YESU NI JIBU

Jumanne, 28 Februari 2023

ZITAMBUE GHARAMA AMBAZO UTAGHARAMIKIA UKIMWAMINI BWANA YESU.

Askofu Zakaria Osward Rude akimwongoza sala ya toba kijana ambaye alifika kanisani hapo na kuamuua kumwamini bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.

 Imebainishwa kuwa kila mwamini anatakiwa kutambua kuwa kuna gharama za kulipa ukimwamini Yesu katika maisha ya kila mwamini ambaye amemkiri kwa kinywa chake kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake.

Hayo yamebaibishwa na askofu Zakaria Oswald Rule wakati akifundisha neno la Mungu katika ibada ya jumapili katika kanisa la Jesus Save Fellowship lilopo Karakata jijini Dar es salaam.

Aidha amesema kuwa kumfuata Yesu kuna gharama ambazo ni lazima kila anayetaka kumwamini na kumfuata atalipa ndipo ataweza kuishi maisha ya kumpendeza.

"Yesu amesema Kila anayetaka kunifuata lazima aikane nafsi yake na ndipo achukue msalaba wake anifuate,huwezi kumfuata Yesu ukiwa na namna ya kutokuwa tayari kulipa hizo gharama".alisema askofu Rule.

Jumapili, 19 Februari 2023

LIJUE KUSUDI LA MUNGU KUKUOKOA NA KUKUACHA ULIMWENGUNI.

 

ASKOFU ZAKARIA OSWARD RULE AKIFUNDISHA KATIKA KANISA LA JSF SOMO LA KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU KUKUOKOA NA UMEACHWA ULIMWENGUNI.

Kila mwamini ameokolewa na kuendelea kuishi ulimwenguni ilikutimiza kusudi la Mungu kwa muda wote atakaoishi.Hayo yamebainishwa na mchungaji Zakaria Osward Rule wa kanisa la Jesus Save Fellowship (JSF)lilopo karakata Dar es salaam wakati akifundisha katika ibada ya jumapili.

   Aidha askofu Rule alisema kuwa kila mwamini anapookoka anapewa jukumu la kufanya kwa muda wote akiwa ulimwenguni.

  Alinukuu kitabu cha yohana 17:11-19 ambapoalisema kuwa Bwana Yesu aliwaombea wale waliomwamini,

 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

   Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

Aliongeza kuwa Yesu alisema kuwa Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

Askofu Rule alifafanua mstari wa 17 kuwa Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.

Mwamini yeyote anapookoka hutakaswa na neno la Mungu ambalo litakuwa ndani ya maisha yake ya kila siku ya wokovu.

"Pasipo neno hakuna mwamini yeyote mwenye nguvu ya kuushinda ulimwengu na anasa zake,maana kuna vishawishi ambavyo ni neno pekee ndilo lenye uwezo wa kusaidia kuushinda"alisema.

Yesu aliwapa waliomjia uwezo na nguvu ya kuiendea ulimwengu na kuwafanya wanaulimwengu kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu kama yohana 17:18 inavyoelezea Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.

Hata hivyo askofu Rule alisisitiza waumini kutenga muda wa kujifunza neno la Mungu maana linaleta hekima,kuongeza maarifa na kuwa na nguvu ya kuushinda ulimwengu.

Ijumaa, 17 Februari 2023

SERIKALI YAPONGEZWA NA WATETEZI UHAI

Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Kutetea Uhai la Human Life International (HLI) Kanda ya  Afrika kwa Nchi zinazozungumza kiingereza, Emil Hagamu amesema kupiga marufuku Vitabu vya Ziada Vinavyotoa mafundisho kinyume na Mila na desturi za Tanzania kuendane na kupiga marufuku chanzo kinacholeta vitabu hivyo.

Alisema pia marufuku hiyo iendane na kukomesha vitendea kazi vinavyowezesha Mapenzi ya jinsi moja na makundi yanayohamasisha matendo hayo maovu zikiwemo Diplomasia zinazohamasisha.

Akizungumza kufuatia hatua hiyo Hagamu ameipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua ya kupiga marufuku vitabu 16 ambavyo maudhui yake yanakwenda kinyume na mila, desturi na tamaduni za Tanzania.

Alisema WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari alisema shule yeyote itakayobainika kuwa na vitabu hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kufuti wa usajili wa shule husika.

“Vitabu hivyo havipaswi kutumika shuleni na kwenye taasisi za elimu kwa kuwa vinakinzana na mila, desturi na utamaduni wa mtanzania”. Alisisistiza Prof.Mkenda

Alivitaja vitabu hivyo kuwa ni diary of a wimpy kid, diary of a wimpy kid-Rodrick rules, diary of a wimpy kid-the last straw, diary of a wimpy kid-dog days, diary of a wimpy kid-the ugly truth, diary of wimpy kid-cabin fever, diary of a wimpy kid-the third wheel, diary of a wimpy kid-hard luck.

Vingine ni diary of a wimpy kid-the long haul, diary of wimpy kid-old school, diary of a wimpy kid-double down, diary of wimpy kid-the gateway, diary of wimpy kid-diper overlode, Is for transgender(you know best who you are), Is for LGBTQIA(Lesbian, gay, bisexual, transgender, queer/questioning(one’s sexual or gender identity) intersex, and asexual/ aromantic/ agender; kwa jinsi mbili kukutana na kuleta ongezeko la Watu" Alisema Hagamu.

Aidha Hagamu pia alivitaka Vyombo vya Habari kukataa, kutangaza habari zilizoko kinyume na desturi, Mila za Watanzania;

that make you you na sex education a guide to life.

