Msomaji nakualika
kufuatilia makala maalum ya ziara ya kinabii nchini Israeli, ambapo jopo la
Watanzania kesho linaondoka kulekea nchini Israeli, kwa ajili ya kutembelea
maeneo matakaifu, kujifunza zaidi Biblia na kufanya maombi.Ziara hii ya Kinabii ni
Maono ya Askofu Mkuu Sylivester Gamanywa wa WAPO MISSION INTERNATIONAl, ili
kuwasogeza Watanzania kuijua zaidi
Biblia na mafunuo yake, na hivyo kuvuna
baraka za Mungu, ambazo zimeahidiwa kwa wote watakaojifungamanisha na taifa
hilo la Israeli.
Wanaziara hao watakaa
nchini Israeli kwa muda wa siku kumi za kazi nzito ya kutembelea maeneo
matakatifu, kujifunza Biblia na kufanya maombi.
Msomaji, kumbuka Ziara nyingine
ya Kinabii kama hii, inatarajiwa kufanyika tarehe za mwanzoni mwa mwezi Desemba
mwaka huu. Unachotakiwa kufanya hivi sasa ni kujiandaa kwa kuanza kulipa fedha
katika benki ya CRDB nambari 02J1080000700, inayopokea dola za Kimarekani pekee.
Akaunti hiyo imefunguliwa kwa ajili
ya watu wanaotaka kushiriki katika Ziara za Kinabii nchini Israeli
zinazoandaliwa na WAPO MISSION INTERNATIONAL. Kwa anayetaka kushiriki anaweza
kuanza kulipa fedha kidogokidogo au kwa mkupuo dola za Kimarekani 3000 tu. Baada ya kufanya malipo,
tunza risiti yako na uwasilishe kopi yake,
kwa mratibu wa ziara Elibariki Minja, anayepatikana katika ofisi za WAPO
Radio FM Kurasini Jijini Dar es Salaam. Nambari za simu za Mratibu wa Ziara
Bwana Elibariki Minja ni 0786205768, 0715 452730 na 0754 452730.
Unaweza kuwasiliana naye sasa kwa
maelekezo zaidi.
Kumbuka katika ziara ya Kinabii ya
mwezi Desemba, ofa maalum ya kuwasafirisha bure watumishi wanaochunga makanisa
itatolewa kwa kigezo maalum! Hivyo changamkia sasa ofa hiyo ili nawe uzuru
Israeli ambako ndiko hasa kwenye chimbuko la imani yako, hususan wewe Mkristo anayemkiri Yesu kama
Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
Msomaji,hebu sasa tunayaangalie
maeneo matakatifu yatakayotembelewa,
ikiwa ni mfululizo wa maeneo hayo, ambayo tulianza kuyachambua tangu wiki
iliyopita.
Eneo ambalo Yesu alibariki
mikate mitano na samaki wa wawili na
kulisha maelfu ya watu, nalo litatembelewa na Wanaziara ya Kinabii kutoka nchini Tanzania , ambao wanaondoka kesho jioni.Ikizungumzia
tukio hilo katika
Injili ya Luka 9: 14, Biblia inaeleza
kuwa:.. akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili waandikie mkutano. Wakala, wakashiba wote; na katika vile
vipande vilivyobakia, walikusanya vikapu
kumi na viwili. Watu waliokula walipata kama elfu tano..(Luka 9:14)
Katika Mathayo 14:15 – 21
Biblia inabainisha kuwa nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila
wanawake na watoto.Eneo
jingine litakalotembelewa na Wanaziara ya Kinabii kutoka nchini Tanzania
ni Mlima wa Heri.Hapa ni pale ambapo kwa
mujibu wa Kitabu cha Injili ya Mathayo 5:3-10, Yesu Kristo aliketi mlimani
akifundisha juu ya Heri tisa.“Heri walio
masikini wa roho, maana ufalme wa
mbinguni ni wao, Heri wenye huzuni,
maana hao watafarijika……”“Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki, maana
ufalme wa mbinguni ni wao…”“Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea
kila neno baya kwa uongo, kwa ajili
yangu, furahini na kushangilia kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni ;kwa
maana ndivyo walivyowaudhi manabii
waliokuwa kabla yangu”.
