YESU NI JIBU

Jumapili, 2 Juni 2013

RUTH FAITH ORGANIZATION WAENDELEA NA MAFUNZO YA MAPISHI:



Kutokana na huduma ya Ruth’s Faith Organization kuamua kutoa huduma ya ujasiriamali na mapishi imedhihirika kuwa mpaka sasa tayari kuna watu wengi ambao wameanza kunufaika na mafunzo yanayotolewa na taasisi hiyo kwa lengo la kuwakwamua watanzania wa kipato cha chini.

Kwa sasa kuna wanafunzi wengi ambao wamepata mafunzo yao katika Taasisi hiyo na wameanza kutangaza kunufaika na masomo hayo kiasi kwamba hata wale waliokuwa wanasubiri matokeo ya kidato cha sita wametangaza na kuelezea jinsi walivyonufaika katika masomo hayo.

wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na mwandishi wa habari hizi wameelezea jinsi walivyoanza na yale ambayo wamepata kutokana na mafunzo hayo.

Happy ambaye ni mhitimu wa kidato cha sita alisema kuwa  tangu yeye aanza masomo hajawahi kukaa nyumbani na kujifunza mapishi zaidi ya kusoma shule za bweni jambo ambalo alisema kuwa kwa mwanafunzi hasa mtoto wa kike atakuwa hana uelewa juu ya  mapishi ya aina yeyote,hiyo akawasa wasichana wenzake wafike kwenye taasisi ya RFO wapate mafunzo mazuri ya mapishi mbalimbali.

Huyu ndiye Happy mhitimu wa kidato cha sita ambaye amefauli kwa kiwango kwa kwanza na anaenda kuchukulia uhandisi
Akihojiwa na WAPO RADIO kuelezea mafanikio aliyopata kutokana na mafunzo aliyopata

Mmoja wa wanafunzi ambao naye amefanikiwa na mafunzo hayo na pia ni mama mchungaji

Happy akitabasamu wa katikati na wa kulia ni mfanyakazi wa mchungaji Peter Mitimingi Christina Mbilinyi na mama mchungaji wakiwa katika picha ya pamoja

Murugenzi wa RFO na pia ni mwalimu Bi Claudin Simba akijiandaa kuwaelekeza wanafunzi wake katika somo la mapishi kwa vitendo
 Mwalimu mama Simba akiwaelekeza wanafunzi wake nao wanfurahia kwa mafunzo hayo wanayopewa kwa vitendo
Mwalimu mama Simba akiwa amekaa kushoto na happy kulia pamoja na wanafunzi wenzake mara baada ya kumaliza kufanya somo la vitendo pia wakimuaga happy ambaye amemaliza masomo yake na anaenda kuendelea na elimu ya juu baada ya matokeo yake ya kidato cha sita kutoka na kuonekan kuwa amefaulu.

Utengenezaji wa keki ndiyo inayoendelea hapo chini ni mafunzo ya mapishi kwa vitendo.

Wanafunzi wa RFO wakiwa picha ya pamoja