Kwa mujibu wa Hagamu licha ya kwamba hatua ya kupigwa marufu Vitabu hivyo.

Jumamosi, 3 Septemba 2022

INTERNEWS YATAKA USAWA KIJINSIA VYOMBO VYA HABARI

 

Ofisa Mipango Mwandamizi wa Internews, Victoria Rowan akito mada katika mafunzo kwa wanadishi wa habari kuhusu usawa wa kijinsia.

NA MWANDISHI WETU

MHADHIRI Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) Zuhura Selemani, amesema vyombo vingi vya habari vinaandika na kutangaza habari zinazowahusu wanaume kuliko wanawake jambo ambalo si sawa.

Katika mada yake kwa wanahabari katika mafunzo ya siku moja kuhusu usawa wa kijinsia hususan katika siasa na uongozi pamoja na nafasi ya wanwake katika vyombo vya habari, Zuhura amenukuu utafiti uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) mwaka 2019, akisema ingawa wanawake wengi huhitimu katika vyuo na vyuo vikuu vya uandishi wa habari kuliko wanaume, bado idadi ya wandishi wa habari wanawake katika vyombo vya habari na taasisi nyingine ni ndogo kuliko wanaume.

“Vyombo vingi vya habari pia havina sera kuhusu masuala ya jinsia na vingi kati ya vilivyo na sera hizo, havizitumii,” alisema.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya Internews kupitia mradi wa Boresha Habari, Msimamizi wa Vyombo vya Habari wa Internews, Alakok Mayombo, alisema vyombo vya habari vinapaswa kuonesha mfano bora kwa kuandika na kutangaza habari kwa kuzingatia usawa wa kijinsia kwa kupaza sauti za watu walio katika makundi maalumu wakiwamo wanawake na wenye ulemavu.

Alisema ukosefu wa usawa wa kijinsia bado ni tatizo kubwa katika jamii katika nyanja mbalimbali zikiwamo za siasa, uwakilishi na uongozi sambamba na nafasi katika vyombo vya habari.

“Bado tatizo hili ni kubwa hivyo, lazima wanawake na wanaume washirikiane kuliondoa maana tunataka wote wasonge mbele hata katika shughuli zenye changamoto ili wapate uzoefu na nafasi ya kupanda juu hata katika vyombo vya habari hivyo, lazima hata wanaume waelimishwe na kushirikishwa katika juhudi hizi ili washiriki kuleta mabadiliko badala ya kuwa watazamaji,” alisema Alakok.

Mtaalamu huyo wa habari alisema lengo la kufikia uwiano wa 50 kwa 50 halipaswi kuwa katika siasa pekee, bali pia katika taaluma mbalimbali ikiwamo ya habari kwa kutoa nafasi sawa kwa wanawake na wanaume.

“Sauti za wanawake zisikike na pia, ni vema zioneshe mafanikio na uwezo wao badala ya wanawake kuoneshwa tu kwa matukio mabaya kama ya kubakwa na kupigwa,” alisema.

Katika mada yake iliyosisitiza tofauti baina ya jinsi na jinsia, Ofisa Mipango Mwandamizi wa Internews, Victoria Rowan, alisema ili kufikia usawa wa kijinsia, lazima wanawake na watu wenye ulemavu wapewe nyenzo na kusaidiwa kwa hali na mali ili kufikia uwiano.

“Si tu suala la wote kupata kwa usawa, bali walio pembezoni wapewe nguvu zaidi ili wafikie wenzao katika nyanja mbalimbali kama siasa, uongozi na kiuchumi kwa kuwa hakuna anayezaliwa akiwa kiongozi, bali wote huandaliwa,” alisema Rowan.

Alisema wanawake hawana budi kujengewa uwezo wa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ukiwamo wa kisiasa huku kukiwa na mazingira wezeshi kama usalama, elimu na nguvu za kiuchumi.

Aliwataka wanawake kutojiweka nyuma zinapotokea fursa mbalimbali, bali wajitokeze na kuzichangamkia.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali inayobadilisha maisha ya wanawake vijana na watoto (TIBA), Marcela Lungu, alisema elimu sahihi na endelevu inapaswa kutolewa kwa jamii  ili kufikia usawa wa kijinsia.

Marcela alisema, “Vyombo vya habari vioneshe nguvu ya wanawake katika jamii ili jamii iwaone na kuwapa nafasi maana wapo wanawake wengi wenye uwezo mkubwa wa uongozi, lakini hawapati nafasi.

Akaongeza, “Tatizo hili linachangiwa pia na mtazamo hasi wa jamii, baadhi ya mila na desturi na baadhi yao wenyewe kutojiamini.”

Akijikita katika nadharia za uongozi katika mtazamo wa jinsia, mtaalamu wa masuala ya jinsia na maendeleo, Michael Marwa, alisema kitendo cha wanawake kujifunza majukumu yao mengi wakiwa katika umri mdogo, huathiri mitazamo yao na uchaguzi wa shughuli zao za kimaisha.

“Hili ndilo husababisha mtazamo kuwa jamii au kundi fulani ni viongozi bora kuliko wengine katika jamii jambo ambalo si kweli,” alisema.

Marwa ambaye pia ni Mkuu wa Mipango katika taasisi ya C-SEMA mkoani Dar es Salaam, alisema ukosefu wa uwakilishi wa kutosha wa wanawake katika uongozi si matokeo ya kinachodaiwa na baadhi ya watu kuwa uwezo mdogo au wanawake kutojiamini, bali imani potofu kuwa wanawake hawawezi kuwa viongozi bora.

“Jamii inapaswa kubadili mitazamo yao na kuweka usawa baina ya wanawake na wanaume,” alisema Marwa.