Hizo ni baadhi ya tisa
ambazo Yesu alizifundisha kwa wanafunzi wake. Wasomi wazuri wa Biblia
wanazielewa sana
heri hizi na mafundisho ya Injili ndani yake.Msikilizaji
eneo hili ambalo linatunzwa sana ni eneo moja zuri sana
lenye bustani safi
za matunda na miti ya Mizeituni. Ukoka safi na maua mengi. Mungu
akusaidie siku moja nawe ufike. Tafadhali wasiliana na Mtaribu Elibariki Minja,
ili uweze kushiriki katika ziara ya mwezi Desemba. Nambari zake za simu ni 0786205768,
0715 452730 na 0754 452730
Msomaji Wanaziara watapata fusra ya kuuona Mlima Hermoni.
Wakazi wa Kanaani yaani Waamori
walikuwa wakiuita Senir,
wakati wakazi wengine wa Sidoni waliuita
Sirion (Zaburi 29:6, 1Nyakati 5:23, Ezekieli 27:5, Kumb 3:9).
Mlima Hermoni Kibiblia ni mpaka wa nchi ya ahadi yaani Kanaani, waliyahidiwa
Wana wa Israeli na Mungu (Kumbu. 3:8), ( Joshua 11:17, 12:3, 13:5)
Vijito vya maji vilinavyotiririka
kutoka katika Mlima Hermoni hukutana na
vingine kutoka katika mapango hayo yanayofahamika kama
Panias na kuungana, kisha kuelekea
katika Mto Yordani na baadaye katika Bahari ya Galilaya.
Kitu cha msingi katika historia ya Biblia Takatifu ni
kwamba, katika eneo hili la mlima
Hermoni lenye miamba na mapango mengi, Yesu Kristo alifika na wanafunzi wake.
Na ndipo alipomwambia Mtume Simon Petro kwamba atampa funguo za Ufalme wa
Mbinguni na lolote atakalolifunga duniani,
litafungwa hata mbinguni.(Mathayo 16:13-20). Hapa ilikuwa baada ya Yesu
kumuuliza Perto kwamba wanafunzi wake wanamnenaje.
Alipomtupia Mtume Perto swali hilo , alimjibu kwamba anamnena kuwa yeye ni Kristo, Mwana wa Mungu aliyehai.
“……Heri
Simon Baryona kwa kuwa mwili na damu
havikukufunulia hili, bali baba yangu aliye mbinguni”, Ndivyo Yesu alivyomjibukwa mujibu wa
Injili ya Mathayo 16:15-17 na Marko 8:27-30..
Msomaji Vilele vya milima ya Golani ni sehemu muhimu kwa Israeli ya sasa. Wanaziara wa Kitanzania watapa fursa ya kuliona.
Vilele vya milima ya Golani
hufahamika kama Golan Heights kwa
Kiingereza, kwa Kiebrania ni Ramat Ha
Golan, wakati kwa kiarabu ni Mustafaatu I-Jawlan. Hivi ni vilele vya milima
ambavyo kimsingi viko katika pembe ya
Kusini mwa milima mingine ya Lebanoni,
ambayo inaunda mpaka wa Israeli na Syria .
Hivi ndivyo vilima vilivyotwaliwa na
Israeli kutoka katika milki ya Syria
kunako mwaka 1967, wakati wa Vita vya
Siku Sita kati ya Mataifa ya Kiarabu na Israeli.Theluthi mbili ya milima hiyo
iko chini ya Israeli, inayoishikilia kwa kiapo cha kutoiachia kamwe, hata kama
ni milki ya Syria .
Umoja wa Mataifa (UN), Jumuiya ya
Ulaya (EU), Uingereza, Marekani, Umoja wa nchi
za Kiarabu na Jumuiya nyingine za
Kimataifa, zinatambua kwamba milima hiyo
ni miliki ya Syria ila tu
Israeli imeikalia kwa nguvu.
Mwaka 1981, Israeli ilipitisha sheria ikijiruhusu
kuvimiliki kisawasawa vilele vya Milima ya Golani, na kuviwekea hadhi ya
umiliki kamili, hatua ambayo ilipingwa
na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa azimio nambari 497. Vilele vya Milima ya Golani vina
kilomita mraba 1,800 sawa na maili
mraba 690.
Kwa
nini Israeli inavishikilia vilele hivi vya milima ya Golani?.
Maji
na Kilimo:
Kuna vyanzo vizuri ya maji
yanayoingia katika Bahari ya Galilaya. Maji kutoka katika Mlima Hermoni huingia
katika Mto Yordani na kuunganika na maji mengine yanayotoka katika vilele vya
Milima ya Golani, na kumiminika katika
Bahari ya Galilaya.
Katika bonde la Milima ya Golani
kuna eneo zuri kwa ajili ya kilimo. Shughuli hiyo huendeshwa katika mashamba ya Shebaa yaliyoko
katika sehemu ya bonde la Mto Yordani, Milima ya Golani na Hermoni. Ni eneo
leye rutuba sana na safi mno kwa kilimo na maji.
Ulinzi
na usalama:
Vilele vya milima ya Golani,
vinatoa nafasi nzuri sana ya suala zima la Ulinzi kwa taifa la
Israeli.Unapopanda katika vilima hivi, unayaona mataifa matatu ya Kiarabu yanayoizunguka Israeli, mataifa
hayo yate kwa namna moja au nyingine ni maadui wa Taifa la Israeli.
Ukikaa katika kilele kimoja kikuu cha Milima ya Golani, unakuwa kama Mfalme aliyekaa katika kiti chake cha enzi, akiwatazama watumishi wake kwa chini. Ukiwa
hapa huweza kuona Mataifa ya Lebanoni, Yordani Syria na Israeli yenyewe.Ni eneo
muhimu la kivita na kiusalama kwa Israeli. Ikiwa Israeli italiachia na
kulikabidhi kwa Syria ,
hakika Israeli itafutiliwa mbali kutoka katika ramani ya uso wa dunia. Golani
ni roho ya ulinzi wa Israeli.
Msomaji, huna sababu ya kukosa
kushiriki katika ziara za kinabii kama Mungu
amekupa uwezo huo.Wasiliana na Mratibu Elibariki Minja, kwa ajili ya ziara ya
mwezi wa kumi na mbili mwaka huu kwa simu nambari 0786205768, 0715 452730 na
0754 452730
Bahari ya chumvi, Dead Sea, au Bahari Mfu ni moja ya maeneo yakayotembelewa na wanaziara
ya kinabii kutoka
Bahari ya chumvi, Dead Sea, au Bahari Mfu ni moja ya maeneo yakayotembelewa na wanaziara
ya kinabii kutoka Tanzania .
Ni Bahari yenye urefu wa Kilomita 76
na upana wa Kilomita 18, ikiwa katika eneo la Kusini Mashariki mwa taifa la
Israeli. Kwa Kiebrania Dead Sea inafahamika kama Yam
Hamelach.
Kuibuka kwa Bahari hii maelfu kwa
maelfu ya miaka iliyopita, wataalam wanasema kulitokana na miamba
inayounganisha Bara la Afrika na taifa la Syria , kuvunjika na kutitia.
Bonde la Mto Yordani, Bahari ya Galilaya na Bahari ya Chumvi au Dead Sea, vyote vinatokana na tukio hilo la
kijiografia, ambalo kwa waliobobea katika maswala ya Jiografia, wana nafasi
nzuri ya kulielewa..
Bahari hii imelala katika uwanda wa
jangwa la Judea , ambalo linakutana na jangwa kubwa kabisa
nchini Israeli, Jangwa la Negev.Chanzo kikuu cha maji katika Bahari ya
Chumvi ni Mto Yordani, unaotiririsha
maji yake kutoka katika pembe ya Kusini ya Bahari ya Galilaya.
Kiasi hicho cha chumvi, kinaizidi
chumvi inavyopatikana katika Bahari ya Mediterania mara kumi.
Takwimu zinaonesha kuwa asilimia
kumi ya chumvi yote ulimwenguni inapatikana katika maji ya Bahari hii
iliyokufa au The Dead Sea .
Madini hayo yaliyoko katika maji ya Dead sea , ni dawa nzuri ya macho kwa wenye matatizo ya
macho. Wengi waliyatumia yakawasaidia, kuona vyema.Watu wengi wanaotembelea
bahari hii ya chumvi, huoga katika maji yake, na kujipaka matope mwilini, ambapo ngozi zao huwang’ara
na kupona magonjwa yaliyokuwa yakizifanya zionekane zimesinyaa na kuchoka.
Katika pwani ya Bahari hii ya chumvi
katika eneo liitwalo Mitzpe Shalem karibu
na Qumran kuna kiwanda kikubwa cha vipodozi.
Pia kuna maduka ya bidhaa nyingine nyingi za kawaida, mahoteli, nyumba za kulala
wageni na beach za stahere mbalimbali.
Zama hizo, Malkia wa Sheba , Kushi au Ethiopia
alifika katika Bahari hii na kuoga, kujipaka matope yake, akang’ara na
kumeremeta sana .
Mfalme Sulemani, Malkia Cleopadra na Herode
the Great wote walipata huduma ya bahari
hii.
Sehemu nyingine ambayo Wanazira wa
Kitanzania watatembelea ni pamoja na Mji wa Kursi. Mji huu uko mashariki mwa Bahari ya Galilaya au ziwa Genezareti, kama kilomita saba kufika njia panda ya kuelekaea katika
vilele vya Milima ya Golani au Kiti cha Mfalme Israeli. Enzi za Yesu Kristo
katika karne ya kwanza, Mji huo uliibuka na rekodi ya kipekee kwa mnyama
aitwaye nguruwe.
Katika kitabu cha Mathayo Biblia
inauelezea Mji wa Kursi kwamba ulikuwa wa nchi ya Wagerasi.Wakati mmoja Yesu
akiwa katika nchi hiyo, Wagerasi wawili
wenye pepo walikutana naye.Mara wale pepo ndani yao walipomtambua Yesu walianza kulia na
kupiga kelele: “Tuna nini nawe Mwana wa
Mungu?, Je umekuja kututesa kabla ya muula wetu?”.
Wakati hayo yakiendelea, tazama kwa
mbele kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe likichungwa na wachungaji. Kilichotokea ni kwamba wale pepo walimsihi Yesu wakimwomba kama anataka kuwafukuza kutoka ndani ya Wagaresi wale, awaruhusu wawaingie nguruwe wale.
Yesu akawaambia nendeni. Wale pepo
wakawatoka wale Wagerasi na kuwainga nguruwe wale. Maskini. Kilichofanyika hapo
ni wale nguruwe wote kupagawa pepo na kukimbia hadi katika Bahari ya
Galilaya na hatimaye kuzama na kufa
maji.Mji wote ulipopata habari ulitoka kwenda kumwona Yesu kwa hofu, na moja
kwa moja, wakazi wa mji huo, wakamsihi aondoke mipakani mwao. (Mathayo 8:28 –
34).
Mji wa Naini ni sehemu nyingine ambayo jopo la
wanaziara ya kinabii kutoka nchini Tanzania litaitembelea.
Ni Mji uliopo karibu na Mlima Tabor
(Mlima Wakubadilika Sura) uliopo Kusini Magharibi mwa Bahari ya Galilaya.Ni
katika eneo la Mji huu, ambapo Yesu Kristo akiwa na wanafunzi wake na watu
wengine walifika katika lango lake na
kukutana na maiti ya mtoto pekee wa
mwanamke mjane, ikipelekwa kuzikwa makaburini.
Katika Luka 7:13-15, ikielezea tukio
hilo Biblia
inaeleza kuwa Bwana alipomwona alimuonea
huruma, akamwambia usilie, akakaribia,
akaligusa jeneza, wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema kijana,
nakuambia inuka. Yule maiti akainuka, akaketi!
Katika mji huu watu wanaotembelea
Israeli, hutumia waombea wajane na watoto wao, ili wakutana na Yesu Kristo,
na kupata suluhu ya kudumu ya dhidi
matatizo yao . Kumbuka Neno la Mungu linatuambia kuwa Yesu
Kristo ndiye mume wa wajane!
Msomaji, hayo ni baadhi ya
maeneo yakayotembelewa na Wanaziara ya Kinabii
kutoka nchini Tanzania
ambao wanaondoka kesho jioni, wakiongozwa na Askofu Sylivester Gamanywa ambaye
ndiye mwandaaji Mkuu na mbeba maono ya Ziara
hizo za Baraka.
Ufanye mwaka huu wa 2013 kuwa wa
baraka za kipekee kwako kwa kushiriki katika Zaira ya Kinabii ya mwezi wa kumi
na mbili mwaka huu.
Wasiliana na Mratibu wa Ziara hiyo
Elibariki Minja katika simu nambari 0786205768, 0715 452730 na 0754 452730
kwa maelezo zaidi.