa kuongoza katika sehemu mpya na ya Zamani.
Aidha Askofu Massawe amesema kuwa ni vyema kiongozi anapochaguliwa ama kuteuliwa ni vizuri kuwatumikia wananchi na sio kutekeleeza matakwa yake binafsi jambo ambalo limesababisha mianya mbalimbali ya rushwa na kushindwa kuleta maendeleo.
''Ili kutokomeza tatizo la rushwa na kushindwa kutekeleza majukumu ya kila siku kiongozi anatakiwa kuwa jasiri na mwadilifu katika majukumu yake ya kila siku kama kiongozi ambaye ni kioo cha jamii'',alisema askofu Masawe.
Hata hivyo amewataka viongozi na wananchi kwa ujumla kusimamia, kulinda na kutunza amani ambayo imeasisiwa na waasisi wa taifa hili kabla ya uhuru mpaka sasa kwa kusudi la kudumisha amani na usalama ndani ya taifa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Amani na Utulivu iliopo nchini ni wajibu wa kila mtanzania kuendelea kulinda na kudumisha maana katika kipindi hiki cha uchaguzi na kuwasihi viongozi mbalimbali kuwa makini na kuwa makini na waadilifu.

AMA KWELI NDUGU MSOMAJI NI VYEMA UKAANGALIA NA KUJIFUNZA YALE AMBAYO HAIMPENDEZI MUNGU NA PIA WANADAMU,MWENYEWE SHUHUDIA WANAUME WATATU WAOANA NCHINI THAILAND



Hawa ndio wanaume watatu waliooana nchini Thailand.
Wanaume watatu waliofunga ndoa siku ya wapendanao {Valentine} nchini Thailand wamepata umaarufu katika mtandao baada ya picha za maandalizi ya harusi hiyo kuenea mitandaoni.
Watu hao walijulikana kama Joke,Bell na Art ambao walioana saa sita, usiku wa tarehe 15 mwezi Februari mwaka huu.
Kulingana na gazeti picha hizo zinawaonyesha wanandoa hao watatu wakiwa wamevalia nguo za utamaduni wa Thai uliochanganyika na utamaduni wa magharibi.
Ujumbe mmoja ulioandikwa katika katika picha moja ulisoma' mapenzi ya kweli hayawezi kuonekana na macho pekee'.
''Iwapo unataka kujua thamani yako basi ni lazima uione na moyo wako''.
katika mtandao wa facebook wa runinga moja ,picha ya wanandoa hao ilipendwa na zaidi ya watu 50,000 huku watu 1000 wakitoa maoni yao.
Hapo sasa ndugu msomaji kujifunza na kuomba kwa bidii kila mtu kwa imani yake maana hizi ni nyakati za hatari wanaume kuoana watatu hiyo ni ya wapi?
Je wewe una maoni gani.
Chanzo BBC.

Jumatano, 25 Februari 2015

HALI INAZIDI KUWA TETE HUKO NCHINI SYRIA WAKRISTO WAENDELEA KUTEKWA NYARA ZAIDI YA 350.

Kuna hofu kuwa raia wakristo kutoka Syria wametekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State.
Duru kutoka kwa jamii hiyo sasa inathibitisha kwamba zaidi ya raia 200 walitekwa nyara Jumanne baada ya vijiji kadhaa kushambuliwa kaskazini mwa Syria.

Wengi wa waliotekwa nyara ni wanawake na wazee.Wakati huo huo, mapigano yangali yakiendelea katika maeneo yaliyoko karibu na mji wa Hassaka.
Kuna taarifa zinazosema kuwa makanisa yameteketezwa moto na kundi la IS katika vita hivyo vikali kati ya wanamgambo hao na makabila ya Wakurdi wanaoungwa mkono na wakristo wenye silaha.

Taswira kamili ya mkasa uliowakumba wakristo hawa wa Syria ndiyo mwanzo unaanza kujitokeza.


 Wakristo kutoka Syria wameanza kutoroka wanakoishi.
Lakini kikundi cha wapiganaji wa kikristo kimetoa madai kuwa idadi hiyo ni kubwa hata zaidi ya hiyo.Hata hivyo kimedokeza kuwa zaidi ya watu 350 wametekwa,huku hayo yakiarifiwa waumii wengine wa kikristo wameanza kukimbia vijiji vyao wakihofia kushambuliwa na wanamgambo wa Islamic State.

Na bado vita vinaendelea huku waislamu hao wakikabiliana na waasi wa kikurdi pamoja na washirika wao wa kiksristo katika mji wa Hassaka.
Source BBC,mshirikishe na mwenzako,unaweza pia kutoa maoni yako.

Jumamosi, 21 Februari 2015

IFAHAMU BIBLIA YAKO 21 FEB JIFUNZE ILI NENO LA MUNGU LIKAE KWA WINGI MOYONI MWAKO MAANA NI TAA YA MIGUU YAKO:



1.Rafiki ni nani ?
answer:ni mtu ambaye unaweza kumwamini ,kujiweka wazi kwake.
              ni mtu anayeweza kuchangia kufaulu na ustawi wako katika maisha.
2.Mfalme yupi ambaye amezikwa katika makaburi ambayo amejichimbia katika mji wa Daudi na alikufa katika mwaka wa ngapi wa utawala wake.
Answer: Ni mfalme Asa aambaye alikufa katika mwaka wa 41 wa kumiliki kwake
               2nyakati 16:13-14
3.Neno kuabudu lina maana gani?
Answer:Ni tendo linalogusa akili,hisia,nafsi na utu wa mtu na mwili pia kwa kusujudu,kuanguka kifudifudi,au uso kwa uso
mwanzo 17:3 Tendo hilo hufanywa pasipo ushawishi wa kitu ,wala si nje ya moyo wa kumtambua Mungu kuwa wa thamani  kuliko kitu chochote anayestahili kupewa ibada ya pekee na kupelekea kujitoa kwake bila unafki wala ubinafsi .
4.Karama Tisa za Roho Mtakatifu zimegawanyika katika mafungu matatu nazo ni zipi
      1.Karama za ufunuo
·       Neno la maarifa
·       Neno la hekima
·       kupambanua Roho
2.Karama za uwezo
·       imani
·       karama za kuponya
·       matendo ya miujiza
3.Karama za usemi
·       Unabii
·       Aina za lugha
·       Tafsiri za lugha
5.Daudi na Jonathani walikuwa marafiki ni kitu (siri)gani kilichosababisha urafiki wao udumu toa sababu  sababu nne ama siri nne.
1.    mwambatano ulianzia katika roho zao.
2.    upendo wa kweli kati yao(1sam 18:1)
3.    utayari wa kila mmojaa wao kuwa mwaminifu katika patano la urafiki wao(1sam18:3)
4.    upendo wenye msukumo wa kutoa na kujitoa kwa hiari kila mtu kwa mwenzie(1sam18:4)