YESU NI JIBU

Jumatatu, 30 Juni 2014

MAISHA YA MWANAMKE MKRISTO HUKO SUDAN BADO YAPO MATATANI.


            Meriam Ibrahim
Mawakili wa mwanamke mkristo nchini Sudan ,Meriam Ibrahim wamesema kuwa watawasilisha ombi mahakamani la kutaka mashtaka ya kughushi stakhabadhi bandia dhidi ya mteja wao kuondolewa.
Bi Ibrahim alikamatwa siku ya jumanne,siku ambayo mahakama ya rufaa ilibadilisha hukumu yake ya kifo hadi kuwa ya uasi.
Kufuatia uamuzi huo alijaribu kutoroka nchini humo kupitia stakhadhi za Sudan Kusini lakini akakamatwa katika uwanja wa ndege wa Khartoum.
Wakili mmoja amekiambia kitengo cha habari cha Ufaransa kwamba ana matumaini mamlaka itamuondolea mashtaka hayo na kumpatia paspoti ya Sudan ili kumruhusu kuelekea nchini Marekani.


                                      Meriam Ibrahim akiwa na watoto wake wawili
Mumewe, ambaye ni raia wa Marekani ameelezea kuwa kulikuwa na mvutano kwenye uwanja wa ndege wa Khartoum, ambapo alikuwa ameongozana na mkewe pamoja na watoto wao wawili kuelekea Marekani, kabla wanausalama zaidi ya 40 kujitokeza na kumkamata upya Meriam.
Hukumu ya Meriam ambayo imezua mijadala ya kimataifa, ilipelekea mashinikizo kadhaa kutoka jumuiya mbalimbali, ikiwemo baraza la Congress nchini Marekani, ambapo wajumbe 38 walisaini waraka wakitaka taifa lao lichukue hatua kuhakikisha usalama wa Meriam na watoto wake wawili, ambapo hivi karibuni alijifungua mtoto wa pili, Maya, akiwa gerezani - huku ikiripotiwa kuwa akiwa kwenye uchungu, bado miguu yake ilikuwa imefungwa minyororo.
Meriam, mwenye umri wa miaka 27 - alikamatwa kwa mara ya kwanza Agosti 2013, baada ya ndugu wa baba yake kuripoti kwamba amezini (baada ya kuolewa na Wani, ambaye ni mkristo), ambapo katika utetezi wake, Meriama ameeleza bayana kwamba yeye ni mkristo, kama ambavyo mama yake amemkuza, baada ya baba yake, ambaye ni muislamu, kuiacha familia hiyo tokea Meriam akiwa mdogo.




Meriam akiwa na mumewe (mwenye shati la manjano) na watoto wake pamoja na jamaa mara baada ya kuachiwa. ©Getty Images.
source mashirika ya habari(BBC)