YESU NI JIBU

Alhamisi, 9 Juni 2016

DENI LA ZAIDI YA MILIONI 100 LASABABISHA KANISA LA SINZA CHRISTIAN CENTER KUTUPIWA VYOMBO VYAKE NJE:

Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya mil 100 kanisa la Sinza Christian Center  latupiwa nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na mmiliki jengo hilo Bwana Prosper Rwendera , akizungumzia tukio hilo  mke wa mmiliki  wa jengo Hilo Bi. Patricia Prosper Alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu." 
Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.
Hili ni eneo la Kanisa Hilo
Viti  vyote vikiwa vimetolewa nje
 Vyombo vya Muziki vikiwa nje
 Magari yakiwa yanatolewa nje
 Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi
 Vikombe nje
 Wametoa vitu vyote
Magodoro na vitanda vyote nje  
 Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa
Kushoto kwa mbali ni Mke wa Mmiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu.
 Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni